Waziri wa Fedha amjibu Prof. Lipumba

Waziri wa Fedha amjibu Prof. Lipumba

NasDaz,
..hivi kwa maoni yako huyu waziri ni NGULI ktk fani ya fedha, au fani ya uchumi?
Kwanza hamjatoa tafsiri rasmi ya huyo NGULI ni mtu wa aina gani! Point of remind ni kwamba, ikiwa utajaribu kuelezea huyo NGULI ni nani hasa, usisahau ku-relate hizo sifa za unguli na mawaziri waliopita...akina Basil Mramba, Zakhia Meghji,Mgimwa, Mkulo n.k!
 
Kila kukicha na jipya lake.... yule naibu waziri wa elimu mkamwandamaaa mpaka kimeeleweka.. hayupo tena kabaki na ubunge wake
 
Hapa sasa umesemaje?

sijaona hoja sana sana ni arrogance kwenye maandishi yako...

Mnaopinga uteuzi hamjanishawishi mnataka awe na diploma, degree au master -anavyo hivyo..

Mnataka awe na uzoefu kiasi gani na wapi? hamsemi..hamjani convince hata kidogo

What you call arrogance, can as well be called the truth. Nina uhakika kuna watendaji wengi sana wenye hizo masters na PHD, the same applies kwa wabunge. Kinachojadiliwa hapa tunataka mtu mwenye something extra. ninaposema Unquestionable Academic Excellence, simaanishi awe na genius Brain ya John Nash. He/she is supposed to be intelligent and capable enough to analyze complex economic models with sheer quality and brilliance, we all know this woman can't do that.
Kwa nchi zetu hizi, si wachache ambao wamefanya kazi na "bosi" asiyejiweza kiasi kwamba kuelezea vitu kwa kina ni sawa na "kumtukana". kwani anakuwa haelewi.mwisho wa haya ni majungu yasiyoisha makazini, oh flani anaringia elimu yake, blah blah blah.
I am sure PS wa hii wizara anakutana na "same dilemma" Kilasiku aki-deal na huyu mama. Kutokujiweza kielimu sio kosa, ni ukweli. Si kila mmoja wetu anaweza kuwa na "academic powers" za kuweza kuwa "minister of finance", ndio maana kwa wale wachache walio na uwezo huo wanatakiwa wapewe nafasi hizo. sio kwenda kuokota watu wenye sifa za kuunga unga na kuwapamba left and right. Tumefikia hatua tunalinganisha uwezo wa elimu na kosa, sio kosa wala arrogance mtu kufahamu vitu kwa kiwango cha juu. kwa nchi zenye ufahamu, hii ni faida kwao. kwani huwatumia watu hao.

Swali rahisi kwako,

looking at our economy $20B plus, if we assume Tanzania is a MNC, it's a $20B gorrila, enough to be a fortune 500 company. can you honestly tell me with a straight face, this woman has what it takes to be the CFO of a forune 500 $20B MNC?
 
