Weekend story! Dare the devil and face your own ghosts!

Weekend story! Dare the devil and face your own ghosts!

Hizi story za Lara 1, zina wafundisha Dada zetu kuwa wasipoteze muda kushindana na wanaume/Waume zao....
Pia Mke bora huwa ni msaidizi na mshauri mzuri Wa Mume wake.
Bravo Lara 1
 
1970'S

"Mama Bryan, nimesema sitaki uende na mwanagu kwenye makanisa yako ya kilokole, tutakorofishanaaa. Mimi baba yake ni mkatolic, bau zake wotee ni wakatolic safiii, na wapagani labda wale kabla ya ujio wa missionary. Sitaki sitakiii umbadilishe huyu mtoto dini, bora unitukane nitakusamehe ila sio kumbadilisha mtoto dini. Na sijui hizi dini za waprotestant umeanzana nazo wapiii na kulowea kabisaa kuliko hao waprotesatant wenyeweee. Hukai nyumbani na mumeo kama zamani, hatwendi out, unashinda kanisani badala ya kushinda na familia yako, unaondoka wiki 2 kwenda hija zisizoeleweka, madai unaniombea unachoniombea kitu gani? Mimi nataka uwe mke wangu sihitaji mchungaji humu ndani, nikihitaji huduma makanisa kama uyoga Dsms hii siku hizi." Bryan hakuelewa kwanini kila siku mzozo wa kanisa haukuisha baina ya wazazi wake, akajikuta kalichukia kanisa katika umri ule mdogo maana ndo lilileta utengano mkubwaaa katika familia yao. Ikawa mama yake akitaka kwenda nae kanisani anakataa tu, anajilizaaa, ili tu baba yake asije kumsema na kumtukana akaanza upagani katika umri mdogo.

Akiwa na miaka 10, mama yake alifariki baada ya kuugua mda mrefu na kuombewa sanaaa, sanaaa, akiamini alikuwa amelogwa, ila alivokuwa mkubwa alikuja kugundua mama yake alikuwa na Pepsic Ulcers ambazo hakufata ushauri zikawa chronic, na hakuzingatia tiba akwa anakazania maombi na yeye ikamla mpaka last stages kabisaaa ndo akaja kufosiwa kwenda hospital. Kufika kule kabla ya operation, Bryan akawa kaenda kumuangalia na baba yake, akamuita akamnongoneza, mwanangu hata nikifa leo, usiwe Mromaa, huo ndo wosia wangu mama yako wa mwisho uuzingatie sanaaa. Bahati mbaya kwenye operation pressure ikashuka akafariki.

Akabaki na baba yake, baba yake akamuuliza mama yako alikwambia nini cha mwisho? Akamdanganya tu, alimwambia anampenda sanaaa, na amtunze yeye baba yake maisha yao yote asimuache, wala asiruhus familia ivunjike. Baba mtu akatirisha machozi tu ya uchungu. Uchungu ukaanza upyaaaa. Wkaishi kama mwaka na baba yake vizuri tu, anaulizwa unakula nini, nikuletee nini, unataka kwenda wapi, hivo baba mshikajiii kabisaaaa. Baba anamuendesha anavotaka yeye. Ila walishindwana swala moja tu la kwenda kanisani Roman Catholic. Baba yake kaongea kachokaaa, haendiiii. Kajaribu kumpiga akaona atakuwa sugu labda mpagani wa kuzaliwa, ikawa kamuacha tu. Akimuacha kidogo anajaribu kumnunulia nguo mpya, kumuahidi vitu vizuri vizuri ila kanisani haendiii. Mwisho akaamua kumuaccha tu.

Baada ya mwaka na nusu, baba yake akaanza kuishi na mama mwingine, mwanzoni akawa anampenda mnooo. Ila alivo beba yeye mimba akakiona cha motooo. Akaanza kumnyanyasa, akamwambia baba yake, baba yake akamtimua na mimba yake hivo hivo, akawa anaomba msamaha wapi, ila sasa akaona baba yake hana furaha kama wakati yule mama mwingine yupo. Akamwambia tu baba mrudishe tu mama. Alivorudishwa akapigwa mkwara mzito sanaaaa.

