Waziri Mwakyembe amebadili gia angani?

Waziri Mwakyembe amebadili gia angani?

Lakini ni wasanii hawa hawa watakaotakiwa kuimba nyimbo majukwani 2020, ama Mheshimiwa anasahau kuwa akina marehemu Komba, akina Hadija Kopa na wenzie pia ni wasanii.? Hivyo watakapopanda jukwaani waimbe mahaba tu.
 
Maana nzima ya kile anachokisema Mh Mwakyembe unakipata kupitia mifano yake ya wanamuziki aliowataja. Nyimbo za kisiasa alizozikataza ni zile zenye kuibua mgogoro kati ya serikali na mwanamuziki. Hapa alitoa mfano wa Fela Ramson Anikulapo Kuti wa Nigeria kuimba nyimbo za kushambulia wanasiasa zilimfanya afe kama chokolaa.
Kwa yeyote mwenye akili, sijui hapa nikikujumisha nitakuwa nimekosea,anafahamu kuwa Mh Mwakyembe hajazuia Mwanamuziki kuimba nyimbo za kuumpa shime,kumuasa na kumkumbusha mwanasiasa,chama na wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii bila nia ya kutweza.
Lakini siasa inapoimbwa, kamwe haiwezi kuwa ni yenye kutukuza tu na kusifu. Lazima kutakuwa na siasa za kupinga, kukosoa. Siasa haina upande mmoja tu.
 
Lilipoibuka sakata la Ney wa Mitego na wimbo wake wa 'Wapo', Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe alijitokeza na kufanya mambo mawili. Mosi, aliondoa zuio la BASATA la kuzuia wimbo huo kutopigwa redioni na runingani. Pia, alimwalika na kukutana na Ney wa Mitego katika Ofisi za Wizara yake huko Dodoma. Wakafanya na mazungumzo.

Kimantiki, wimbo wa 'Wapo' una mambo ya kisiasa. Unaongelea mambo mbalimbali ya kisiasa katika minajiri ya kukosoa na kadhalika. Ni wimbo huo ndio Waziri Mwakyembe aliufungulia na kufanya mazungumzo na mwimbaji wake. Tena, alitaka wimbo huo uboreshwe na kubeba na maudhui ya wala rushwa, wakwepa kodi na kadhalika.

Jana, alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule (Prof. J-CHADEMA), Waziri Mwakyembe amewaasa wanamuziki waache kuimba siasa kwakuwa wanaweza 'kuishia kubaya'. Ndiyo kusema, Waziri Mwakyembe amepiga marufuku wanamuziki wa Tanzania kuimba kuhusu siasa. Anataka waimbe mambo mengineyo.

Kadiri ya uelewa wangu na kwa jinsi ninavyofuatilia muziki, kuna mambo mawili makubwa ya kuyaimbia kwenye muziki. La kwanza, ni siasa. Siasa ni maisha ya watu katika namna mbalimbali. Siasa ni maisha ya kila siku katika uzuri au ubaya wake. Hata Hayati Bob Marley aliyepata umaarufu mkubwa ulimwenguni aliimba siasa pia. Jambo la pili la kuimbia ni mapenzi.

Je, katika mtitiriko wa kauli na matendo ya Waziri Mwakyembe, Waziri amebadili gia angani?
NDIYO..............anafuata convinience. Tanzania yenye msimamo aliondoka nayo JKN.
 
Wanafiki ndivyo walivyo Mkuu! Hawa watu kauli zao si za kuziamini hata chembe! Dakika hii wanaweza kukwambia hili na dakika inayofuata wakaikana kauli yao ya awali.

Lilipoibuka sakata la Ney wa Mitego na wimbo wake wa 'Wapo', Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe alijitokeza na kufanya mambo mawili. Mosi, aliondoa zuio la BASATA la kuzuia wimbo huo kutopigwa redioni na runingani. Pia, alimwalika na kukutana na Ney wa Mitego katika Ofisi za Wizara yake huko Dodoma. Wakafanya na mazungumzo.