Khaaa! Hizo conclusion zako za ajabu ajabu sijui unazitoa wapi! Yaani mtu aki-respond statement after statement ni mbishi na arrogant, aisee!! Labda nikuambie kitu kimoja; i hate this kind of response lakini wakati mwingine unajikuta unalazimika kufanya hivyo! Unakuta mtu ame-include hoja nyingi zinazohitaji majibu sehemu moja, what can you do if not responding one after another this way? It's very boring but sometimes inakosa best alternative.
Nadanganya vipi wakati hamna popote niliposema kwamba Saada ni mwadilifu? Ina maana kusema tatizo kubwa kwa watendaji wetu ni uwajibikaji na uadlifu ni sawa na kusema Saada ni mwajibikaji na mwadilifu?
Unaona sasa! Kama ingekuwa suala ni uanamke na Uislamu wake basi angepewa yeyote yule coz' kuna wanawake na waislamu wengi tu! Hapahitaji shahada kufahamu kwamba kigezo hakikuwa uislamu au uanamke wake vinginevyo angekuwa amepewa nafasi hiyo hapo kabla badala ya Marehemu Mgimiwa! Tukumbushane, huyu wizara wa fedha wa Bara bali wa URT.
Inferior compared na vyuo vya wapi? Tanzania, or? Moja kati ya nchi ambazo zimepiga hatua sana kwenye sekta ya fedha ni Malaysia, so how come tena nchi yake useme ina inferior universities?
May be or may be not unless kama unataka kuniambia kila anayetoka TZ akiwa form VI na kwenda kusoma adv diploma nchi nyingine, huyu alikosa nafasi pale UDSM and the like. But all in all, it doesn't matter; what matter ni kwamba alisoma form six kisha akaenda kusoma advanced diploma Malaysia labda wewe mwenye shaka na elimu yake ndie u-prove adv diploma aliyosoma isn't worthwhile!
Tuanze hapo na kwenye Watt na Heriot-Watt. Hivi mimi nikisema nimesema Kairuki itakupa shaka kwamba ni Herbert Kairuki Memorial University? Tatizo lako umeshakuwa na negativity kuhusu huyu mama ndo maana hutaki kabisa kuamini kwamba Heriot-Watt! Tukija suala la exhaustive kwenye university ranking, nakubaliana na wewe lakini angalau umekubali kwamba unaiamini ile ya Times! Kwavile nako bado una shaka shaka, kuna ranking nyingine ya URAP ambao wanatumia sensible indicators. Out of 93 universities in UK, Heriot-Watt ni cha 38! Bado una mashaka nacho hasa ukizingatia na ubora wa vyuo vya UK? Ukiangalia kwenye hiyo ranking, utakuta kuna vyuo kadhaa maarufu vya UK ambavyo vipo chini ya Heriot-Watt....wakati unatafakari haya, usisahau ukiritimba uliopo kwenye UK universities katika kujiunga!
Naona umeng'ang'ania sana hilo suala la Uislamu, sijui lina tija gani kwenye mjadala huu. Lakini tukija kwenye hoja yako kwamba elimu yake ni sawa na zero huku bara basi ni hoja ya kushangaza inayobeba sifa za kuwekwa kwenye jumba makumbeusho ili watu wakaishangae! Hivi utasemaje kwamba mtu mwenye Masters Degree in Finance, baada ya kuwa na postgraduate Diploma na Advanced Diploma huyu elimu yake ni sawa na ZERO? Mbona Mgimwa alikuwa na Advanced Diploma kutoka IFM, akaja kuchukua Postgraduate Diploma hapo hapo IFM kabla hajachukua Masters pale Mzumbe ya zambani ambayo ilikuwa wala haijapata hadhi ya university! Yaani huyu ndo msomi lakini Saada aliyepitia njia ile ile ya Mgimwa na kuchukua Masters Scotland, yeye ndo kapuku!Mnashangaza sana aisee, labda kama mna lingine!
Kuhusu Mgimwa kuna watu tuliona kuongelea weakness ya uteuzi wake, na watu wengine walisema labda influence ya Lukuvi ili saidia na pia kuna swali alilouliza akiwa Bungeni ikaonyesha "umahiri" maana yeye kasomea micro economics na watu labda waliona ange faa mtu wa Macro, kwa hiyo usifikirie kwampa watu wana personal iisue ya Saada. au Dini, maana kuna wakati watu wame msema Prof. ole Gabriel Katibu Mkuu wa Habari nk.
Kuhusu wewe kutoa ushauri ukiwa ni Teller tu, Manager alishindwa au hakuwa na hiyo idea. Kuna vitu in life vina hitaji General idea au akili ya kuzaliwa ambayo unayo ndio maana ukaweza kutoa ushauri, ni sawa sawa na Mimi ingawa si Dr lakini labda naweza kuongoza wizara ya afya kwa mfano, lakini likija suala la utaalamu la kumuhusu Dr nitakuwa nime tolewa knockout.
Sasa tukija wizara ya fedha, labda watu wana danganyika na jina Finance na kufikia knowledge inayotakiwa hapo ni ya Finance kama MB Finance and ze like.
Lakini ukweli wa mambo pale sehemu kubwa ni mambo ya uchumi could both Macro na micro economics na jinsi gani ya kuongeza revenue through it , investments zenye return , then mambo ya kodi, fedha na budgetary control.
Sasa kama wewe strength yako ipo kwenye Budgetary control, wakati tatizo kubwa la tz ni kwenye issue ya macro, micro economics na investment, na ndio maana unaona unemployment ipo kubwa, miundo mbinu mibovu, umeme hakuna nk nk
Sasa waziri mwenye kukosa muono kama huo au mwenye ku lack some expose, experience au uweledi katika mambo hayo huoni kwamba itakuwa ni minus ktk juhudi zetu za kuondoa umasikini? n.k
 
Mkuu NasDaz,
Awali nilikuuliza je unajua majukumu ya waziri wa fedha ni yepi? Jibu lako likaashiria moja kwa moja kwamba haujui kwani ukasema kwamba its a good question na umewasiliana na jamaa zako waliopo hazina ili wakupe job description, ambayo hadi sasa haujaileta; katika hali hii mkuu NasDaz, unamtetea mama yetu mpendwa kwamba anafaa kutekeleza majukumu yepi?hauoni kwamba kwa mapungufu haya peke yake hoja yako kumtetea inakosa mashiko?

Ukirejea mabandiko ya nyuma katika uzi huu, nilieleza general roles and responsibilities za waziri wa fedha katika mataifa mengi, na nikatumia such roles and responsibilities kuhoji iwapo mama yetu mpendwa anatosha au hatoshi;kwahiyo angalau binafsi nilikuja na maelezo yanayojitosheleza juu ya nini naamini ni majukuu ya waziri wa fedha na kwanini sidhani huyu mama anatosha;wewe mkuu hadi sasa unajenga hoja kwamba anafaa huku ukiwa bado unasubiri kupata majibu kutoka kwa wenzako hazina juu ya majukumu ya waziri wa fedha ni yepi;

Wadau wengi humu kama Nguruvi3, Kimweri, JokaKuu na wengine wanajenga hoja huku wakieleza nini wanaelewa juu ya majukumu ya waziri wa fedha ni yepi, wewe mkuu unapingana nao huku ukisubiria kupata majibu kwa jamaa zako hazina, je mkuu hauoni kuna tatizo hapo?

