BARD AI
JF-Expert Member
- Jul 24, 2018
- 3,376
- 8,120
Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Nape Nnauye amesema hilo linatokana na ongezeko la Wananchi zaidi ya 50% kutumia Intaneti ambapo kama kuna mtu ana mawazo ya hovyo atatamani kufanya majaribio yake huko, hivyo Serikali imekuwa ikitunga Sheria zitakazowalinda watumiaji wake.
Akizungumzia suala la Usajili wa Watumiaji wa VPN amesema suala hilo linafanyika ili kuwatambua Watumiaji wake pamoja na kuzuia uhalifu Mtandaoni na Serikali haiwezi kuacha kila mtu aingie kiholela na akafanya anachokitaka na tayari wapo Watu ambao wamefikishwa Mahakamani na wengine wamefungwa kutokana na matumizi yasiyo sahihi ya Mtandao.
Ameongeza "Tutaendelea kupafanya Mtandaoni kuwa sehemu salama kwasababu maisha ya sasa yanategemea Mtandao, usipofanya mtandao kuwa salama unafanya Nchi kutokuwa salama na msimamo wetu ni kwamba njia yoyote ya mawasiliano itumike ikiwa salama".