Akawa hamnyanyasi ila anambagua mpaka mtoto anajua kabisaa hampendiiii. Kwa hio Bryan akakua hivo hivo akakosa mapenzi ya mama. Baadae mama wa kambo akaanza kudai Bryan ana majini mengi ndo maana haendi kanisani. Akamshika shika mumewe akili wakamleta mchungaji aje amuombee majini yamtokeee. Bryan akakubali basi yule mchunaji anavoomba akawa anafurahia ana enjoy kabisaaa. Akamuwekea mikono akapigwa radi hadi akaanguka pembeni jasho linamtokaa. Mama yupo onaaa, nilisemaaaa, ana majini mengi sanaaaa.

Mchungaji akamwambia huyu mtoto hana majini,wala hata kijini cha kupita hanaaa, ana upako mkubwa sanaaaa, ana nguvu kubwa sanaaa za kiroho. Baba mtu akanza kukataa sasa, mambo gani tena kwa mwanae nunda asieenda kanisani. Mchungaji akamwambia mama mtu, huyu mtoto kaa nae vizuri sanaa, ana nguvu kubwa sanaa ya upako, akikunuia lolote baya litakupata, kaa nae mbali kabisaaa, nguvu alio nayo huyu kijana siifikii hata robo. Yule mama akaogopa kabisaaaa, akawa anamtetemekea sasa, Bray mwanangu unataka nini, nikupukie nini. Yaani ikawa mchungaji kabadili mambo kabisaa pale ndani. Akamuomba baba ake awe anampeleka kanisa la mchungaji yule aliekuja. Ikabidi wawe wanasali huko sasa. Akona heri mwanae awe mlokole kuliko mpagani.

Shule ya sekondari akaacha tena kwenda kanisani kabisaaa. Akawa muhuni tu kama teenagers wengine suguuu. Kukwepa kwenda kipindi cha dini akaanzisha dini yake, inaitwa dini ya Bryan. ALianza na wahuni wenzie kumi, akawa ana hubiri kivivu tu, wanaimba mapambio, wana rap humo humo injili. Mara ikafika watu 100 wiki ya kwanza, Wiki ya pili wakazidi kujaa, akapata wazo awe anakusanya sadaka. Akakusanya akapata hela nyingi. Akazidi kuiboresha dini yake ya Bryani, anatumia biblia kutapeli sadaka. Akisimama pale mbele wala hajiandai, maneno yamajia tu, na vifungu vinamjia tu kichwani naturally, anaona amen za kutoshaaa kwa sanaaa. Kujipatia sadka akawa anaombea ufaulu wa masomo, matatizo ya wazazi, matatizo ya kifamilia, uchumi wa wazazi. Dini ikawa kubwaa ikahamia hall. Vipindi vyote vya dini vikawa vyeupeee. Na watu wakawa wanatoa ushuhuda kufunguliwa mambo yao kiukweli kabisaa baada ya kuombewa na Pastor Bryan. Sadaka zikazidiii, akawa hana shida ya hela kabisaa, anakula bata refu mnooo. Mademu anajisevia kwa kujileta au kuwa manipulate kutumia hudumaaa. Anasema alikula nyuchi si kidogooo. Wazazi wanamtumia hela kwa watoto wao za shukrani. Alikuwa don.

Mwalimu mkuu akaja kumpa suspencion kwa kuendesha kipindi cha dini bila kibali, na kuifuta dini ya Briyan rasmi hapo shuleni, na Bryani akahamishwa shule na mzee wake. Kilichomuuma mzee wake ni hilo kosa la kuanzisha dini feki. Akampiga stop kujihusisha na shughuli za kichungaji kwa namna yoyote ile. Alivomaliza Olevel akaenda nje ya nci ambapo hamna dini kabisaaa, akarudi tena upagani. Akapata demu wa kizungu ana hela balaaa, sema Mcatholic wakamwagana baada ya Bryan kukaa nje ya fence ya kanisa siku ya msiba wa baba wa huyo binti. Binti akaona Bry hayupo serious. Kinachomzuia kuingia kanisani Roman kitu gani. Kumbe wosia wa mama yake.


Alivomaliza degree zake, akarudi bongo na mtaji wa kutosha, maana kule alipiga box la maana, na alikuwa na vision akifika bongo atusue vipi. Akarud kajipanga kabisaaaa. Na dollar anazo mfukoni. Plan yake kubwa alitaka kuinvest kwenye entertainment industry, akarudi na vifaa vyake vya kisasa vya kupigia Disco, awasambazie watu rahaaaa. Enzi hizo 1990s Disco ilikuwa habari ya mujini. Akakodi ukumbi kabisaa, akwa kapiga,mwezi wa kwanza kukajaa kukafurika, ila kama kawaida ya wakazi wa dar kuchungulia kijiwe kipya, baadae akawa anaajiendesha kwa hasara, akaacha akafungia vyombo ndani kwao.

