Werewolves, binadamu wanaoweza kujibadilisha na kuwa mbwa mwitu

Da Vinci XV

JF-Expert Member
Dec 7, 2019
3,837
6,372
SEHEMU YA I
(Vitu vyote visivyo vya kawaida vina maelezo yake ya kisayansi, maana kufanya hivyo huondoa fumbo lilipo juu yake.)
NB: Makala haya yanaweza kwenda tofauti na unakiamini au Unachokifahamu si mbaya kuongeza kitu KILA KUNDI KATIKA JAMII TOFAUTUTOFAUTU, LINAAMINI KWA NAMNA YAKE, wako wanaoamini hii ni myth tu za walatini kama ilivyo myth za medusa na Gorgons, Wapo wanaomini ni Aina ya uchawi tu unaofanya na watu kujigeuza hivi na wako wanaomini ni Supernatural power na ni real kabisa kama walivyo binadamu wengine wenye uwezo tofauti.

Utachagua upande wa kusimama.

Shuqraan

Wasalaam,

DA52123A-0E8A-4ADC-9DF0-E101504315F3.jpeg

Kila mtu ana zamani yake , kila mtu ana kale yake inayomfanya akumbuke mambo kadha wa kadha
Na si mwajua pia kila mtu ana Asili yake.

Na Kila mtu ana uoga /phobia juu ya jambo lake .

Nakumbuka wakati ule miaka ile, ningali bado kinda ambaye misuli ya mwili wangu bado haikuwa na weledi wa kupambana na Adha na Maudhi ya ulimwengu.

Ni wakati huu huu ambao hata akili yangu haikuwa ikiwaza na kung'amua vyenye kuang'atika.

Lakini kwa mapenzi yake Mwenyezi Akaniongezea Ari katika ufahamu si kwa vile nipendavyo mimi bali kwa mapenzi yake yeye MwenyeziMungu.

Na ndio wakatii huu huu nikaanza kuunganisha zile doti , nikivuta taswira ya zile Siries ambazo niliwahi kuzitazama kabla.

Ushawahi kuona au kusikia na kusoma watu waliokuwa na Super Powers ambao sio kawaida kwa jina lingine mnawaita Superhumans ,,Najua pengine wewe umeishia kuona katika movie na kuhifadhi kama ni uwezo wa waandaji kuzikonga furaha za kuta za moyo wako kila utazamapo, Binafsi mwenyewe sina majawabu.

042BF59E-708A-4870-AC68-42E26AA1ABC5.jpeg

Siries kama TEEN WOLF, GU. TALE OF FOX CHILD, NINE na nyingine nyingi ambazo zilimwonyesha mwanadamu katika uhusika wa namna Mbili.

Mwanadamu anaebadilika na kuwa Mbwa , Mbwa wa mwituni.

Wakati nilipotazama siries kama hizi, Akili yangu bado iliendelea kuamini ni zile fiction kama za Marvel kumgeuza Perter parker kuwa buibui mwenye kutoa utando na kubembea katika ghorofa bna minara ya kule New york.

Usingenilaumu na ubongo wangu huu wa kiafrika ungewaza nini tena alimradi ushazoea kushindishwa ugali na dagaa kila iitwapo leo.

WEREWOLVES ni nini!?

2B6F1562-8CBF-4ED9-B5EC-B3A969C1E328.jpeg

Werewolf, mtu-mbwa mwitu au tuseme mbwa mwitu-mtu.
Kiumbe (mtu) huyu ana uwezo wa kudevelop na kuwa na umbile na tabia kama za mbwa mwitu (shape-shifter).

Kwa Wenzetu walatini , neno linalotumiwa kuwatambulisha hawa viumbe werewolves ni Lycaon, linalomaanisha “mnyama wa aina ya mbwa-mwitu.”

werewolf ni binadamu mwenye uwezo wa kujigeuza na kuwa kiumbe anayefanana na mbwa mwitu.
Haijulikani ni namna gani mabadiliko hayo yanafanyika, lakini kulingana na hadithi, zinaelezea kuwa hii mara nyingi huwa ni laana zaidi kuliko tabia ya kawaida.

Lakini pia watu wanaong'atwa na werewolves huwa Wanadevelop na kuwa kama wao , na athari hii yaweza kuwa ya kudumu au ya mda mfupi katika mwili wa mwathiriwa.

