Wazo: Kampuni ya Wakulima na Wafugaji-JamiiForums | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Wazo: Kampuni ya Wakulima na Wafugaji-JamiiForums

Discussion in 'Kilimo, Ufugaji na Uvuvi' started by Ericus Kimasha, Jun 2, 2010.

 1. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #1
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Kwa miaka ambayo nimekuwepo hapa JF kama mwanachama, nimeelimika vilivyo, nimeburudika kiasi cha kutosha, nimefarijika na kufaidika na mengi kwa ujumla. Moyo wangu daima unajihisi kukosa fadhira kama sishirikishi au kurejesha hata sememu ya faida hizi kwa wengine au jamii.

  Ni usemi wa siku nyingi kuwa "Ndege wenye mabawa yanayofanana.........." na hivyo basi wakati wote mimi huamini kuwa kujificha nyuma ya kompyuta na kuemdeleza matumizi ya majina bandia katika kuchangia mada makini humu ndani kunatakiwa kuwa na kikomo. Nikiazima kaulimbiu ya Invisible "Ficha Upumbavu, Usifiche Hekima" nadhani huu utaratibu wa kujificha inabidi tuuvunje kwa wanachama wenye mawazo sawa, mtazamo unaofanana na kuwajibika kunakoshabihiana kukutana wazi tukiwa na dhamira moja tu; Kuhalisia Fikra Zetu. Nimesoma mahali kuwa baadhi yetu wamewahi/hukutana.
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/39210-project-funding-sources-5.html#post927666 Ni jambo jema na si vibaya wengi zaidi tukajulishwa ni jinsi gani ya kuungana nao.


  Najua JF kuna majukwaa mengi. Na watu wanavivutio, hisia, mitazamo na malengo tofauti kulingana na majukwaa wanayopendelea. Binafsi, mie mtoa wito ni mpenzi wa Jukwaa la Biashara na Uchumi. Na wito wangu nautoa kwa Wadau wa Jukwaa la Biashara na Uchumi kukutana na kutengeneza Mpango stahimilivu utakaowezesha kuhalisia mawazo na mitazamo yetu.

  Kuna hazina kubwa juu ya Mustakabali wa Biashara na Uchumi imehifadhiwa hapa JF. Rasilimali-Watu na taarifa zilizomo humu ndani juu ya Kilimo, Ufugaji na Biashara kwa ujumla ni LULU huwezi pata bure kokote ufikiliapo. Nimejaribu kujikumbusha nyuzi na michango LULU kama:

  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/37026-kwa-wanaopenda-ufugaji-mkubwa.html#post908785
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/52203-sirudi-nyuma-3.html#post896885
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/62887-biashara-ya-mboga-mboga-ulaya.html#post934969
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/50511-bwawa-la-samaki-2.html#post936693
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/60458-kilimo-cha-milonge.html#post936948
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/60262-kilimo-cha-mitiki-utaalamu.html#post937049
  https://www.jamiiforums.com/jukwaa-la-siasa/38756-kwa-nini-tanzania-ni-nchi-maskini-19.html#post888920
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/49326-nisaidieni-5mil-kuanzia-biashara-10.html#post877391
  https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/35182-mbuzi-wa-maziwa.html#post565339
  https://www.jamiiforums.com/matangazo-madogomadogo/33587-nauza-rozera.html#post518819
  https://www.jamiiforums.com/business-and-economic-forum/32130-namna-ya-kuanzisha-biashara-itakayofanikiwa.html#post509060

  Shime: Natuone thamani iliyomo katika maandishi haya. Tujithanini kwa kutoa hii michango yenye thamani namna hii. Natujiweke tofauti na Walivyozoeleleka Watanzania: Wajuvi wa kueleza matatizo na kutoa masuluhisho kwa maneno bila vitendo. Na kisha tujipange kukutana kuuunganisha haya mawazo na kujenga umoja/chombo kitakachotoa nafasi kwetu sisi kuyafikia malengo. Chombo hicho yaweza kuwa Kampuni

  Naomba kuwakilisha

  Entare Yehirungu
  Kasindaga.

  E-mail: kageratea@gmail.com
  Mob: 0762-444-266
   
 2. M

  Malila JF-Expert Member

  #2
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mkuu wewe kiboko,nimefunua hizo thread zote hapo juu,nimekumbuka mengi sana. Tatizo letu ni malezi ya paper work tuliyozoea. Ni kweli mimi na baadhi ya jf members tulikutana Lunch time Hotel 5may2010 jioni. Ni moja ya siku nzuri sana kuwahi kutokea kwangu. Wakati jukwaa la kiuchumi likiendelea pale Mlimani city na sisi tulikuwa na jukwaa kama lao pale Lunch time Hotel.

  Tulionana uso kwa uso na kukubaliana mambo fulani ambayo hapa si mahali pake kwa leo. Ila moja ya vitu muhimu ni kwamba ndege wa aina moja basi waruke pamoja. Kwa ufupi uko mle mle tulimopitia kuelekea ktk nchi hiyo ya asali na maziwa.

  Mimi naamini tunaweza kufanya maajabu bila kukopa fedha ko kote.
   
 3. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #3
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Tushirikishane kwa PM basi mkubwa Malila, niko very interested na ujasiriamali
   
 4. L

  Lady JF-Expert Member

  #4
  Jun 2, 2010
  Joined: Apr 12, 2010
  Messages: 280
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Wadau, mnipm na mimi mnapokutana, I like Ujasiriamali 100%. I 'll get at least some tips on how and where to start.
   
 5. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #5
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Heshima Saaana Mkuu Malila,

  Hakika likija suala la Kilimo, Biashara na Uchumi nakukubali kama M.M Mwanakijiji na Uchambuzi wa Siasa, Invisible na Ufundi wa Mawasiliano (ICT), FMES na Habari motomoto, ukweli na hakika au Nyani Ng'habu katika eneo lake; kutaja wachache. Binafsi najikubali kama Mjasiriamali-Muadilifu. Mwenye shauku kubwa na mafanikio yake binafsi na ya jamii inayomzunguka. Nina uzoefu wa kutosha katika sekta ya Matunda, Mboga mboga na Viungo. Pia nimetoa mchango usiofutika katika jitihada za kuijenga sekta ndogo ya ufugaji nyuki. Eneo hili yeyote mwenye kuhitaji kuielewa sekta hii au kuwekeza huku anaweza kunitafuta.

  Bila kuandika mengi, niseme tu mnikumbuke. Mnapoandaa ndege wa aina yetu kukutana, msiniache kando tafadhari. Kibali cha kuingia Lunch-Time Hotel iwe ya pale Mabibo au Manzese nitakuwanacho.
   
 6. M

  Malila JF-Expert Member

  #6
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Poa mkuu, ila jina sio Malima ni malila.
  Hujachelewa hata kidogo,Lunch time Hotel 5may ilikuwa ni siku ya kwanza kabisa,fikiria mnapanga kukutana na watu ambao hujawahi kuwaona. Anyway,maendeleo ni mazuri,tumeshaanza kuijenga crew hii mpya. Tumeunganisha vipaji vyetu ili kwa pamoja tutoke. Tunakwenda taratibu kwa sababu tunataka wanaomaanisha tu ndio turuke pamoja. Miradi tuliyochagua ni ile ambayo mtu aliyeajiriwa anaweza kuifanya bila pressure akiwa ofisini. Lakini silaha kuu iliyotuunganisha ni uaminifu miongoni mwetu,kujitolea kwa ajili ya wenzako hasa muda na rasilimali ulizo nazo. Kwa mbali tunaona mwanga unakuja. Tunataka tuwe na kijiji chetu kwanza around Dar, eneo tayari tumelipata ambalo kila mtu ananunua kwa kadri ya uwezo wake. Tukishakuwa na kijiji cha marafiki basi safari itakuwa imeanza. Tumechoka kusimulia mafanikio ya wenzetu kila wakati. Kwa hiyo kila project tunajitahidi kufanya ktk eneo moja,hili limesaidia kupunguza gharama za uendeshaji wa project zetu.
   
 7. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #7
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Hii ni hatua kubwa sana ya mafanikio toka JF. Niwapongezeni ninyi ambao mu-miongoni mwa Mabalozi wa Mafanikio ya jamvi letu pendwa JF. Hivi karibuni nimeona mijadala mingi ni JF imedoda, imefulia, na maneno mengi tu ya jinsi hiyo. Kwa mtazamo wangu mie sishangai maana ni asili yetu kuishi na dhahabu, almasi, asali, maziwa na kulalamika umaskini. Wao badala ya kutumia jamvi kwa manufaa kama ninyi mlivyofanya wao wanasubiri ma-breaking newz!.