Akafungua bar, nayo ikabamba mwanzoni baadae ikafa kibuduuuu. Baba yake akamuongezea mtaji kumsapoti, na this time akawa anashinda mwenywe hapo bar, ana manage 24/7 wapiiii. Ana kuja na idea mpya siku hadi siku ila hatusui. Akahisi ni location mbaya labda, akaja mtu kufungua bar maeneo yale yale akawa anajazaaa mpaka wanakosa pa kukaa wanakunywa bia wamesimama. Mmmmmmhhh! Bryan akaona itakuwa tu sio riziki, manake bar yake ya kisasa, safi, bei zile zile , ipo comfortable anatoa value added services ila wateja wana furika uswahilini pub. It was too much for his ego akafung bar. Akafungua botic, wakaagiza nguo nje, perfumes, vitu classic. Vilkakaa dukani wee mpaka wakagawia ndugu na kufunga duka. Basi Baba ayke akamwambia afikirie kitu cha kufanya yeye atatoa mtaji, ila Bryan akamwambia acha tu ngoja nikaajiriwe tu, sina mkono wa biashara.

Basi CV nzuriii, anajieleza vizuriiii, anajibu maswali inavotakiwa lakini haitwi kazini wala nini. Baba yake akataka kumfanyia mpango kazini kwao kwenye shirika la mafao, alishaingiza watu zaidi ya w 5 nduguze hawana hata vyeti vya maana, ila alihangaika kumuingiza Bryan mpaka kesho haikufanikiwa. Akawaomba kaka zake na dada zake kwenye kampuni zao nako ikashindikana, wakawa wanashangaa maana pass zake nzuri sanaaaa. Bryan akaanza kukata tamaa. Baba mtu akaanza kumshawishi maybe arudi nje, manake kule mambo yake yalikuwa fresh sanaaa. Labda nyota yake hapo bongo.

Akaja mshikaji wake kumshauri wakacheki kwenye katibaaa, huenda kuna mtu kumzima nyotaa yake na kumtupia mikosi, Bryan alivokuwa kachoka akakubali fastaaa. Akapelekwa kwa babu, wacha watimuliweeeeeeee. Mganga kawatimua akisema Bryan asikanyage tena hapooo. Mshkaji akashangaaa, akasema anyway waende kwa wataalamu wa vijini hawa wa mjini wengi magumashi. Wakaenda handeni, njiani akaja mtu katumwa na mganga waishie ahapo hapo mganga hataki kuwaona kwake kabisaa, keshawaona kwenye radar na hawatakiwi.

Akawa kalost mjinii na kaanza kumlostisha mzee wake maana hela za mzee wake za akiba alimpa afanye biashara, biashara ikawa imekzikata humo humo. Akiwa anatafakari afanye nini linamjia wazo fungua kanisa. Analipuuzia. Zinakuja kumbukumbu dini yake ya Bryan ilivobamba what if akiipeleka next level, akawa anawahubiria watu wazima wenye hela zao? Akawa anasita tu huenda likafeli. Akaota mara 3, anamuona Yesu anngaa sanaa akimwambia fungua kanisaaa. Akajua tu tamaa zake za sadaka. Akapuuzia. Akaota mara ya 4, na asubuhi yake akaumwa homa kali sanaaa, hadi wakawa wanamuwekea kijiko asimeze ulimi, afu usiku, sasa hio kazi ya kijiko ikashindikana kumkimbiza hospitali, akaitwa mchungaji akawa anamuombea kwa mbali mbali, akatulia kabisaaa na kuamka kabisaaa. Kuuliza vipi? Mchungaji akamwambia unatakiwa kumtumikia Mungu, fungua kanisa, mkono wa Mungu uko pamoja nawe.

Akamwambia mzee wake nimeona nifungue kanisaa, akamwambia sawa, mimi na mke wangu mama yako na dada zako tutakuwa waumini wa mwanzo, nitawaambia na baba zako wadogo, wake zao, na ndugu zetu wengine, ndugu wa mama yako waje kukusapoti. Kupanga logistics mzee akamtoa mpangaji kwenye nyumba yake moja akampa afanye kanisa. Sasa mzee akamwambia waibomoe, waijenge kisasa, kanisa hata wafanyakazi wenzie wakija waone eeeh kweli manae ana kanisa, sio ubabaishaji. Bryan akamwambia baba ustumie hela haa kumi, tutaanza kutumia nafasi ya bebuleni, watu wakiongezeka tunatumia nje pale, kama Mungu yupo pamoja ansi kweli basi mafanikio tutapata tu. Akakubali kishingo upande.

