Mkuu Nguruvi3, ni yapi uliyoyaona ambayo baada ya kuyatafakari kwa kina yakakushawishi kutoa kauli hitimisho kwamba hoja yangu imejikita kwenye Uzanzibari? Mimi ni mtu wa Lindi kwa 100% kwahiyo sina maslahi yoyote ZNZ labda kama unataka kunipa complement kwamba naitetea ZNZ ingawaje sina maslahi nayo; if so, then i'll take that complement ingawaje nitalazimika kuirudisha at the right time coz' I don't deserve it since my argument had nothing to do with Uzanzibar ama Uzanzibara!NasDaz
Nashukuru kuona kuwa utetezi wako umelenga katika uzanzibar na ubara na siyo experience na CV. At least hilo umeliweka wazi. Nirejee hoja zako kama ifuatavyo.
Nakubaliana na wewe but this diploma things ni system ambayo Tanzania ipo so, sidhani kama kuna mtu aliyefika angalau kidato cha sita na akashindwa kutofautisha kati ya diploma na advanced diploma. Ila tu nikukumbushe kwamba CV ya Saada haisemi alisoma diploma bali Adv Diploma na ndio maana nikasema hayo maelezo yake kwamba ana diploma ya...., bila shaka alimaanisha Advanced Diploma coz' ndiyo inayoonekana kwenye CV.Advance diploma na Diploma ni vitu viwili tofauti kabisa na si mbwembwe kama ulivyosema. Kwa ufupi advance diploma ina hadhi yake tofauti kwa curriculum na recognition
You missed my point here. Watu tulijikita kuona magumashi ya elimu yake baada ya kuona kwamba elimu yenyewe ni kutoka OUT otherwise sijui inakuwaje tuone elimu yake ni ndogo wakati ana Masters! Kutokana na hilo ndipo nikasema hiyo elimu ya OUT ambayo watu wanaijadili wala haipo kwenye CV na kilichopo kwenye CV ni ile Advanced Diploma, Postgaraduate na Masters ambazo zote sio za OUT!Endapo waziri hakuona sababu ya kuweka sifa zake za OUT kwas sifa,umesahau kuwa hatukuhitajikujua kasoma secondary, kuweka sekondari badala ya sifa za graduate ni udhaifu wa hoja yako.
Nakubaliana na wewe kwa 100%, lakini wala haielekei kwamba wale wanaopinga hapo ndipo zimejikita hoja zao. Hoja za wale wanaopinga ni kwavile tu hawaoni majina ya vyuo vikubwa vikubwa kwenye CV! REMEMBER, hata mwanzilishi wa mjadala huu, Profesa Lipumba ndiko alijikita....wala hatukumsikia akizungumzia hayo mengine unless kama Waandishi waliamua kuacha mambo ya msingi ambayo Lipumba aliyasema na badala yake wakaon hili la wapi amesoma ndiyo issue. Lakini kwa upande mwingine, huyu mama isn't academician, and in fact not politician either, so huo mchango wake kitaaluma na kifikra ulitarajia tuone wapi? Huenda sijakupata vizuri. UKiangalia CV zilizo tovuti ya bunge, zinaishia tu kutaja education background, wapi alifanyia kazi na few including publications! Saada imetaja hayo mawili ya mwanzo but no publication. Lakini hata hivyo, ni Masters Holders wangapi wenye publication wakati sio academician? But wakati hizo publication hazipo, inaonekana wakati anachukua MBA yake pale OUT, Research yake ilikuwa on: Challenges of managing foreign aid in Zanzibar.Usomi haushii katika vyeti na wala vyeti havitengenezi usomi. Usomi ni matumizi ya elimu katika weledi. Hatuangalii usomi wa Saada kwa makaratasi bali mchango wake kitaaluma au kifikra. Hakuna mahali tunaweza kuona Saada ameshiriki. Hayo si mbwembwe au sifa ni sehemu ya CV.
Mkuu wangu Nguruvi3, can we at least be fair to this woman? Hivi unataka kuniambia kwamba leo hii tuki-pick at random very qualified MPs who were once gov employees, CV zao kwenye tovuti zitaonesha kwamba alishiriki shughuli hii na ile, huku na kule? Can you try to check from bunge website? Haya mambo mengine reference yake ni kule alikofanyia kazi na sio tovuti ya bunge. Tovuti ya bunge inatoa simplified CVs.Je aliwahi kuwa policy maker au aliwahi kushiriki shughuli yoyote ndani na nje ya nchi ambayo tunapaswa kujua? Lazima CV ieleze si miaka ya shule tu bali uthabiti wa mtu katika nafasi na fani.