Kimantiki, wimbo wa 'Wapo' una mambo ya kisiasa. Unaongelea mambo mbalimbali ya kisiasa katika minajiri ya kukosoa na kadhalika. Ni wimbo huo ndio Waziri Mwakyembe aliufungulia na kufanya mazungumzo na mwimbaji wake. Tena, alitaka wimbo huo uboreshwe na kubeba na maudhui ya wala rushwa, wakwepa kodi na kadhalika.

Jana, alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule (Prof. J-CHADEMA), Waziri Mwakyembe amewaasa wanamuziki waache kuimba siasa kwakuwa wanaweza 'kuishia kubaya'. Ndiyo kusema, Waziri Mwakyembe amepiga marufuku wanamuziki wa Tanzania kuimba kuhusu siasa. Anataka waimbe mambo mengineyo.

Kadiri ya uelewa wangu na kwa jinsi ninavyofuatilia muziki, kuna mambo mawili makubwa ya kuyaimbia kwenye muziki. La kwanza, ni siasa. Siasa ni maisha ya watu katika namna mbalimbali. Siasa ni maisha ya kila siku katika uzuri au ubaya wake. Hata Hayati Bob Marley aliyepata umaarufu mkubwa ulimwenguni aliimba siasa pia. Jambo la pili la kuimbia ni mapenzi.

Je, katika mtitiriko wa kauli na matendo ya Waziri Mwakyembe, Waziri amebadili gia angani?
 
Maana nzima ya kile anachokisema Mh Mwakyembe unakipata kupitia mifano yake ya wanamuziki aliowataja. Nyimbo za kisiasa alizozikataza ni zile zenye kuibua mgogoro kati ya serikali na mwanamuziki. Hapa alitoa mfano wa Fela Ramson Anikulapo Kuti wa Nigeria kuimba nyimbo za kushambulia wanasiasa zilimfanya afe kama chokolaa.
Kwa yeyote mwenye akili, sijui hapa nikikujumisha nitakuwa nimekosea,anafahamu kuwa Mh Mwakyembe hajazuia Mwanamuziki kuimba nyimbo za kuumpa shime,kumuasa na kumkumbusha mwanasiasa,chama na wananchi juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea katika jamii bila nia ya kutweza.
Unamaanisha waimbe nyimbo kama ccm mbele kwa mbele sio?
na sio kama zile mueshimiwa unamjua bashite ili jipu jipya kutoka kolomije eee
jitafakari upya na utetezi wako sawa eee
 
hii nchi ina watu vigeu geu sijapata kuona
Kama amekana andiko lililompa PhD atashindwa kugeuka kwa hili? Kwanza ashajua waTanzania tumeshasahau alivyofanya mazungumzo na Ney. Kwahiyo this is a new thing. Bongo raha sana
 
Ile Sumu imekula kitu kabsa na ni waziri sijui ingekua kapuku kama mimi ungekuta nishakua kichaa sasa
 
Wewe una akili halisi ama ya kugushi, kazi ya mwanamuziki ni kuimba anachoona kina maslahi kwake! Tatizo ni kwamba watu hawapendi kusikia jinsi upande wa pili unavyowatathmini!!! Shame on you
Usipanic, huna uzoefu wa maoni huru
 
Mwakyembe is insane, mbona hata hao CCM wanachukua wasanii kipindi cha kampeni ili waimbe siasa!? ikiwa mziki una wafaidisha wao ndio wana upenda ukiwa mziki unawaumiza wana uchukia.
Nyimbo za siasa zilikuwepo toka kipondi cha TANU, kets say toka watu wana pigania uhuru, siasa ni maisha na wasanii huimba vitu vilivyoko kwenye maisha, either kwa kuonya , kuelimisha au kuburudisha ndio kazi ya fasihi hiyo, ana PHD fake huyu
Kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Kyela , naomba radhi sana kwa kauli na matendo ya mbunge wetu .
 