Ningependa nimalizie kwa maswali mengine makuu matatu:

Kwanza - je unajua moja ya sifa kuu muhimu kwa mujibu wa katiba za kuteuliwa uwaziri ni ipi? Nadhani unajua kwamba ni "mbunge"; je unajua kwanini katiba ilisema hivyo?

Pili, ni mawaziri wangapi katika historia ya nchi yetu waliteuliwa uwaziri moja kwa moja mara mara tu baada ya kushinda ubunge wa jimbo au kuteuliwa ubunge? Unajua kwanini?

Mwisho, rasimu mpya ya katiba inapendekeza kwamba mawaziri wasitokane tena na ubunge, je unajua ni kwanini?

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Swali rahisi kwako,

looking at our economy $20B plus, if we assume Tanzania is a MNC, it's a $20B gorrila, enough to be a fortune 500 company. can you honestly tell me with a straight face, this woman has what it takes to be the CFO of a forune 500 $20B MNC?
Mkuu

Embu tufafanulie wewe how is the question posed related to national economics (social policies) hili tuone kama experience ya huko matters so much in being a minister.

Ukute labda jamaa wanafaa katika advisory role tu, kuna kitu ambacho tunakwepa hapa au atukiangalii sibishii umuhimu wa kujua uchumi au finances lakini siafiki umahiri unaodaiwa. Kwanza kumbuka kwenye developed societies policies nyingi wakati zipo kwenye mchakato zina involve stake holders. Kwa maana hiyo kama ni sera ya corporate tax katika hatua za mwanzo kuangaliwa representing groups will be involved to contribute on the effects of the policy intended kwanzia makampuni, consumer groups and other necessary stakeholders.

Hivyo basi ndio unaweza ona waziri ana ana angle nyingi sana za kutetea hoja ni kwa sababu keshasikiliza argument za concerned representative kabla hawajaamua na hivyo kuonekana mjuaji au kutoyumbishwa hovyo bungeni, hivyo utaratibu huo sidhani kama kwetu hupo kwa sana, hilo halimpi waziri kuonekana mjuaji zaidi ya kutegemea mawazo yake, management ya biashara si sawa na ya kisiasa especially a ministry of finance.

Labda ufafanue were the similarities lie.
 
@NasDaz hoja yangu kubwa ni kuwa hata kama si academician, just show us something about her hata kutumia hansard za bunge.
Hata ka conference alikozungumza. Ukiacha kuteuliwa she has nothing to show us

NasDaz tunahangaika kumzunguzia kwasababu huyu mama CV ni white, experience katika nafasi kubwa kama hiyo hakuna. Msome Mchambuzi kuhusu hoja ya Amina Salum

Ndio maana watetezi wake wanasema anashambuliwa kwasababu ni mwanamke, na wajinga wengine wakitumia dini na wengine uzanzibar. Wanofanya hivyo wanajua hwana cha kushikiza kwasababu hana kishikizo.
Hana kitu cha kuzungumziwa, wala hana kitu alichozungumza.

Ukiacha nafasi za kuteuliwa, katika uwanja wa ushindani Mkuya hapata kazi hata TRA kanda ya Kinondoni.Misogope jamani hili ni tatizo kubwa sana. Msione aibu kusema
Nguruvi3,
Unamaanisha nini unaposema nitoe angalau conference aliyoongea ama kutoka kwenye hansard? conference za aina gani unayozungumzia hapa? Zile za Davos and Zurich, or? Hansard? Unamaanisha vile ambavyo anachambuana na wabunge,au nini hasa unachohitaji katika hilo? Nikiri wazi kwamba hapo sijakuelewa!
Kuhusu Mchambuzi, tayari nimeshamjibu...binafsi siamini kwamba ameteuliwa kv tu yeye ni mzanzibar na mwanamke coz' Saada ni Mzanzibar na mwanamke since the day she was born, so kama hicho kingekuwa ndicho kigezo basi hata pale alipopewa unaibu waziri, angepewa uwaziri badala ya Mgimwa!

Duh! Hawezi kupata kazi hata TRA? Anyway, hata hivyo ina fahamika kwamba doesn't take qualification alone to be employed with TRA...hilo lipo wazi! Na kwa hakika ikiwa ni Saada mwenye Masters hawezi kupata kazi TRA wakati pale kuna wengi tu wenye kadgrii kamoja, basi hoja yangu tanguzili ina-reflect uhalisia.
 