Hivi ulitarajia CV zilizopo pale tovuti ya bunge ziwe na mambo yote hayo? Kwamba, huyu bibi alikuwa Commissioner for External Finance na ame-achieve ABC! Before that alikuwa Treasure kama Administrative Officer na kazi zake zilikuwa XYZ, and these were her accomplishment! Is this what you're trying to say? Anyway, labda nikukumbushe tu kwamba ndio maana post yangu ya kwanza kabisa kwenye mjadala huu nilimkosoa Lipumba kwamba kwa jinsi alivyokosoa hadi kuita media, nilidhani alifanya research in advance kumbe katumia tovuti ya bunge as a reference!!! Kwavile Lipumba ni CUF na CUF wapo kwenye system kule ZNZ basi nilidhani kwamba alipata tips kutoka huko!Uzoefu wa kazi wa miaka 10 hautuelezi uwezo wake wa jukumu kubwa na zito alilo nalo. Anaweza kuwa alikuwa desk officer kwa miaka 8.Kukaa kazini hakuna maana uzoefu, uzoefu ni pamoja na nini amefanya
Hapo kwenye BLUE ni bridge ya kuunganisha hizo two red sentences. The bridge sounds like u're not sure! But all in all, her last post was Commissioner for External Finance. There's no way tunaweza kusema hii ni junior post. Ingawaje sina uhakika na organisation structure ya ZNZ lakini hata kwa kuangalia Wizara ya Fedha muungano, Commissioner For Finance ni senior post. Lakini hata hivyo, ZNZ hakuna wasomi wengi as compared to bara, kwahiyo I doubt kama mwenye Masters in Finance anaweza kuwa junior staff in Zanzibar.Ukumbuke nafasi alizoshika huko ZNZ ni ndogo sana japo majina ni makubwa. CommiSsioner wa fedha znz anaweza kuwa sawa na nafasi nyingine kama hiyo katika ngazi ya mkoa. Inabidi uangalie nafasi hiyo ilikuwa na ina simamia ukubwa kiasia gani.
Kwahiyo kigezo nini? Labda niseme hivi, kigezo kwamba Kamishna wa NY ni tofauti na yule wa URT si kutokana na ukubwa wa uchumi husika bali changamoto za particular economy! Challenges in NY's economy is absolutely different to that of URT; so ingawaje NY wana uchumi mkubwa kabisa kuliko URT, lakini Commissioner wa kule anaweza kushindwa ku-deliver hapa coz' challenges are different! Wakati yeye labda alikuwa very competent in stuffs like money and financial markets, and the like, huku atakuta masuala ya Kilimo Kwanza na wakati hata pamba inafananaje hajui! Wakati NY economy is how to have addition sources of revenues huku atakuta wafanyabiashara hawataki kutumia EFDs! So, the point here isn't how large the economy is but challenges facing that economy!Uchumi wa New York city ni mkubwa kuliko wa Tanzania. Commissioner wa fedha wizara ya fedha Tanzania ni tofauti na commissioner wa fedha wa New york. Hoja ikiwa ni kuwa nafasi alizoshika huko znz si kigezo muhimu cha kupewa jukumu kubwa la JMT.
Nakubaliana na wewe kwa 100% lakini hizo competency ulizotaja huwezi kuziona kwenye CV; sasa kwanini tumuhukumu kwamba she's dumbest choice ever happened wakati nowhere in public papers unakoweza kuona alifanikisha au aliharibu XYZ Negotiation? Why should we judge her wakati nowhere kwenye public papers unakoweza kuona kwamba due to this poor decision once done by this woman, nchi ikaenda msobemsobe! I was once working with NMB, nilikuwa junior employee (Teller) by that time! Siku moja Branch Manager akaitisha Branch Management meeting...aliitisha kikao hicho baada ya kuitwa HQ na CEO na CEO alimtaka kila Manager aende na recommendation ya nini kifanyike ku-improve operation. Branch Management Meeting ikakaa kwa dakikaa kadhaa bila kupata even a single input! Ikabidi Manager aniite na kuniomba input. From nowhere, nikatoa my input haidhuru hata kama Manager alienda kwa CEO na kujifanya input hiyo ni yake! Na input yenyewe mpaka kesho NMB wanaitumia....nimekupa story hiyo ya kweli kukuonesha kwamba sometimes doesn't need a very huge post for one to have contribution in a particular area! Na huo huo u-administrative offier wake unaweza kukuta amefanya mambo makubwa kuliko Senior Super Consultant! Mwenye kuyafahamu haya ni bosi wake na wala sio sisi coz' you can't find them in CVs or Presentation papers!Nafasi aliyopewa Saada ni kubwa na muhimu sana kwa uchumi wa taifa. Inataka mtu si mwenye elimu tu bali weledi wa kuchambua mambo. Waziri wa fedha atakuwa na majadiliano na akina Christine Lagard na wenzake wa EAC, SADC, WB na IMF. Ni mwakilishi katika maamuzi makubwa ya kiuchumi yanayoathiri nchi.
