Hii ndio orodha ya wasanii, maproducer, watangazaji wababe kwenye Bongo Flava, kichapo nje nje!!

NetMaster

JF-Expert Member
Sep 12, 2022
1,454
4,853
Tutawazungumzia kwa kigezo cha kipindi wakiwa kwenye ubora wao, Hata Tyson huwezi kumjudge ubora wake kwa sasa maana umri umeshaenda, hayupo active kama zamani.

1. DUDU BAYA
1692095224426.png

chuma kilichokuwa kinasumbua kikiogopwa na kuogopeka kwa wasanii na KWA MAPROMOTAR NA MA D. J MARADIO PRISENTER NI OIL CHAFU THE MAMBA ngumi zilikuwa njenje, wasanii waliomsema vibaya OIL CHAFU walipata tabu sana vibaya mno, Kuna msanii aliewahi kuwa maarufu sana enzi hizo na pesa nyingi alikuwa anatembea na mabodigadi lakini oil chafu ilimchafua vibaya mno, tena ni mara mbili.
promoter umzurumu, zitapigwa ngumi pia msanii alieongoza kuwa na kesi na RB vituo vyote vya polisi unavyo vijua ni OILCHAFU nakumbuka mapromotar matapeli walichafuka kwa oil chafu SIYO KITOTO kwa sababu ya ulaliaji na kuwanyonya kazi na haki za wasanii ndo aliwaonyesha njia kwa harakati zake kwamba wasanii wana pigwa za uso, mie waga na muita kidume RIGENDER

hii ilipelekea hadi radio presenters kwa amri ya mtemi aliependa kunyenyekewa (rip) wakaamua kumpoteza mazima pamoja yeye na wasanii wengine kama kina Sugu, Lady-Jaydee na wengine waliodai haki ya wasanii, hadi sasa wasanii wana lipwa vizuri kupitia harakati za hii miamba.

Na hata ukicheki Diamond nae aliwahi kuwa na ukaribu na MAMBA, Ni kwamba Diamond nae aliwahi kukutana na haya mambo ya unyonyaji na ukandamizaji, ilikuwa apotezwe mazima na mtemi kwenye ulimwengu wa music akapambana nao sana mpaka akashinda vita ndomana automatically ikawa wana ukaribu flani na OIL CHAFU.

2. LORD EYES
1692206863318.png

Lody ni hatari sana hata Pina mwenyewe naamini alikuwa anamgwaya kiasi coz amepiga bujuruu, karet na Kick boxing, ana mkanda mweusi, huyu mbabe wa kaskazini siyo mtu wa kawaida kiivo

Kuhusu lile varangati lililotokea pale Slipway Nako2Nako vs Kikosi cha Mizinga, Kikosi Cha Mizinga walikodisha dojo ndio wakaenda slip way kuwafuata Nako2nako, baada ya Lord eyes kuondoka tu wakawavamia, kilichofanyika ni uhuni, endelea kusoma nitaelezea zaidi tukio hili sehemu ya Pina.

Lody kuna kipindi aliwahi kupigwa Beto huko huko A town, wakiwa pamoja na Bou na mwenzao (siwezi kumtaja) kuna ule ubabe wa Arusha wahuni walikuwa wanatamani kutesti mitambo kwa huyo mwenzao ambae alikuwa na muonekano wa ki ganster basi wakawa wanataka kumtesti, Palichimbika hapo lilikuwa ni varangati, Lody akakalisha kadhaa ila moja wao akamchoma kisu cha tairi.. ilikuwa mbaya hiyo alikaa ICU zaidi ya wiki Moja.

3. KALA PINA
1692099196309.png

Naweza kusema Pina alikuwa muhuni zaidi kuliko msanii, Tena ni ule uhuni wa kiselam**i na uhuni wa kimagenge, lile genge lake ndio lilimpaisha aonekane mbabe pamoja na uchanaji wake wa kigumu gumu sambamba na freestyle zenye matusi ambazo hazikupigwa redioni zilimkuza zaidi.

Huyu Pina alikuwa na uhuni ambao kiukweli ulikuwa ni toxic kwake na hata kwenye game, alishawahi kumteka Solo Thang, walikuwa ni ndugu, Solo alikuwa ni mtoto wa shangaz yake, huu sio ubabe wa kumpa mtu title bali ni uselam**i, aliwahi kwenda kwa P-Funk pamoja na wenzake wakiwa na mapanga wapewe biti ambalo hajalipia wakafanyie show, pamoja na ubabe wake Majani hakuwa tayari kupigana na kundi la watu wenye mapanga kisa Biti, ikabidi awape tu na hata baadae Pina alivotoka kwenye show alipeleka hela ila majani akaikataa. inaonyesha wazi kabisa Pina uwezo wake binafsi wa kuwa mbabe bila backup ulitia shaka.