Kuhusu Mgimwa kuna watu tuliona kuongelea weakness ya uteuzi wake, na watu wengine walisema labda influence ya Lukuvi ili saidia na pia kuna swali alilouliza akiwa Bungeni ikaonyesha "umahiri" maana yeye kasomea micro economics na watu labda waliona ange faa mtu wa Macro, kwa hiyo usifikirie kwampa watu wana personal iisue ya Saada. au Dini, maana kuna wakati watu wame msema Prof. ole Gabriel Katibu Mkuu wa Habari nk.
Kuhusu wewe kutoa ushauri ukiwa ni Teller tu, Manager alishindwa au hakuwa na hiyo idea. Kuna vitu in life vina hitaji General idea au akili ya kuzaliwa ambayo unayo ndio maana ukaweza kutoa ushauri, ni sawa sawa na Mimi ingawa si Dr lakini labda naweza kuongoza wizara ya afya kwa mfano, lakini likija suala la utaalamu la kumuhusu Dr nitakuwa nime tolewa knockout.
Sasa tukija wizara ya fedha, labda watu wana danganyika na jina Finance na kufikia knowledge inayotakiwa hapo ni ya Finance kama MB Finance and ze like.
Lakini ukweli wa mambo pale sehemu kubwa ni mambo ya uchumi could both Macro na micro economics na jinsi gani ya kuongeza revenue through it , investments zenye return , then mambo ya kodi, fedha na budgetary control.
Sasa kama wewe strength yako ipo kwenye Budgetary control, wakati tatizo kubwa la tz ni kwenye issue ya macro, micro economics na investment, na ndio maana unaona unemployment ipo kubwa, miundo mbinu mibovu, umeme hakuna nk nk
Sasa waziri mwenye kukosa muono kama huo au mwenye ku lack some expose, experience au uweledi katika mambo hayo huoni kwamba itakuwa ni minus ktk juhudi zetu za kuondoa umasikini? n.k
August, kwanza nianze kusema kwamba hilo la dini kwangu wala halina nafasi...alimradi siamini kwamba amechaguliwa kutokana na dini yake vilevile siwezi kudhani kwamba anakuwa attacked kutokana na dini yake! Hata hivyo, wala sitashangaa kuona kwamba wapo ambao wanamu-attack kwa ajili tu ya dini yake au uzanzibar wake! Kwangu mimi, huwa wala sipotezagi muda na watu kama hao na ndio maana hata hawa akina JokaKuu, Nguruvi3, Mchambuzi ambao najadiliana nao, wao hoja zao hazipo huko. Post yangu uliyo-quote, nilikuwa namjibu mtu ambae aliweka mbele suala la dini na ndio maana utaona hata majibu yangu yalikosa adabu kidogo coz' alinikera from the beginning alioanza na suala dini ya Mkuya!

Turudi kwenye mada! Kwanza nakubaliana na wewe kwamba tunahangaika na jina Wizara ya FEDHA wakati kinachohitajika sana hapo ni uchumi. Siku anateuliwa Mgimwa, nakumbuka mie hoja yangu pia ilijikita kwenye utaalamu wa Mgimwa(mambo ya fedha) na wizara ambayo niliona inahitaji sana mchumi kuliko mtaalamu wa mambo ya fedha! Hata hivyo, baadae nilipokuja kuchunguza CV za mawaziri wengi wa fedha wa miaka ya karibuni, nikagundua kwamba wengi ni wataalamu wa mambo ya fedha...nikadhani labda kuna kitu wenyewe wamekiona...labda wamegundua tatizo kuu lililpo wizarani ni financial management kuliko haya mambo mengine ambayo kila idara ina wataalamu wake. Lakini linapokuja suala la ku-manage finance, halihitaji mtalaamu mtalaamu mtendaji tu kama ilivyo kwenye upangaji sera bali linahitaji mtu mwenye uwezo wa kulifuatilia suala hilo...
 
Mnamwonea tu kwa vile ni Mzanzibari

Ndio maana yake..hizi ni nyakati za mwisho kuchukua hatamu katika Tanganyika..hebu nambie zenji wanachangia Pesa za hazina kiasi gani...Kama unamaanisha tunamchukia kwamba ni mzenji bora sisi tunaanza Hv Leo maana zenji mmeanza kuwachukia wa TAnganyika muda mrefu..what's goes around comes around ...you heard.?
 
Hana historia yoyote kuhusu performance.
Uwaziri ni nafasi ya kisiasa yenye maamuzi mazito kuhusu maisha yetu.

Hatuwezi kuonyesha kushindwa kwake kwasababu hajawahi kuwa katika nafasi ya kuonekana.

Kwa maneno mengine uzoefu wake ni hakuna katika nafasi nyeti na hivyo ni sawa na kutolea maelezo kitu kisichokuwepo.

Hajawahi kushika nafasi kubwa akiwa kiongozi, sijui tutawezaje kuongelea mapungufu yake ambayo hayapo ab intio.

Elimu yake imekuwa ya kificho sana. Haiwezekani web ya bunge iseme fulani ana sifa ABCD bila kutaja vyuo.Kwanini alikuwa anaficha vyuo alivyosoma.

Ni mchanga katika uongozi, siasa na hana chochote anachoweza kuweka mbele iwe publications au makala katika gazeti ambayo tunaweza kumuelewa au kutomuelewa.

Hatujui mchango wake ndani au nje ya bunge, hansard za bunge hazionyeshi kama aliwahi kutoa mchango unoweza kufikirisha akili za watu

Tunawasi wasi na uwezo wake wa kuwasiliana na wenzake katika nyanja za kimataifa
Tunashaka na uwezo wake katika kusimamia uchumi
Tunashaka na uwezo wake wa kushauriana na gavana wa benki kuu

Tuna mashaka kwa kila jambo lake, mashaka yasiyo na shaka hata kidogo.
Historia ya nchi hii inaonyesha ni waziri wa kwanza wa fedha aliyeteuliwa from nowhere with nothing on hand.

Ndugu yangu huyu hafai, sumu haijaribiwi kwa kuonja.
Mwisho wa majaribio yake ni maafa kwa maisha yetu.
Tuzuie hili janga. Msione aibu tuseme ukweli hana sifa. Period

Maneno mazito sana!
 