You're very right! Lakini usisahau, wakati JK anamteua Sitta watu walisema anamuua kisiasa na kuona it wasn't enough post for him kv EAC watu tuliichukulia ni kama wizara ya jinsia na maendeleo ya watoto! Majuzi hapa ndipo nikaja kugundua it's very right decision Sitta kuwa pale...kv sipendi kuwa ni mtu mwenye hinda, sioni taabu kusema kwamba Baba Riz aliona mbali hata kama watatokea wa kusema kwamba hakuna cha kuona mbali wala nini bali lengo ilikuwa ni kumpoteza as if alikuwa analazimika kwamba no matter what lazima ampe uwaziri!JK kumwacha Sitta EA ni makusudi kwa kuelewa changamoto zilizopo
Kuwa mbunge wa kuchaguliwa au kuteuliwa sio issue lakini sitaunga mkono uteuzi huo hata mara moja simply because Lusinde hata Form Four yenyewe sidhani kama amemaliza. Hata hivyo, Saada Mkuya ana MBA (Finance); the different between the two guys is very significant!Hivi leo utajisikiaje ukiona Lusinde(Kibajaji)ndiye mwakilishi wa Tanzania katika EAC. Arguably ni mbunge tena wa kuchaguliwa na si kuteuliwa kwanini tudhani hataweza kuwa!!!!!
Huo mfano wako wa Paris Club sijauona lakini kama ni muhimu, basi wakija leo wataambiwa kwamba huyo Waziri wa sasa alihudumu kama Naibu Waziri wa wizara hiyo hiyo kwa miezi 18; na kama huo kwao hautakuwa uzoefu basi watakuwa watu wa ajabu! Lakini tukumbushane tu kwamba Wizara ya fedha ina watendaji wake…ina Katibu Mkuu na Msaidizi wake, ina wakurugenzi kwenye idara mbalimbal, ina makamishina katika idara mbalimbali. Hawa ndio msingi wa Wizara kwavile ndio watendaji. Though elimu na experience ni necessary lakini tunachohitaji zaidi ni very responsible and committed minister, the one with high integrity level, and so on! If you're an expert in solving complex economic models, you'll be where you belong to assist this responsible minister! If you got A+ in Econometric and Quantitative Methods, you'll be provided with the right desk.Nimetoa mfano kuwa Paris Club ilikataa majadiliano hadi waletwe wazoefu.
Mkuu Nguruvi3, mbona unaapiza wakati huyu mama humfahamu?! Usiseme wapi umeapiza, ni dhahiri kwamba sentensi yako kuna pahala imeficha neno, ama Haki ya Mungu, au Yesu wangu na kuwa "haki ya mungu, Saada hafai kabisa kwenye hii nafasi!!!!" Labda niseme hivi; mtu akiingia ndani na kuwasha swichi ya umeme lakini taa zisiwake, picha ya kwanza atafikiria TANESCO wamekata umeme! Akichugulia nje na kukuta nyumba za jirani taa zinawaka, ata-conclude kwamba tatizo si TANESCO...labda units za LUKU zimeisha! Akiangalia LUKU na kukuta zimejaa, huenda akafungua jokofu ili aone kama linapiga mzigo... in short, atajaribu hiki na kile hadi aone tatizo! Tumewasha swichi na taa haziwaki lakini tulipoangalia nyumba za jirani tukakuta taa zinawaka, tukagandua tatizo sio TANESCO! Hii nyumba ya jirani ni Wizara ya Elimu, Hii nyumba ya jirani ni Wizara ya kilimo, hii nyumba ya jirani, ni wizara ya maji; n.k n.k n.k! Huko kote kuna magwiji wenye wasifu usio shaka, lakini hakuna kitu! Waonaje basi tusipokata tamaa ili tuendelee kuwasha chombo hiki na kile, ikibidi tupande darini hadi tugundue tatizo ni nini hasa? Isije ikawa panya wamekata nyaya za umeme darini na kusababisha yoooooote haya!! Tukifanya hivyo, tutaepuka kupeleka jokofu kwa fundi akala pesa zetu bure!Nafasi ya waziri wa fedha ni kubwa sana, na kwa kuangalia wasifu wa Saada nasema wazi hakupaswa wala kufaa kupewa jukumu hilo.
Last edited by a moderator: