Waziri wa Fedha amjibu Prof. Lipumba

Waziri wa Fedha amjibu Prof. Lipumba

Mim ninafikiri hii nchi imekwisha na sababu ni soga na kiherehere tu. people are not working ni kushauri na kuingia kwenye mitandao kutafuta elimu za wengine! Niambie mtu mwenye duka lake, mtu mwenye kakiwanda kake na wengine wa namna hii hwana nafasi ya kuanza kuwaongelea watu ambao wameteuliwa sasa na hawana hata week 2 ofisini! We have to be fair! Huyu mama muacha achape kazi ndiyo maana kuna wasaidizi wake hii ni pamoja na PS na Junior minister etc! Kazi itafanyika tu wewe let us give her time na mtaona tu! Mimi ninaona kuna na kawivu tu!!!!!!!!!!!!!!!!!

Bila shaka ni mnufaika wa uteuzi wa kipuuzi kiasi hiki.
 
Kumbe nilikuwa na kila sababu ya kupuuza habari ile. Ina maana source ya Lipumba ilikuwa Tovuti ya Bunge na si kwamba alifanya utafiti na kugundua bi mdada elimu yake ni full magumashi?
NasDaz,

..kwa CV hiyo ha-qualify kuwa waziri wa fedha.

..hebu angalie CV za mawaziri wa fedha wa nchi zinazofanya vizuri kama Botswana, Ghana, Mauritius, etc.

..wizara ya fedha siyo mahali pa kumuweka mtu ambaye siyo mzito ktk taaluma ya uchumi, mabenki,au fedha.

..hata Manaibu waziri ktk wizara ya fedha wanatakiwa wawe na utaalamu na uzoefu ktk sekta wanazosimamia.

..hebu angalia CV ya Seth Tekper waziri wa fedha wa Ghana:
GhanaWeb, Validation Error

..angalia wasifu wa Xavier-Luck Duval waziri wa fedha wa Mauritius:
Xavier-Luc Duval - Wikipedia, the free encyclopedia

cc Mchambuzi, Ogah, Sikonge,
 
Watu mnalalamika nini sasa? Yaani ni kama vile hamumjui Kikwete?

Mtu gani mwenye akili timamu anaweza kumteua mtu kama Mwigulu Nchemba?

Huyu huyu rais alimteua Mulugo kuwa naibu waziri. Huyu huyu rais kamteua Jenista Mhagama kuwa naibu waziri.

Huyu huyu rais kawahi kusema hajui kwa nini Tanzania ni maskini.

Nawaonea huruma mliompigia kura mwaka 2005 na mliokuwa na matumaini ya maisha bora kwa kila Mtanzania kwa hisani ya nguvu mpya, ari mpya, na kasi mpya.
 
Minister of finance is the second most important cabinet post after the Prime Minister. Waziri wa fedha ni architect (kwenye level ya baraza la mawaziri) wa financial & budgetary policy of a nation. Kwa maana hii, waziri wa fedha anatakiwa kuwa ni mtu ambae ni well trained katika masuala ya uchumi au yanayofanania, tena from a reputable institution. In addition, waziri wa fedha anatakiwa awe na proven track record and achievements katika kusimamia masuala ya fedha in public or private sector. Hoja kwamba tumewahi kuwa na mawaziri wenye vigezo hivi lakini they didn't perform ni 'self defeating' kwani ni suala lililo wazi kwamba utendaji wa wizara ya fedha na hata benki kuu always umekuwa undermined na political interefence .

Mama yetu sio tu kwamba hana sifa na vigezo vya hapo juu kumfanya atoshe kuwa waziri wa fedha katika uchumi kama wa Tanzania, uchumi ambao unakimbilia kuwa kumi bora as fastest growing economies duniani, bali pia hana experience ya kuitwa "waziri mwandamizi" suala ambalo pengine lingemsaidia kufikiriwa "on merit".

