Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,280
- 25,858
Lilipoibuka sakata la Ney wa Mitego na wimbo wake wa 'Wapo', Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Dr. Harrison Mwakyembe alijitokeza na kufanya mambo mawili. Mosi, aliondoa zuio la BASATA la kuzuia wimbo huo kutopigwa redioni na runingani. Pia, alimwalika na kukutana na Ney wa Mitego katika Ofisi za Wizara yake huko Dodoma. Wakafanya na mazungumzo.
Kimantiki, wimbo wa 'Wapo' una mambo ya kisiasa. Unaongelea mambo mbalimbali ya kisiasa katika minajiri ya kukosoa na kadhalika. Ni wimbo huo ndio Waziri Mwakyembe aliufungulia na kufanya mazungumzo na mwimbaji wake. Tena, alitaka wimbo huo uboreshwe na kubeba na maudhui ya wala rushwa, wakwepa kodi na kadhalika.
Jana, alipokuwa akijibu swali na Mbunge wa Mikumi, Mhe. Joseph Haule (Prof. J-CHADEMA), Waziri Mwakyembe amewaasa wanamuziki waache kuimba siasa kwakuwa wanaweza 'kuishia kubaya'. Ndiyo kusema, Waziri Mwakyembe amepiga marufuku wanamuziki wa Tanzania kuimba kuhusu siasa. Anataka waimbe mambo mengineyo.
Kadiri ya uelewa wangu na kwa jinsi ninavyofuatilia muziki, kuna mambo mawili makubwa ya kuyaimbia kwenye muziki. La kwanza, ni siasa. Siasa ni maisha ya watu katika namna mbalimbali. Siasa ni maisha ya kila siku katika uzuri au ubaya wake. Hata Hayati Bob Marley aliyepata umaarufu mkubwa ulimwenguni aliimba siasa pia. Jambo la pili la kuimbia ni mapenzi.
Je, katika mtitiriko wa kauli na matendo ya Waziri Mwakyembe, Waziri amebadili gia angani?