HERY HERNHO

Member
Mar 4, 2022
70
313
20230415_15_1243646_L.jpg

Vyanzo vya habari vinasema Waziri Mkuu wa Japani, Kishida Fumio, hajajeruhiwa na ameondoka kwenye eneo la bandari ya magharibi mwa Japani baada ya milipuko mikubwa kusikika kabla hajatoa hotuba.

Kishida alikuwa anazuru bandari ya Saikazaki mkoani Wakayama leo Jumamosi asubuhi.
Waziri Mkuu wa Japan Fumio Kishida ameondolewa bila kujeruhiwa kwenye tukio la hadhara baada ya kile kilichoonekana kuwa kurushiwa bomu la moshi.

Mtu mmoja alizuiliwa katika eneo la Wakayama, ambapo Bw Kishida alipaswa kutoa hotuba, vyombo vya habari vya ndani viliripoti.

Shuhuda mmoja alisema waliona mtu akirusha kitu, na kufuatiwa na moshi, huku mwingine akisema walisikia kishindo kikubwa.

Picha zilionyesha maafisa wakirundikana juu ya mtu anayeaminika kuwa mshukiwa.

Polisi wanasema wamemkamata.

Shirika la utangazaji la umma la Japan NHK lilionyesha kanda zilizoonekana kuonyesha umati wa watu wakikimbia kutoka eneo la tukio.

Bw Kishida alikuwa ndio kwanza ameanza kutoa hotuba baada ya kuzuru bandari ya wavuvi huko Wakayama kifaa hicho kiliporushwa na kujifinika kuashiria kujikinga, NHK iliripoti.

Tukio hilo linawadia baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu Shinzo Abe kuuawa kwa kupigwa risasi akiwa kwenye kampeni mwaka jana
 
Sielewi nini kinaitikisa Japan! Wenye uelewa tunaomba maelezo hasa nini kinafanya nchi ya Japan viongozi wae wakuu kushambuliwa?

Alianza Waziri mkuu mstaafu Shinzo Abe kwa kupigwa risasi na kuawa kabisa, jana Waziri mkuu wasasa karushiwa bomu la machizi! Shida nini katika nchi ya Japan?
 
65331658_906.jpg

Walinzi wa Waziri Mkuu wa Japan, Fumio Kishida wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa anayedaiwa kurusha Bomu la Moshi karibu na kiongozi huyo wakati akihutubia katika jiji la Wakayama.

Serikali meimarisha Ulinzi wa Viongozi wake tangu Waziri Mkuu wa zamani, Shinzo Abe auawe kwa risasi kwenye kampeni mnamo Julai 2022. Tukio lililoshtua dunia kutokana na Nchi hiyo kutokuwa na matukio makubwa ya uhalifu.

Japan itakuwa mwenyeji wa mkutano wa Wakuu wa Mataifa yenye Nguvu Duniani (G7) huko Hiroshima mwezi Mei 2023. Tayari msururu wa mikutano midogo mingine ya G7 inaendelea Nchini humo.

=============
Japanese Prime Minister Fumio Kishida was safely evacuated from an event in the city of Wakayama after what was reported to be a "smoke bomb" was thrown at him. A suspect has been apprehended.

Japan's Prime Minister Fumio Kishida was rushed from a speech after a smoke bomb was thrown near him in the city of Wakayama on Saturday, public broadcaster NHK said.

The prime minister was safely evacuated from the scene, the broadcaster added.

"Police are investigating the details of the loud explosive sound at the previous speech venue," Kishida said when he resumed his campaign speeches, in video broadcast by Japan's national broadcaster NHK. "I am sorry for causing many people to be concerned. We are in the middle of an important election for our country. We must carry this on together."

His Liberal Democratic party said on Twitter that scheduled campaigning events on Saturday and Sunday would be held as planned.

"We are very sorry for your concern," the party said.

What do we know so far?
Japanese media reported a blast followed by smoke filling the area as Kishida began his speech.

The Jiji news service said a pipe-like object was thrown at him. NHK reported the prime minister was taken to the Wakayama prefectural police headquarters and was safe.

News footage appeared to show officers subduing and detaining a suspect at the scene. NHK said he was held on suspicion of obstruction of business.

There were no immediate signs of injuries or damage.

When the incident occurred, Kishida was touring a fishing harbor in Wakayama to support his ruling party's candidate in a local election.

Politicians receive extra protection after Abe assassination
Japan has bolstered security for its politicians after former Prime Minister Shinzo Abe was shot dead on the campaign trail in July 2022. The incident shocked a country that witnesses little violent crime.

Japan will host the G-7 summit for world leaders in Hiroshima next month. A series of G7 meetings were underway in Japan ahead of next month's summit.

AFP/DW
 
Japani kulikoni wafadhili wetu wakubwa!! Naangalia NHK world tv station pendwa iliyopo DStv namba 431,naona live Pm anajificha kukwepa mlipuko!!! anajificha chini ya meza!!
Hawa jamaa sijui shida ni Nini!? Hivi karibuni kuna mwingine aliuwawa na Pm wetu alihudhuria maziko!!.

Ngoja waje sasa wale wanaotaka kutufungia mabarabara siku nzima kisa mtoto wa mkulima anataka kupita. Kumbe yote ni janja la nyani ni tu lengo kuu ni kujimwambafy kwao tu dhidi ya umma.
 
Huku kwetu tunalalamika tu, Kama Sasa hivi malalamiko ya kuacha kutumia mkaa na kuni, gesigesi, wao wapo juu, hata makande wanapikia gesi, kweli aliyeshiba hamkumbuki mwenye njaa.
 
Back
Top Bottom