Capital
JF-Expert Member
- Oct 12, 2010
- 1,452
- 1,038
Wakuu GT.. nawasalimia sana.
Niende moja kwa moja kwenye mada.
1. Utangulizi
Hapana shaka kuwa kiwango cha maendeleo ya nchi au bara hutegemea ubora wa raslimali watu katika nchi/bara husika. Ubora huu wa raslimali watu ndo hutofautisha nchi na nchi, bara na bara katika maendeleo ya kiuchumi, kwa maana kwamba chi zenye maendeleo makubwa ni bayana wana raslimali watu wa ubora wa hali ya juu.
Raslimali bora bila shaka ni zao la elimu. Hivi karibuni kumekuwepo na mapitio ya sera ya elimu kwa mtazamo kwamba changamoto tulizonazo kiini chake ni sera za elimu zisizokidhi. Hili liko sahihi. Leo nitajikita katika kuonesha tunapokosea, ili kama itawapendeza watunga sera na wadau wa elimu, waweze kuazima vitu kadha wakadha, huenda ikasaidia.
2. Elimu ya "blackbox"
Black box au tafsiri isiyo rasmi boksi jeusi ni aina ya elimu ambayo ni ya kijuu juu sana, ni elimu ambayo inamfundisha muhitimu mambo madogo madogo kabisa ambayo hayana manufaa kwa nchi. Muhitimu hufundishwa mambo tu ya kutumia kitu au teknolojia na si elimu ya kutengeneza hiyo technolojia au kifaa.
Blackbox education ni kwamba wahitimu wamepitishwa tu juu juu (skimming) na hawakupelekwa ndani haswa (deep to the core) katika mfumo mzima wa mafunzo husika. Binafsi hiyo blackbox education naiona kama sifuri kabisa inayopoteza muda wa wahitimu na ndio mtego mkubwa katika maendeleo ya nchi yetu na bara letu. Muhitimu wa blackbox education, kimsingi hana msaada kwa nchi yake, kwa continent yake na kwa dunia.
Hii ndiyo aina ya elimu tunayotoa katika mashule yetu, vyuo vyetu hapa nchini na mahali karibu pote katika bara la Africa. Ndiyo sababu, hakuna teknolojia, vifaa, falsafa iliyozalishwa ambayo chanzo chake ni Tanzania/Africa. Washindi wa Nobel wa Africa ni wale wa kimchongo, wapiga midomo, kwa elimu ya aina hii, hatakuja kupatikana Laureate wa Chemistry, Physiology, Physics, Engineering, nk.
3. Tatizo ni nini?
Kwa mtazamo wangu, nadhani vyanzo vya tatizo ni vingi mno vikiwemo ukoloni, nafasi ya Tanzania au Africa katika uchumi wa dunia.. kwamba Afrika katika mizania ya nguvu, imejikuta ikiwa upande wa omba omba zaidi kuliko mtoaji. Tatizo lingine ni watu wenyewe wakiwemo viongozi ambao nao ni wahanga wa blackbox education.
Kwa hiyo nachelea kusema kuwa mara zote mtu atatenda kadri anavyofahamu. Kwamba hao wataalam hawawezi kufikiria nje ya wanachokijuwa, nje ya black box. Kuna swala la uvivu wetu sisi kama raia katika swala zima la elimu. Ni sahihi kwamba elimu deep ni ngumu, inayohitaji utulivu, uhamasishaji na uvumilivu mkubwa. Lazima jukumu hili tulibebe kama tunataka mabadiliko.
4. Kumulika ndani ya boksi jeusi
Hebu tuone namna ya kupindua meza, tuondokane na aina hii ya elimu ya hovyo hovyo. Tunahitaji kufanya kazi kweli kweli. Tunahitaji kuwafundisha watanzania na Wafrica mambo makubwa, ya ndani (deep) kabisa katika sayansi hasa zile sayansi msingi.
Nitatoa mfano: mtu anasoma Chemistry, lakini unakuta anachokijuwa katika chemistry ni upuuzi tupu, anajuwa tu vitu vya juu juu. Mtu kama huyu hawezi kuwa na uwezo wa kutengeneza dawa, hata dawa rahisi kama panadol. Unakuta mitaala ya vyuo vikuu ni black box tupu, yaani mhitimu hana ufahamu wa ndani katika eneo alilohitimu.
