Waziri wa Fedha: Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’

Shujaa Mwendazake

JF-Expert Member
Jul 11, 2015
3,734
6,292
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’, “hili ni eneo jipya ambalo tunalifanyia kazi, katika bajeti zinazofuata litakuwa ingizo jipya. Mataifa mengi yanageukia kodi hii.”

Kazi na iendelee!
 
Mwigulu Nchemba waziri wa fedha wa hovyo kabisa kutokea tangu tupate Uhuru.
Mwigulu Nchemba original Ni msukuma na yupo, anajulikana.

Alipochana bungeni bajeti ya kambi rasmi ya upinzani akathibitisha kwa mara nyingine.

Funika bovu ni pale alipoanza kujiandika kwenye mawe na majabali nchi nzima kwamba yeye Ni raisi.
Kupiga chata alifanya ras jeff kapita enzi zile akiwa kijana mdogo, chini ya miaka 18
 
Je itatozwa Google, Facebook, n.k au Jamii Forums tu? Hao jiants tayari wamekingiwa kifua na OECD.
 
Mwigulu Nchemba waziri wa fedha wa hovyo kabisa kutokea tangu tupate Uhuru.
Natamani sana kukijua Chuo Kikuu kilichompa hiyo 'Doctorate' yake hiyo ili nikidharau kama ninavyomdharau Yeye.

Nashukuru hajasoma Chuo Kikuu changu bora, pendwa na barikiwa cha SAUT Mwanza au hiki cha Dar es Salaam ( School of Graduate Studies ) Msimbazi Center ambacho kinatoa 'Geniuses' tupu nchini Tanzania.
 
Waziri wa Fedha, Dk. Mwigulu Nchemba, amesema Serikali itaanzisha ushuru wa huduma za mitandaoni ‘Digital Service Tax’, “hili ni eneo jipya ambalo tunalifanyia kazi, katika bajeti zinazofuata litakuwa ingizo jipya. Mataifa mengi yanageukia kodi hii.”

Kazi na iendelee!
Ujinga wa viongozi wa Tanzania ni kutokuwa na akili inyojitegemea, kila kitu ni ku copy toka kwa wengine as if nchi zote duniani zinafanana
 
Huu ni mtindio wa ubongo, wizi au ufisadi unaosimamiwa na hii serikali yetu iliyochoka na kuchakaa kimawazo. Hivi serikali ya CCM iliwekeza nini kwenye mitandao? Mbona ni kama vile wanataka kuvuna wasichopanda!

Waliogharamia, kuwekeza na kutuletea mtandao wanashauri matumizi yake yawe karibu sawa na bure, mchovu wa akili PhD holder Mwigulu anapanga kuvuna kwenye shamba la watu! This is stupidity at its best!
 
Back
Top Bottom