Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

CCM inataka wachovu sio wafanyakazi. Sasa Dr Magufuli anafanya kazi wanaingiza siasa. Kazi na siasa havichanganyiki. Na ndo maana miji iko kiholela tu, foleni, kila kitu vululuvululu. Kama vipi Dr jiuzulu waachie serikali yao.
 
Hon. PM,

It is ridiculous & laughable political statement ---- I register my support for Dr. Magufuli. Magufuli might be wrong/bad with good intentions PM might be right/good with bad intentions. My stand is based on the platform chosen by his hon to rebuke Hon. Magufuli while he is his boss.

My take:

A good leader is fearless for his actions. Magufuli does on govt/your behalf why his boss denies Magufuli's actions before public. Is it a continuation of politicking everything? Hon Magufuli is exemplary leader who is ready to bear consequences of his actions. I admire him so much!

God Bless Tanganyika, God Bless Magufuli
 
ametoa maagizo kwa staili ile ile magufuli aliyotoa maagizo yake kwa mameneja wa tanroads. La sivyo nyumba za waannchi zingebomolewa bure

hawa ndio ccm kila mtu na lake. Utashangaa hata jk kumshangaa magufuli.
 
Dk Magufuli yupo sahihi kabisa.

Namuunga mkono Dk Magufuli.

Kitu Ambacho Waziri Mkuu angefanya ni kuagiza elimu kwa wananchi na pia Waziri Mkuu angetoa pesa za kufidia wananchi ambao nyumba zao zitabomolewa.

So Waziri Mkuu hajatoa jibu ila ameahirisha matatizo

Problem Prime Minister
 
Bongo mm inaniacha hoi, hivi hawa wakubwa, hawakai kwanza wakakubaliana wafanye nn na wasifanye nn? This is disgusting!
Ni sawa na familia, mama anawambia mtoto nenda shule, baba baadae anamwambia usiende, mwishowe mtoto anachanganyikiwa! anaona baba na mama wote wazushi!

hii ni dalili ya kukosa mipango. Kila mtu ana yake na wengine hawana kabisa ndiyo maana sasa wanaiga cdm. Wameisahau hata ilani yao
 
magufuli usikate tamaa ...wewe bomoa bomoa tu....hakuna nchi inayoweza kuendelea au kupendeza bila sheria kufuatwa ...kama watu wamejenga sehemu zisizotakiwa bomoa tu....ili mradi ni kwa ajili ya maendeleo ya wengi....nchi nyingine hata hapo nairobi tu wanabomoa maghorofa ya maana yaliyojengwa kwenye hifadhi ili kupitisha barabara......hapa tunabembelezana nini??

Serikali isiyojiamini taabu sana>>>> bora watu wakuchukie ...lakini wakiyaona maendeleo watakupenda tu......nani anasahau hali iliyokuwapo manzese kabla ya barabara mpya ......ile barabara ilikuwa kama uchochoro.....


namuunga mkono magufuli.....na ccm wajuwe wasipompa magufuli ugombea mwaka 2015..chadema wanachukua nchi!!!...kama wanamdhoofisha ajiunge chadema!!
 
Kimsingi Mheshimiwa Pinda ni boss wake Magufuli, hatupingi kwa hali ilivyo kwa sasa, taifa hili lenye matatizo lukuki na makali ya umeme si wakati muafaka wa Ndugu Magufuli kupiga chini nyumba zilizoko pembeni mwa barabarani kinyume cha sheria kwa sasa. Labda kisiasa zingeachwa hadi baadaye kidogo baada ya Serikali kutatua matatizo ya kiuchumi, hali ngumu ya maisha na kujibu maswali magumu yaliyo mezani kwao.

Nilitarajia ndugu Pinda amshukuru ndugu magufuli kwa ujasiri wake wa kusimamia sheria za taifa hili kwa ujasiri mbele ya wapiga kura wake.

Baadaye ndug Pinda angemshtua kijane wake ofisini wadiscuss ndani kisha amwache kijana apostpone amri yake mwenyewe. Kazi ya ndg Magufuli ni ndg Pinda. Angetumia busara kidogo kujenga ushikamano ndani ya serikali.

Kwa hali hii.... Sisi wananchi tuwaelewe vipi?

Waheshimiwa penda si msipende kwa upeo wetu sisi watanganyika wa kawaida tunajifunza kwamba ukiwa na moyo wa kufanya kazi na kutumikia taifa kwa moyo wote basi serikali hii si mahali pake.

Mungu baba utuongoze kwa kila kitu.
 
Aah magufuli yuko ndani ya mfumo wa kifisadi..kuanzia rais wake mpk mawaziri.hawezi fanya lolote hata kama anasimamia misingi ya sheria na haki.namhurumia sana jemedari huyu!!inabidi awe mpole tu..aje ndani ya CDM!
 
Pinda yuko sawa, hivi hali hii ya maisha ilivyo sasa unambomolea mtu nyumba bila fidia unategemea nini. Huyu Magufuli wananchi wanamsifia mno mpaka anapata kichwa, lazima hili suala watu wakae wadiscus na kutoa majibu yenye maana sio kupumuruka kutaka sifa. watu walipwe fidia zao watabomoa tu haki ifuatwe.
 
Kisheria ni aibu kubwa kwa waziri mkuu kutengua agizo la waziri wake.

Makufuli anafanya kazi kwa makini na kwa kupitia sheria na katiba ya nchi.. Sasa mambo yameanza kuwa mazuri wanampiga stop kwa nini?

Kama waziri mkuu angekuwa na shida na agizo hilo au ameona linaleta shida basi angetakiwa kuwasilisha taarifa yake kwa wizara husika an siyo kwenda kwenye vyombo vya habari na kusitisha.

Sasa kwa maoni yangu nadhani kwanza makufuli atafute sababu za msingi ni kwa nini zoezi hilo lisitishwe na je linamaslahi ka taifa..??? Kama ni la kisiasa zaidi basi namshauri yeye na mwakyembe wajiuzulu.
 
in the mean time tunaweza kusema kwamba anavunjwa miguu asifike na masifa yake 2015. lkn kiuhalisia ni kwamba ccm wanajisafisha baada ya kuona wamemwagiwa mavi na chadema.
 
The worst sin towards our fellow creatures is not to hate them, but to be indifferent to them. That is the essence of inhumanity.
 
na yeye anachoendelea kukaa huko ni nini? si ahame icho chama aje huku kwingine achukue urais?
 
Hivi Mkwere yupo nchini au bado anatalii, ningemuomba aingilie kati suala hili, amruhusu Magufuli aendelee kusimamia sheria za nchi.
 
Hii ina maana gani, Magufuli atasimama vipi kuendesha shughuli za wizara yake...!!

Mchapa kazi ndani ya mafisadi haivi kapisa.. ...

Magufuli Nafikiri umejifunza ... kilichotakiwa kujifunza ....so take action now!!
 
Naona ingekuwa vizuri kama WM (PM) angemwagiza yeye mwenyewe Makufuri kusitisha zoezi hilo ili kuepuka kumdhalilisha na kumvunja moyo waziri wake? Yawezekana kweli kukawepo na jambo mgongoni mwa agizo hilo

Tatizo lake Magufuli ,hasomi mazingira wala hajifunzi kutokana na yaliyopita ,kumbe wenzake wamo kazini kumumaliza.Anafikiri yupo enzi za mkapa, yumkini waliompa kazi wanamuwinda.

Hajifunzi wale samaki wa magufuli, hajifunzi ile restaurant ya kijito nyama alipokuwa waziri wa ardhi.

Na hata hivyo mie nambeza tu, naye Magufuli hana mema juu ya taifa lake,kwani Magufuli ni moja wa watu wachache kabisa ambao wanaweza isambaratisha ccm na kujizolea umaarufu.
 
Kuna mtu alisema na leo napenda nirejee tena kwamba 'huwezi ukawa ccm na ukaendelea kuchapa kazi zako kwa uhuru huku ukizingatia sheria'. Hiki chama kimeshikwa na kikundi kidogo cha watu. Ukifanya kinyume na matakwa yao lazima ukione cha mtema kuni. Magufuli anadhani anaweza kuendelea na style yake chini ya jk!! Amenoa!
 
Mh PM alishindwa nini kumwita Waziri na kuizungumzia hii issue kimya kimya ofisini? Hii ingeondoa a lot of embarassment kwa Waziri.

Angeeleza mwenyewe kwamba baada ya kutafakari kwa kina ameonelea ni vyema kwanza kuweka mpango mzuri wa kubomoa hizo nyumba.

Sasa mzee mkubwa ameenda kuiongelea hii issue kwenye jimbo lake Waziri halafu amempa na kazi ya ziada ya kusimamia kilimo. Kwa kweli nilipigwa na mshangao kidogo.
 
Hapana nadhani kwa hili nitampongeza Pinda!!! Ndiyo! Sheria anayoingangania Magufuli ni ipi? Sheria zipo kumlinda mwananchi asipokonywe haki yake! Kwa sheria za ardhi, anzia zile za mkoloni hadi za kikwetu, ardhi inapohitajika kwa matumizi ya shughuli za kijamii( public purpose) kama kupanua barabara serikali inayo mamlaka ya kuitwaa lakini humhamisha yule mtu(Resettlement) na kumlipa fidia. Hili linaeleweka sana. Na tena pale ambapo mwananchi atakuwa amevamia ardhi lakini hakubugudhiwa kwa zaidi ya miaka 12, sheria humpa haki mmiliki huyu mwananchi na kwa ajili hii anastahilishwa kuhamishwa na kufidiwa (Limitation Act).

Tulichokisikia kwa Magufuli ni kurupuka kwamba kuna watu wamevamia hifadhi za barabara, hatuelezi ni lini walivamia. Na kwa kauli yake anasema hawatastahili kulipwa fidia. Fikiria mwananchi aliye na nyumba yake maeneo yale tangu miaka ya 1970, hajui mahali pengine ni hapo tu, leo hii unamwambia aondoke na humsaidii kwa chochote. Si sawa! Sheria zote za Ardhi( natamani ningekuwa na muda nizinukuu zote ili msomaji wangu upate kulielewa).

Sio mara ya kwanza Magufuli amejaribu kuwaonea wananchi kwa visingizio vya sheria. Kule Rombo alishindwa na serikali ililipa fidia kwa wananchi wale, Kigoma na Shinyanga hawakuambulia kitu, nadhani kwa sababu hawakuthubutu kumkatalia. Pale Mwanza alivunja kituo cha Mafuta, matokeo yake mahakama iliamuru serikali imfidie yule mhindi, na ilikuwa ni fedha nyingi (pande zote zilikubaliana zimalizane nje ya mahakama).

Kinachotakiwa sio mabavu, ni busara na kuandika mradi wenye kuwafikiria hawa raia kwa kadiri ya sheria zinavyoruhusu, na sheria sio moja tu ziko nyingi. Ukiacha kuziangalia zote wananchi watakaoathirika wanaweza wakaiburuza serikali mahakamani na serikali ikalipa fedha nyingi kuliko ilivyopasa, upande wa pili ikawa umewaumiza wananchi bila sababu na kuongeza hasira na chuki dhidi ya serikali bila sababu.

Dr Magufuli ni muhimu akajali maslahi ya wananchi, maana sheria zetu sio gandamizi kama anavyotaka tuamini. Mfano hata ingekuwa vipi, Jengo la Tanesco pale Ubungo- lina michoro na vibali vyote, maana yake Mamlaka husika kwa kupitia sheria zote ziliridhia pajengwe. Huwezi ukakurupuka ukasema utabomoa kwa kuwa tu umeitwa Waziri wa Ujenzi. Hawa kina Magufuli ni wale wasiojali maslahi ya taifa na wananchi. Maana uamuzi wowote ule utagharimu serikali na pili wananchi wenye mali.

Nalazimika kumuunga mkono Pinda! Magufuli asingefaa Chadema maana ana vurugu huyu, ana umimi, anataka aonekane yeye ndiye kafanya, sio collective responsibility ya serikali !
 
Back
Top Bottom