Tumesikia katika vyombo vya habari kuwa Pinda kamsimamishama Magufuli asiendelee na zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa pembeni mwa barabara kinyume cha sheria au kupisha upanuzi wa barabara kwa ajili ya kupunguza msongamano.
Hivi hii ni sawa?
Wazee nimesikia kwenye taarifa ya habari usiku huu kupitia RFA kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesitisha ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara nchini kote.
Najua ubomoaji huo ulikuwa unafanywa kwa amri ya Mhe. Pombe Magufuli. Hii amri ya Pinda, imekaaje wazee? Au ndiyo mwendelezo wa tabia ile ile ya serikali yetu ya sasa ambapo kila kiongozi anafanya kazi na kutoa statements kadri anavyojisikia?
Mhe. Magufuli atajisikiaje?
Insubordination of Magufuli at its highest degree for 2015....... tena kwa kumtumia kiranja mkuu..... CCM hureeeeee............. Kwa wana-mapinduzi lets applaud CCM.....
Hatutapiga hatua yoyote ya maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu kama tutaendelea kubembelezana unavyotaka. Tumekua wa hovyo mno. Tunavunja sheria na taratibu,alafu tunajitetea ujinga. Wengi wa hao unaosema wanaonewa ni ama waliingizwa chaka na wamiliki wa maeneo hayo ambayo tayari walikwisha fidiwa ama walijenga kibabe wakijua watapata utetezi wa wanasiasa aina ya Pinda siku nyumba zao zikitaka kubomolewa.
kosa la magufuli alishindwa kutambua kuwa mabso wake ni waziri mkuu na rais akaanza kutukuza vyombo vya habari kuliko mabosi wake, kila kukicha mabosi wake wanasikia tu mara hili kesho mara lile, yaani hata briefing hamna. Ikabdi afungwe gavana kwanza.agizo la waziri mkuu alilolitoa kwenye mkutano wa hadhara huko chato linalomtaka waziri magufuli kusitisha mara moja bomoa bomoa ya majengo yaliyoko kwenye hifadhi ya barabara, linamweka waziri huyo kwenye mtihani mkubwa. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati anaingia madarakani aliapa kulinda na kusimamia sheria za nchi; hivi sasa akionekana kutii agizo la pinda ili kulinda kibarua chake, na hivyo kushindwa kuisimamia sheria, watu wengi makini watamwona kuwa ni mtu hasiyekuwa na msimamo.
Yale yaliyomkuta spika wa bunge la tisa, Samuel Sitta sasa huenda yakamkuta waziri wa ujenzi Joni Magufuli.Inaaminika Sitta aliwekwa pembeni kwa hila katika kinyang'anyiro cha uspika kwa sababu tu"ya kusimamia bunge la tisa katika misingi ya uwazi,haki,viwango na kuisimamia serikali vizuri.
Sitta alienguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uspika wa bunge la kumi kutokana kile ambacho ccm walikiita "mda umefika kwa wanawake kuongoza mhimili ya serikali" lakini ukweli wa mambo zile zilikuwa ni hila za kumwanusha bwana Sitta" zilikuwa njama za mafisadi waliojeruhiwa na bunge makini la tisa"
Pinda waziri kuu amemdhoofisha bwana Magufuli kwa kutoa amri ya kusimamisha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa karibu na hifadhi ya barabara. Awali magufuli alikuwa ametoa amri ya kubomoa nyumba ambazo zimejengwa maeneo ya hifadhi ya barabara.
Amri ya magufuli ipo katika misingi ya sheria za nchi ambazo kamwe hazitakiwi kuvunjwa wala kupindishwa kama amri ya Pinda alivyopindisha. Lakini bwana Pinda ameamua tu kumdhoofisha, kumdhalilisha maghufuli mbele ya umma wa watanzania. Pinda anatumiwa,pinda yupo kimkakati.
Wakati sasa wakosaji na waliovunja ile sheria ya kujenga kwenye hifadhi ya barabara wanamzomea Magufuli anaonekana kachemka ukizingatia Pinda aliotoa amri hii ya kinafiki akiwa jimboni kwa Magufuli.
Lakini kuna haja ya kutafakari kwa undani juu ya kile kilichomsukuma Pinda kutoa amri ya kupindisha taratibu,kama anasukumwa, basi ni kwa maslahi ya nani.Pinda amenukuliwa na gazeti la mwananchi akisema bomoabomoa isimishwe kwanza mpaka hapo baraza la mawaziri litakapoketi kujadili suala hilo. Magufuli anateleza sheria ambazo zimewekwa na bunge kwa niaba ya wananchi.
Kabla ya kupelekwa bungeni baraza la waziri liliridhia sheria hiyo. pinda anataka kuwaaminisha kwamba Magufuli anakurupuka ,amri ya kubomoa haina baraka za baraza la mawaziri.
Kule kukaa tena kwa baraza la mawaziri ni kwa maslahi ya nani. Mafisadi?
Serikali hii imelala, inathibitiwa na mafisadi kwa "REMOTE"
Pole sana Magufuli kwa kudhalilishwa na bosi wako pinda,chukua maamuzi magumu. Fanya kama Martha Karua, aliyekuwa waziri sheria wa kenya katika serikali ya mseto.