Weekend story! Dare the devil and face your own ghosts!

@lara1 utatuua we mwanamke, this is so sweet to be short aaaaaiiii.
Btw huko coco vepeeeeee wa mkoani ndio imekula kwetu au?
 
Jamani Lara anatumia mtandao ganii....nijitolee.afu Lara,nimewaza Jana,io issue yako ya redundant officin,chukulia kama changamoto.zama izi kujiajiri ndo issue,hasa ktk upande wa chakula,changamoto zigeuze fursa, utaona utavyotusua na shetani atacheza regge km sio mdundiko jinsi mambo yako yatakavyokuwa supa.......ideas nyingibtu,maji ya jumla,bakery, confectionery.... Etc.utatusua mjini apa.naa ivi besdei pati za mababy zilivyo nyingi....hatare....
 
Jamani Lara anatumia mtandao ganii....nijitolee.afu Lara,nimewaza Jana,io issue yako ya redundant officin,chukulia kama changamoto.zama izi kujiajiri ndo issue,hasa ktk upande wa chakula,changamoto zigeuze fursa, utaona utavyotusua na shetani atacheza regge km sio mdundiko jinsi mambo yako yatakavyokuwa supa.......ideas nyingibtu,maji ya jumla,bakery, confectionery.... Etc.utatusua mjini apa.naa ivi besdei pati za mababy zilivyo nyingi....hatare....
duuh huu uandishi wako mkuu duh!!
 
Jaman thanks for concern, ila sijachukua redundacy wala nini, nimefanya maamuzi magumu nibakie, niwalambe makalio, wakinitimua niende mahakamani. Hahahaaaa! Japo roho inaniuma ningekuwa nimejaa sahivi zingetosha kwenda China.

Ni kwamba jana kulikuwa na shoti ya umeme so sikuwa na power kabisaaa ila ndo naandika sahivi.
 
Jaman thanks for concern, ila sijachukua redundacy wala nini, nimefanya maamuzi magumu nibakie, niwalambe makalio, wakinitimua niende mahakamani. Hahahaaaa! Japo roho inaniuma ningekuwa nimejaa sahivi zingetosha kwenda China.

Ni kwamba jana kulikuwa na shoti ya umeme so sikuwa na power kabisaaa ila ndo naandika sahivi.
Ok sawa.
We are waiting for yu
 
Jaman thanks for concern, ila sijachukua redundacy wala nini, nimefanya maamuzi magumu nibakie, niwalambe makalio, wakinitimua niende mahakamani. Hahahaaaa! Japo roho inaniuma ningekuwa nimejaa sahivi zingetosha kwenda China.

Ni kwamba jana kulikuwa na shoti ya umeme so sikuwa na power kabisaaa ila ndo naandika sahivi.
Uniite ukiweka....!
 
Violla akaona ngoma nzitooo, akaamua kujipanga upya sasa ili aweze kukabiliana na pastor. Akaona kwa uzito wa pastor anahitaji mbinu za ki nuclear. Akaamua aende nae kwa stage maalumu. Maana watu wa Mungu nao, wanafiki afu wagumu balaaaa. Ukitaka kwenda nao kwa pupa hutowezaaa.

Akamuanzia stage one, ambayo yeye Violla anakuwa mtumwa wake, no matter what, when where, hata amafanyie ukatili gani au amfanye nini, yeye anakuwa kama zuzu tu. Anakubaliana na yote kila siku kujifanya mjinga. Juu ya hilo pia anakuwa kinganganizi hatari. Hata kama hatakiwi yumooo. Usikubali fate yako kiboya boya tu, we mtu ushamuelewa, even if the heavens were not kind enough to cross your stars, it is not the end of the world, work up, you get some astronomy to do, and cross your own stars. If you want anything done correctly do it yourself. She is going to make her own luck.

Kesho akiwa kazini bored kama kawaida akapiga yule dada wa mume mwenye gubu, kumshukuru. Akasema tangia ajitoe kwenye ushindani wao, mumewe amebadilika amekuwa na wasiwasi kama anaoga nje. Kila siku anamuliza mbona huna furaha kama zamani, au nakutesaaa, au unataka kuniachaaa? Anamuangalia tu. Hana mda nao kabisaaa, anaishi yeye kama yeye. Tena kaanza zake kujifugia kuku wake, akirudi anakuwa busy na kuku, badae anawasimamia wanae wafanye homework,, anahakikisha wanae wamekula, wamelala baaaaasss! Analala roho nyeupeee.

