Wazungu wanamtaka mwanangu!!

CHAI CHUNGU

JF-Expert Member
Feb 20, 2012
7,113
930
Wakuu nina mtoto wa kiume ambaye ndiye first born wangu mwenye miaka9,huyo dogo nilikuwa nikiishi nae hapa dar,lakini nilikua nikipata kesi nyingi za ugomvi every day,mwaka jana nikakata shauri nikampeleka kwa bibi yake yaani mamangu mzazi kijijini kwetu Musoma.

Wiki iliyopita nilipigiwa simu na mamangu kwamba dogo kampiga dogo mwenzie mwenye miaka 12 mpaka kamng'oa meno kwa hiyo kuna kesi na inatakiwa elfu70 ya matibabu,nikatuma hiyo pesa.

Leo asubuhi nimepigiwa simu tena kwamba jana kulikuwa na mashindano ya box (ngumi) kuanzia watoto wa miaka 10-15,bcoz my soon ni mdogo aliamua kudanganya umri kwamba ana11 na ana uwezo wa kupigana then akaruhusiwa kupigana.

Mdogo wangu ndiye aliyetoa ruksa hiyo kwa lengo la kumkomesha dogo ili adundwe aache ugomvi mtaani,cha ajabu dogo alipafom mpaka jukwaa zima wakawa wanamshangilia,alipigana pambano1 na alishinda kwa round ya kwanza tena kwa kumpiga ngumi 6 tuu adui yake,na akapata zawadi ya tsh150,000 cash.

Sasa kuna jamaa wa Holland wana academy ya box Kenya wamempenda dogo wanataka wamchukue waende nae Kenya na baadae Holland wamesema nikiwakabidhi wao watamuhudumia kila kitu mpaka atakapofikisha umri wa kujitegemea na akifikisha miaka 12 wataanza kumlipa some amounts.

Nimewambia waje Dar tuonane na watakuja ijumaa this week.

Nipo tayari kumwachia but mamake hataki kusikia habari hiyo ya ngumi,pls ushauri.
 
huyo mtoto hasomi?
huna mpango na huyo mtoto?
Inakuwaje unawataka waachia watu kirahisi au si mwanao?
Ingekuwa vizuri kama we nae ungekuwa unaishi huko holland ili iwe rahisi kutrack kinachoendelea
 
Ingieni mkataba nao,unaweza kuwa unamtembelea kila baada ya miezi mitatu au aje yeye tz,,gharama zao,,mkataba uthibitishwe nakusimamiwa na serikali kupitia wizara ya wamama watoto na jinsia,,elimu mpaka chuo,na mambo mengine,
 
huyo mtoto hasomi?
huna mpango na huyo mtoto?
Inakuwaje unawataka waachia watu kirahisi au si mwanao?
Ingekuwa vizuri kama we nae ungekuwa unaishi huko holland ili iwe rahisi kutrack kinachoendelea
Ni mwanangu wa kumzaa na anasoma std3.
 
Mtani umezaa Tyson? kama ana kipaji bembeleza mama yake dogo aanze kuingiza hela badala ya kupiga watu mtaani na wewe kuingia gharama za kutibu watu.

Kama ni shule atasoma huko huko, make sure unafuata taratibu za kisheria au kama hujui tafuta wakili akuelekeze taratibu zote na akuwakilishe wakati hao Waholand wanamchukua kama mtakubaliana masharti.
 
Ingieni mkataba nao,unaweza kuwa unamtembelea kila baada ya miezi mitatu au aje yeye tz,,gharama zao,,mkataba uthibitishwe nakusimamiwa na serikali kupitia wizara ya wamama watoto na jinsia,,elimu mpaka chuo,na mambo mengine,
Offcourse that's why nimewaomba tuonane ingawa inaonyesha wako very interesting na hata sasa wako nyumbani kwa mother wakijaribu kupata history ndogo na wanarecord baadhi ya picha na mazingira ya nyumbani kwetu kijijini.
But dogo hawajamkuta maana alikua na ratiba ya kwenda kuchunga leo but nimewambia wamfuate.
 
Mtani umezaa Tyson? kama ana kipaji bembeleza mama yake dogo aanze kuingiza hela badala ya kupiga watu mtaani na wewe kuingia gharama za kutibu watu.

Kama ni shule atasoma huko huko, make sure unafuata taratibu za kisheria au kama hujui tafuta wakili akuelekeze taratibu zote na akuwakilishe wakati hao Waholand wanamchukua kama mtakubaliana masharti.
Mtani nilikua nina 100% kwamba my soon atakua mtu wa football maana hiyo mi surprise ya jezi na njumu niliyokua namnunulia usipime,badala yake upepo umegeuka,kwa kweli mtani huyu dogo ni mbavu kishenzi,maana ata mamake alishashindwa kudhibiti kwa stick that's why nikampeleka bush.Maana nilihisi labda picha za kichina zimemuharibu.
 
akichemsha tu wanamtelekeza,sasa amua moja lakini vizuri mtoto akae na mama au baba yake kwa makuzi mazuri
 
Bado mdogo sana huyo kumkabidhi kwa watu usiowafahamu. Wazungu si watu wa kuamini wanaweza kabisa wakawa wanamgeuza mwanamke. Kama una mtu huko Holland (Mtanzania) unayemwamini kumfuatilia mwanao kwa karibu sana hakuna tatizo vinginevyo OGOPA!!!
 
