newmzalendo
JF-Expert Member
- Mar 23, 2009
- 1,378
- 550
true true,Kwa miaka ambayo nimekuwepo hapa JF kama mwanachama, nimeelimika vilivyo, nimeburudika kiasi cha kutosha, nimefarijika na kufaidika na mengi kwa ujumla. Moyo wangu daima unajihisi kukosa fadhira kama sishirikishi au kurejesha hata sememu ya faida hizi kwa wengine au jamii.
Ni usemi wa siku nyingi kuwa "Ndege wenye mabawa yanayofanana.........." na hivyo basi wakati wote mimi huamini kuwa kujificha nyuma ya kompyuta na kuemdeleza matumizi ya majina bandia katika kuchangia mada makini humu ndani kunatakiwa kuwa na kikomo. Nikiazima kaulimbiu ya Invisible "Ficha Upumbavu, Usifiche Hekima" nadhani huu utaratibu wa kujificha inabidi tuuvunje kwa wanachama wenye mawazo sawa, mtazamo unaofanana na kuwajibika kunakoshabihiana kukutana wazi tukiwa na dhamira moja tu; Kuhalisia Fikra Zetu. Nimesoma mahali kuwa baadhi yetu wamewahi/hukutana.
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/39210-project-funding-sources-5.html#post927666 Ni jambo jema na si vibaya wengi zaidi tukajulishwa ni jinsi gani ya kuungana nao.
Najua JF kuna majukwaa mengi. Na watu wanavivutio, hisia, mitazamo na malengo tofauti kulingana na majukwaa wanayopendelea. Binafsi, mie mtoa wito ni mpenzi wa Jukwaa la Biashara na Uchumi. Na wito wangu nautoa kwa Wadau wa Jukwaa la Biashara na Uchumi kukutana na kutengeneza Mpango stahimilivu utakaowezesha kuhalisia mawazo na mitazamo yetu.
Kuna hazina kubwa juu ya Mustakabali wa Biashara na Uchumi imehifadhiwa hapa JF. Rasilimali-Watu na taarifa zilizomo humu ndani juu ya Kilimo, Ufugaji na Biashara kwa ujumla ni LULU huwezi pata bure kokote ufikiliapo. Nimejaribu kujikumbusha nyuzi na michango LULU kama:
https://www.jamiiforums.com/busines...kwa-wanaopenda-ufugaji-mkubwa.html#post908785
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/52203-sirudi-nyuma-3.html#post896885
https://www.jamiiforums.com/busines...biashara-ya-mboga-mboga-ulaya.html#post934969
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/50511-bwawa-la-samaki-2.html#post936693
https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/60458-kilimo-cha-milonge.html#post936948
https://www.jamiiforums.com/busines...62-kilimo-cha-mitiki-utaalamu.html#post937049
https://www.jamiiforums.com/jukwaa-...i-tanzania-ni-nchi-maskini-19.html#post888920
https://www.jamiiforums.com/busines...ieni-5mil-kuanzia-biashara-10.html#post877391
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/35182-mbuzi-wa-maziwa.html#post565339
https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/33587-nauza-rozera.html#post518819
https://www.jamiiforums.com/busines...isha-biashara-itakayofanikiwa.html#post509060
Shime: Natuone thamani iliyomo katika maandishi haya. Tujithanini kwa kutoa hii michango yenye thamani namna hii. Natujiweke tofauti na Walivyozoeleleka Watanzania: Wajuvi wa kueleza matatizo na kutoa masuluhisho kwa maneno bila vitendo. Na kisha tujipange kukutana kuuunganisha haya mawazo na kujenga umoja/chombo kitakachotoa nafasi kwetu sisi kuyafikia malengo. Chombo hicho yaweza kuwa Kampuni
Naomba kuwakilisha
Entare Yehirungu
Kasindaga.
E-mail: kageratea@gmail.com
Mob: 0762-444-266
tatizo mawazo na nia huwa nzuri,pia watanzania huwa hatuna utamaduni wa kubishana,tunakubaliana vizuri ktk vikao hvi,then hatutekelezi lolote,
nashauri wale wenye vitendo wakutane kwanza na sisi wa blablah ktk komputer na forums tukabaki humu humu.
Mr,Malila, nimepata shamba mkuranga hekari 30,nimeanza kusafisha,ntalima papai na rosela kwanza