Pdidy
JF-Expert Member
- Nov 22, 2007
- 61,023
- 36,865
Mh Waziri Mkuu,
Hongera kwa Mungu kukupa nafasi uliyonayo na kazi unayoifanya. Pongezi kubwa kwako.
Nianze kutoa malalamiko yangu kuhusu yanayoendelea Kipunguni. Wananchi wa Kipunguni wanakusubiri urudi waje ofisini kupiga magoti. Wanaumizwa na majambazi, wanakufa kwa presha, kisukari na magonjwa yasiyotibika yanayotokana na msongo wa mawazo.
Mheshimiwa, wananchi wako 1,886 tangu mwaka 2017 waliletewa barua wasijenge na waondoe wapangaji ndani ya miezi mitatu. Wenye nyumba walitii, wakawapa notisi wakijua watalipwa. Baada ya miaka kadhaa kupita, TAA wakaja tena na Wizara ya Ardhi kufanya uhakiki upya.
Tangu 2022 wananchi walipewa tena barua wasijenge kwa kuwa wanalipwa. Leo ni Februari 2026, waliolipwa ni 560 kati ya wote. Mheshimiwa, hawa wamelipwa baada ya makelele na mikutano mingi na Mkurugenzi wa TAA pamoja na waandishi wa habari.
Hivi naandika, Kipunguni imekuwa kama msitu. Kuna nyumba ziko peke yake. Hata ukipiga kelele huwezi kupata msaada.
Usalama wa watoto wanaorudi usiku kutoka shuleni ni mdogo kabisa. Mauaji yanafanyika kila kukicha. Hata serikali za mitaa wamezoea hizi kero kama jambo la kawaida.
Mheshimiwa, kuna malalamiko mengi. Ukija wananchi watakuambia. Kule TAA Airport tumekuwa kama nyumbani, kwa wiki tunaenda mara mbili hadi tatu. Kwa DC tumeenda sana, tukaambiwa njoo kesho. Mwisho akasema atawaita anasubiri taarifa kutoka serikalini. Wananchi wakawa wanamsubiri.
Tukaona suluhisho ni TAA. Mkurugenzi naye akatuchoka. Kila tukifika tunaambiwa yuko safarini. Tukauliza amehamishiwa Dodoma au la.
Wananchi hawataki shida na hatutaki kuendelea kukaa pale. Tunataka kulipwa na kuondoka, tuwaachie maeneo yao wafanye watakavyo.
Mheshimiwa Waziri Mkuu, usalama umekuwa mbaya sana. Kituo cha Stakishari kimechoka. Kila siku nyumba zinavunjwa na majambazi. Wameanza kuvunja hadi mchana. Wakikuta kufuli wanaangalia kulia na kushoto, wakiona hakuna watu wanaondoka na kila kitu.
Kwa sasa hakuna mtu anayekubali kupanga Kipunguni. Tumechoka. Tunaomba msaada tafadhali.
Tumsifu Yesu Kristo.
Assalamu Alaykum.
Mungu ibariki Tanzania na watu wake.