Mkuu NasDaz,
Awali nilikuuliza je unajua majukumu ya waziri wa fedha ni yepi? Jibu lako likaashiria moja kwa moja kwamba haujui kwani ukasema kwamba its a good question na umewasiliana na jamaa zako waliopo hazina ili wakupe job description, ambayo hadi sasa haujaileta; katika hali hii mkuu NasDaz, unamtetea mama yetu mpendwa kwamba anafaa kutekeleza majukumu yepi?hauoni kwamba kwa mapungufu haya peke yake hoja yako kumtetea inakosa mashiko?

Ukirejea mabandiko ya nyuma katika uzi huu, nilieleza general roles and responsibilities za waziri wa fedha katika mataifa mengi, na nikatumia such roles and responsibilities kuhoji iwapo mama yetu mpendwa anatosha au hatoshi;kwahiyo angalau binafsi nilikuja na maelezo yanayojitosheleza juu ya nini naamini ni majukuu ya waziri wa fedha na kwanini sidhani huyu mama anatosha;wewe mkuu hadi sasa unajenga hoja kwamba anafaa huku ukiwa bado unasubiri kupata majibu kutoka kwa wenzako hazina juu ya majukumu ya waziri wa fedha ni yepi;

Wadau wengi humu kama Nguruvi3, Kimweri, JokaKuu na wengine wanajenga hoja huku wakieleza nini wanaelewa juu ya majukumu ya waziri wa fedha ni yepi, wewe mkuu unapingana nao huku ukisubiria kupata majibu kwa jamaa zako hazina, je mkuu hauoni kuna tatizo hapo?

Ningependa nimalizie kwa maswali mengine makuu matatu:

Kwanza - je unajua moja ya sifa kuu muhimu kwa mujibu wa katiba za kuteuliwa uwaziri ni ipi? Nadhani unajua kwamba ni "mbunge"; je unajua kwanini katiba ilisema hivyo?

Pili, ni mawaziri wangapi katika historia ya nchi yetu waliteuliwa uwaziri moja kwa moja mara mara tu baada ya kushinda ubunge wa jimbo au kuteuliwa ubunge? Unajua kwanini?

Mwisho, rasimu mpya ya katiba inapendekeza kwamba mawaziri wasitokane tena na ubunge, je unajua ni kwanini
Mkuu Mchambuzi naona hunitendei haki manake hata wewe nilikupa changamoto ya kuleta hiyo kitu ili kunogesha mjadala baada ya kukuambia kwamba wengi wetu tunafahamu roles zake! Na ikiwa kumtetea kwangu kunakosa uhalali kwavile tu sijaweka hapa majukumu yake, basi hata nawe kupinga kwako kunakosa uhalali kwavile hujaweka hapa kazi zake na tukajiridhisha kwamba ni kweli, kwa majukumu haya, Saada Mkuya isn't fit for the position!! Don't rely on roles peke yake na kutoa hukumu coz' hizo roles zinafahamika.

Hata hivyo, ukitumia General Roles peke yake ambayo ni kusimamia sera za uchumi basi moja kwa moja ana-fit! Kinachohitajika zaidi kwenye kusimamia ni commitment. Commitment haipatikani darasani na hili ndilo tatizo kuu la nchi hii...people are not commited and responsible enough! Hili ndilo linafanya wasomi wetu wenye wasifu usio shaka, nao wanashindwa ku-deliver; coz' wana-miss kitu hiki cha msingi ambacho hakipatikani darasani!

tukirudi kwenye hoja yako tangulizi, in short, nimepata baadhi ya job responsibilities zake. Kutokana na ukweli na kwamba MoF ina idara mbalimbali zenye watalaamu kulingana na idara husika; kisha nikachukua elimu ya "Mama yangu Mpendwa" na uzoefu wake, am very certain she can deliver...nasubiri siku Mchambuzi&CO mtakapoziba nyuso zenu kwa kutumia viganja!
  • Huyu ndie msimamizi mkuu wa sera za uchumi! Kusimamia sera hakuhitaji mtu kuwa expert in solving complex economic models...panahitaji responsible and committed person hata kama hatupuuzi umuhimu wa elimu na uzoefu ambavyo "Mama Yangu Mpendwa" anavyo.
  • Huyu ndie anayeongoza majadiliano na mashirika ya kimataifa kv WB, IMF, ADB , DFID, SIDA, n.k! Naona kukutajia hayo mashirika ndo umeshaanza kutaharuki! Remember, yeye ndie anaongoza na si kwamba anafanya binafsi. Kuna team from MoF ambayo inakuwa nyuma yake. Ukumbuke kwamba wanaenda kwenye majadiliano kwa mtindo wa maswali ya papo kwa papo ya PM bali wanajadili sera zetu wenyewe! Wanaenda pale wakiwa wameshajiandaa huku wakiwa wanafamu wanaenda kujadili nini! Kikubwa kinachohitajika mezani ni how to defend! Kwa kuzingatia kipindi nilichomuona akiwa bungeni, "Mama yangu Mpendwa" ana uwezo huo!
  • Huyu ndie msimamizi wa taasisi za fedha nchini including commercial banks.
Huyu bwana aliyenipa haya yupo busy na safari; sijui wanaenda wapi sijui...kwahiyo haidhuru ukiongezea mengine tuyajadili.

