Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Polisi Kanda Maalum ya Dar kumsaka na kumhoji Askofu Mwingira

"...ni ajabu kama yote hayo alitendewa na bado hakuwasilisha malalamiko kwenye vyombo vya dola inaleta ukakasi."

"...hivi kweli utendewe yote hayo muda wote huo ndiyo usubiri hasi Krismasi useme?!" Amehoji Simbachawene.

"....kwasababu yupo hapa Dar es Salaam na ametoa tuhuma nzito namna ile namuagiza sasa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amwite na amuhoji kuhusu tuhuma hizo." Amesema Simbachawene Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo Millard Ayo.

=====

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameelekeza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar kumtafuta Askofu Josephat Mwingira na kupata maelezo zaidi, kufuatia tuhuma mbalimbali alizotoa ikiwemo kutishiwa maisha

Amesema, "Ni tuhuma nzito, zinapotolewa na Kiongozi wa Kijamii/Kidini na ambaye ni maarufu na anajulikana tunapata shida kidogo. Kama matukio haya yote ndivyo yalikuwa yanatokea kwanini hatoi taarifa Polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa kuwatafuta wahusika"

Ameongeza, "Tamko la Askofu Mwingira mimi nimelisikia kwenye Mitandao. Nimepata 'clip' lakini sijasikia vizuri maana kama haina sauti. Bado tunaendelea kulifuatilia"
Kuna Nchi moja hivi....Viongozi wa namna hii wanaitwa "Viongozi wa Matukio" AIBU.
 
Anatafuta Kiki tu waliopoteza. Maisha nawengine mpaka leo hawajulikani walipo bado anahisi mwingira ni muongo aanze na hao kwanza
 
Kuna mambo mengi mazito watu wamepitia na wanaendelea kupitia. Nchi isiendelee kutisha waliochoka kukaa kimya, ni wajibu wao kuchunguza na ukweli ujulikane kwa watu wote. Waliohusika wote sheria ichukue mkondo wake
 
ndumilakuwili ni mtu hatari sana watu kama hawa inafaa hata wapotezwe kabisa
 
Ile kauli ya Ikulu inaongozwa na shetani na kiongozi mkuu wa ikulu ni mtoto wa shetani kwakweli sio kauli ya kiungwana hata kidogo. Awajibike kwa kauli hiyo aeleze alimaanisha nini.
Mkuu wa Malaika.Unajua Shetani naye ni malaika?
 
"...ni ajabu kama yote hayo alitendewa na bado hakuwasilisha malalamiko kwenye vyombo vya dola inaleta ukakasi."

"...hivi kweli utendewe yote hayo muda wote huo ndiyo usubiri hasi Krismasi useme?!" Amehoji Simbachawene.

"....kwasababu yupo hapa Dar es Salaam na ametoa tuhuma nzito namna ile namuagiza sasa Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amwite na amuhoji kuhusu tuhuma hizo." Amesema Simbachawene Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi.

Chanzo Millard Ayo.

=====

Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene ameelekeza Kamanda wa Polisi Kanda Maalum Dar kumtafuta Askofu Josephat Mwingira na kupata maelezo zaidi, kufuatia tuhuma mbalimbali alizotoa ikiwemo kutishiwa maisha

Amesema, "Ni tuhuma nzito, zinapotolewa na Kiongozi wa Kijamii/Kidini na ambaye ni maarufu na anajulikana tunapata shida kidogo. Kama matukio haya yote ndivyo yalikuwa yanatokea kwanini hatoi taarifa Polisi ili hatua ziweze kuchukuliwa kuwatafuta wahusika"

Ameongeza, "Tamko la Askofu Mwingira mimi nimelisikia kwenye Mitandao. Nimepata 'clip' lakini sijasikia vizuri maana kama haina sauti. Bado tunaendelea kulifuatilia"
Waziri ni wakala wa ibirisi. Jeshi la polisi linatumika na ibilisi
 
Watu wametekwa na hawajulikani walipo na wengine kujeruhiwa na wengine kuuwawa huyo Simbachawene hajawahi kutamka chochote.! Hovyo kabisa.
 
Simbachawene Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, unda tume huru ya kuchunguza kifo cha JPM .
.Usisubiri hadi 2025 wananchi wanahoji na Hakuna majibu na majawabu sahihi kuhusu kifo cha JPM.
Mwenyekiti wa tume hiyo awe Dr Bashiru Ally Kakurwa na mke wa marehemu JPM awe mjumbe wa hiyo tume.
Ili mgundue nini?
 
'Kama kuna kosa tulilifanya basi ni kutowamaliza Wahuni'-Humphrey
Mhuni Mkuu aliyekuwa anafuga wahuni kama Sabaya Kwa SASA Yuko Jehanamu kwenye Moto wa Milele
Namaanisha Mzee Mwendakuzimu
 
Back
Top Bottom