Wengine wanaamini kwamba shape shifters hawa wanaweza kuwa wamekumbwa na nafsi ya watu ambao huacha miili katika hali ya kiroho na kwenda kwenye uwindaji hivyo hutumia figure ya Mbwa mwitu
Kiumbe huyu maelezo yake huonekana kutofautiana katika kila utamaduni.

kwa kawaida kiumbe huyu ana mambo ya tofauti na pia anayo yanayofanana na mbwamwitu wa kawaida
Wakati kiumbe huyu anabadilika kutoka kwa mnyama hadi umbo la mwanadamu, kwa kawaida huwa dhaifu,huishiwa nguvu, na kudhoofika, na kupata mfadhaiko mkubwa wa neva.

Katika hadithi za zamani zinaeleza kwamba viumbe hawa werewolves walikuwa ni wanawake wazee na wachawi ambao waliokuwa wana uwezo wa kujibadilisha.

Mbinu ya kuwatambua werewolf kutoka kwa wanadamu wengine pia inatofautiana sana katika tamaduni mbalimbali.

Wengi walitumia njia ya ya kukata mwili wa mtu anayeshukiwa kuwa anaweza kuwa ni mbwa mwitu ili kusaidia kumtambua.

Hiyo ni kwa sababu manyoya yangeanza kujitokeza kwenye jeraha.

WEREWOLVES KATIKA HISTORIA

3F7AD1C5-52DD-4BC3-AD7D-486C6C409A4B.jpeg

Leo ukikatiza taratibu na kujongea maeneo ya Iringa basi , Historia inayoibeba eneo hili ni Shughuli nzito aliyoifanya Mzee Mkwawa miaka kadhaa iliyopita na hii historia inabeba utambulisho wa wahehe wa Iringa
Au ukikatiza kule kilimanjaro waliko ndugu zetu wachaga ukiwauliza utambulisho uliobeba historia ya Eneo lile ni uwepo wa mlima mrefu barani Afrika Mlima kilimanjaro

Basi vivyo hivyo Werewolves wamekuwepo kwa siku tele.

Baadhi wamekubali kwamba werewolves ni viumbe halisi, lakini ni baadhi ya watu bado hawaifikiani na hilo.
Kitu cha kwanza kilichowahi kuwatambulisha viumbe wa mtindo huu kabla ya werewolves tunaowazungumzia ni Watu wanaofanana na mbwa mwitu lakini si werewolves , hawa ni watu wenye hali inayojulikana kama Hypertrichosis inayojulikana pia kama werewolf syndrome.

Ambapo watu hawa huwa na nywele nyingi kwenye miili yao.

Mtu wa kwanza aliekuwa na ugonjwa huu inaelezwa . alikuwa na mwonekano kama wa mbwa mwitu na nywele nyingi kwenye mwili wake, kwa hiyo na kimwonekano alionekana kama mbwa mwitu.

07BC2408-7ABD-440A-9664-676B5BD09614.jpeg

Werewolf syndrome

TABIA ZAO NA SAIKOLOJIA
Werewolves wanajulikana kwa kuwa na fujo nyingi sana, hilo lipo hata baadhi yao wakiwa katika umbo la kibinadamu. Walakini mara nyingi viumbe hawa wamekuwa na tabia zenye kufanana.

Ushawahi kuishi au kukutana na mtu mwenye hasira kali kuliko kawaida akafikia hatua ya kupasua vitu kama simu au hata kujichanana mwili wake ., basi viumbe hawa moja ya tabia zao ni hasira kali isiyomithilika
Binadamu wa aina hiyo mara nyingi alikuwa na shida kudhibiti hasira zake akiwa katika umbile lake la ubinadamu wa kawaida , hii humkuta sana kiumbe huyu anapokuwa bado mchanga yaani hajakomaa (werewolf ambae anabalehe)

Pia wanaweza kuonyesha sifa fulani za ajabu, ambazo zinaweza kuchochewa na uchokozi ambao anaweza kuwa wamefanyiwa na kiumbe kingine chochote, lakini pia huwa na nguvu isiyo ya kawaida ya kimwili .
lakini huwa hawawezi kubadilika kikamilifu.

Pia, werewolves huwa wana joto la juu la mwili kuliko wanadamu wa kawaida nadhani hili hata kwenye movie kadhaa tulizobahatika kutazama zinaonyesha hii sifa yao kwa uthabiti kabisa.

Pia macho yao huwa yanageuka na kuwa ya manjano huku wakiwa na hasira kali sana.

Vichochezi vinavyopelekea Viumbe hawa kubadilika

Wengi katika werewolves wana vichochezi vyao ambavyo huwafanya wao kubadilika.

Kwa mfano, ikiwa werewolf yuko katika umbo la mwanadamu na vichochezi hivyo vikapanda basi mara moja atabadilika.

Vichochezi hivyo ni kama hasira kupita kiasi, kuumia na kupata majeraha(physically na pyschologycal), kuongezaka kwa adrenaline nyingi mwilini , au kujilinda kutokana na kitu au mtu.

UHUSIANO WAO NA FULL MOON

637E5EF6-2DCD-4C72-97F1-90B2840E3D35.jpeg

Hili movie karibu zote limeonyesha waziwazi achilia tu movie hizo pia kuna documentary karibu zote zilizoweka wazi jui ya hili.

Kwamba Wakati wa mwezi kamili (Full moon) baada ya jua kutua, basi viumbe hawa watabadilika na kuwa umbo la mbwa, wakifanana sana na mbwa mwitu. Ingawa viumbe hawa wao huwa wakubwa zaidi ya mbwa mwitu wa kawaida.

Wanaweza pia kutofautishwa na mbwa mwitu wa kawaida kwa tabia yao ya nguvu isiyo ya kawaida na kasi ya ajabu.

Japo kifacts hakuna sababu yoyote isipokuwa ni myth tu vinginevyo facts zilisema mabadiliko mengine tu ya kawaida kama hasira au kujihami hupelekea wao kubadilika na kuwa katika form ya mtindo huo

NAMNA WATU WANAVYOAMBUKIZWA NA KUBADILIKA KUWA WEREWOLF.

229DD6CD-A22B-402F-A32B-8FDB29888FA4.jpeg

Hapo awali, Inaelezwa viumbe hawa wote walikuwa wanadamu ambao waliambukizwa walipong'atwa au kuchanwa na kiumbe wa aina ile aliyebadilishwa au kubadilika.

Inaweza kuwa kwa kung'atwa kwa meno au kuchanwa na kucha hapa wao wanafanana na Vampires katika njia yao ya kuambukizana.

Kwa Werewolves ni kawaida zaidi kuliko viumbe wengine wa ajabu, kwa kuwa wanadamu wanaweza kuambukizwa kwa njia zaidi ya kuumwa au kukwaruzwa ,hasa hasa muambukizaji akiwa amebadilika katika kipindi cha mwezi kamili.

Kikawaida Werewolves wakiwa katika fomu yao ya mbwa mwitu huwa hashambulii, isipokuwa pale tu anapoisi kushambuliwa au wale werewolves wachanga ambao hawawezi kudhibiti mabadiliko yao bado.

Kiumbe huyu atamwachia kovu au alama ya kuuma maisha yake yote baada ya kumwambukiza mwathirika. Hii hufanya werewolves kuwa rahisi kutambuana wakiwa katika hali yao ya kibinadamu.

Inafikiriwa kuwa wanadamu wana hatari zaidi ya kukumbwa na lycanthropy wakati wa miaka yao ujana.
Hii ndiyo sababu 50% ya werewolves wako kati ya umri wa 11 na 17.

Pia inaseemwa ni kwa sababu baadhi ya mabadiliko ya ghafla ya homoni yanayotokea wakati wa kubalehe hufanya kijana awe katika hatari zaidi ya lycanthropy.

Lakini wako pia ambao huzaliwa wakiwa katika mfumo wa viumbe hawa baada ya ku inherit genes kutoka kwa wazazi ambao tayari walishabadilika kuwa mbwamwitu. Hawa huitwa pure blood werewolves

PURE BLOOD WEREWOLVES

35F52B52-38D2-4743-A5AF-E6CFB362A7F5.jpeg

Watoto ambao wamezaliwa na wazazi wote ambao ni wolves basi hawa huitwa pure bloods , damu safi ya mbwa mwitu. Hata katika makabila yao basi hii ni nguzo moja wapo ya viumbe hawa pure blood na mara nyingi hawa ndiyo huwa viongozi wa makundi yao.

Naam hapa nimekukumbusha kuhusu Royal Blood line ambayo inaishirikiana zile bloodline nyingine kuongoza dunia basi siri iliyo ndani ya damu zao hata huku kwa viumbe hawa ipo na ndiyo maana mara nyingi hutukuzwa na hutawala makundi yao.

AINA ZA WEREWOLVES NA UWEZO WAO

ALPHA

DF136DB4-9EE1-4FC2-9891-E85944629B37.jpeg

Alphas hawa ndio huwa viongozi wa makundi yote ya viumbe hawa na ndio huwa viumbe hatari zaidi kuliko jamii nyingine yoyote ile hatari zaidi.

Wao ni huwa ni wakubwa, wenye kasi ajabu na nguvu zaidi ya jamii yoyote ile ya viumbe hawa, Alpha huwazidi hata purebloods kwa uwezo wao.

Hawa wao wanaweza pia kudhibiti uwezo wao na mihemko yao vizuri sana.

Hawa hata wakiwa Katika umbile la mbwa mwitu bado wao huruma huendelea kuwepo

Alphas wana macho mekundu tofauti na makundi mengine ambao wao huwa ya njano au rangi ya dhahabu.

Makundi mengine kama wale Purebreeds au kundi la Betas au hata Omegas zinaweza kuwa alfas kwa njia mbili Mosi, Ama kwa kumshinda na kumuua alfa mwingine , kwa hivyo kuiba au kuchukua mamlaka za alpha na uwezo wake pia kwa waliotazama teen wolf nadhani hii watarejesha kumbukumbu zao hapa.

Au Njia ya pili kwa kuwa na power karama ya ukuaji na nguvu ya tabia zao, wema, au kupendwa na makundii na jamii yake.hapa kama ilivyo karama ya uongozi katika jamii zetu mpaka mtu anafanikiwa kuwa raisi au Mfalme basi kutokana na mwenendo na karama yake basi hata katika makundi ya viumbe haya haya hii ipo
Hawa huitwa Alphas wa uKweli na ni nadra sana Alphas wa mtindo huu kutokea.

Lakini Alphas anaweza kugeuka kuwa mbwa mwitu halisi kabisa pasi na kuwepo maumbile ya ubinadamu kwake, lakini kwa mwonekano yeye huwa mkubwa zaidi.

Alpha mara nyingi huweza ha kuzungumza hata akiwa katika umbo la mbwa mwitu na kuchanua makucha hata akiwa katika umbo la ubinadmu.

Ndiyo viongozi wa jamii zote

BETA

5DD7977A-7369-4B79-9AD0-194C456A7B35.jpeg

Beta hawa ni aina ya kawaida ya werewolf. Na hawa ndiyo wapo wengi sana katika idadi , hawa wana nguvu kuliko kundi lingine linalowafatia ambao ni Omegas.

Wana uwezo wote kama tulivotaja huko juu kuwahusu viumbe hawa Betas wana macho ya rangi ya chungwa na mara nyingi wao huwa kama askari wa makundi yao.

Betas werewolves kawaida hutumia miguu yao miwili lakini wanaweza kusimama kwa miguu yote minne na wanaweza kutembea hivyo.

Betas wana makucha na meno yenye nguvu sana na makali.

DELTA

EE32F748-4B9E-4945-9E5E-B19101E4F978.jpeg

Delta hawa ni mbwa mwitu wadogo kwa kulinganisha na hao waliotangulia hapo juu na wao pia huwa walinzi katika makundi yao hawa wana miguu minne kama mbwa mwitu wa kawaida lakini wao huwa wakali zaidi kuliko mbwa mwitu wa kawaida
Mbwa mwitu wa kundi la Delta wana macho ya manjano, wa urefu kiasi na kasi zaidi.

GAMMA
Gammas ni aina kundi la hini kabisa na hufanywa kuwa wawindaji katika makundi yao,

Mbwa-mwitu wa Gamma huonekana kama mbwa mwitu wa kawaida lakini ni wakubwa kidogo. Uwezo huu unatumiwa na wakuu wao katika kuwafanya maskauti na majasusi wa makundi yao.

Mbwa mwitu wa Gamma wana macho ya kijivu na wana makucha marefu kuliko werewolves wengine.

OMEGA
Omega ni werewolves wasio na cheo chochote katika makundi ya viumbe hawa

Omega hukua na kuwa na nguvu sana.

Wana macho ya bluu na umbile kubwa

Kwa ujumla wao husimama kwa miguu miwili lakini wanapokimbia hutumia miguu yao yote minne.
Hawa hutumika kama chambo katika mapambano

VARGULF
8214CC84-E526-434D-82DA-84748AECC3F0.jpeg

Vargulfs ni mbwa mwitu wasio na utulivu wa mwili na wala kiakili, kwa maneno mengine ni mbwa mwitu ambao vicheche au vichaa.

Huwa na macho meusi na hawana roho yoyote hata ya mfano wa ubinadamu.

Hawa wakiwa wamebadilika katika umbili lao la mbwa mwitu kilicho mbele yao ni Sunna Bila kusema wao ni kupeleka maafa , hawa ni wanyama wakali sana wenye kiu ya kuu mda wowote wanapobugudhiwa

ITAENDELEA

Na DaVinci XV

SEHEMU YA II

-UTHIBITISHO WA KISAYANSI.
-MABADILIKO YAO.
-JE UNATAKA KUWA WEREWOLF.
-NGUVU NA UWEZO.
 
Stories za kusukumia muda uende unahadithia ukiamini ni kweli.... Ukiwa unaamini kila kitu mtandaoni huchanganyi na za kwako....utaishia kuonekana kituko.
 
Wengine hubadilika mpaka nyoka ni suala la kuwa na macho ya kuona tu.
 
Stories za kusukumia muda uende unahadithia ukiamini ni kweli.... Ukiwa unaamini kila kitu mtandaoni huchanganyi na za kwako....utaishia kuonekana kituko.
Sijui hata nikupe msaada gani...maana NB nliiweka mwanzoni kabisa mwa nyuzi .
 
SEHEMU YA I
(Vitu vyote visivyo vya kawaida vina maelezo yake ya kisayansi, maana kufanya hivyo huondoa fumbo lilipo juu yake.)
NB: Makala haya yanaweza kwenda tofauti na unakiamini au Unachokifahamu si mbaya kuongeza kitu KILA KUNDI KATIKA JAMII TOFAUTUTOFAUTU, LINAAMINI KWA NAMNA YAKE, wako wanaoamini hii ni myth tu za walatini kama ilivyo myth za medusa na Gorgons, Wapo wanaomini ni Aina ya uchawi tu unaofanya na watu kujigeuza hivi na wako wanaomini ni Supernatural power na ni real kabisa kama walivyo binadamu wengine wenye uwezo tofauti.

Utachagua upande wa kusimama.

Shuqraan

Wasalaam,

View attachment 2309134

Kila mtu ana zamani yake , kila mtu ana kale yake inayomfanya akumbuke mambo kadha wa kadha
Na si mwajua pia kila mtu ana Asili yake.

Na Kila mtu ana uoga /phobia juu ya jambo lake .

Nakumbuka wakati ule miaka ile, ningali bado kinda ambaye misuli ya mwili wangu bado haikuwa na weledi wa kupambana na Adha na Maudhi ya ulimwengu.

Ni wakati huu huu ambao hata akili yangu haikuwa ikiwaza na kung'amua vyenye kuang'atika.

Lakini kwa mapenzi yake Mwenyezi Akaniongezea Ari katika ufahamu si kwa vile nipendavyo mimi bali kwa mapenzi yake yeye MwenyeziMungu.

Na ndio wakatii huu huu nikaanza kuunganisha zile doti , nikivuta taswira ya zile Siries ambazo niliwahi kuzitazama kabla.

Ushawahi kuona au kusikia na kusoma watu waliokuwa na Super Powers ambao sio kawaida kwa jina lingine mnawaita Superhumans ,,Najua pengine wewe umeishia kuona katika movie na kuhifadhi kama ni uwezo wa waandaji kuzikonga furaha za kuta za moyo wako kila utazamapo, Binafsi mwenyewe sina majawabu.

View attachment 2309162

Siries kama TEEN WOLF, GU. TALE OF FOX CHILD, NINE na nyingine nyingi ambazo zilimwonyesha mwanadamu katika uhusika wa namna Mbili.

Mwanadamu anaebadilika na kuwa Mbwa , Mbwa wa mwituni.

Wakati nilipotazama siries kama hizi, Akili yangu bado iliendelea kuamini ni zile fiction kama za Marvel kumgeuza Perter parker kuwa buibui mwenye kutoa utando na kubembea katika ghorofa bna minara ya kule New york.

Usingenilaumu na ubongo wangu huu wa kiafrika ungewaza nini tena alimradi ushazoea kushindishwa ugali na dagaa kila iitwapo leo.

WEREWOLVES ni nini!?

View attachment 2309139

Werewolf, mtu-mbwa mwitu au tuseme mbwa mwitu-mtu.
Kiumbe (mtu) huyu ana uwezo wa kudevelop na kuwa na umbile na tabia kama za mbwa mwitu (shape-shifter).

Kwa Wenzetu walatini , neno linalotumiwa kuwatambulisha hawa viumbe werewolves ni Lycaon, linalomaanisha “mnyama wa aina ya mbwa-mwitu.”

werewolf ni binadamu mwenye uwezo wa kujigeuza na kuwa kiumbe anayefanana na mbwa mwitu.
Haijulikani ni namna gani mabadiliko hayo yanafanyika, lakini kulingana na hadithi, zinaelezea kuwa hii mara nyingi huwa ni laana zaidi kuliko tabia ya kawaida.