Nirudi kwenye maswali yako! Kwanini katiba imetaka waziri awe mbunge! Sidhani kama naweza kuwa na jibu la swali hili hasa ukizingatia mie sio mtalaamu wa masuala la katiba na sidhani kama katiba yenyewe imesema WHY!

Kuhusu ni mawaziri wangapi waliteuliwa moja kwa moja uwaziri baada ya kupata ubunge! Hivi unadhani ni rahisi kujibu hilo swali hasa ukizingatia kwamba ni ngumu kuwa na written document ambayo imetaja mawaziri wote tangu uhuru na kutaja siku wamepata ubunge na siku waliteuliwa? Anyway, it's possible ikiwa mtu ameanza kufuatilia siasa since then lakini kwa akina sisi ambao tumeanza from miaka ya karibuni, i guess ni kazi ngumu kutaja! Binafsi nawakumbuka sana mawaziri wa JK na wachache wa Mkapa hususani wale ambao walikumbwa na scandals kama akina Mbilinyi, Yona, Mramba n.k! Lakini kama shida ni idadi yoyote, basi ni Muhongo na Saada Mkuya.

Kwamba rasimu mpya inataka mawaziri wasiwe wabunge na kwanini, hapo hakuna jibu la moja kwa moja...kwani ni maoni ya watu na kila mmoja ana sababu yake! Mathalani, wabunge wao wanaona mawaziri ambao ni wabunge wanatumia nafasi ya uwaziri wao kujiependelea kwenye majimbo yao! Wapo wanaodai kwamba wanaingiza political interests za chama.
 
Last edited by a moderator:
Huyu mdada haha cv nyingine zaidi ya kumjua jk, darasa lenyewe la Saba aliungaunga tunao mjua tulishanga kusikia amemaliza form four
Prof LIPUMBA

View attachment 135021

Waziri wa fedha amjibu Prof. Lipumba

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba, amelishushia tuhuma nzito Baraza la Mawaziri, baada ya kudai baadhi ya mawaziri walioteuliwa hawana elimu ya kutosha.

View attachment 135020
Waziri wa Fedha, Saada Mkuya

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana, Profesa Lipumba alisema mmoja wa mawaziri hao ni Waziri wa Fedha, Saada Mkuya.

Alisema chama chake, kina wasiwasi na elimu ya Waziri Mkuya, kutokana na wasifu wake kutoonyesha vyuo alivyosoma wakati wa kupata shahada ya kwanza na ya pili katika masuala ya biashara.

Alisema katika tovuti ya Bunge, wasifu wa waziri huyo umeonyesha sehemu aliyosoma elimu ya sekondari na kuhitimu kidato cha sita.

Alisema katika tovuti hiyo, haionyeshi chuo alichosoma shahada ya kwanza ya biashara, ingawa inaonyesha masomo aliyochukua jambo ambalo linatia mashaka uhalali wake kuongoza wizara hiyo nyeti.

“Ukiingia kwenye tovuti ya Bunge, utaona wasifu wake kuanzia elimu ya msingi hadi kidato cha sita na shule alizosoma, lakini kuanzia elimu ya shahada imeonyesha masomo aliyochukua na kupata shahada ya kwanza ya biashara, haionyeshi vyuo, jambo ambalo linatia mashaka,” alisema Lipumba.

Alisema nafasi aliyopewa inahitaji kiongozi mwenye upeo wa hali ya juu, kuweza kupambanua mambo yanayohusu uchumi wa nchi kwa kushirikiana na taasisi mbalimbali za kifedha za ndani na nje ya nchi.

“Napata wasiwasi kama Rais Jakaya Kikwete, aliangalia wasifu wa waziri wake kwa sababu asingeweza kumchagua kushika nafasi kubwa kama hii, wakati vyeti vyake vina mashaka,” aliongeza.

Alisema kitendo cha kumuweka mtu mwenye vyeti vya mashaka, kunaweza kusababisha nchi kuyumba kiuchumi, kuongezeka kwa deni la taifa, kwa sababu uamuzi wake unatokana na ufahamu wake.

WAZIRI AJIBU

Akizungumza na MTANZANIA Jumatatu kuhusu madai hayo, Waziri Mkuya alisema elimu yake wala haina mashaka, kwani alisoma kidato cha tano na sita katika Shule ya Sekondari Lumumba mjini Zanzibar.

Baada ya hapo, alijiunga na masomo ya diploma ya Biashara katika Chuo cha Stamford cha Malaysia, ambapo pia alichukua diploma nyingine ya biashara nchini Uingereza.

Alisema mbali na masomo hayo, pia amesoma shahada ya pili ya biashara katika Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT) na kuhitimu mwaka 2009.
“Nimehitimu Shahada ya Uzamili ya Utawala na Biashara (MBA) ya Chuo Kikuu cha WATT kilichopo Edinburgh, Scotland.