Wengi ya wanaoshabikia uteuzi huu ni watu wenye mtazamo kwamba kuteuliwa uwaziri ni "kuula" na sio kwenda "kutumikia wananchi" kwa vigezo vya elimu na uzoefu. Na kwa vile mjadala husika umetawaliwa zaidi na akili za kuteuliwa uwaziri ni "kuula", wachache wenye hoja tofauti hawawezi kueleweka.

As an architect of budgetary and financial policies wa taifa letu on the cabinet level, waziri wa fedha anawajibika moja kwa moja na uchumi wa nchi nzima kwa maana ya kwamba kuwa na uwezo wa ku identify vipaumbele vya taifa na kwenda kuvijengea hoja kwenye cabinet level hivyo kuwa in charge of government finance, fiscal policy, financial regulations etc. Vile vile kwa nchi kama yetu ambayo haina a truly independent central bank, waziri wa fedha also "has oversight of monetary policy", hivyo hata Gavana wa BOT, Professor wa Uchumi anayetambulika duniani Benno Ndullu ( a Berkeley PhD holder) hana powers kumzidi huyu mama hata katika suala la monetary policies. Given all this, seriously watanzania wenzangu, kweli one to two years experience ya unaibu waziri makes her fit for the job? Hivi kweli mamlaka ya uteuzi ilikosa wengine wenye sifa zaidi? Hivi kweli ingekuwa mawaziri hawatokani na wabunge na huyu mama ange apply for the post angekuwa hata short listed for an interview? Sidhani.

It will remain a fact kwamba huu uteuzi ni wa kisiasa zaidi - politics of gender, the union (kuelekea bunge la katiba), or both, kwani ni vigumu kutushawishi kwaba uteuzi una uhusiano wowote na kutafuta mtu makini ambae atasimamia kikamilifu sera zetu za uchumi katika kipindi hiki kigumu. Hakuna mjadala kwaba she's on job training na tusije shangaa ziara zake to the IMF and World Bank Washington zikishindwa kuzaa matunda, na haitakuwa ajabu kusikia wamemsusia kwani she clearly lacks substance.

Kwa kawaida, taifa lolote lile duniani uchumi wake huwa uhathirika sana na chaguzi kuu. Kwa waziri tulienae, athari za uchaguzi mkuu wa 2015 kwa wananchi walio wengi zitakuwa kubwa kwa kiwango ambacho hakijawahi kutokea.

But again, kwa walio wengi, uteuzi huu ni "kuula", and any criticisms zinakuwa labeled as wivu kwani wajenga hoja husika hawana weledi wa kutofautisha baina ya kazi ya umma na maisha binafsi. Kuelekea 2015 chini ya waziri husika, kilichobakia kwa wananchi walio wengi hakuna kingine bali kusubiri tu "kula wa chuya".



Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Hebu tujiulize, wakati wenzetu wanateua kina Nobel Laureattes wa uchumi as treasury secretaries sie tunamuweka mtu aliyeshindwa kwenda University through Direct entry. Seriously???
Some people just don't grasp how hard The mathematics in Economic theories are, they are the kind of Maths Engineers avoid, leo hii unampeleka bidada wa style hii kweli? sasa huyu akikutana na Kina Jacob Lew wataongea nini?si atabaki kushangaa tu huyu?

Waziri wa fedha ni kama CFO wa nchi, kuna standards anazotakiwa kuwa nazo, ndio maana kwenye private sectors unaambiwa huwezi kuwa CFO mpaka uwe na CPA etc etc,wanafahamu umuhimu wa hivi vitu.Huwezi kumuweka mtu aliyeunga unga diploma kuwa CFO wa a bilion dollar company. Tanzania tuna GDP ya 20-30 Billion, so most likely we are a very complex $20B company, how can this company finances be put on the hands of such a person?

One of the real tests for her and Mr Nchemba would be how both of them will be able to attend, present and carry on series of technical/intelligent conversations or meetings or even presentations with the likes of Christina LaGarde, Jim Yong Kim, Jacob Leuw or even their Kenyan counterparts.
I have nothing against this lady, but her resume and experience are too shallow to make her a Treasury Sec/Minister of Finance of any country. She would be a good fit for other cabinet posts but not Treasury/Finance.
I'm pretty sure that even Mr Kikwete knows this very well.
 