Sasa tukija noma lililotokea Pale Slipway, ile siku Nako2Nako wakiwa kama watatu Bou, Ibra Da Hustler na A Nako, muda huo Gnako alikuwa Arusha, kilichotokea ni kwamba Pina alikuja na watu wake kama 10 hivi kuwavamia N2N, na hapo Pina hakupigana kwa ngumi alikuwa kaja na nondo kama sio rungu, msanii flani wa N2N alipigwa na hilo rungu kichwani likampata mdomoni, huu ni uhuni wa kiselam**i, ni sawa na mcheza mpira kukodishia panya road waende nae kumvunja miguu mchezaji wa timu mwengine, kama ni battle ilibidi walipange sehemu neutral kila mtu awe na wake 1 on 1, zichapwe kavu bila silaha.

Kiufupi huyu bwana uwezo wake binafsi ulikuwa wa kawaida ila alikuwa na uhuni wa kimagenge, na hata ile siku kamshushia kichapo Chidi stejini ni kwamba Chidi alikuwa kashazama kwenye matumizi, anyway kwa sasa Pina wa sasa siyo yule kipindi kile, kwasasasa ni mwanaharakati wa kusaidia vijana walioathirika na madawa ya kulevya.

4. PFUNK MAJANI
1692102742443.png

Kwa waliowahi kubahatika kumuona mwamba huyu miaka hio kwenye peak yake alikuwa ni mbavu vibaya mno, Tizi alikuwa anapiga hadi sio poa. Enzi hizo maproducer wakali walikuwa wachache hawazidi watatu, wasanii wengi walipenda ubora wa kazi zake lakini huyu Mwamba alikuwa ni mbabe, hata wagosi wa kaya walipotaka kuhama label kwenda kwa Majani walikiri kwenye Interview kwamba MJ aliwaambia mapema Majani ni mbabe wategemee mazingira tofauti ya kazi, wasanii waliofika bongo records wakiwa wachanaji walilazimishwa kuimba chorus, Wengine walijichanganya walichezeshewa, kuna moja alikuwa anaambiwa asivute bangi hapo bongo records yeye anakaidi amri, kilichotokea alitoka kama mshale getini.

5 CHIDI BENZ
1692102796034.png

Mtoto wa ilalaaaa, Mwamba alikuwa kasimama imara enzi za peak yake, Body kama lote, Watu walishachezeshewa hapa ila mziki wake ulivuma zaidi na kuzifunika hizo habari. tatizo alipoanza kutumia ilimuathiri sana hata mwili. ,

6. ADAM MCHOMVU
Photo by Adam Mchomvu on July 24, 2023. May be an image of 1 person, eyewear and turban..jpg

si wa kumchukulia poa kisa eti mpo laivu kwenye kipindi ama tamasha, anything can happen, Kina Q, Mbasha, Fety ni mifano michache washapigwa mabanzi na mabuti laivu bila chenga. #anotherone kutoka Atown.#wasanii #wasafitv #bongoflava #AzamTV #hiphop #punchchallenge
 
Mbona Kalapina aliwadunda hao Nako2nako...na hawakujibu Hadi wanasarambatika....Dudu Baya zaidi ya Mr Nice alishawahi mdunda nani?
Kalapina hapo kawadunda wote ...


Anyway thread za watoto hizi kushabikia ugomvi..ndo maana Castro akampiga kisu Steve 2K na mambo ya kupigana kwenye bongo Flava yakawa history....
 
Mbona Kalapina aliwadunda hao Nako2nako...na hawakujibu Hadi wanasarambatika....Dudu Baya zaidi ya Mr Nice alishawahi mdunda nani?
Kalapina hapo kawadunda wote ...


Anyway thread za watoto hizi kushabikia ugomvi..ndo maana Castro akampiga kisu Steve 2K na mambo ya kupigana kwenye bongo Flava yakawa history....
Lile varangati la pale Slipway, Nako 2 Nako walikuwa wachache, Pina akaja na wenzake wengi hapakuwa na uwiano, Halafu mda huo Lord eyes hakuwepo. Pina yeye kama yeye alikuwa wa kawaida sana ila anapenda ubabe kwa kutumia backup ya kikosi.

Tunakumbushana tu history
 
Sasa unamuweka Adam Mchomvu choko moja hilo. Linaonea wanyonge mbona hajitusui akamzingua mtu kama Ney wa Mitego. Alimpiga Mbasha mtama sababu ni mnyonge, Q Chief teja.

Adam Mchomvu ni boya moja lisilokuwa na staha wala heshima. Lilishawahi post picha mikamasi ikimchuruzika, lilishawahi kujamba on air. Kwa kifupi Adam ni mnyonge sana mbele ya wanaume. Linahitaji kupakatwa, kwa wale waliosoma Ntinda View Kampala wanalijua kuwa lilikuwa jinga moja tu.

1692193510628.png
 
Sasa unamuweka Adam Mchomvu choko moja hilo. Linaonea wanyone mbona hajitusui akamzingua mtu kama Ney wa Mitego. Alimpiga Mbasha mtama sababu ni mnyonge, Q Chief teja.

Adam Mchomvu ni boya moja lisilokuwa na staha wala heshima. Lilishawahi post picha mikamasi ikimchuruzika, lilishawahi kujamba on air. Kwa kifupi Adam ni mnyonge sana mbele ya wanaume. Linahitaji kupakatwa, kwa wale waliosema Ntinda View Kampala wanalijua kuwa lilikuwa jinga moja tu.

View attachment 2719029
Eti naye mbabe haha

Ova
 
Back
Top Bottom