Lakini pia watu wanaong'atwa na werewolves huwa Wanadevelop na kuwa kama wao , na athari hii yaweza kuwa ya kudumu au ya mda mfupi katika mwili wa mwathiriwa.

Wengine wanaamini kwamba shape shifters hawa wanaweza kuwa wamekumbwa na nafsi ya watu ambao huacha miili katika hali ya kiroho na kwenda kwenye uwindaji hivyo hutumia figure ya Mbwa mwitu
Kiumbe huyu maelezo yake huonekana kutofautiana katika kila utamaduni.

kwa kawaida kiumbe huyu ana mambo ya tofauti na pia anayo yanayofanana na mbwamwitu wa kawaida
Wakati kiumbe huyu anabadilika kutoka kwa mnyama hadi umbo la mwanadamu, kwa kawaida huwa dhaifu,huishiwa nguvu, na kudhoofika, na kupata mfadhaiko mkubwa wa neva.

Katika hadithi za zamani zinaeleza kwamba viumbe hawa werewolves walikuwa ni wanawake wazee na wachawi ambao waliokuwa wana uwezo wa kujibadilisha.

Mbinu ya kuwatambua werewolf kutoka kwa wanadamu wengine pia inatofautiana sana katika tamaduni mbalimbali.

Wengi walitumia njia ya ya kukata mwili wa mtu anayeshukiwa kuwa anaweza kuwa ni mbwa mwitu ili kusaidia kumtambua.

Hiyo ni kwa sababu manyoya yangeanza kujitokeza kwenye jeraha.

WEREWOLVES KATIKA HISTORIA

View attachment 2309140

Leo ukikatiza taratibu na kujongea maeneo ya Iringa basi , Historia inayoibeba eneo hili ni Shughuli nzito aliyoifanya Mzee Mkwawa miaka kadhaa iliyopita na hii historia inabeba utambulisho wa wahehe wa Iringa
Au ukikatiza kule kilimanjaro waliko ndugu zetu wachaga ukiwauliza utambulisho uliobeba historia ya Eneo lile ni uwepo wa mlima mrefu barani Afrika Mlima kilimanjaro

Basi vivyo hivyo Werewolves wamekuwepo kwa siku tele.

Baadhi wamekubali kwamba werewolves ni viumbe halisi, lakini ni baadhi ya watu bado hawaifikiani na hilo.
Kitu cha kwanza kilichowahi kuwatambulisha viumbe wa mtindo huu kabla ya werewolves tunaowazungumzia ni Watu wanaofanana na mbwa mwitu lakini si werewolves , hawa ni watu wenye hali inayojulikana kama Hypertrichosis inayojulikana pia kama werewolf syndrome.

Ambapo watu hawa huwa na nywele nyingi kwenye miili yao.

Mtu wa kwanza aliekuwa na ugonjwa huu inaelezwa . alikuwa na mwonekano kama wa mbwa mwitu na nywele nyingi kwenye mwili wake, kwa hiyo na kimwonekano alionekana kama mbwa mwitu.

View attachment 2309143

Werewolf syndrome

TABIA ZAO NA SAIKOLOJIA
Werewolves wanajulikana kwa kuwa na fujo nyingi sana, hilo lipo hata baadhi yao wakiwa katika umbo la kibinadamu. Walakini mara nyingi viumbe hawa wamekuwa na tabia zenye kufanana.

Ushawahi kuishi au kukutana na mtu mwenye hasira kali kuliko kawaida akafikia hatua ya kupasua vitu kama simu au hata kujichanana mwili wake ., basi viumbe hawa moja ya tabia zao ni hasira kali isiyomithilika
Binadamu wa aina hiyo mara nyingi alikuwa na shida kudhibiti hasira zake akiwa katika umbile lake la ubinadamu wa kawaida , hii humkuta sana kiumbe huyu anapokuwa bado mchanga yaani hajakomaa (werewolf ambae anabalehe)

Pia wanaweza kuonyesha sifa fulani za ajabu, ambazo zinaweza kuchochewa na uchokozi ambao anaweza kuwa wamefanyiwa na kiumbe kingine chochote, lakini pia huwa na nguvu isiyo ya kawaida ya kimwili .
lakini huwa hawawezi kubadilika kikamilifu.

Pia, werewolves huwa wana joto la juu la mwili kuliko wanadamu wa kawaida nadhani hili hata kwenye movie kadhaa tulizobahatika kutazama zinaonyesha hii sifa yao kwa uthabiti kabisa.

Pia macho yao huwa yanageuka na kuwa ya manjano huku wakiwa na hasira kali sana.