Lakini, hebu tujaribu kutenda haki katika kukosoa kwetu.

Hivi, kwani kuongoza hiyo wizara waziri anatakiwa awe na sifa gani?

Hizo sifa zimeorodheshwa sehemu? Nani anazijua?

Na kabla hajawa waziri kamili huyu mama si alikuwa naibu waziri?

Sasa ina maana kwenye hiyo nafasi ya unaibu waziri hakupata uzoefu wowote?

Na kwani ili mtu awe mtendaji mzuri wa kazi ni lazima awe na mashahada yenye maherufi ya kutisha tisha?

Na je, kuwa na mashahada lukuki ni sawa na utendaji bora?

Wangapi wenye mishahada lukuki tena mikubwa mikubwa lakini utendaji wao ni mbovu?

Hiyo wizara si ilishawahi kuongozwa na profesa? Huyo profesa alifanya maajabu gani hapo wizarani?

Na mawaziri wote (mpaka sasa) ambao wamewahi kuongoza hiyo wizara, wote walikuwa na mashahada mengi ya chuo kikuu?
 
Lakini, hebu tujaribu kutenda haki katika kukosoa kwetu.

Hivi, kwani kuongoza hiyo wizara waziri anatakiwa awe na sifa gani?

Hizo sifa zimeorodheshwa sehemu? Nani anazijua?

Na kabla hajawa waziri kamili huyu mama si alikuwa naibu waziri?

Sasa ina maana kwenye hiyo nafasi ya unaibu waziri hakupata uzoefu wowote?

Na kwani ili mtu awe mtendaji mzuri wa kazi ni lazima awe na mashahada yenye maherufi ya kutisha tisha?

Na je, kuwa na mashahada lukuki ni sawa na utendaji bora?

Wangapi wenye mishahada lukuki tena mikubwa mikubwa lakini utendaji wao ni mbovu?

Hiyo wizara si ilishawahi kuongozwa na profesa? Huyo profesa alifanya maajabu gani hapo wizarani?

Na mawaziri wote (mpaka sasa) ambao wamewahi kuongoza hiyo wizara, wote walikuwa na mashahada mengi ya chuo kikuu?

umeongea la maana, huyo njemba hapo magogoni wanajesshi na polisi wasingejiwekea taratibu zao kuna siku angetuwekea IGP, koplo na CDF angemnyofoa captain mmoja pale makao makuu. halafu kuna vichwa maji humu wangemtetea kuwa hizo nafasi hazihitaji ujuzi, uzoefu na weledi wa kutosha.

wakati wenzetu wanapeleka chumi zao kwenye hatua nyengine, sisi tunacheza makida makida na kufanya upatu na mambo ya msingi kabisa.
 
Lakini, hebu tujaribu kutenda haki katika kukosoa kwetu.

Ni haki kwa kila mmoja wetu kukosoa pale palipo na walakini.

Hivi, kwani kuongoza hiyo wizara waziri anatakiwa awe na sifa gani?
Kwanza unatakiwa uwe mchumi na mwenye shahada ya uchumi kutoka chuo kikuu ambapo ulikaa kwa miaka mitatu

Pili, uwe na uzoefu wa masuala ya uchumi na fedha kwa ujumla na mara nyingi unaanzia kazi Benki kuu au hazina moja kwa moja baada ya kupita usaili pale BOT au Hazina penyewe.

Na sifa zingine kama za kufahamu masuala ya ukaguzi wa ndani na nje na masuala yoote ya uchumi na fedha kwa ujumla.

Nne, mbunge wa kuchaguliwa na pia uwe mjumbe wa kamati mbalimbali za uchumi na fedha za bunge.

Hizo sifa zimeorodheshwa sehemu? Nani anazijua?