Ahsante kwa ushauri!
 
Mkuu,

Waombe DATA zao kwanza na nenda ubalozi wa Netherland na UWAHAKIKI kama kweli ni Shirikisho la kweli la michezo.

Kama ni mzuri na anaweza kupokea kipigo na kurusha kipigo, basi pia jaribu kumtafuta mtu anaitwa REMY BONJASKY ambaye ana shule yake nzuri sana ya hii michezo ya watu wenye Maguvu yao.
Akishakuwa huko, hata kama atachemsha, bado anaweza kuwa kashafahamiana na WAKALI duniani. Remy kwa sasa anamfundisha kijana wa ki-Congo na jamaa anazipiga si kawaida.

Remy ni wale Weusi wanaoishi Uholanzi na wana asili ya koloni lao liitwalo SURINAM.

Jamaa anafahamika sana duniani kwani alishakuwa hadi bingwa wa dunia wa K-1, mchezo ambao ni Brutal sana.

WEBSITE yake ni: http://www.remybonjasky.com/

Kuhusu umri, nachelea kusema umeshaanza kuchelewa kwani kwa wenzetu, alitakiwa kuwa kashaanza mazoezi siku nyingi sana. Maisha ni PATA POTEA, hujui Dogo ndiyo inaweza kuwa kipaji chake hicho.

Kesho anaweza kuja kuwa hata kocha kama akina Mlundwa au Promotor.
 
header03.jpg

Wanamwita "The Flying Gentleman".

Kwenye Video akiwa na Danyo Ilunga (Congo) kwenye shule yake: Bonjasky Academy : Danyo Ilunga in world championship training with Remy Bonjasky + Interviews - YouTube
 
Mtani umezaa Tyson? kama ana kipaji bembeleza mama yake dogo aanze kuingiza hela badala ya kupiga watu mtaani na wewe kuingia gharama za kutibu watu.

Kama ni shule atasoma huko huko, make sure unafuata taratibu za kisheria au kama hujui tafuta wakili akuelekeze taratibu zote na akuwakilishe wakati hao Waholand wanamchukua kama mtakubaliana masharti.

ha ha ha ha
 
Mhhhhhhh!Mkuu Dunia imekuwa ya ajabu sana,unaweza kuwaamini watu baadae ukaja kujuta.Kwa kifupi wazungu siyo watu wa kuamini kabisa.Ila uamuzi ni wako
 
Mtani umezaa Tyson? kama ana kipaji bembeleza mama yake dogo aanze kuingiza hela badala ya kupiga watu mtaani na wewe kuingia gharama za kutibu watu.

Kama ni shule atasoma huko huko, make sure unafuata taratibu za kisheria au kama hujui tafuta wakili akuelekeze taratibu zote na akuwakilishe wakati hao Waholand wanamchukua kama mtakubaliana masharti.
Kweli kabisa coz mayweather floyd jr alikuwa na historia kama hii.
 
Hawa watu weupe sio wa kukurupuka kuwaamini,hata kitendo cha wao kuwaruhusu warekodi mambo ya kwenu na historia ya mtoto ni dili tosha kwao,mi nakushauri kwanza wafuatilie sana kwa undani bila wao kujua maana wakijua hawakawii kujipanga sawasawa!usitoe mtoto kirahisi,maana mtoto si nguo,ukaomba mtu!ukiamua wamchukue ushauri wa bure ni kwamba wajamaa hawa wajanja sana,unaweza jikuta kwenye mkataba umeingia kichwakichwa ukakosa mwana hivihivi,na usikubali kuingia mkataba kwa mwanasheria wao,awe ni mwanasheria uliyemchagua wewe,na shirikisha serikali yako ktk kila hatua ya makubaliano
 
Wewe mwenyewe ulimshindwa ukaamua kumpeleka kwa bibi yake lakini wamekuja waholland wamegundua kipaji chake unaweza kumzuia lakini usimtimizie kile anachohitaji matokeo yake akageuka kibaka au jambazi lakini kule mbali ya kumpatia mafunzo kutakuwa na wataalamu wa saikolojia ambao watamrekebisha tabia ili wakati anaendeleza kipaji chake vilevile aweze kuishi vizuri na jamii cha muhimu kama mzazi hakikisha hao wetu ni kweli wanahusika na shuguri hizo na pia tatakuwa katika mikono sala,a
 
Kuna kaka tunafahamiana, mwanae wa kujifunzia alichukuliwa kwa staili hii. Kumbe akawa anatumika kusafirisha madawa ya kulevya. Alikuja kufia China, in a hotel baada ya vidonge kupasukia tumboni. Mamake hakuweza hata ku-claim mwili kwa hofu.

Kuwa extra careful aisee!
 
Back
Top Bottom