Some strangers who turnout to be relatives.
Kiukweli haya mambo ya mimba yaliumaaaa sanaaa, sanaaaa. Yalinivurugaaaa vurugaaa. Mwanaume shubhamit yule kapotelea kusiko julikana, na the worst part huwezi hata kuwaambia watu wa karibu kama Lidya. Manake wote watasema we told you so. Nilikuwa nataka mtoto ndio ila sio kwa design hii jamaniii.
Na katika vitu nisivo vipenda maishani ni kuonewa huruma, kuwa kitu kinachotia huruma. Basi nikawa najikaza mpaka basi. Nje naonekana bonge moja ya jasiriiii. Ila moyoni niko nyanganyanga. Vipande vipandeee haya mambo yasikie tu kwa mwenziooo.
Mpaka kuna muda nikawa nawaza hivi ina maana mi mdhambi sanaaa, kupita watu wote dunianiiii, au kuna baya gani kubwa nililolifanyaaa mimi mpaka kupewa adhabu hiziiii. Nikajitahidi kukumbuka pengine nilimdhulumu mtu labda au kuna binadamu nilimfanyia ubaya. Sikupata jibu kabisaaa.
Ndugu msomajiii mimi hamjanijua tu, ni mtu mwenye upendo sanaa. Sina uchoyo kwa wanaume, , sina ubaguziii, sihesabu favor. Mimi nikimpenda mtu nampenda jumlaaa jumlaaa. Sijuagi kubakishaaa. Hata watu waandamane waseme nini mimi nitasimama na mpenzi wangu mpaka mwisho. Katika maisha yangu kupenda ile kumpenda mwanaume nimependa wanaume wawili tu, Dee na Msomali na wote walinikimbia bila sababuuu. Kupenda kumekula kwangu mara 2.
Really i might have not admitted before, ila kama msomali angenihitaji kwa ndoa nilikuwa tayari, i was waiting for him to ask me to mary me. Hata alipoomba nimzalie, it broke my heart but it was something. Low key i was seeing myself spending the rest of my life with him. Japo nje ndo nazuga aaah hana future, hana issue, sizitaki hizi mbichiii mnajua tena wasomaji. Mimi mwanaume yule nilimpenda sanaaa. Na anavojua kufanya sasa, alinimaliza kabisaaaa.
Na kilichonivuruga zaidi ni kuwa Tonny nae anadai hii mimba yake. Kuna uwezekano mkubwa. Uwezekano upo ila kama sio yake je? Alafu Tonny na msomali ni kulia na kushotooo. Yaani huwezi hata kumbambika mtoto. And he was not making it easy for me all. Yaani Tonny ana mambo ya umama sanaaa, mpaka anakeraaa.
Mi tumeongea nikamwambia mi sijuiii, ila kama wewe ni baba siwezi kukunyima haki za mwanao. Utamlea na utakuwa kwenye maisha yake bila tatizo lolote. Ila subiri kwanza unaweza kufanya mambo kibao ukakuta mtoto sio wako. Mnaelewana vizuriiii kabisaa, dakika 10 nyingi, ana badilika nataka kukuhudumia sijui nini! Sasa namuuliza unihudumie toto likitoka la kisomali je? Utarudishiwa na nani hizo gharama zako. Mnaelewana sawa atasubiri.
Siku ya siku kamleta mama yake mzazi aje tufahamiane sijui nini. Yaani alinitibuaaa. Nikamwambia sasa hata kama huyu mtoto ni wako sikupiiii. We si unajitia baba bora ndo sikupi sasa. Inshort niliwachukia watu woteeee wa kile kikundi. Kasoro Dee, maana nae kumchukia ni buree tu, hata ukimchukia ni kazi bure atakutapeli tapeli mpaka utashangaaa. Na ujinga wake hajaaacha mara oooh mama mjamzito wa moto sanaa, nipe nitanue njia basi, utaenda ukutwe njia imefungwaaa. Mxiuuuuuuuuu.
Kwenda clinic nikamkuta mdada. Mi sikuwa na time, nikaa zangu kimya. Akaanza kunisabahi. Akaniuliza mbona haupo na mwenzio. Nikadanganya tu anaumwa. Akasema aah! Tell him to put a ring on it. Nikatabasamu tu kinafki. Mara ya pili nikamkuta tena, Dr wetu mmoja, na zamu yetu kumuona ni siku moja. Ikatokea tumezoeana, tunaenda kunywa juice, na kula ubuyu. Hajui mi ni nani, wala nafanya nini, na mimi sijui yeye ni nani na anafanya nini.
Siku akanialika kwake akaniambia njoo na mwenzio. Nikasema sawa, ila sikwendaaa, mwenzio hioo vepeeee. Akanialika amra ya 2, nikatoa sababu.Akasema basi wao waje kwangu. Nayo pia sitaki maana wangenikeraaa kubebishan bebishanaa wakati mi napambana na hali yangu nikatoa sababu. Akawa ananichimbaaa ajue undani wangu. Nikasema nini bora nimwambie mwenyeweee cause atasikia tu.