Sifa hizo zipo ofisi ya raisi na ni yeye ambae hupitia sifa hizo ingawa huweza kuziweka pembeni kutokana na maslahi fulanifulani. Sifa hizo zinaweza kuwa zipo sehemu zingine ambazo mhusika amewahi kufanya kazi na kuwa na rekodi kabisa ya performance yake, na ni rekodi hiyo ndio inayotakiwa mahali popote pale inapotokea unahitajika.

Na kabla hajawa waziri kamili huyu mama si alikuwa naibu waziri?

Ndio lakini jambo la kodi ya SIM card ni yeye aliekuwa na task ya kuhakikisha linapitishwa ili serikali ipate fedha za haraka haraka kutokana na kukosekana pesa ya kujiendesha, hivyo kuendelea kumwangamiza mwananchi wa kawaida na wachuuzi wa hizo SIM cards.

Sasa ina maana kwenye hiyo nafasi ya unaibu waziri hakupata uzoefu wowote?

Hakuwa na majukumu mengi zaidi ya kuandaa taarifa na kumsaidia alekuwa waziri marehemu Mgimwa ambae alikuwa ni nguli wa masuala ya uchumi na fedha na hata WB na IMF walimtambua.

Na kwani ili mtu awe mtendaji mzuri wa kazi ni lazima awe na mashahada yenye maherufi ya kutisha tisha?

Cha msingi ni shahada ya kwanza hasa ya uchumi, na iwe ya daraja la kwanza, pili uwe na shahada ya uzamili na mara nyingi pale Mlimani wanakuwa wanafahamu ni nani anafaa kwenda hazina. Kama una shahada za nje basi usaili wako utafanyiwa upembuzi yakinifu.

Na je, kuwa na mashahada lukuki ni sawa na utendaji bora?

Kama alivyosema mkuu Mchambuzi mara nyingi utendaji bora huingiliwa na siasa na matokeo yake ni kuharibu uchumi na kusababisha mifumuko ya bei na kupandd kwa gharama za maisha. Marehemu profesa kighoma malima alileta VAT na akaanzisha TRA ambayo tunaiona leo hii ni ishara ya kwamba aliona mbali kwamba ni lazima tuwe na chombo maalum cha kukusanya kodi.

Nae Profesa Simon Mbilinyi alikuja na masuala mbalimbali likiwemo la kodi kubwa kwa bia zinazotoka nje ya Afrika, ingawa kuna watu wakaja kuendeleza urafiki na wafanya biashara.

Wangapi wenye mishahada lukuki tena mikubwa mikubwa lakini utendaji wao ni mbovu?

Kwa serikali hii hao ni wengi na tumeona jinsi wanavyoboronga na kuendelea kuweka watu kwa visingizio vya usawa au mengine ni hatari.Mbona hata Kinana alisema kwamba kuna mawaziri mizigo humo?

Hiyo wizara si ilishawahi kuongozwa na profesa? Huyo profesa alifanya maajabu gani hapo wizarani?

Nimeeleza hapo juu

Na mawaziri wote (mpaka sasa) ambao wamewahi kuongoza hiyo wizara, wote walikuwa na mashahada mengi ya chuo kikuu?

Bila shaka, kuanzia Cleopa Msuya, Edwin Mtei, Kighoma Malima (marehemu) Simon Mbilinyi na Dr Mgimwa (marehemu) na wengine wenye ilm hasa ya uchumi na fedha au fwedha.
 
Hii wizara hata JK mwenyewe aliiongoza,kigezo kikubwa ni ukada,period.Ingekuwa ni kazi walizofanya,je JK alifanya nini hapo,wizara ya mambo ya nje je?
 
Kuna mengi ya kujiuliza kwa kinachoendelea nchini kwetu na huu mjadala ni matokeo ya hayo ya kujiuliza. Naungana na wengi hasa uchambuzi wa Mchambuzi juu ya dhima na majukumu ya Waziri wa Fedha vs sifa za mteule. Jibu la haraka lisilo na chembe ya kumung'unya ni kwamba kwa Wizara hiyo tungehitaji mtu mwenye sifa zaidi ya hizo. Lakini maswali ya msingi ni hayo alokuja nayo Nyani Ngabu. Mfumo wetu umeiweka Wizara ya Fedha kama Wizara nyingine tu kwamba Rais anaweza kuteua mtu yeyote as far as she or he's in favour with President, then anataeuliwa.

