Jambo la kushangaza ni kuwa pamoja na ukweli kuwa Ikulu hawana hata website kwa kipindi chote hiki ila ni kuwa gharama za Internet zilizoombwa ni kiasi cha shilingi 38,400,000.
Hizi fedha zipo kwenye kifungu 2002 mawasiliano serikalini, kwenye kasma namba 260104 ya kitabu cha bajeti ofisi ya rais ikulu,
wameandika hivi ,nanukuu..Kasma hii hutumika kulipia gharama za mawasiliano ya mtandao kwa njia ya internet .katika mwaka wa fedha 2008-2009 zinaombwa shilingi 38,400,000.
Maswali ya kujiuliza ni kuwa kama kutuma tuu internet wanahitaji kiasi chote hicho kwa mwaka ni gharama halisi ama ni mchezo wa Salva et all?
Kwa ujumla gharama za mawasiliano ,habari na utoaji huduma zimeobwa kiasi cha shilingi 60,475,000. na hizi ni kwa ajili ya vitu kama gharama za simu 2,400,000,gharama za posta 500,000, Internet 38,400,000,uchapishaji 4,200,000, huduma za utangazaji 12,675,000 na tepu,rekodi na diski 800,000.
Hya angalieni wenyewe jinsi internet inavyokula pesa zetu je wakiweka na website si ndio tutakwisha kabisa?