Ibada ya kwanza, wakajikuta Bryan, baba yake, mama yake, na dada zake basi. Hata ndugu zake hawakuja. Mzee anamwambia basi tukatangaze clouds labda, au tutafute fancy location, ile kumtia moyo mwanae. Wiki hio akaprint posters yeye Bryan akaanza kuzibandika mji mzimaaa. Akawa anapata simu simu hizi. Jumapili wakawa watu 20, na familia yake. Wakakusanya sadaka sh 10,000. Baba mtu anamshukuru kila muumini aliekuja siku hio kushiriki nao. Akafanya maombi ya siku 7 ikiwa Mungu kampa kibali na hio kazi basi ajidhihirishe.

Wakatarajia wiki hio watakuwa labda 30, wakibahatika. Mweee, mweeeeeeeee! Watu walikuwa kibaooooo, kisebule hakikutoshaaa. Wiki inayofata wakaweka mahema nje, na kufunga music system. Waimbaji wa mwanzo kabisaa mdogo wake wa secondari na wenzie. Wanafanya mazoezi wanaimba kwenye mic. Watu wakashonana mpaka nje majirani wanaulizana kunani tenaaa? Wanaambiwa kanisaaa. Watu wakajaaa zaidiiii. Wkakusanya sadaka Million 4. Baba yake akawa hasikii hili wala lile akabomoa nyumba ile na kujenga kaka jihall kubwaaa. Wakawa wanajazaaa tu. Hajawahi kujua idaid ya waumini wake, walikotoka au wamemjuaje.

Akaanza huduma rasmiii sasa. Ila baba yake bado anangangani waji commercialize, wasiridhike na small seady growth wafanye promotion, road shows, massive marketing cause church business pays. Maana mtu anakaa kwenye nyumba yake mwaka mzima anamgea million3, wao kwa siku moja tu wamekusanya 4 million. Bryan anapata maono ya kumkataza ile sio biashara ni hudumaa. Ndo mpaka leo wamehamia sehemu kubwa sanaa alipowakuta Violla sasa.

Violla akamuuliza kwa nini asiende Roman Catholic tena parokia ileile aliokuwa akisali mama yake, ataujua ukweli kwanini mama yake alimwambia vile, what didi she have aginst Catholics? Bila hivo he will always live as a curious man.

ITAENDELEA SAA 5 USIKU
 
Mara nyingi nimekwambia kwa hizi stori zako ni bora ukatoa vitabu wadau tusaport.
Saivi ungekuwa unaukaribia u milionea,....Lara 1 levo zako ni za kina Hussein Issa Tuwa.
 
Mimi nasubiri iishe ndio niisome yote.
Siwezi ku-handle pressure za lara 1
Mwenzangu saivi sitaki nipitwe... Nilikua nafatilia story ya sex slave nikaacha siku kadhaa ili nikute imeisha nijisomee kwa raha... Ni mpaka na leo sijawahi iona tena toka nlipokomea naumiaje roho.... Huyu Lara 1 mimi ntaenda nae sambamba
 
Pastor akagoma kwenda hio parokia wala kufatilia lolote. Viola akajua kazi yake ni ngumu kuliko alivohisi itakuwa, maana Pastor kumbe sio fake Pastor, ni Pastor kweli kiuhalali. Akaenda kumshusha kwa dada yake akaondoka zake. Akiwa kwa dada yake akaanza kuona point ya shemeji yake pale anajibana bureeee. bora tu apange, na hivi kibuzi cha sahii ni pastor hawezi kuingia lodge heri tu apange ghetto lake, akae humo.

