HERY HERNHO
Member
- Mar 4, 2022
- 70
- 314
Vyanzo vya habari vinasema Waziri Mkuu wa Japani, Kishida Fumio, hajajeruhiwa na ameondoka kwenye eneo la bandari ya magharibi mwa Japani baada ya milipuko mikubwa kusikika kabla hajatoa hotuba.
Kishida alikuwa anazuru bandari ya Saikazaki mkoani Wakayama leo Jumamosi asubuhi.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameondolewa bila kujeruhiwa kwenye tukio la hadhara baada ya kile kilichoonekana kuwa kurushiwa bomu la moshi.
Mtu mmoja alizuiliwa katika eneo la Wakayama, ambapo Bw Kishida alipaswa kutoa hotuba, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.
Shuhuda mmoja alisema waliona mtu akirusha kitu, na kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa.
Picha zilionyesha maafisa wakirundikana juu ya mtu anayeaminika kuwa mshukiwa.
Polisi wanasema wamemkamata.
Shirika la utangazaji la umma la Japan NHK lilionyesha kanda zilizoonekana kuonyesha umati wa watu wakikimbia kutoka eneo la tukio.
Bw Kishida alikuwa ndio kwanza ameanza kutoa hotuba baada ya kuzuru bandari ya wavuvi huko Wakayama kifaa hicho kiliporushwa na kujifinika kuashiria kujikinga, NHK iliripoti.
Tukio hilo linawadia baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Shinzo Abe kuuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye kampeni mwaka jana