Waziri Mwakyembe amebadili gia angani?

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
10,197
25,517
Lilipoibuka sakata la Ney wa Mitego na wimbo wake wa 'Wapo', Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe alijitokeza na kufanya mambo mawili. Mosi, aliondoa zuio la BASATA la kuzuia wimbo huo kutopigwa redioni na runingani. Pia, alimwalika na kukutana na Ney wa Mitego katika Ofisi za Wizara yake huko Dodoma. Wakafanya na mazungumzo.

Kimantiki, wimbo wa 'Wapo' una mambo ya kisiasa. Unaongelea mambo mbalimbali ya kisiasa katika minajiri ya kukosoa na kadhalika. Ni wimbo huo ndio Waziri Mwakyembe aliufungulia na kufanya mazungumzo na mwimbaji wake. Tena, alitaka wimbo huo uboreshwe na kubeba na maudhui ya wala rushwa, wakwepa kodi na kadhalika.

Jana, alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule (Prof. J-CHADEMA), Waziri Mwakyembe amewaasa wanamuziki waache kuimba siasa kwakuwa wanaweza 'kuishia kubaya'. Ndiyo kusema, Waziri Mwakyembe amepiga marufuku wanamuziki wa Tanzania kuimba kuhusu siasa. Anataka waimbe mambo mengineyo.

Kadiri ya uelewa wangu na kwa jinsi ninavyofuatilia muziki, kuna mambo mawili makubwa ya kuyaimbia kwenye muziki. La kwanza, ni siasa. Siasa ni maisha ya watu katika namna mbalimbali. Siasa ni maisha ya kila siku katika uzuri au ubaya wake. Hata Hayati Bob Marley aliyepata umaarufu mkubwa ulimwenguni aliimba siasa pia. Jambo la pili la kuimbia ni mapenzi.

Je, katika mtitiriko wa kauli na matendo ya Waziri Mwakyembe, Waziri amebadili gia angani?
 
Mwakyembe is insane, mbona hata hao CCM wanachukua wasanii kipindi cha kampeni ili waimbe siasa!? ikiwa mziki una wafaidisha wao ndio wana upenda ukiwa mziki unawaumiza wana uchukia.
Nyimbo za siasa zilikuwepo toka kipondi cha TANU, kets say toka watu wana pigania uhuru, siasa ni maisha na wasanii huimba vitu vilivyoko kwenye maisha, either kwa kuonya , kuelimisha au kuburudisha ndio kazi ya fasihi hiyo, ana PHD fake huyu
 
wasanii wasipoingia kwenye siasa, Nchi itakuwa imepiga maendeleo sana.Ila wanatumika pote tu ingawa hata US tuliwaona wasanii wako upande wa mama Hilary ila kwetu wamezidi
Kila mmoja afanye kazi zake.
 
  • Thanks
Reactions: SDG
Akina Mbaraka Mwinshehe, Salum Abdalah, Lucy Dube, Mirium Makeba, Paul Simon na wengine wengi wamekuwa maarufu sababu ya kuimba nyimbo za siasa zinazotetea wanyonge sasa sijaelewa anataka Kamanyola au Pepe Kale?
 
kazi za wasanii ni sanaa na sanaa haina mipaka.

anayemuunga mkono Mwakyembe kwenye hili ni wa kutiliwa shaka uwezo wake wa kufikiri.
Pamoja na yote, Msanii mwenye nia ya kufika mbali na wa kudumu inabidi ajitenge na siasa. Lengo ni kuwa na mashabiki wa pande zote na hii inamuongezea Mashabiki na kipato. Tatizo hakuna mpaka kati ya siasa na Wimbo wowote wa ukombozi wa Fikra, kukemea Uovu katika jamii na wanasiasa, Kukataa ukandamizaji, Muda wowote mtu yoyote anaweza kutasiri haya yote kama siasa wakati ukweli ni kwamba yanatakiwa kufananishwa na Uzalendo zaidi.
 
Huwezi kuwa Waziri ambae juzi ulimsifia Nay na wimbo wake unaozumgumzia siasa halafu after few days unasema ni marufuku kwa wanamuziki kuimba siasa.

Unawatolea mfano Diamond na Ali Kiba kwamba wamefanikiwa kimuziki kwasababu hawaimbi siasa.
Umeshasahau nyie CCM mlivyomwimbisha diamond kwenye kampeni zenu na baadhi ya nyimbo zake akazi badili na kua mwelekeo wa siasa na hata juzi ametunga wimbo wenye mwelekeo wa kisiasa na cover la album kaweka picha ya Mwl Nyerere.

Waziri Hasara.
 
Nashauri Ney wa Mitego aongeze verse ya mistari ya mwakyembe kwenye wimbo wake wa wapo then apige collabo Na Roma mkatoliki waachie kitu ya hatareeee!!!!
 
jana kasema kama serengeti boys watashindwa kutwaa ubingwa gabon atapata ugonjwa wa moyo.

mtu anayejuwa soka hawezi kutamka maneno hayo.
 
Back
Top Bottom