Akamwambia dada yake nia yake ya kupanga., dada yake hakuwa na neno kabisaaa, akamwambia kama umeona vema basi sawa, wewe kapange tu kwako. Akatafuta nyumba ya peke yake, kajumba kadogo ila kanajitegemea, akalipia akawa kaingia ana kitanda na godoro basi na kapeti chini. Akaanza kujijenga mdogo mdogo. Huku Raul anarudi kwa kasi ooh ashafanya maamuzi anamuacha yule wa nje, anamuoa yeye Violla. Violla akamuuliza unamuachaje mzazi mwenzio? Maybe kumsuspend ila wazazi hawaachani ngooo, wanakumbushiana daily, yeye hizo stress hazitaki kabisaa. Raul anajieleza jamani alizaa kabla ya kukutana nae, sasa tatizo ni nini? Hawezi kurudisha mda nyuma awe hana mtoto. Violla anamwambia hio imekula kwako. Ila Raul akajua akimlainisha vizuri Violla atajaa tu nyavuni. Ikawa hachoki.

Ikawa kaanza kumkaribisha pastor kwake, for maombi you know anahamia nyumba mpya. Pastor mjanja akataka atajiwe location ya nyumba ilipo ili aende kwa mda wake hata akiombea nje ya geti upako utaingia tu. Tobaaa. Violla hatakia anadai kwa urafiki wao, pastor sio wa kuombea nje, ni wa kuingia ndani kunywa bia 2 ,3 na kumfanyia maombi chumba mpaka chumba. Pastor kagoma hio huduma. Violla akamwambia mimi napika kama huji shauri yako, afu nitakushangaa sanaaa. Yesu mwenyewe aliingia nyumbani kwa Martha na dada yake, akaaa akala mpaka chakula cha mchana jikumbushe Luka 10:38 sasa mtumishi wewe vipi you make exceptions? Pastor akakubali kweli she has a point and Jesus did enter Marthas home., yet still kutokana na kazi kumbana hatoweza kwenda pale kwa ratiba ya Violla.


Violla akamtega "what is it you are afraid of more? Me or the devil inside you?" Pastor akaichunia. Violla akaja kugundua Pastor akibanwa kuliko aseme uongo bora akae kimya tu, to keep you guessing. Basi Violla akamsisitiza mimi napika, manake ni siku jema, nafanya uasafi, najiandaa na ujio wa bwana nyumbani kwangu. Ile kufosi kingi mule mule mwenye imani. Pastor hakutoa guarantee kama ataenda au hatoendaaa. Violla wiki hio kavunja kibubu kanunua makochi dining, sebule ikangaa siku moja. Akawa kajiandaa si kidogo oraaaaaaa. Anaona siku haifikia. Kama leo kesho ndo siku yenyewe akamtumia sms kumkumbushia tu kuwa kesho ndo kesho mda wa mchanaaa. Asubuhi dada yake kamuomba amsindikize kariakoo, akasingizia tumbo la bleed limembana sanaaa hawezi kwenda. Kumbe anasafisha hata nzi hatakiwi. Kila mda anapulizia airfresher.

Saa 4 kaanza kuandaa mahanjumati, macaroni ya cheese yaliyochanganywa na nyama ya kusaga. Kajipikilisha hapo kwa you tube mpaka saa 7. Akatia kwenye hot pot akaweka dining, na sahani zake mpyaa za maana, glass zake. Juice alitengeneza jana iko kwenye friji. Matunda kwenye friji. Akaiweka na bible juu maana atauliza tu yule mtumishi. Saa 8, kimyaaa. Saa 9 kimyaaa, saa 10 kimya, saa 11 ikaingia sms. Akakimbilia simu, akavuta kwanza pumzi kuisomaa hio sms. Akaamua kuisoma sasa akifungulia pale pale kwenye notification bar. Tobaaaaaaaa!

Imeandikwa "MPAWA inakopesha mpaka 500000 kwa siku, jiunge leo.............."Akashusha pumzi kwa hasira kali. Akachukua kile chakula akakitia kwenye makontena akakibwaga kwenye friji. Akawasha muvi, hainogi kabisaaa. Akachukua PC yake akanza kuangalia muvi za kutishaaa ili tu zimboost mood japo ya kutishika ila mawazo yaondoke huko kwenye kuchomeshwa mahindi na pastor. Akachagua muvi ya Appocalypse now ambayo ashaiangalia mara 10. Ikawa haimleti mzuka kabisaaa. Akaamua kuangalia Neria walau imtie tu uchungu hata wa msiba. Bado mood hana kabisaaaa. Akakata shauri aiangalie movie za kinigeria za kichawi. Wapiiii. Akaamua kujikalia. Akajaribu tena na movie ya Hanibal Rising ya world war 2, kidogooo ikampata attention yake. Manake hio movie ni ya world war 2 inatisha haswaaaa, watoto wa 2 wameachwa na wazazi wao, peke yao wakiume na wa kike. Sasa Nazi wale wakaja kujificha kwao. Wakawa wanakula vibudu vikaisha, baadae wakakosa kabisa chakulaa, wakamchinja yule mtoto wa kike na kumla kidogo kidogo kwenye friji. Mwishoni yule Nazi wakatoroka wakamuacha yule mtoto wa kiume. Akaishi mda mpaka akaja kuokolewa na majeshi yauingereza ila alikuwa haongei afu anapiga kelele sanaa usiku.