kazi zao ni kuimba, waimbe nini tuwaachie wao. Upande unaoongoza kuwatumia wanamuziki ni serikali na CCM. Tatizo wao wakiwatumia wanamuziki 30 sio tatizo ila upande fulani ukiwatumia wawili tu ni tatizo. Huku ni kutojiamini kwa kiwango cha PhD.
Sasa kama wao CCM ndio wanufaika wakuu wa miziki na wasanii, Tatizo liko wapi wapinzani kuona wao ndio lengo. Kwa makadilio yako CCM ndio walipaswa kulia sana. Katika hili sina upande ila BASATA wanajua nini ni sahihi na nini sio sahihi. Ila sio sawa kila msanii anaweza kujiimbia anachoona ni sawa. Vinginevyo pangekuwa hakuna haja ya kuwa na vyombo vinavyosimamia sanaa hizo
 
Lakini siasa inapoimbwa, kamwe haiwezi kuwa ni yenye kutukuza tu na kusifu. Lazima kutakuwa na siasa za kupinga, kukosoa. Siasa haina upande mmoja tu.
Zote ulizotaja hazikatazwi bali nyimbo za siasa za kushambulia serikali au wanasiasa. Utapata msukosuko mkubwa. Kama mlezi wa tasnia hiyo kawaonya waache.
 
Ndio mawaziri wa Awamu ya Tano kweli watatuletea viwanda mawaziri vigeugeu?
 
Unamaanisha waimbe nyimbo kama ccm mbele kwa mbele sio?
na sio kama zile mueshimiwa unamjua bashite ili jipu jipya kutoka kolomije eee
jitafakari upya na utetezi wako sawa eee
Hapo unamshambulia mwanasiasa kupitia sanaa yako. Lakini ukiamua kutumia maudhui hayo kuionya jamii kuhusu udanganyifu wa vyeti bila kutaja wadhifa na majina yenye nasaba na mwanasiasa ya utani au kweli, hapo utakuwa unaelimisha. Lakini ukiamua kujificha kwenye sanaa ya muziki kumshambulia mwanasiasa utashughulikiwa.
 
Lilipoibuka sakata la Ney wa Mitego na wimbo wake wa 'Wapo', Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe alijitokeza na kufanya mambo mawili. Mosi, aliondoa zuio la BASATA la kuzuia wimbo huo kutopigwa redioni na runingani. Pia, alimwalika na kukutana na Ney wa Mitego katika Ofisi za Wizara yake huko Dodoma. Wakafanya na mazungumzo.

Kimantiki, wimbo wa 'Wapo' una mambo ya kisiasa. Unaongelea mambo mbalimbali ya kisiasa katika minajiri ya kukosoa na kadhalika. Ni wimbo huo ndio Waziri Mwakyembe aliufungulia na kufanya mazungumzo na mwimbaji wake. Tena, alitaka wimbo huo uboreshwe na kubeba na maudhui ya wala rushwa, wakwepa kodi na kadhalika.

Jana, alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule (Prof. J-CHADEMA), Waziri Mwakyembe amewaasa wanamuziki waache kuimba siasa kwakuwa wanaweza 'kuishia kubaya'. Ndiyo kusema, Waziri Mwakyembe amepiga marufuku wanamuziki wa Tanzania kuimba kuhusu siasa. Anataka waimbe mambo mengineyo.

Kadiri ya uelewa wangu na kwa jinsi ninavyofuatilia muziki, kuna mambo mawili makubwa ya kuyaimbia kwenye muziki. La kwanza, ni siasa. Siasa ni maisha ya watu katika namna mbalimbali. Siasa ni maisha ya kila siku katika uzuri au ubaya wake. Hata Hayati Bob Marley aliyepata umaarufu mkubwa ulimwenguni aliimba siasa pia. Jambo la pili la kuimbia ni mapenzi.

Je, katika mtitiriko wa kauli na matendo ya Waziri Mwakyembe, Waziri amebadili gia angani?
Mh. Waziri anajichanganya tuu! Inaonesha hata muziki wa bongo flava ameanza kusikiliza kipindi hiki alichopewa dhamana ya wizara husika.
Wamarekani weusi wasingekuwa huru na kutetea Uhuru wa waafrika, bila ya kufanya harakati za kujikomboa kwa kutumi Rap & Hip hop.
Yeye awape tahadhari kuwa wasijiingize na kushabikia chama Fulani cha siasa, maana inaweza leta mtafaruku na kuigawa jamii kwa msingi ya kisiasa.
 
Back
Top Bottom