Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Gosbertgoodluck, Mar 6, 2011.

 1. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #1
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0

  Wazee nimesikia kwenye taarifa ya habari usiku huu kupitia RFA kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesitisha ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara nchini kote.

  Najua ubomoaji huo ulikuwa unafanywa kwa amri ya Mhe. Pombe Magufuli. Hii amri ya Pinda, imekaaje wazee? Au ndiyo mwendelezo wa tabia ile ile ya serikali yetu ya sasa ambapo kila kiongozi anafanya kazi na kutoa statements kadri anavyojisikia?

  Mhe. Magufuli atajisikiaje?
   
 2. M

  MsandoAlberto JF-Expert Member

  #2
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 2, 2010
  Messages: 1,019
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Sijalisikia hili ila inawezekana. Swali linabaki, kwani angempa maelekezo Magufuli kuhusu utekelezaji wa amri ya kubomoa ingekuwaje? Au ni lazima atangaze kwamba amesimamisha?
   
 3. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #3
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Ndicho kinachonishangaza. Serikali inayoendeshwa kwa umakini na ustaarabu, haiwezi kuwa na statements za viongozi wake waandamizi kama mawaziri zinazokinzana. Nionavyo mimi nadhani Pinda ilikuwa vizuri na hekima kumwita Mhe. Magufuli na kujadiliana nae kuhusu zoezi hilo la bomoabomoa. Baada ya majadiliano, kama ingeonekana ni muhimu zoezi lisitishwe basi amri ya kusitisha angeitoa Mhe. Magufuli mwenyewe na siyo Pinda. Njia hiyo isingejenga taswira mbaya mbele ya wananchi na kwa Magufuli mwenyewe.
   
 4. Waberoya

  Waberoya Platinum Member

  #4
  Mar 6, 2011
  Joined: Aug 3, 2008
  Messages: 11,570
  Likes Received: 3,869
  Trophy Points: 280
  Ndiyo siasa hizo

  Anathibitisha yeye ni mtoto wa Mkulima! hakuona morogoro road ilivyokuwa kabla na baada ya upanuzi?
  Hajaona barabara ya Mbagala ilivyokuwa kabla na baada ya upanuzi?
  Hakuona Sam Nujoma ilivyokuwa kipindi kile na baada ya upanuzi?

  List goes on and on......

  Nakubali kama waziri mkuu angetoa hilo tamko na angesema kuanzia sasa serikali na taasisi za serikali zinaamishiwa dodoma , hata hivyo upanuzi wa barabara ungekuwa pending tu , kwani jiji linavyokuwa kwa kasi ni lazima hakuna jinsi.

  Au angesema zinajengwa barabara mpya ambazo lazima nazo kungetokea tu ubomoaji!

  Hili tamko halijaathiri tamko la mama Tibaijuka? waliojenga 100m from baharini?

  Amesema kutuliza mzuka wa kisiasa nothing else!
   
 5. Joss

  Joss JF-Expert Member

  #5
  Mar 6, 2011
  Joined: May 28, 2009
  Messages: 729
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 33
  Ku over-rule amri ya waziri wake hadharani ni jambo baya sana. Kwa nini wasingejadiliana halafu akamuacha Magufuli asitishe? Hii inaonesha kuwa CCM na serikali yake imechanganyikiwa, kila mtu atakuja na lake irimradi kujisafisha kumbe wanatibuana na kuadhiriana. Kama hakujadiliana na Magufuli mi nashauri Magufuli ajiuzulu tu, maana kafanywa hajui kazi.
   
 6. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #6
  Mar 6, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Centralised Government, Hii yote ni vita ya urais 2015, kama unakumbuka EL nae aliwahi kutengua maamuzi ya Prof Mwandosya kuhusu kuzuia ujenzi wa Hotel kwenye mbuga ya wanyama.

  These types of decisions flows always comes out of corrupt governments anywhere in the world. If the Gov wanted to rescind its decision that comes from its legitimate official, should do so via the same official who initiated it, when a higher authority comes out to the public to rescind the decision made by a legitimate surbodinate is an insult to that surbodinate in the face of public. In a such circumstance it eludes the ability of such surbodinate to perform his/her duties in Public. I URGE DR MAGUFULI TO SUBMIT A RESIGNATION LETTER AS HIS ABILITY TO DELIVER HAS BEEN IMPAIRED BY THIS DECISION.
   
 7. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,810
  Trophy Points: 280

  Hii Serikali hovyo kabisa! Hivi hawana hata mikutano muhimu ya Baraza la Mawaziri kujadili maamuzi yao muhomi toka kila Wizara? Huu usanii utaisha lini ndani ya hii Serikali? Magufuli anasema bomoa, Pina anaseme usibomoe! Dah! Kazi kweli kweli...na mkuu wao wa kazi kama kawaida yake yuko kimyaaaaa anacheka cheka tu!
   