Kwa upande wa pili, tukiri kwamba kuanguka kwa wasomi wetu katika kusimamia kile wanachokijua kutokana na taaluma walizonazo ni swali jengine ambalo linatupeleka kwenye "bora liwalo". Mchambuzi umekuja na wasifu wa chuo wa Gavana wetu, kwamba na graduate wa UCB, moja kati ya vyuo vinavyoheshimika sana kwenye nyanja ya Uchumi. Lakini tuangalie uhalisia wa UCB na deliverance ya Ndullu. Tukiacha masuala ya kisera kwa kisingizio kwamba ni ya Wizara ya Fedha na Ikulu (kwamba kuna interest zao); je vipi kwenye masuala madogo ya kusimamia sheria zilizopo za Benki Kuu. Ni kweli kwamba Ndullu hajui kuziondosha sarafu za shilingi 1, 5, 10, 20 katika mzunguko bila sababu maalum ni kutengeneza "currency-price surge"? Hajui kwamba udhibiti dhaifu kwenye matumizi ya Dola ni kujipunguzia uwezo wa kudhibiti mzunguko wa fedha? Haya ni baadhi ya mambo madogo ambayo mchumi huyu wa UCB anatuangusha hali inayowafanya baadhi ya watu wahoji umuhimu wa maprofesa katika ujenzi wa nchi yetu.

Ingawa "wasomi wabovu" si utetezi wa hoja hii, lakini mimi naamini kwa nature ya Nchi yetu, hata mwenye Advanced Diploma ya CBE anaweza kuwa Waziri wa Fedha na akitaka anaweza kudelever, matokeo mazuri ya Wizara ya Fedha "yetu" hayahitaji uzoefu wala elimu kubwa. Ni kuwa jasiri wa kuzuia interest za watu (wanasiasa na wafanyabiashara wakubwa) kupitia misamaha ya kodi, ukusanyaji wa kodi, na upanuaji wa vyanzo vya Kodi. Haya hayaitaji waziri kuwa na taaluma ya 'financial derivation models' katika Wizara ambayo ina watendaji wataaluma wazuri. Waziri wetu hatuhitaji mtu wa kuletewa proposal za kukidhi interest za watu kwa kusubiri document nzuri zilizoandikwa na kusanifiwa. Asimamie makusanyo ya Kodi na Awe mkali kwenye kugawa fedha kwa kufuata vipaumbele ambavyo vitachochea sekta nyinginezo za Uchumi.

Lakini kwa upande mwingine tena, nadhani tuna tatizo na "system" yetu ya Ikulu kama ilivyo. Kwa yeyote atakayeingia 2015, itabidi ajitahidi kwa kiasi kikubwa kuifumua. Kuna kila dalili kwamba wanatumia mwanya wa "Undergraduate merit" ya Rais kumshauri vitu vibovu kwa makusudi ili waendelee kufaidika na Interest zao. Haiwezekani kwa System nzuri inayojua kiwango cha elimu cha Mkuu, then wakamshauri ateue waziri Mkuu mwenye kiwango alichonacho. Hii ni big failure; vyovyote iwavyo, uwezo wa undergraduate level ni mdogo sana kuelewa mantiki ya ushauri. Kuna tofauti kubwa sana baina ya viwango hivi viwili vya elimu(kwa wale waliobahatika kupata elimu bora ya ngazi hizo). Ni system hii hii imetoa ushauri wa kuteuliwa Naibu waziri wa elimu mwenye taaluma isiyotofautiana na aliyemtangulia ambaye amelalamikiwa kutokana na uwezo wake kitaaluma. Haiwezekani, haya si makosa ya Rais. Tuna tatizo la kulinda interest za watu.

