saidoo25
JF-Expert Member
- Jul 4, 2022
- 602
- 1,407
WAZIRI MWIGULU NCHEMBA AACHE HASIRA! KUJIBU MASWALI YA WABUNGE NI WAJIBU SIO FADHILA!
1) Ohooo...!! Nadhani hiyo statement ya Dkt. Mwigulu Nchemba ("Daktari wa Uchumi" na Waziri wa Fedha) kuhusu "Honorary Degrees" mbona haijakaa vizuri, hasa ukizingatia hata Rais Samia Suluhu Hassan juzi tu katunukiwa Digrii ya Heshima na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
2) Tafadhali rejea hiyo video clip yenye urefu wa dakika 6:08 ya Waziri Mwigulu Nchemba akimwaga povu Bungeni.
3) Ningemshauri Waziri Mwigulu ajitahidi kuwa anajibu Maswali ya Wabunge (na hata kuwaelimisha) bila:
a) Kufoka.
b) Hasira.
c) Ukali.
d) Kiburi.
e) Hamaki au mihemko.
f) Kejeli (na matusi)
g) Majigambo.
4) SIFA mojawapo ya Msomi na Mtaalam mzuri ni unyenyekevu na kupenda kutumia nguvu za hoja badala hoja za nguvu.
5) HAIPENDEZI kabisa Waziri wa Fedha kila siku kujigamba:
a) "Mimi nimesoma sana!"
b) "Mimi Daktari wa Uchumi, nikisema huo ndio ukweli!"
c) "Hii sio Honorary Doctor, nimeingia darasani!"
d) "Mheshimiwa Spika hatuwezi kupoteza muda wa Bunge kuelimisha Watu wasiotaka kuelewa!"
e) Na kadhalika.
6) Narudia!
a) Kwa upendo mkubwa, heshima na taadhima, namshauri msomi na mtaalam mwenzetu Mwigulu Nchemba ajitathmini na kujirekebisha.
b) Naamini angependa kuziangalia hizi video clip za matamshi yake Bungeni (au anapohojiwa kwenye runinga), mwenyewe ataona tatizo ni nini.
c) Na asipoona tatizo, basi tatizo linalomsumbua Mheshimiwa wetu litakuwa kubwa zaidi!
d) Hakika haipendezi kila siku watu wote (namaanisha wengi) wakawa siku zote wanakujadili wewe tu, tena kwa tatizo lilelile. Mfano: Mpambano wake na Spika Tulia Ackson Bungeni kuhusu Hesabu za Asilimia za Darasa la Sita! Au Mahojiano ya ITV alipowafurumusha Watanzania wanaolalamikia tozo wahamie Burundi!
7) MUNGU IBARIKI TANZANIA!
BJC. DSM. 07.02.2023. 1412hrs.