Akamwambia kuna siku mume kasafiri kwenda Morogoro kamuaga dada yake basi. Yeye kampigia hapatikani mpaka saa 5 usiku. Akasema asilale ndani kizembe, akaanza kuzunguka hospitali zoteee mjini labda alipata jali huko ama vipi, akifika anawaambia nimepotelewa na mume wangu, wanamuonesha majeruhi ambao hawajatambuliwa na ndugu zao wa siku hio. Mwisho akaamua ampigie simu dada yake saa 11, waanze kuangalia maiti za siku hio ambazo hazijatambulika sasa mochuwary, labda ndo keshakufa tayari huko kaibiwa simu, huwezi jua. Wakaingia na dada yake ambae mtu mzima kidogo, kila jokofu likitaka kuvutwa nguvu zinamuishaaa anataka kuzimia, wakikuta sie, anapata nguvu. Kaanglia wa 5, akamwambia dada yake amuangaliziea. Wakaanza Amana, Temeke, Muhimbili, Lugalo. Ikawa ishafika saa 7 mchana. Wakakata shauri wampigie wifi yake sasa tenaa, maana toka jana akipigiwa simu anakata.

Ndo wifi akapokea sasa hio simu, basi dada mtu anamuelezea bwana sikia mume wa huyu mdogo wetu hajarudi jana usiku, sasa tushamaliza hospital zote usiku wa janaaaa, hapa navoongea na wewe yupo hoi, toka jana tunakupigia. Sasa tumekupigia tushauriane, kama kwenda ofisini kwake kutoa taarifa ama vipi. Wifi yupo aaaaaahhhhh, nilisahau kumwambia Mumewe alienda Morogoro kwa inshu zake, ilikuwa ghafla hajamuaga, katoka kunipia sasa hivi ameibiwa simu yake, nimpe namba ya mkewe, maana hanayo kichwani ana ya kwangu tu. Ila yupo salamaa, poleni sanaaa, mimi nami msahaulifu sanaaaa. Dada yake akamtukana matusi ya nguoni yasiyoandikika hapa akakata simu. Anamwambia Violla embu fikiria situation ilivokuwa mbayaaaa na alivumilia yote hayooo.

Ila sahivi akianza mama J, kabla hata hajamalizia anachotaka kusema anamwambia sawa tu haina neno. Basi wifi anakuwa mkali sawa unajua nachotaka kukwambia? Anamwambia chochote utachotaka sawa tu, mimi sina nenooo kabisaa, hata ukimtaka kaka yako ukalale nae, mimi sawa tu mwenziooo juu yenu sasa hio guest mtayoenda, ukitaka chupi zangu kabatini chukua zote mimi sawa tu, sina nenooo, hata ukitaka kizazi changu nimzalie mumeo mimi sawa tu, sina neo kabisaaaaaaa. Wifi chochote unachotaka kufanya fanya wala usiniulizeeee.

Wifi gaidi ila anajua mtu alefikia point of no return anakuwaje. Ujue mtu saa zingine akijitia chizi unamuonesha uchizi zaidi yake, anatulia mwenyeweeeee. Sahivi amekuwa mpole, inakuwa sasa wifi ndo anabembelezaa. Akashukuru kweli kwa mchango wa ushauri wake. Mume nae ndo kujishuku shuku maana dada mtu aliekuwa anamtegemea kanyooshwa. Kikubwa kilichotokea mume akasimamishwa kazi mwenzio. Akawa kachanganyikiwa. Kaenda kwa dada mtu amuwezeshe anayumbishwa tu, mara hili mara lile mradi msaada hapewi. Ukapita mweziii. Yeye anamuangalia tu na dada yake bwana, anavohadhirikaaa. Dadake akamwambia auze nyumba wafanye business, akamuomba ushauri mkewe akamwambia utafaa nini ushauri wangu? Nishawahi kukushauri nini ukanisikiliza na kutomsikiliza dadako? Mi nangoja dada yako akufilisi kila kitu nikucheke vizuriii ukiwa unahadhirika. Umemuomba dadako ushauri mke hunaaa? Uza hata watoto ukishauza nyumba. Mume akasita kuuza nyumba akawa kalost home anaangalia tv.