Mwisho nimshauri Waziri Mteule, kazi yake ameanza vibaya kwa watu kuuliza kiwango chake cha utaaluma na uzoefu. Jibu rahisi kwake ni kuwaambia wanaohoji wamuulize aliyemteua ndio mwenye majibu. Kwa vile amejibu tena amejibu vibaya, anatakiwa afe kifo cha kishujaa (Kwani kifo cha underperformance Wizara yetu ya fedha ni lazima). (1) Akubali kuondoa/kuua interest za wakubwa; (2) Aachane na traditional sources of revenue kwa kuwaambia wataalamu wake wamletee vyanzo vipya na predictable vya mapato (3) Afute misamha ya Kodi bila kuogopa kelele za watu kwani haohao wanaopiga kelele pindipo misamaha iikifutwa ndio haohao wanaokuja kulalama uwezo mdogo wa Wizara ya Fedha. (4) Awapange TRA kukusanya mapato halisi, ikibidi hata aweke "jeshi lake la uhakiki". TRA hawakusanyi mapato, wanajikusanyia mapato hili liko wazi kabisa (aachane na wahindi wanaomanipulate EFD kifedha na system na badala yake zisambazwe kwa wafanyabiashara kwa bei rahisi) . Hakuna namna yoyote inayomfanya afisa mwenye miaka 3 ya Kazi kumiliki utajiri wa zaidi ya mil.200.

Kinyume cha kuwa mkali katika haya, muda mfupi ujao hapa tutarudi na ku-prove habari hii kwamba uteuzi wake ni "hidden agenda".
 
Kuna tetesi mtaani kuwa Mgimwa hakufa natural death. Kwa uteuzi uliofanyika wizara ya fedha, unaweza ukaamini hizi tetesi.
 
Ni haki kwa kila mmoja wetu kukosoa pale palipo na walakini.

Sawa, kukosoa ni haki ya yeyote yule lakini pia, ukosoo wenyewe wapaswa uwe wa haki basi. Na si kukosoa tu ili mradi mtu umekosoa.

Kwanza unatakiwa uwe mchumi na mwenye shahada ya uchumi kutoka chuo kikuu ambapo ulikaa kwa miaka mitatu

Imeandikwa hivyo wapi palipo rasmi? Unaweza kunionyesha au kunielekeza nami nikapasome?

Pili, uwe na uzoefu wa masuala ya uchumi na fedha kwa ujumla na mara nyingi unaanzia kazi Benki kuu au hazina moja kwa moja baada ya kupita usaili pale BOT au Hazina penyewe.

Tafadhali nielekeze huko ulikoipata hii sifa ambayo umeiorodhesha kama ya pili.

Na sifa zingine kama za kufahamu masuala ya ukaguzi wa ndani na nje na masuala yoote ya uchumi na fedha kwa ujumla.

Sawa, nielekeze huko ulikoitoa na hii.

Nne, mbunge wa kuchaguliwa

Hii una uhakika nayo? Kwamba ni lazima uwe wa kuchaguliwa tu na si kuteuliwa?

na pia uwe mjumbe wa kamati mbalimbali za uchumi na fedha za bunge.

Na hii umeitoa wapi?

Sifa hizo zipo ofisi ya raisi na ni yeye ambae hupitia sifa hizo ingawa huweza kuziweka pembeni kutokana na maslahi fulanifulani. Sifa hizo zinaweza kuwa zipo sehemu zingine ambazo mhusika amewahi kufanya kazi na kuwa na rekodi kabisa ya performance yake, na ni rekodi hiyo ndio inayotakiwa mahali popote pale inapotokea unahitajika.

Wewe umejuaje zipo ofisi ya rais? Ushawahi kuziona? Rais alikuonyesha?

Hakuwa na majukumu mengi zaidi ya kuandaa taarifa na kumsaidia alekuwa waziri marehemu Mgimwa ambae alikuwa ni nguli wa masuala ya uchumi na fedha na hata WB na IMF walimtambua.

Unguli wake pamoja na kutambuliwa kwake huko WB na IMF kumesaidia vipi kuinua uchumi wa Tanzania na maisha ya Mtanzania ya wa kawaida?