  Mie napenda haya majukwa ya kijamii yanisaidie kukutana na watu wenye mtazamo wa kwangu; Mjasiliamali-Muadilifu au mzuri zaidi. Hivyo basi ninasubiri kwa shauku kubwa kupata kibali cha kuwa mmoja wa ndege wa kundi lenu la Kijiji cha Marafiki.
   
 8. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #8
  Jun 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Niwie radhi Mkuu. Nimerekebisha.
   
 9. M

  Malila JF-Expert Member

  #9
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Ngoja niwashirikishe wadau wenzangu,na kwa sababu wamo humu,utawaona tu muda si mrefu. Ikimpendeza mungu chai ijayo tutakunywa pamoja.
   
 10. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #10
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Idea nzuri sana hii manake ili ndio linakuwaga kikwazo. Malila bado nasubiri PM yako Mkuu
   
 11. M

  Mokoyo JF-Expert Member

  #11
  Jun 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2010
  Messages: 14,828
  Likes Received: 1,991
  Trophy Points: 280
  Hii ndiyo kitu watu wanaogopa wanaona kila mtu ni threat kwake lakini sio kweli cha muhimu ni uhaminifu na determination tu kama anavyosema Malila
   
 12. M

  Malila JF-Expert Member

  #12
  Jun 2, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mimi binafsi nimefaidika mno na jf. Wajanja wapo ila usiogope sana, Mtangulize Mungu atakuepushia. Kuwakwepa wajanja,jitahidi kufanya kwa vitendo zaidi. Kwenye vitendo wengi tuko hoi.
   
 13. kanyagio

  kanyagio JF-Expert Member

  #13
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 10, 2009
  Messages: 986
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Ntareyehirungu............ upo kaka, unaendeleaje na ujasiriamali..
   
 14. M

  Malila JF-Expert Member

  #14
  Aug 1, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Jamaa alisema tumwalike pale Lunchtime Hotel,tukafanya hivyo,jamaa hakutokea. Ngoja tusubiri atatujulisha maendeleo yake.
   
 15. N

  Ntamb Member

  #15
  Aug 1, 2010
  Joined: Feb 13, 2008
  Messages: 18
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hatua hii mliyoichukua inatia moyo sana.
  Naona wenzetu memchoka kuendelea kuwa ma-NATO.
  You have every reason to be proud of your decision.

  Endeleeni kutumegea mtakapokuwa njiani.

  Nawatakia kila la heri, na naimani mtafanikiwa.

  Thadeo.
   
 16. M

  Malila JF-Expert Member

  #16
  Aug 2, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Mkuu asante,na utuombee.
   
 17. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #17
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Samahani sana kwa kutoroka jukwaani kwa muda. Kama mnavyowezahisi, tulikuwa na shughuli pevu toka tarehe 14 baada ya NEC kuhakikisha tunaimarisha ngome ya ushindi Bukoba Vijijini. Asante MUNGU maana sasa kwa kumpitisha Rwehekiza nina hakika agenda ya maendeleo itasonga kwa mwendo tuutakao.

  Kanyagio, nimerudi tulisongeshe....
   
 18. Ericus Kimasha

  Ericus Kimasha Verified User

  #18
  Aug 2, 2010
  Joined: Oct 27, 2006
  Messages: 488
  Likes Received: 126
  Trophy Points: 60
  Malila,
  Samahani sana kwa kutopata ujumbe wenu wa mwaliko ikiwa ni kuitikia ombi langu.
  Je, mlitumia njia gani (email, PM, SMS, or...). Yaani, sijapata mawasiliano yoyote yakinitaka kuwa eneo husika! Hiyo nafasi kwangu ni dhahabu.
   
 19. M

  Malila JF-Expert Member

  #19
  Aug 2, 2010
  Joined: Dec 22, 2007
  Messages: 4,410
  Likes Received: 733
  Trophy Points: 280
  Tulitumia pm kwa wasio na e-mail,tulitumia simu. Hapana mbaya mkuu,tutakuwa na mkutanao tena huko mbele ili libeneke lisilale. Nitaku-pm mara nyingi zaidi ili tukupate.
   
 20. K

  Kasungura Member

  #20
  Aug 3, 2010
  Joined: Mar 12, 2007
  Messages: 72
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Aksante sana tena sana ndugu Kasindaga, kwa post yako.
  wazo lako nilithamini sana pamoja ma mawazo mengine mengi tu yaliyotolewa hapa JF na wanachama.
  nitakutafuta utupe mwanga zaidi. thx sana wana Jf wote wenye michango ya kimaendeleo.
   
Loading...