Dada kapunguza kuja asilimia 90, akimtafuta sababu haziishi. Alivoona akili imemkaa vizuri, akakopa saccos hela akaagiza mchele Mbeya gunia 300, na kukodi fremu. Wiki mbili zikaisha kauza kilo 20, afu anaonjihisi kudhalilika na kazi ya kuuza mchele na masters yake mkononi. Looooh! Hapo wifi kaja kukopa kilo 25. Mmmmmhhh! Bi dada akaona mkopo wa watu ataadhirika, akaanza kuwaambia wenzie kazini jamani nauza mchele, anawaonesha sample ofisini, niletee kilo 10, huyu 20, huyu 30. Anawaambia waambieni na wenzenu, basi ndani ya wiki kilo 300 zikaishaaa. Hela anapokea mumewe. Wala hamuulizi hela zangu aje, umetumiaje au vipi. Mchele ulioisha akamwambia leta rejesho la mwezi huu, nisikuone humu ndani nenda mbeya kafatilie mchele, kwanini tununue kwa dalali we unakaa tuu humu ndani. Mume akakubali kwenda huko shamba, wakakubaliana akae wiki 3. Ukaisha mwezi hajarudii wala nini. Akimpigia ooh sijapata mchele mzuriii natafuta usiwe na wasiwasi mke wangu. Akawaza isjekuwa kala hela ya mchele ananizugaaaa! Mwezi na nusu. Wiki ya 7 akakuta nyumbani pembeni kumepigwa bati koteee mmmmh! Akashangaaa! Kumpigia mumewe akasema eeh nimemtuma mimi huyo mtu, hakutaka kubishana kwenye simu.

Wiki ya 8 akapanga amfate huko huko manake keshamtia shoti ya frame miezi 2 hakuna mzigo hela haizunguki. Amewaza hivo leo, kesho kaja na gunia 1000 wakati walikubaliana gunia 400. Ndo kisa cha kupiga bati. Gunia za mchele site kote, stoo, mpaka vyumbanii, nje koteee, ikawa ni shidaaaa. Bibie akaanza kuutoa ofisni kwao sasa capacity ya ofisi yao ni gunia 300 kwa mwezi, ndani wana gunia 1070 na hawawzi kusubiria maana mchele unaota wadudu. Akaanza kazini ana google catering Tanzania, anatafuta facebook watu wa catering, akipata namba zao anawaambia kuna mchele wa Jumla nawafanyia bei nzuri, wanakuja kuungalia, Akapigia kama watu 100. Weekend akauza kama gunia 300 maana wote wana harusi na matukio. Wakaoda tena gunia 300. Zikabaki kama 100 hivi tu, ambazo zikawa tu dukani wakawa wanakuja wafnyakzi wenzie na wafankazi wenzake kuchukua kwa familia. In 3 weeks wana kilo 20 za kula wao.

Mume akamrudishia mtaji wake wotee akalipe saccos. Pili akamgea faida yake, za zile gunia 600 aliweka NSSF yake kumbe humoo. Akamwambia bwana acha kazi tufanye hii business. Mke akamwambia sitaki, kesho atakuja dada yako kuwa ndo anaamua kwenye hii biashara sitakiii. Fanya wewe mi nitakuwa nakusaidia tu, afu pia napenda kazi sababu tu inaniwezesha kuoga na kupendeza kila siku hata kama hamna nalo lipata. Hahahaaaa! Basi akamwambia anataka alete gunia 3000, wanafanyaje sasa wife? Wife akamwambia we letaa, mi nitatafuta tenda za hoteli, migahawa, maduka ya jumla, supermarket, dar yote hii nitaimaliza. Leta 9000 ila zipishane kwa interval ya 3000 kila mwezi uhakika. Shmba wakajenga bonge la ghalaaaa. Akaleta, na wana tenda hoteli kama 30, catering, shule 5 za masista na binafsi, kwa mwenzi wanauza gunia 5000, wako kwenye kuu brand mchele wao, na kuutafutia vibali wausambaze nchi nzimaaa.

Mume anamtetemekeaaaa. Yani dada mtu sahivi hakohoi, almanusra kuchapwa makofiiii live live. Akikohoa mume huyu hapaaa. Kuna siku mafanyakazi alikuwa hajamjua kama ndo mke wa boss, akamkosea adabu alitimuliwa kama mwiziii, almanusura kupigwa ngumiii, mpaka akamuombea msamaha kwamba bado mdogo na hakujua kama yeye ndo maza house. Akaambiwa shukuru kakuombea msamaha. Mume wivu umezidiii, akitoka kazini anamfataaa kila siku, siku 5 kwa wiki, mwezi mzima, mwaka mzimaaa. Kama ni outing jioni waongozane, kama ni kuwahi home, wawahi wote. Kitchen party anapelekwa, anafatwa. Gari ingine ipo lakini kuiendesha labda weekend, ila kumuendesha ni wajibu wa mume, madai mapenzi kumbe anamchungaaaa. Akikumbuka aliondoka na mabegi hakufatwa kituoni akaa masaa 2, anacheka tu, akimkumbusha mumewe hata hachangiiii, wala hacheki.