Alivokuwa mkubwa, akawatrack wale Nazi wote waliokuwa nyumbani kwao, akaanza kuwaua mmoja mmoja, walivobaki 2 wakatafutana hao Nazi wakaanza kumtafuta yule dogo. Baadae akamuua mmoja tena, sasa wa mwisho kabla hajamuua akamwambia mambo ya kumtatanisha kidogo, kuwa sawa nilimua mdogo wako tukamfanya chakula, hakikuwa kitu kizuri, na kimenitesa maishani yangu yoteee. Lakini nashindwa kuelewa wewe kaka mtu hasira yako kubwa ni kwamba tulimuua mdogo wako au na wewe ulimla na kuendelea kumla mpaka siku ulipookolewa na wanajeshi wa uingereza? Which makes you more mad? Hannibal akamuua yule mtu bila kujibu lile swali wala nini. Picha likaisha.

Kustuka kuangalia mda saa 3 usiku. Akajua tu haji wala nini. Akakata shauri ampigi simu maybe hata hakujua anampigia amwambie nini sasa. Ila akampigia anyway. Ikawa inakatwa, baadae ikazimwa.Akawa sasa yuko really pissed. Akataka kwenda kukimwaga kile chakula ila akata shauri sio Pastor mwanaume peke yake mwenye mdogo wa kula msosi ule. Sababu pastor kadengua wapo wanaume wengi tu wangeupenda msosi ule na kushukuru. Akachukua simu akampigia Raul! Raul coz anajijua yupo bench hakujivunga, Violla akamuuliza are you busy, Raul akamwambia not for you dear, hata kama niko chooni nanya, ukiniambia nije wala simalizii navaa hivo hivo nakuja. Hhahahaaaa! Wakacheka wote.

Violla akamwambia bwana nimeamia new crib, karibu upaone, kuna msosi mwingi tu hata ukija sahivi, utaukuta. Raul akamwambia SAY NO MORE. Niko hapo dakika sifuri. Dakika 20 nyingi anagonga, akamwambia kachukua boda boda msosi usije kupoa bure. Akamkaribisha mezani, akaanza kukipasha kile chakula from the friji, akaweka sahani zile zile, glass, juice, matunda. Raul anasema ama kweli Mungu wake ni mwenye nguvu, si kwa ugomvi ule, na kuwa ignored ghafla tu, kaitiwa sosi la maana usiku huo. Akambeep na shetani nae akiwa kwenye mstari usiku huo uchi atapata pia sio haba kwa Jumapili moja moja kama hizo ataongeza sadaka.

Akajipakulia sosi la baba mwenye nyumba, ana jitutumua kama faza house, juice anajaza glass, chakula mlimaaa, anakisifia kitamu sanaaa, sijui nini. Wakaongea fresh tu mpaka wakawa wanacheka kabisaaa. Anasimulia habari za yule mtoto wake wa kule kaongea nae that week anajua vitu ni balaaa. Amemwambia anataka Jordans genuine, $ miangapi sijui anakiona cha moto. Anamuonesha na picha zake kab isaa, picha za mama mtu. Story story saa 5 hii hapa. Raul hana hata nia ya kuondoka kabisaa, kajiwekea na mechi kwenye Dstv ya mwenzie. Baba mwenye nyumba tenaaa.

Akasikia honi piiiiiiiiiiiiiiiiiii! Akastuka kwanza. Akajipa moyo sio pale. Honi zikaendeleaaaa. Akaanza kupata mashaka sasa. Simu jikoni ikawa inaita, roho ikawa inamwenda mbio, kuangalia Pastor Bryan calling! Akaiweka silent. Ikapiga tena akapokelea huko huko jikoni, Hi! Kwa bashasha la kufumaniwa, akajibu Hi! Nimechelewa kumaliza huduma so i thought better late than never! Maana ungenila nyama wewe mwanamke, njoo unifungulie geti, akaitikia tu hayaaa. Huku akili inamwenda race kabisaaaa. Anawaza anamtoaje Raul pale, geti lenyewe moja hilo hilo na si mpaka Raul akubali kutoka. Akakata shauri akamfata sebuleni Raul!