Mhitimu anayefanya fani ya electronics, hajui hata chip inatengenezwaje, anajuwa labda inatumika kufanya nini, hii ndo blackbox education sasa. Nisiseme mengi katika hili, ila niseme tu kuwa kwa elimu kama hii, ni ndoto kwamba tutaweza hata siku moja kuja kutengeneza machine au kifaa au falsafa yetu kama watanzania/waafrika.
Kwa hiyo tutaendelea kulipa kwa gharama kubwa ili kukidhi mahitaji yetu kiteknolojia kutoka kwa nchi zinazofundisha 'whitebox education'.
5. Tunatokaje kwenye tope hili?
Nakiri kuwa safari ya kujikwamua katika kadhia hii siyo ya kitoto. Hivi visera vya elimu vinavyopendekezwa, kwangu naona ni visera uchwara ambavyo havina dhima wala dira ya kuitoa Tanzania kutoka kwenye blackbox education ambayo kimsingi haina manufaa yoyote.
Ndo maana utakuta nchi inanunua huduma za wahandisi kutoka nje katika miradi yake, jambo ambalo ni hasara kubwa sana kwa sababu unaishia ku "export" pesa ambayo umeipata kwa shida sana kwa kuuza korosho, ufuta na vitu vya aina hiyo au kuwatoza kodi wamachinga.
Mchakato wa kuondokana na kadhia hii , kwa mtazamo wangu lazima uanze na kubadili fikra za viongozi wa Tanzania na Africa kwa ujumla.
i. Uwekezaji katika elimu. Mikakati ya sasa hivi ya uwekezaji katika elimu ni ya ajabu, ya hovyo ambayo haina dira ya kutuondoa kwenye tope la blackbox education. Haiwezekani ukasimamisha kuta nne na kuezeka bati la sufuria ukaita hicho ni darasa halafu usiishie na blackbox education.
Darasa ama liwe la shule ya msingi sekondari au chuo cha kati au kikuu, lazima liwe na viwango au ngazi fulani ya kiwango itakayokubalika miongoni mwa wadau wa elimu. Mfano, minimally, darasa ili liwe darasa lazima liwe na vitu kadhaa kama vile meza na kiti kwa kila mwanafunzi, idadi ya wanafunzi ijulikane kama 30-35.. nk.
ii. Mafunzo na qualifications za waalimu
Tanzania kama zilivyo nchi za Afrika, walimu hasa wa ngazi za chini ni kundi ambalo halina mafunzo na qualifications stahiki kukidhi mahitaji ya kuwa walimu. Katika mwelekeo huo, serikali huwa inawalipa ujira kidogo kwa sababu kutokana na qualifications duni, wahusika hawana upenyo wa kudai hata stahili zao.
Hili lazima likome, ili watu wote watakaopewa jukumu la kufundisha taifa, wawe watu wenye viwango vya juu kitaaluma, na vivyo hivyo, ujira wao uwe ni wa juu kabisa kuliko au kulingana na kada zilizoko juu.
Kwani kumlipa mwalimu wa msingi mwenye sifa stahiki sh millioni 3, au wa secondari 3.5M au wa chuo cha kati 4M au wa chuo kikuu 8M utapungukiwa na nini? Unashindwa kumlipa mwalimu ujira wa staha kwa kisingizio huna hela halafu kila mwaka unalalamika wezi wameiba 15trilion.. huu ni ujinga first class.
iii. Figisu za mabeberu
Mabeberu wanafahamu fika kuwa Tz na Afrika ikikoma kuwapa watu wake blackbox education nao watakuwa wameisha, kwisha habari yao. Kuondokana kwetu na blackbox education ndo utakuwa mwanzo wa kutengeneza machine zetu, magari yetu, nguo zetu, nk.
Tutajuwa kutumia raslimali zetu za asili, mfano, gas yetu, upepo wetu, jua letu, ardhi yetu kwa manufaa yetu. Hakika mabeberu watakuja kutuomba kama sisi tunavyoenda kuwaomba omba.
Sasa hawa lazima kuwa macho nao sana.. nafikiri ziko mbinu, ila kwa vile wanaotakiwa kutekeleza mbinu hizi, kwa bahati mbaya, nao ni wahanga wa blackbox education, huenda ikawa changamoto.
6. Hitimisho
Kwa ambao mtakuwa mmenielewa, nawakaribisha sana mtoe michango. Kukaa kila mwaka tunasingizia sera na kuzibadilisha, wakati mzizi wa tatizo hauguswi, ni kupoteza muda na pesa na kujidanganya. Blackbox education haitaifanya Tz itoboe, katika eneo lolote kitaaluma, kiteknolojia, na kifikra.
Asanteni sana na karibuni tuelimishane.