“Kwa sasa nachukua Shahada ya Uzamivu (PhD) ya Utawala wa Biashara Chuo Kikuu Huria cha Tanzania, tawi la Dar es Salaam,” alisema Mkuya.

source: darnewsline.blogspot.com
 
Mkuu Mchambuzi naona hunitendei haki manake hata wewe nilikupa changamoto ya kuleta hiyo kitu ili kunogesha mjadala baada ya kukuambia kwamba wengi wetu tunafahamu roles zake! Na ikiwa kumtetea kwangu kunakosa uhalali kwavile tu sijaweka hapa majukumu yake, basi hata nawe kupinga kwako kunakosa uhalali kwavile hujaweka hapa kazi zake na tukajiridhisha kwamba ni kweli, kwa majukumu haya, Saada Mkuya isn't fit for the position!! Don't rely on roles peke yake na kutoa hukumu coz' hizo roles zinafahamika.

Hata hivyo, ukitumia General Roles peke yake ambayo ni kusimamia sera za uchumi basi moja kwa moja ana-fit! Kinachohitajika zaidi kwenye kusimamia ni commitment. Commitment haipatikani darasani na hili ndilo tatizo kuu la nchi hii...people are not commited and responsible enough! Hili ndilo linafanya wasomi wetu wenye wasifu usio shaka, nao wanashindwa ku-deliver; coz' wana-miss kitu hiki cha msingi ambacho hakipatikani darasani!

tukirudi kwenye hoja yako tangulizi, in short, nimepata baadhi ya job responsibilities zake. Kutokana na ukweli na kwamba MoF ina idara mbalimbali zenye watalaamu kulingana na idara husika; kisha nikachukua elimu ya "Mama yangu Mpendwa" na uzoefu wake, am very certain she can deliver...nasubiri siku Mchambuzi&CO mtakapoziba nyuso zenu kwa kutumia viganja!
  • Huyu ndie msimamizi mkuu wa sera za uchumi! Kusimamia sera hakuhitaji mtu kuwa expert in solving complex economic models...panahitaji responsible and committed person hata kama hatupuuzi umuhimu wa elimu na uzoefu ambavyo "Mama Yangu Mpendwa" anavyo.
  • Huyu ndie anayeongoza majadiliano na mashirika ya kimataifa kv WB, IMF, ADB , DFID, SIDA, n.k! Naona kukutajia hayo mashirika ndo umeshaanza kutaharuki! Remember, yeye ndie anaongoza na si kwamba anafanya binafsi. Kuna team from MoF ambayo inakuwa nyuma yake. Ukumbuke kwamba wanaenda kwenye majadiliano kwa mtindo wa maswali ya papo kwa papo ya PM bali wanajadili sera zetu wenyewe! Wanaenda pale wakiwa wameshajiandaa huku wakiwa wanafamu wanaenda kujadili nini! Kikubwa kinachohitajika mezani ni how to defend! Kwa kuzingatia kipindi nilichomuona akiwa bungeni, "Mama yangu Mpendwa" ana uwezo huo!
  • Huyu ndie msimamizi wa taasisi za fedha nchini including commercial banks.
Huyu bwana aliyenipa haya yupo busy na safari; sijui wanaenda wapi sijui...kwahiyo haidhuru ukiongezea mengine tuyajadili.

Nirudi kwenye maswali yako! Kwanini katiba imetaka waziri awe mbunge! Sidhani kama naweza kuwa na jibu la swali hili hasa ukizingatia mie sio mtalaamu wa masuala la katiba na sidhani kama katiba yenyewe imesema WHY!

Kuhusu ni mawaziri wangapi waliteuliwa moja kwa moja uwaziri baada ya kupata ubunge! Hivi unadhani ni rahisi kujibu hilo swali hasa ukizingatia kwamba ni ngumu kuwa na written document ambayo imetaja mawaziri wote tangu uhuru na kutaja siku wamepata ubunge na siku waliteuliwa? Anyway, it's possible ikiwa mtu ameanza kufuatilia siasa since then lakini kwa akina sisi ambao tumeanza from miaka ya karibuni, i guess ni kazi ngumu kutaja! Binafsi nawakumbuka sana mawaziri wa JK na wachache wa Mkapa hususani wale ambao walikumbwa na scandals kama akina Mbilinyi, Yona, Mramba n.k! Lakini kama shida ni idadi yoyote, basi ni Muhongo na Saada Mkuya.

Kwamba rasimu mpya inataka mawaziri wasiwe wabunge na kwanini, hapo hakuna jibu la moja kwa moja...kwani ni maoni ya watu na kila mmoja ana sababu yake! Mathalani, wabunge wao wanaona mawaziri ambao ni wabunge wanatumia nafasi ya uwaziri wao kujiependelea kwenye majimbo yao! Wapo wanaodai kwamba wanaingiza political interests za chama.

