Salary Slip
JF-Expert Member
- Apr 3, 2012
- 47,023
- 144,381
Hili jambo nimeliongea mara kadhaa huko nyuma na leo napenda kuliriudia kwani ni kikwazo kwa watu katika kujitafutia maendeledo yao na pia katika kutatua changamato zao za kifedha.
Kwa wasiolewa, sheria hii inalenga kuhakiksha mtumishi habaki na take home ndogo isiyokidhi mahitaji yake na ya familia yake au kubaki na take home zero kabisa kama ilivyokuwa huko nyuma kwa baadhi ya watumishi kabla serikali haijaingilia kati na kuja na huu utaratibu wa kutaka` kila mtumishi kubaki na walau mojab ya tatu ya mshahara ghafi wake(basic salary) baada ya makato yote(ya kisheria na yasiyo ya kisheria).
Hata hivyo, sheria hii imeweka watumishi wote katika kapu moja, yaani anaepokea mshara wa milioni mbili kwa mwezi, anabanwa na sheria ile ile kama yule anaepokea mshahara wa shilingi laki tatu au nne kwa mwezi jambo ambalo si sahihi kabisa.
Tutazame mifano hii:
1/3 ya 300,000 ni 99,999.99
1/3 ya 500,000 ni 166,666.66
1/3 ya 600,000 ni 199,999.99
1/3 ya 1200,000 ni 399,999.99
1/3 ya 1400,000 ni 466,666.66
1/3 ya 1500,000 ni 499,999.99
1/3 ya 1800,000 ni 599,999.99
1/3 ya 1950,000 ni 649,999.99
1/3 ya 2000,000 ni 666,666.66
1/3 ya 2500,000 ni 833,3333.33
1/3 ya 3000,0000 ni 999,999.99
Hapa nimejaribu kutoa viwango hivyo kama mifano kuonyesha utofauti uliopo katika kutafuta hiyo moja ya tatu ambayo kila mtumishi anastahili kubaki nayo baada ya makato yote yakiwemo na makato ya mikopo.
Sasa tujuilize, kama serikali imeona mfanyakazi mwenye mshahara wa shilingi 600,000/= akibaki na take home ya walau shilingi 200,000/=, anaweza kuishi, ni kwanini mtumishi mwenye mshahara wa shilingi 1500,000/= alazimishwe kubaki na take home ya 500,000 wakati wote tunaishi katika nchi moja?
Nafikiri wakati umefika serikali ipitie upya sheria hii ili kuwezesha watumishi wenye mishahara mikubwa kutumia mishahara yao kukopa katika mabenki na taasisi zingine za kifedha badala ya kuwabana wote na sheria moja ili hali wana tofauti kubwa ya kipato.
Tafakari hii:
Mtu anataka kukopa amalizie nyumba yake ahamamie, ila kutokana na sheria kama hii, mtumishi anakuwa hakopesheki, hivyo anaendelea kulipa kodi na hapo hapo serikali inaamini sheria hii inamlinda mfanyakazi kumbe inamuumizi kwa kumfanya aendelee kulipa kodi kwasababu tu ameshindwa kukopesheka kisa anatakiwa kubaki na moja ya` tatu ya mshahara wake baada ya makato yote.
Waziri wa Utumishi na serikali kwa ujumla, wakati umefika sheria/utaratibu huu upitiwe upya na ikiwezekana serikali ifanye tathimni upya na kuweka kiwango ambacho ni shariti kibaki katika mshahara wa kila mtumishi na utaratibu uzingatie range fulani ya mishahara(wenye mshahara kuanzia kiasi fulani mpaka kiasi fulani wabaki na kiasi fulani kulingamna na mishahara yao) na sio kwa kutumia huu utaratibu wa moja ya tatu usiozingatia tofauti kubwa ya mishahara iliyopo baina ya watumishi wa umma.
Nawasilisha.