Violla akamsaidia tu kufurahiaaaa, mambo yake yalivonogaaaa. Akamwambia njoo unitembelee, ningekwambia tukanywe bia mdogo wangu ila shemeji yako anakaba mpaka penalty siku hizi, atataka awepo kwenye hizo bia sasa ndo mambo gani hayo sasa. Violla akaona hapo hapo ndo penyewe, akamwambia kama vipi nae atakuja shemeji, so watakuwa 2 by 2 wale wakiongea mpira ampee huo umbea vizuriii

Shoga akubali, wakapanga jumamosi ijayo wafanye huo mpango. Violla akaanza kuwaza sasa atampataje pastor kwenye huo mtoko, maana coz kuna wale wanandoa pale, pastor hatoona ugumu , na dhamira yake ilivo nyepesi, kidogo ataona unafuuu. Akaanza kumpelemba pastor, kuna mahali naomba unisindikize. Pastor akaanza kujitia yuko busy kukwepa vishawishiiii. Violla akamkumbusha alivomsindikiza fellowship. Pastor bado akawa mgumuu kama lubaaaa kukubali. Ikabidi sasa abadilishe formation, akamwambia walau ungejua wapi, na kuna nini? Sikia mimi kuna rafiki yangu Mungu kawabarii sanaa na mumewe, karibuni, hakika wameuona mkono wa bwanaa, wanauza mchele unatokaaa kama cocaine, sijui kama unanisoma pastor, sasa mimi nimeshawishi watoe shukrani kwa Mungu, na wewe Pastor utawasaidia zaidi kiimani na kuleta Mungu zaidi kwenye business zao, maana walipitia majaribu makubwa sanaaa. Believe they rich, would offer handsome 1/10 scarifise, not to mention the shiloth and other sacrifises.

Pastor akamwambia mimi nitaenda, sio sababu ya sadaka, mimi mtumishi wa Mungu, Mungu ananiangalia tumeambiwa tusibebe fimbo, wala mkoba, ikiwa maua yanavikwa vizuri kondeni na ndege hawalimi wala hawavuni je mimi mtumishi wa bwana sitopungukiwa na kitu. I will go because Mungu amejidhihirisha kwa hao watu, labda ana nia yake mimi nikutane nao kupitia wewe, labda kuna huduma natakiwa kuitoa, so nitaenda na wewe, ila sio kwa sadaka wala fungu la 10. Sadaka wakatoe huko huko wanakosali ikiwa wataona ni vyemaaa. Mmmmmmhhhh! Violla akaona pamoja na yote hilo la kwenda ndo muhimu katika maongezi yote.

Jumamosi wakaamua wakutane pub moja mida ya jioni flani amazing. Violla akajua Pastor ataagiza soda, Paster akaagiza castle light! Mmmmh! Wakatambulishana pale, na Pastor kama kawaida yake akajitambulisha ni pastor, zikaanza story za Jehova Jire jioni yooote. Shoga akasahaulika kabisaaa. Wanandoa ndo kujielezaa na kujifanya wanamsaka Mungu kwa tochi, kisa tu wamemuona Pastor pale. Basi pastor nae akaanza utabiri, anaona hela nyingiii zinakuja upande wao, anaona brand kubwaa ya mchele kuletwa na wao. Almanusura yaanze maombi. Violla akawa kawachoka kabisaaa. Jioni yote ikawa vifungu vya kujifngua uchumi wako, wakaanza kuandika mistari ya kusimamia kujikomboa kifedha, kujiimarisha kibiashara, kuomba barakaa katika bishara zako, kadhalika wa kadhalikaaa. Mpaka giza nene likaingia. Violla kajuuta kuja na pastor pale. Pastor akaalikwa mpaka nyumbani kwao, makubwaaaaa.

Mda wa kurudi Violla anajiongeza ujue nimepata wazo, ufungue kanisa kubwaa, mi nakuwa nakuletea waumini wealthy kama hawa, unaonaaa, tutafika mbali sanaaa, tutakuwa kama Gwajima in no time. Pastor akamwambia tu hakuwa pastor ili apate hela, sababu kuna mambo mengi sanaa angeweza kuyafanya akapata hlea nyingi zaidi ya kuwa pastor. Yeye amechaguliwa na Mungu kama Yona alivochaguliwa kwenda Ninawi na amehangaika sanaaaa kukataaa huo witoooo, amefanya mambo mengi kupigana na huo unabiii, na hakuna kitu hajafanya ilimradi tu asiwe Pastor ila ikashindikana. Ndo maana yupo kama kanasaaaaa. Sababu Violla ni mgumu kuelewa, mwepesi kusahau imemlazimu Pastor kumsimulia story yake ambayo watu wengi hawaijui.

ITAENDELEA SAA 2 USIKU KIUKWELI NA UHAKIKA.
 
Back
Top Bottom