Cha msingi ni shahada ya kwanza hasa ya uchumi, na iwe ya daraja la kwanza, pili uwe na shahada ya uzamili na mara nyingi pale Mlimani wanakuwa wanafahamu ni nani anafaa kwenda hazina. Kama una shahada za nje basi usaili wako utafanyiwa upembuzi yakinifu.

Huh? Kwa mtaji huo basi Mwigulu Nchemba anafaa kabisa kuwa waziri wa hiyo wizara! Perish the thought!

Marehemu profesa kighoma malima alileta VAT na akaanzisha TRA ambayo tunaiona leo hii ni ishara ya kwamba aliona mbali kwamba ni lazima tuwe na chombo maalum cha kukusanya kodi.

Aliivumbua yeye hiyo VAT? Halafu huyo si alikuwa na kashfa za ufisadi huyo? Au nachanganya madesa?

Nae Profesa Simon Mbilinyi alikuja na masuala mbalimbali likiwemo la kodi kubwa kwa bia zinazotoka nje ya Afrika, ingawa kuna watu wakaja kuendeleza urafiki na wafanya biashara.

Huyu naye hakujiuzulu huyu? Yeye hakuwa na kashfa?
 
hahahaha still ya kupanga panga..lipumba yuko right kudoubt hio cv yake..
 
attachment.php

Mama wa watu anazidi-kuwa grilled hapa hadi inatia imani
 
Rais anaweza kuteua mtu yeyote as far as she or he's in favour with President, then anataeuliwa.


[h=2]MEMBER OF PARLIAMENT CV[/h][TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 3, align: left"]GENERAL[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Salutation[/TD]
[TD]Honourable[/TD]
[TD="width: 42%, align: center"]Member picture
1625.jpg
[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]First Name:[/TD]
[TD]Juma[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Middle Name:[/TD]
[TD]Selemani[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Last Name:[/TD]
[TD]Nkamia[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD="width: 20%"]Member Type:[/TD]
[TD="width: 38%"]Constituency Member[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Constituent:[/TD]
[TD]Kondoa kusini[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Political Party:[/TD]
[TD]CCM[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Location:[/TD]
[TD]Box 2, Kondoa - Dodoma[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Phone:[/TD]
[TD]+255 756 479494[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Ext.:[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office Fax:[/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Office E-mail:[/TD]
[TD]jnkamia@parliament.go.tz[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Member Status:[/TD]
[TD]Current Member[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Date of Birth[/TD]
[TD]1 January 1972[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 5, align: left"]EDUCATION[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH="width: 35%"]School Name/Location[/TH]
[TH="width: 27%"]Course/Degree/Award[/TH]
[TH="width: 15%, align: center"]Start Date[/TH]
[TH="width: 13%, align: center"]End Date[/TH]
[TH="width: 10%, align: center"]Level[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]The School of Journalism and Mass Communication, Tanzania[/TD]
[TD="align: center"]Diploma (Mass Communication)[/TD]
[TD="align: center"]1997[/TD]
[TD="align: center"]1999[/TD]
[TD="align: center"]DIPLOMA[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]National Radio (RTD)[/TD]
[TD="align: center"]Basic Broadcasting Skills[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]1996[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]-[/TD]
[TD="align: center"]International Braodcasting Skills[/TD]
[TD="align: center"]1999[/TD]
[TD="align: center"]1999[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]British Broadcasting Corporation BBC, London[/TD]
[TD="align: center"]Journalism Skills[/TD]
[TD="align: center"]2004[/TD]
[TD="align: center"]2004[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Voice of America, Washington[/TD]
[TD="align: center"]Computer[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]France[/TD]
[TD="align: center"]Certificate in International Sports Reporting[/TD]
[TD="align: center"]2009[/TD]
[TD="align: center"]2009[/TD]
[TD="align: center"]CERTIFICATE[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Same Secondary School[/TD]
[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1989[/TD]
[TD="align: center"]1990[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Sengerema High School[/TD]
[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1991[/TD]
[TD="align: center"]1991[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mzumbe High School[/TD]
[TD="align: center"]A-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1991[/TD]
[TD="align: center"]1992[/TD]
[TD="align: center"]HIGH SCHOOL[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Mpwapwa Secondary School[/TD]
[TD="align: center"]O-Level Education[/TD]
[TD="align: center"]1985[/TD]
[TD="align: center"]1988[/TD]
[TD="align: center"]SECONDARY[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Bicha Primary School, Kondoa[/TD]
[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1978[/TD]
[TD="align: center"]1980[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Iyoli Primary School, Kondoa[/TD]
[TD="align: center"]Primary Education[/TD]
[TD="align: center"]1980[/TD]
[TD="align: center"]1984[/TD]
[TD="align: center"]PRIMARY[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 4, align: left"]EMPLOYMENT HISTORY[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH]Company Name[/TH]
[TH="align: center"]Position[/TH]
[TH="align: center"]From[/TH]
[TH="align: center"]To[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]Ministry of Information,Youth,Culture and Sports[/TD]
[TD]Deputy Minister[/TD]
[TD="align: center"]2014-01-20[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Voice of America, Washington DC[/TD]
[TD]Journalist[/TD]
[TD="align: center"]2009[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tanzania Broadcasting Corporation - (TBC)[/TD]
[TD]Journalist/Editor[/TD]
[TD="align: center"]2006[/TD]
[TD="align: center"]2009[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]British Broadcasting Corporation BBC, World Service[/TD]
[TD]Journalist[/TD]
[TD="align: center"]2003[/TD]
[TD="align: center"]2006[/TD]
[/TR]
[TR]
[TD]Tanzania National Radio (RTD)[/TD]
[TD]Journalist[/TD]
[TD="align: center"]1995[/TD]
[TD="align: center"]2003[/TD]
[/TR]
[/TABLE]
[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TH="colspan: 4, align: left"]POLITICAL EXPERIENCE[/TH]
[/TR]
[TR]
[TH="class: text_menu, width: 47%"]Ministry/Political Party/Location[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 31%, align: center"]Position[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 12%, align: center"]From[/TH]
[TH="class: text_menu, width: 10%, align: center"]To[/TH]
[/TR]
[TR]
[TD]The Parliament of Tanzania[/TD]
[TD]Member - Kondoa South Constituency[/TD]
[TD="align: center"]2010[/TD]
[TD="align: center"]2015[/TD]
[/TR]
[/TABLE]