Mkuu NasDaz,

Ni dhahiri kwamba majibu yako nadhani post no 407 juu ya majukumu yalikuwa ya jumla jumla na ya assumptions, tafadhali rudi ukajisome uone mwenyewe kama kweli nimekuonea mkuu;

Kuhusu mimi kutokuja na understanding of this role, sio kweli, nisome bandiko nadhani namba 84 au 184, sikumbuki na natumia simu so can't tell u for sure;

Vinginevyo hoja yako kwamba ipo siku tutakuja ficha nyuso zetu mama yetu aki deliver ni ushahidi tosha kwamba kateuliwa kujaribiwa na sio kutenda; kwa maana nyingine, unajaribu kutetea mfumo wa kuteua watu kwa kuwajaribu na sio kwa uhakika juu ya uwezo wao;

Nitarejea hoja zako nyingine baadae;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi kwamba ama tupeane darsa kidogo au tukumbushane kwamba unapotaja post No, anza na ile # sign ambayo uki-click moja kwa moja itakupeleka kwenye post kusudiwa....Post #407 , #84 , #184 . Nimelazimika ku-rewrite hapa ili nikipata wasaa nikazitupie macho!

Kwamba mtaficha sura kwa viganja vya mikono ndo iwe ushahidi tosha kwamba mama yetu aenda kujaribiwa, kikwetu hiyo inaitwa hoja lazimishi...na aghalabu, hoja lazimishi zinakuja pale hoja za msingi zinapokuwa hazipo; kwahiyo muhusika atalazimisha hoja hii ama ile alimradi tu kutegeshea na kusikilizia kwa chati kuangalia endapo hii ya sasa itapita!! Mama yetu Saada Mkuya hajapelekwa MoF kujaribiwa but she deserves to be there...lakini kwavile kuna kizazi cha Tomaso cha akina Mchambuzi, JokaKuu, Nguruvi3, basi nyie stahiki ni hadi pale Bwana Yesu atakapowatokea rasmi na kuwaonesha viganja vyake vya mkono huku akiwaambia: :"Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo."

"
 
Mkuu, naelewa umuhimu wa hash key, simu inasumbua, nipo mbali kidogo vijijino ndio maana response yangu inategemeana sana na simu;niwie radhi kwa mapungufu ya hapa na pale, nakusoma na ntakurudia hoja kwa hoja;

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Last edited by a moderator:
Mkuu Mchambuzi kwamba ama tupeane darsa kidogo au tukumbushane kwamba unapotaja post No, anza na ile # sign ambayo uki-click moja kwa moja itakupeleka kwenye post kusudiwa....Post #407 , #84 , #184 . Nimelazimika ku-rewrite hapa ili nikipata wasaa nikazitupie macho!

Kwamba mtaficha sura kwa viganja vya mikono ndo iwe ushahidi tosha kwamba mama yetu aenda kujaribiwa, kikwetu hiyo inaitwa hoja lazimishi...na aghalabu, hoja lazimishi zinakuja pale hoja za msingi zinapokuwa hazipo; kwahiyo muhusika atalazimisha hoja hii ama ile alimradi tu kutegeshea na kusikilizia kwa chati kuangalia endapo hii ya sasa itapita!! Mama yetu Saada Mkuya hajapelekwa MoF kujaribiwa but she deserves to be there...lakini kwavile kuna kizazi cha Tomaso cha akina Mchambuzi, JokaKuu, Nguruvi3, basi nyie stahiki ni hadi pale Bwana Yesu atakapowatokea rasmi na kuwaonesha viganja vyake vya mkono huku akiwaambia: :"Angalieni mikono na miguu yangu, ya kwamba ni mimi mwenyewe. Nipapaseni mkanione, maana mzimu hauna mwili na mifupa kama mnionavyo.""
Nilitegemea tungepata maelezo ili U-tomaso ututoke, naona hakuna isipokuwa tunalazimishwa kuambiwa 'she deserves to be there'

Tunaambiwa tusubiri hadi amalize muda wake kwanza ili tuweze kumtathmini.
Kwamba tkjubali operesheni ya tumbo ifanywe na mhasibu kwakuwa mwisho wa operesheni tutajua kama tumepona au la.
Tunaambiwa hata tukifa hakuna shida mbona Havard na Muhimbili wanapasuliwa na kufa?

Hatuonyeshwi track record ya mama Mpendwa.
Nimepitia mahali mara moja kutafuta wasifu wa Benno Ndulu wa BoT, kitu nilichokutana nacho ni jinsi alivyosimamia uanzishwaji wa consortium ya uchumi Afrika.
Ni jinsi alivyoshiriki katika kuamsha uchumi wakati wa Mkapa na jinsi alivyoshihiriki katika mashirika ya kimataifa achilia mbali publications n.k.

Nikiangalia CV ya mama upande wa elimu naona sekondari maana vyuo alificha.
Nikiangalia executive role sioni mahali ninapoweza kusema anaweza kusimamia 'Fortune 500' kama alivyosema Kimweri. Nikiangalia uzoefu naona ni miezi 18.

Naangalia ukubwa wa dude alilobeba na kubaki na utomaso. Mbona size ya mguu wake ni 5 lakini amevaa viatu size 11?

Jamani mimi Tomaso, naomba mnishawishi kwa hoja mama mpendwa ameingia wizara ya fedha akiwa na nini mkononi?

Tunajua akiondoka atakuwa na kitu ambacho ni uwaziri wa fedha, je ameingia na nini kinacholingana au kuzidi atakachoondoka nacho?

sad sad sad ! but anyways, she has atleast 2 budget terms before we get rid of these jokers in the name of ministers, I hope constitution review will entail transparent process in further nomination for ministerial position, we can pick a leaf from our Kenyan neighbours:angry:
 
Back
Top Bottom