Akampigia magoti mawili na kuunga mikono ishara ya kumuomba mtu msaada mkubwa, akanza sound "Raul for the sake of old times nakuomba niko chini ya miguu yako binadamu mwenzio nakuomba ujifiche chooni kwenye hiko chumba usitoke wala usiongeee, hata kujamba mpaka nije kukutoa, nakuomba baby pleaseeee! Nipo chini ya miguu yako sema chochote nitafanya mradi tu huyu mtu anaekuja humu ndani asijue upo wala ulikuwepo." Raul akacheka kwa dharau kubwa sanaaaa. Afu akasunyaaaa kwanza. Violla bado kapiga magoti hapo.

Raul akamwambia haiwezekaniiiii, unachoniomba sio kitu cha kiume hata kidogo. It is impossible, my ego as a man or any other man hawezi kukubali kuingia chooni, ili demu anaempendaaa aingize mwanaume mwingine, mpigane miti humu humu mimi nimetulia tu chooni, haiwezekaniii. Siingii chooni wala sijifichi, ningeweza kukufanyia ushenzi nikaingia afu nikatoka mda ambao hujapanga ukaaibika zaidi, maadam umenipigia magoti binadamu mwenzio na Violla nakujua ulivo jeuri wewe kupiga magoti hivo itakuwa unampenda sanaa huyu mwanaume, mimi nakupa fair chance ujiokoe kwenye makucha yangu kama utaweza na mbingu zitakuchekea au muujiza kushuka, sababu nakaa hapa hapa, sitingishikia, na akija humu naweka karata zote mezaniiii. Sitokusingizia mambo machafu ila nitafanya kila niwezalo to fight for what i want with this guy that is you. It will get nasty in here dear. Kafungue geti tu picha lianze.

Violla akamsujudia Raul, sema chcohcote unachotaka ila usifanye hivo please! Raul akamjibu nachotaka ni wewe tu, sina kingine and i am not a coward kukupa kwa kustrike a deal au a silly bargain, im fighting for you fair and square with the guy. Honi zikawa zimezidiiii. Akakata shauri akafungue. Badala ya kufungua Violla akatokea kigeti kidogo na kuingia kwenye gari ya Pastor mzima mzima, lets go for a late night snack! Ile kutaka kumbabatiza pastor wageuzie nje kwa nje. Pastor kachomoa, nataka kula ulichopika huko, sijala siku nzima. Akaanza kujitetea, i didnt tell you im noa very good cook you know, chakula chote kimeungua ujue. Pastor akamwambia i cook very delicious meals napika mimi. Violla akajitetea cha kupika hamna maybe tukanunue, pastor kagomaa anyway sisikii njaa wala nini? Twende niombe nilale hapa hapa nimechoka kweli! Violla akawaza tumeeeeee, tobaaaaaaaaaaa! Akawa kanasa pale, pastor kaingia kigeti kidogo kiko wazi, akafungua geti kubwa mwenyewe akapaki ndani, wakashuka mguu kwa mguu. Violla mzitoooo, ila tafanyaje akawa anaomba Mungu tu dua zoteee Raul awe amekata shauri la kuingia chooni mwenyewe.

Pastor yupo pananukia sanaaa, kitakuwa kitamu kweli. Kuingia sebuleni tu Raul kajilaza kwenye sofa na pens tupu, shati kalivua liko chini ya kochi, nywele kavurga vuruga, eti anamkaribisha karibu mgeni, anajinyoosha kichovu mida mibaya hii, ila mgeni hafukuzwi karibu. Violla anachemka kwa gadhabu, akimuangalia Violla Raul anaminyia jicho la kibandiduu. Bryani akampa mkono Pastor Bryan! Raul yupo, ooooohhhhh! Bryan the pastor she cant stop to talk about your spiritual healing! My honor to meet you, Im Raul her BF. Anasmile. Violla akadakia XBF. Raul akadakia it is complicated.