Nikamwambia nikamwambiaaaa kila kitu, mpaka kwamba sijui mimba ya nani, nipo kama sipo akasema usikate tamaaaa. Kuwa na imaniii. Nikashangaaa maana kila mtua aasema kwani we hukuona mwisho utakuwa hivo? Akasema hata yeye aliteseka mnnooo mnoo kumpata mumewe wa sasa. Kama sio imani na kuvumilia basi leo hii ingekuwa story. Ndo kuanza kunipa ubuyu jinsi yeye na mumewe walivo leteana mapicha picha.
Sally mi sikufichiii, mimi nimejitunzaaaa, nimejitunzaaa kweliiii. Mpaka naanz kazi bado bikra. Nimesoma diploma, degree, zoteee sijatoaaaa uchi, namtunzia mume wangu. Nilikuwa mchoyo si wa nchi hiii. Nilikuwa na bwana toka diploma ananipendaaa mi simpendiii na akawa anasubiri sababu anajua mi bikraaa. Nimeajiriwa TBL, bado bikraaa. Sasa kuna mkaka TBL ambae ndo mume sasa anaitwa Michael akawa ananitongoza. Miezi 6 namzungusha.
Mwezi wa 7 ndoo kuanza kudat. Hapo yule bwana wa chuo kapata kazi serengeti, kanunu gari, hyundai kanipaaa, yeye si ana ya kampuni. Michael hajui kama ile gari ya BF. Michael mtu wa mjiniii sanaaa, bata ndefu na nini. Huku na huku akaja kunibembelezaaa nikampa mchezooo. Japo roho iliniumaaa sanaa kujitunza kote nimeshindwa kumtunzia mume mda mfupi tu umebakiaa. Bf alivojua akachukua gari lake, na tukaachana kiroho safi. Anasisistiza wewe huyo mwanaume humuweziii wa mjini sanaaaa.
Kila mtu TBL alijua mimi na Michael ni wapenzi. Huku na huku mapenzi kukolea na bikra kashakulaaa anakuja kuniambia ana mwanamke mwingine anasoma chuo. Jamaniiii! Roho ilinitokaaa. Nikawekwa pembeniii. Niliumiaa niliumiiaaaa ndugu msomaji usitake kujuaa. Ila bado nampendaaaa. Ikaenda ikaenda huyo dada anakuja ofisini, wanaonekana viwanja mi nipo kama sipo. Nikasema sasa basi. Nikawa pembei tu. Wakaja kushindwana wenyewe.
Akarudi mikono nyuma nikampokea, mapenzi yakarudi upyaa, tukawa tunaishi wote mi nikakubali, tukawa tunaenda kazini na gari moja, tunapendana sanaaa. Sasa cha ajabu akaja mmarekani mbongo, na mambo yake ya marekani walikutana msibani, akamwambia atamfanikishia hio ndoto yake ya kuhamia marekani. Karudi msibani, simu masaa 24. Akaingia kuoga nikaiba ile namba. Wameenda kuzika kila kituo anampigia simu kujua anaendeleaje. Nawatizama tu. Nikasikia anarudi kesho dar.
Nimekaaa sina hili wala lile asubuhi naambiwa mama endesha gari yako. Nikaleta upinzani kwanini wakati tunaelekea sehemu moja na kila siku tunaenda wote. Akakaza kila mtu kimpango wake siku hio, kajinunishaaa hatari. Tumetoka wote, kufika njiani kanipotea, nikajua namkuta kazini. Kufika nakuta katoa udhuru anaharisha. Nikajua labda tumbo limemuanza kwenye gari. Piga simu yake siku nzima hapokei.
Jioni bado hapokei. Nimekaa na watu bar mpaka saa 5 wakaniaga oyaaa kesho kazini. Nampigia ndo akapokea namwambia baby uko wapi nahitaji funguo nirudi nyumbani, nimechokaaa. Ananiambia nenda kwa dada yako mi nitachelewa kururdi. Mmmmmh! Nikasema hunijui nikarudi nyumbani. Tunakaa compund moja na best yake.
Inavoonekana alikuwa anajua kila kitu, kunionaaa akaanza kupiga simu kwa fujo.. Mara Michael akarudi. Kanunaaa bila sababu. Kafungua nimeingia. Natafuta nguo zangu kwani niliziona sasa. Saa zima sioni chochote. Ikabidi nimuulize baba ake nguo zangu ziko wapi akanionesha kabatini chini kwenye mavitu, zimechopekwaaa, mpaka chupi yangu mbichi ya asubuhi. Loooooh! Wanaume hawaaaa waoneni hivi hivi. Nawaambia hata wewe msoamji kwa jinsi kulivopigwa masasa usingestuka anaishi na mwanamke.
Nikamuuliza tu Joan ulimleta humu leo? Akasema ndio. Bila hata kuzunguka wala kuangalia pembeni, kanikazia mijicho hatari.