TCRA yasimamisha kipindi cha EFATHA cha Nabii Josephat Elias Mwingira kwa miezi mitatu, Star TV yapewa onyo

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Kamati ya Maadili ya TCRA imesema Kituo cha Star Tv kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja, kwa kuruhusu maudhui yenye ukakasi ambayo ni kinyume na Kanuni za Mawasiliano

TCRA ikimnukuu Askofu Josephat Mwingira imesema maneno yake kwamba "Serikali fanyeni upuuzi wenu Mungu amewaruhusu, lakini muda sio mrefu atakuja kumalizana na upumbavu wenu" yanafedhesha kutokana na Lugha isiyo na staha kwa Mamlaka ya juu ya Nchi

Kipindi cha EFATHA kimesimamishwa kwa miezi mitatu, huku Star Tv ikipewa onyo na kuamriwa kuomba radhi watazamaji na umma kwa siku tatu mfululizo kuanzia Januari 25 - 27, 2022

Pia soma: Askofu Mwingira: Nimenusurika kuuawa mara tatu na watu wa Serikali

Pia soma: Waziri wa Mambo ya Ndani aagiza Polisi Kanda Maalum ya Dar kumsaka na kumhoji Askofu Mwingira

Pia soma: Polisi Dar yampa saa 24 Nabii Mwingira ili ajisalimishe kwa Mahojiano

 
Kwa hiyo lile tamko la Simbachawene na Muliro la kumtaka huyo Askofu na Nabii Mwingira kuripoti kituo cha polisi kati ndani ya masaa 24, ndiyo limeishia hapa sasa!

Bila shaka Askofu ameshinda. Maana ujumbe umefika. Serikali iachane na mambo ya kipuuzi na kipumbavu! Badala yake itumie nguvu kubwa kuwaletea wananchi maendeleo.
 
Mamlaka ya Mawasiliano Nchini (TCRA) imesema Kituo cha Star Tv kimeonesha uzembe na udhaifu katika kusimamia kipindi cha EFATHA Ministries ambacho hurushwa kwa matangazo ya moja kwa moja...

Screenshot_20220124-131257.jpg
 
Sidhani kama TCRA watamfunga mdomo kwa style hiyo, huyu mtu naona muda wake wa kuongea umefika, ni kama vile alikuwa anateseka kwa kujiuliza nafsini mwake aseme au anyamaze, sasa ameamua kusema kwake liwalo na liwe, heri awe na amani ya nafsi kuliko kumfurahisha mtawala huku akikosa amani ya nafsi yake.
 
Back
Top Bottom