Vichochezi vinavyopelekea Viumbe hawa kubadilika

Wengi katika werewolves wana vichochezi vyao ambavyo huwafanya wao kubadilika.

Kwa mfano, ikiwa werewolf yuko katika umbo la mwanadamu na vichochezi hivyo vikapanda basi mara moja atabadilika.

Vichochezi hivyo ni kama hasira kupita kiasi, kuumia na kupata majeraha(physically na pyschologycal), kuongezaka kwa adrenaline nyingi mwilini , au kujilinda kutokana na kitu au mtu.

UHUSIANO WAO NA FULL MOON

View attachment 2309146

Hili movie karibu zote limeonyesha waziwazi achilia tu movie hizo pia kuna documentary karibu zote zilizoweka wazi jui ya hili.

Kwamba Wakati wa mwezi kamili (Full moon) baada ya jua kutua, basi viumbe hawa watabadilika na kuwa umbo la mbwa, wakifanana sana na mbwa mwitu. Ingawa viumbe hawa wao huwa wakubwa zaidi ya mbwa mwitu wa kawaida.

Wanaweza pia kutofautishwa na mbwa mwitu wa kawaida kwa tabia yao ya nguvu isiyo ya kawaida na kasi ya ajabu.

Japo kifacts hakuna sababu yoyote isipokuwa ni myth tu vinginevyo facts zilisema mabadiliko mengine tu ya kawaida kama hasira au kujihami hupelekea wao kubadilika na kuwa katika form ya mtindo huo

NAMNA WATU WANAVYOAMBUKIZWA NA KUBADILIKA KUWA WEREWOLF.

View attachment 2309157

Hapo awali, Inaelezwa viumbe hawa wote walikuwa wanadamu ambao waliambukizwa walipong'atwa au kuchanwa na kiumbe wa aina ile aliyebadilishwa au kubadilika.

Inaweza kuwa kwa kung'atwa kwa meno au kuchanwa na kucha hapa wao wanafanana na Vampires katika njia yao ya kuambukizana.

Kwa Werewolves ni kawaida zaidi kuliko viumbe wengine wa ajabu, kwa kuwa wanadamu wanaweza kuambukizwa kwa njia zaidi ya kuumwa au kukwaruzwa ,hasa hasa muambukizaji akiwa amebadilika katika kipindi cha mwezi kamili.

Kikawaida Werewolves wakiwa katika fomu yao ya mbwa mwitu huwa hashambulii, isipokuwa pale tu anapoisi kushambuliwa au wale werewolves wachanga ambao hawawezi kudhibiti mabadiliko yao bado.

Kiumbe huyu atamwachia kovu au alama ya kuuma maisha yake yote baada ya kumwambukiza mwathirika. Hii hufanya werewolves kuwa rahisi kutambuana wakiwa katika hali yao ya kibinadamu.

Inafikiriwa kuwa wanadamu wana hatari zaidi ya kukumbwa na lycanthropy wakati wa miaka yao ujana.
Hii ndiyo sababu 50% ya werewolves wako kati ya umri wa 11 na 17.

Pia inaseemwa ni kwa sababu baadhi ya mabadiliko ya ghafla ya homoni yanayotokea wakati wa kubalehe hufanya kijana awe katika hatari zaidi ya lycanthropy.

Lakini wako pia ambao huzaliwa wakiwa katika mfumo wa viumbe hawa baada ya ku inherit genes kutoka kwa wazazi ambao tayari walishabadilika kuwa mbwamwitu. Hawa huitwa pure blood werewolves

PURE BLOOD WEREWOLVES

View attachment 2309158
Watoto ambao wamezaliwa na wazazi wote ambao ni wolves basi hawa huitwa pure bloods , damu safi ya mbwa mwitu. Hata katika makabila yao basi hii ni nguzo moja wapo ya viumbe hawa pure blood na mara nyingi hawa ndiyo huwa viongozi wa makundi yao.

Naam hapa nimekukumbusha kuhusu Royal Blood line ambayo inaishirikiana zile bloodline nyingine kuongoza dunia basi siri iliyo ndani ya damu zao hata huku kwa viumbe hawa ipo na ndiyo maana mara nyingi hutukuzwa na hutawala makundi yao.

AINA ZA WEREWOLVES NA UWEZO WAO

ALPHA

View attachment 2309148

Alphas hawa ndio huwa viongozi wa makundi yote ya viumbe hawa na ndio huwa viumbe hatari zaidi kuliko jamii nyingine yoyote ile hatari zaidi.

Wao ni huwa ni wakubwa, wenye kasi ajabu na nguvu zaidi ya jamii yoyote ile ya viumbe hawa, Alpha huwazidi hata purebloods kwa uwezo wao.

