Ngoja tumsaidie huyu Dada maana naamini ni memba tu humu JF
Mimi ngelikuwa ndiye Waziri Mteule ningeanza kuwaonyesha watanzania mambo yafuatayo:-
1. Katika Bajeti yangu ya Kwanza (2014/15), ningefuta ununuzi wa magari yote ya thamani Serikalini kwa ngazi zote isipokuwa mawaziri na Wakuu wa Mikoa. Badala yake ningeruhusu ununuzi wa RAV4, SUZUKI na Hard Top tu, kwani anaweza kutoa mwongozo huu. Sambamba na hilo, ningetangaza kuyapiga mnada magari yote ya thamani ya Serikali yanayotumiwa na Wakurugenzi, Makamishna, Makatibu Wakuu na mfano wake kwa nchi nzima. Kwani kimsingi hali ya Miundombinu yetu kwa sasa inaridhisha hivyo hatuna sababu ya kutumia magari haya. Hakuna sababu kwanini Mkurugenzi afuatwe na V8 masaki, Osterbay au Tabata hali ya kuwa afisa wake mwenye cheo cha principal anaekaa Chanika anatumia Vitz yake. Ni wakati wa kubadilika watanzania haya magari si kwamba gharama tu kuyanunua, lkn pia ni gharama ya kuya-run, na wengi wanayatumia kwa shughuli binafsi hadi weekends. Hili lingeonyesha mweleko wake katika matumizi ya Serikali ambacho ndio kilio kikuuu cha Nchi.
2. Misamaha ya Kodi iliyopo kisiasa yote ningeifutilia mbali, bila kujali malalamiko yatakayotolewa na wadau. Hakuna ubishi kwamba Taasisi zinazopokea misamaha ndizo zenye huduma ghali kuliko kawaida.
3. Ningeanzisha mchakato (kwa kushirikiana na mamlaka za ajira zilizopo) ajira za mkataba wa miaka 5 (renewable under performance) kwa taasisi zilizo chini ya Wizara ya Fedha (TRA, BOT, Posta nk). Hawa jamaa wamejisahau sana kupita maelezo, wao wanajua kutengeneza "deal" tu basi. Au ningeangalia namna ya ku-harmonize salaries zinazolipwa kwa Agencies zilizopo mfano TRA, BOT, EWURA, SUMATRA, TCRA, TMAA nk. Ni kwanini hizi taasisi zina mishahara mikubwa sana lakini ndizo zinazoongoza kwa poor performance isiyojali wananchi? Na ndizo zinazooonekana kupiga deal za ajabu ajabu. Na pia zinaongeza kudorora kwa ufanisi katika mawizara.
4. Tatu ningeanzisha mchakato wa "special vetting" (kwa kushirikiana na mamlaka husika za ajira) kwa waajiriwa wa taasisi hizi kujua uzalendo wao kwa Taifa na utayari wao wa kuishi kulingana na kipato halali cha kazi zao
5. Tano ningeondoa au kupunguza kiwango cha fedha wanazolipwa watumishi wanaosafiri nje ya nchi na badala yake ziongezwe kwenye mishahara badala ya kufanya watu wawe wacheza deals za safari za nje zisizo na tija. Pia ningekuwa serious zaidi ya Pinda kwenye suala la Posho wanazolipana. Sambamba na hilo, ningetoa muongozo wa kupiga marufuku mafunzo ya muda mfupi kwenda vyuo vya nje ya nchi. Badala yake wizara/idara zitafute wataalam au taasisi zilizobobea zije kutoa mafunzo hapa (hata kama watumishi hao walipwe posho sawa na nje). Hii Sera imeisaidia sana nchi ya Rwanda kupata wataalamu wazuri wa kuwafundisha watumishi wao ndani ya Rwanda.
6. Ningeanzisha mchakato mahsusi wa kuimarisha e-payments badala ya mfumo wa cash huu ambao unapoteza fedha nyingi sana. Pamoja na kupanua wigo wa Kodi effective na bajeti ijayo.
Hivi vingekuwa dira yangu na ikitokea nakutana na vikwazo vya wanasiasa, au mamalaka yoyote then ninge-resign uwaziri, naenda kuwa mwalimu na kusibiri kufa.