Pastor akamwambia nimekuja kuombea nyumba, not agood time but im here we can get it done with. Raul akainama uvunguni direct kuchukua shati yake akavaa, na kusema you can proceed pastor. Pastor akaomba pale kuwabariki wakazi wa humo, akamaliza wakaitikia Amen. Violla kakaa kwenye kochi kachokaaaa mwili na roho anawaza atakavo mla nyama Raul kuliko Nazi walivomla mdogo wake Hanibbal. Pastor akajisemesha i havent eaten all day any left overs, Raul akawahi dining, akafungua hot pot, chakula kimo akajibu, no left overs pastors, we are so sorry. Violla kwanini umepika kidogo, mtumishi anaenda na njaa yake tutalaaniwa, ngoja nikuoa nitakupeleka ukafundwe. Pastor akacheka na Raul akachekaaa. Violla akawa anawaza tu amuue kwa njia gani Raul si kwa kumuharibia kule leo, her life dream imeharibiwa kizembeee. Pastor akaanza kuangalia mpira, Raul akamwambia it is a bit late pastor, i dont want to sound rude but you look tired, you should go and have a rest. Pastor akasema definately. Violla akdakia ngoja nikutoe nje. Raul akamuwahi pastor mimi namtoa nje wewe toa vyombo ujiandae na tulivoongea basi tu to add insult to injury.

Pastor akatoka zake, nje ya geti akamwambia Raul, ile ishu na baba yako muimalize, itakuletea shida sanaa ishaanza kujirudia kwako na mwanao. Usipochukua hatua itakugharimu sanaa. Ubarikiwe. Akaingia kwenye gari, Raul akaingia ndani akahakikisha kawasha gari kaiondoa akarudi ndani. Violla kaa pale pale alipomuacha. Raul kapani kwanini unamwambia basha wako mambo yangu na mwanangu? Mmekosa cha kuongea? Violla akamsuta yeye hayo mambo yake na mwanae yasioyofaa kutangazwa kayajuajeee? Raul nae akawa anamuuliza Violla sasa pastor kajuaje? Violla akamwambia kaoneshwa kwenye ulimwengu wa roho, Raul akapoa kwanza kwa mda kuaytafakari.
Baadae aka bullshit.

Violla akwambia naomba utoke njeeeeee, na usikanyage hapa kwangu. Raul anajitetea wapi. Ikawa mzozo mkubwa, makelele, Raul analalamika nae kaumizwa, for once alijua amependwa, wamepatana kaandaliwa msosi, kumbe msosi kaandaliwa mtu mwengine ambae alivochelewa akaitwa yeye, he felt betrayed! Na kama mwanaume kimemuuma sanaa, he felt used! Ndo maana akaenda out of propotion kuwakomoa wote, na pamoja nayote anampena Violla and he wants her back in his life. Violla akwa hana pakuanzia kumlaani Raul ila akamwambia tu tokaaaaaaa. Raul anadai sijaja na gari saa 7 hii, nikikabwa, nalala hapa hapa. Ukawa ugomvi wa kama dakika 15, Violla akwambia baki nakumwagia maji ya moto, akayabandika. Raul akaondoka analalamika lakini yeye ndo victim pale, Violla anamsindikiza na mitusi, Lose my number, usilete tena pumbu zako humu, matusi makubwa makubwa. Raul yupo najua kimekuuma sababu unanipenda sanaa mimi, Violla yupo nampenda pastor sasa kwa taarifa yao. Makelele, akamtimulia mbali Akaloki geti karudi ndani.

Akasikia ngooo ngooo, akajua tu Raul atajifanya kakosa uasfiri, akaamua kama kuliwa na sima alie ila mlango hafungui. Yule mtu akendelea kugonga mlango hapo nje akaona kero akaenda kumtukana kwa ndani mtu yuko je. Tukana sanaaa. Akashangaa mbona hajibu, maana akili za Raul angerudishia, akajimbia atakuwa mjumbe watu wameenda kushtaki kelele zimezidi. Akikusanya kafungua mlango, kajiandaa na utetezi mzitoooo. Kumbe Pastor! Afu safari hii hana gari. Akawa mdogooo kapigwa butwaa si kwa mitusi ile aliotukana. Akili ikawa inamzunguka kasikia kuanzia wapi, kwa Raul au wapi? Akawa kabungaaa, Pastor Akaingia akaloki geti akabana na kufuli kabisaaa.

Akampiga denda kwanza kaitika kubungaaa kwake afu akambeba kuelekea ndani sasa. Bado kapigwa butwaaa.

ITAENDELEA KESHO SAA 5 ASUBUHI.
 
Back
Top Bottom