Hawa wao wanaweza pia kudhibiti uwezo wao na mihemko yao vizuri sana.

Hawa hata wakiwa Katika umbile la mbwa mwitu bado wao huruma huendelea kuwepo

Alphas wana macho mekundu tofauti na makundi mengine ambao wao huwa ya njano au rangi ya dhahabu.

Makundi mengine kama wale Purebreeds au kundi la Betas au hata Omegas zinaweza kuwa alfas kwa njia mbili Mosi, Ama kwa kumshinda na kumuua alfa mwingine , kwa hivyo kuiba au kuchukua mamlaka za alpha na uwezo wake pia kwa waliotazama teen wolf nadhani hii watarejesha kumbukumbu zao hapa.

Au Njia ya pili kwa kuwa na power karama ya ukuaji na nguvu ya tabia zao, wema, au kupendwa na makundii na jamii yake.hapa kama ilivyo karama ya uongozi katika jamii zetu mpaka mtu anafanikiwa kuwa raisi au Mfalme basi kutokana na mwenendo na karama yake basi hata katika makundi ya viumbe haya haya hii ipo
Hawa huitwa Alphas wa uKweli na ni nadra sana Alphas wa mtindo huu kutokea.

Lakini Alphas anaweza kugeuka kuwa mbwa mwitu halisi kabisa pasi na kuwepo maumbile ya ubinadamu kwake, lakini kwa mwonekano yeye huwa mkubwa zaidi.

Alpha mara nyingi huweza ha kuzungumza hata akiwa katika umbo la mbwa mwitu na kuchanua makucha hata akiwa katika umbo la ubinadmu.

Ndiyo viongozi wa jamii zote

BETA

View attachment 2309159

Beta hawa ni aina ya kawaida ya werewolf. Na hawa ndiyo wapo wengi sana katika idadi , hawa wana nguvu kuliko kundi lingine linalowafatia ambao ni Omegas.

Wana uwezo wote kama tulivotaja huko juu kuwahusu viumbe hawa Betas wana macho ya rangi ya chungwa na mara nyingi wao huwa kama askari wa makundi yao.

Betas werewolves kawaida hutumia miguu yao miwili lakini wanaweza kusimama kwa miguu yote minne na wanaweza kutembea hivyo.

Betas wana makucha na meno yenye nguvu sana na makali.

DELTA

View attachment 2309151

Delta hawa ni mbwa mwitu wadogo kwa kulinganisha na hao waliotangulia hapo juu na wao pia huwa walinzi katika makundi yao hawa wana miguu minne kama mbwa mwitu wa kawaida lakini wao huwa wakali zaidi kuliko mbwa mwitu wa kawaida
Mbwa mwitu wa kundi la Delta wana macho ya manjano, wa urefu kiasi na kasi zaidi.

GAMMA
Gammas ni aina kundi la hini kabisa na hufanywa kuwa wawindaji katika makundi yao,

Mbwa-mwitu wa Gamma huonekana kama mbwa mwitu wa kawaida lakini ni wakubwa kidogo. Uwezo huu unatumiwa na wakuu wao katika kuwafanya maskauti na majasusi wa makundi yao.

Mbwa mwitu wa Gamma wana macho ya kijivu na wana makucha marefu kuliko werewolves wengine.

OMEGA
Omega ni werewolves wasio na cheo chochote katika makundi ya viumbe hawa

Omega hukua na kuwa na nguvu sana.

Wana macho ya bluu na umbile kubwa

Kwa ujumla wao husimama kwa miguu miwili lakini wanapokimbia hutumia miguu yao yote minne.
Hawa hutumika kama chambo katika mapambano

VARGULF
View attachment 2309154

Vargulfs ni mbwa mwitu wasio na utulivu wa mwili na wala kiakili, kwa maneno mengine ni mbwa mwitu ambao vicheche au vichaa.

Huwa na macho meusi na hawana roho yoyote hata ya mfano wa ubinadamu.

Hawa wakiwa wamebadilika katika umbili lao la mbwa mwitu kilicho mbele yao ni Sunna Bila kusema wao ni kupeleka maafa , hawa ni wanyama wakali sana wenye kiu ya kuu mda wowote wanapobugudhiwa

ITAENDELEA

Na DaVinci XV

SEHEMU YA II

-UTHIBITISHO WA KISAYANSI.
-MABADILIKO YAO.
-JE UNATAKA KUWA WEREWOLF.
-NGUVU NA UWEZO.
Miaka miwili imepita
 
Back
Top Bottom