Nikachukua nguo zangu nikatia kwenye buti, nikaondoka zangu kwenda kusiko fahamika. Njiani nikaihia Johan simu, nikajitambulisha mie Debby girlfriend wa Michael, mbona umenichukulia bwana? We umetoka huko USA kuja kupora mabwana za watu si ndio?Analeta uzungu mwingiiio, i didnt know, ooooh sorry, so sorry. Nitaongea na Mike kuwapatanisha. Niachie mimi. Nikamuona bonge mpja ya mzunguuuu.
Na Michael kazini kanifungia vioo. Alijua kunichoka vibaya jibaba lile. Nikimsalimia kimyaaaa. Naumiaaaa moyo sababu nampenda. Nikaamua kumpigia Joan sasa, si alisema atatusuluhisha. Hapo nishajua ni mke wa mtu, aliolewa na black america, wana 2 kids na mumewe. Na ndo kilichonipa moyo kwamba ana onja tu hana nia ya kujitaifishia bwana wangu.
Nikampigia akapokea Michael, anauliza unataka nini sisi tunalala mda huu. Nikamwambia namuomba Johan, akampa simu. Nikamuuliza ushaongea nae kutupatanisha? Akageuka you bich, mambo yako na bwana wako msinihusishe kabisaaa. Hapo loud speaker hivooo. Katuana katukanaaa.Nikamuuiza mimi single woman na wewe mke wa mtu who is a bich?
Msidhani Mike alikuwa hajui kaolewa ana watoto wawili, anajua na harusi alihudhuria vilevile, yote hio afanikishiwe mipango yake ya kuhamia marekani tu. Kumbealimwambia ataachana na mumewe black america waende wakaishi wote marekani. Basi bozo langu lilikuwa linazama chumvini daily. Marekaniii mbaliii msizanie masihara.
Wakawa close msisikie. Akaondoka tena yule dada. Kaka kanifata kuniomba msamaha mrefuuuuuuu kama mto nile. Kaihakikishia its over and done. Tupendane daima. Mimi nampenda nikamsamehe kwa moyo mmoja. Tukawa safiii. Mpaka alivokujatena. Safari hii akajiwahiii naeda kuachana nae rasmiiii. Alivoenda simu ndo hakupokea mpaka keshoooo ndugu wasomaji. Sana sana akaja kunipigia Joan kwamba vitu vyangu kavitupaaa vyote pale home nisihangaike kuvifata.
Siku hio nikachokaaaa, nikavamia saa 2 usiku, nakuta nyumba yoooote imewashwa mishumaa romantic, sikuwahi kuwashiwa mishumaa hata siku ya kutolewa bikra. Nimeingia chumbani nimekuta mipicha picha yao ya kimahaba chumba kizima sijui wamepiga lini. Nikachana chana yote, pigana pigana na Joan, Mike ananipiga mimi kumtetea Joan, kwa nguvu za maumivu ya moyo niliwakunguta wote mpaka wakakimbilia kwa majirani uchiii. Msomaji mimi ni betinabetina haswaaa. Huyo Joan pande la mtu. Majirani wanakuja kuangalia Tyson gani kawakunguta hawa wananikuta Betina, wakacheka tu na kuhisi Mike na jimama lake wanatafuta kiki kinguvu mtaani.
Nikapitisha maamuzi, mimi na Mike baaaassss. Joan akaondoka baada ya kutulizwa nyege zake, Mike akapata mdada mkaliiii, hatariiii anaitwa Romana. Kichangu tu cha mjini hamn anachofanya. Ndugu wasomaji huyu Romana ni kituuuuuu, ni gomaaa la hatari, ukioneshwa yule ndo kakupora bwana unajipa talaka 7 bila ndoa.
Mie sikuwa namjuaaa. Siku naona wanaume wa TBL hawatuliii ofisini wanaitanaa. Wanasifia Mike MAFIA. Si kwa toto lile, ilikuwa gumzooo. Ndugu wasomaji nilipat Period siku ya 12 badala y 30 stres zake. Watu wanunga mkono usimfnnishe Roman na vitu vya ajabu ambavo ndo mimi. Jamaniiii. Betinaa nilikomaa. Kuja Romana pale TBL ilikuwa kawaida sanaaaa. Na akija sihemiiiii. Ingekuwa tunajiumba ningerudi maabara kujiboresha.
Siku ya siku nikashindwaaa kabisaaaa. Usiku peke yangu chumbani nikaandika 24hrs resignation bila kushurutishwa na mtu yoyote. Sio kwamba mimi wa kishuaaa sanaaa ila ilinibidi. Nilianza kudataaa, nikaona kuna maisha mengine zaidi ya Mike na Romana bora niwaachie washinde wao nijiweke pembeni.
Shangaaa mwenyekiti sherehe za kuniaga ni Mike, tena hana habariiii. Hapo tushaacha mchuno we just talk like normal people. Nikaagwa kazini, nimeacha kazi na kazi sinaaa. Kuka home ikawa double stress. Baba akaona nadataaaa. Akamwambia bamdogo USA hii USA iliotaka kunitoa roho mwenzenu, anialike nikae kae kule walau nisahau hali yangu haikuwa nzurii. Akatuma invitation, nikaenda kuomba VISA, nikapata.
Sasa pale ubalozii, kuna watu walikuwa TBL zamani kumbe wanampa taarif zote Mike, kajaa, Visa kapataaa, kila kitu. Mi siku ya siku nikazama kwa Bush enzi hizo. Najiachia tu kwa uncle
Charge imeishaaa tukutane keho