 
Mi nadahani JK yoko sawa. Muda wa uchaguzi unakaribia. Ukiweka mtu makini, mtaalmu, mweledi, mzalendo atafanya kazi na Nchemba na Malima?, mihela ya kulaghai watanzania ktk kampeni za uchaguzi zitatoka? Mambo ya kuporomoka kwa uchumi, na raslimali za taifa ni upepo tu vitapita, Rais ajaye atarekebisha, chama kwanza uchumi baadae.
 
NasDaz,

..kwa CV hiyo ha-qualify kuwa waziri wa fedha.

..hebu angalie CV za mawaziri wa fedha wa nchi zinazofanya vizuri kama Botswana, Ghana, Mauritius, etc.

..wizara ya fedha siyo mahali pa kumuweka mtu ambaye siyo mzito ktk taaluma ya uchumi, mabenki,au fedha.

..hata Manaibu waziri ktk wizara ya fedha wanatakiwa wawe na utaalamu na uzoefu ktk sekta wanazosimamia.

..hebu angalia CV ya Seth Tekper waziri wa fedha wa Ghana:
GhanaWeb, Validation Error

..angalia wasifu wa Xavier-Luck Duval waziri wa fedha wa Mauritius:
Xavier-Luc Duval - Wikipedia, the free encyclopedia

cc Mchambuzi, Ogah, Sikonge,

Sawa mkuu. Mfano mwengine ni aliyekuwa chairman federal reserve of USA Alan Greenspan Alan Greenspan - Wikipedia, the free encyclopedia
 
Back
Top Bottom