 8. Gosbertgoodluck

  Gosbertgoodluck JF-Expert Member

  #8
  Mar 6, 2011
  Joined: Mar 3, 2008
  Messages: 2,866
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 0
  Indeed, resignation will keep Magufuli's credibility at its most top level. Pinda who claims himself to be a 'son of a peasant' (I feel this slogan has its hidden agenda) has handled this issue mistakenly and definitely he has discouraged Magufuli. Let's wait and see how Magufuli will respond.
   
 9. Wacha1

  Wacha1 JF-Expert Member

  #9
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 21, 2009
  Messages: 12,766
  Likes Received: 920
  Trophy Points: 280
  Sasa Magufuli kama ana ubavu ajiuzulu ili pawe patamu zaidi au aendelee kufanya kazi yake na kumdharau Pinda bomoa hizo nyumba zilizojiingiza kinyemela. Hii inaonyesha Pinda jinsi alivyo mkurupukaji na mfata upepo kama JK alivyosema.
   
 10. BAK

  BAK JF-Expert Member

  #10
  Mar 6, 2011
  Joined: Feb 11, 2007
  Messages: 70,496
  Likes Received: 81,810
  Trophy Points: 280
  Ana ubavu wa kujiuzulu Mkuu!? tusubiri tuone kama ana ubavu huo.
   
 11. N

  Nonda JF-Expert Member

  #11
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 13,223
  Likes Received: 1,958
  Trophy Points: 280
  Mkuu
  Hiyo hovyo ina-apply kwa jamii yote..watu hovyo wanapata serikali hovyo...tunapokubali mambo ya hovyo maana yake tumeyabariki au vipi?

  Tumeridhika na "amani na utulivu" na tunacheka cheka!

  Siku tukiacha kuwa hovyo na tukiacha kucheka cheka juu ya haya mambo ya hovyo wanayotufanyia basi wataanza kuwajibika..kwa sababu tutawataka wawajibike.
   
 12. Zegreaty

  Zegreaty JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 24, 2010
  Messages: 638
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  tena sio peke yake yeye na naibu wake Mwakyembe
  "Pinda amegeuzwa vuvuzela la Mafisadi"
   
 13. c

  carefree JF-Expert Member

  #13
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 19, 2010
  Messages: 265
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 45
  Ubabaishaji tu unasitisha zoezi na ubomoaji wa nyumba kwenye hifadhi ya barabara unapopanua barabara inapita juu ya nyumba? Wanamuziki wengi huwa wanatumia vileo hasa majani kuondoa aibu pinda atakuwa amewaiga nini?
   
 14. Mtumiabusara

  Mtumiabusara JF-Expert Member

  #14
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 18, 2009
  Messages: 473
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 33
  Inawezekana walishajadiliana hata kwa njia ya simu, Vinginevyo PM angesema kuwa atamwomba waziri asitishe ubomoaji (lugha ya ustaarabu)
   
 15. makoye2009

  makoye2009 JF-Expert Member

  #15
  Mar 6, 2011
  Joined: Jun 12, 2009
  Messages: 2,646
  Likes Received: 500
  Trophy Points: 280
  This is a proof that CCM is governing our country using a Management by crisis style! In other words it's a disorganised Government!!!
  Ni kichekesho kuwa hii serikali ya CCM kwa sasa kila kiongozi kukicha ana KURUPUKA NA LA KWAKE.

  Magufuli anasimamia sheria na taratibu za Wizara. Sasa Pinda anapozuia kubomoa hizo nyumba zilizojengwa kweny RESERVE ROADS anataka kuwaambia nini Watanzania??????????

  Kama ni harakati za Urais 2015 basi tutasikia mengi sana kabla ya Uchaguzi 2015! Ni vioja tupu.
   
 16. kipindupindu

  kipindupindu JF-Expert Member

  #16
  Mar 6, 2011
  Joined: Dec 16, 2010
  Messages: 1,051
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  naunga mkono hoja Magufuli ajiuzulu.
   
 17. Ndahani

  Ndahani JF-Expert Member

  #17
  Mar 6, 2011
  Joined: Jun 3, 2008
  Messages: 14,316
  Likes Received: 1,784
  Trophy Points: 280
  Hii meli tunayosafiria inapita katika mawimbi makali....kweli uongozi sio mchezo wa maigizo. Its something more than what we thought
   
 18. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #18
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Hivi viongozi wetu wamesomea wapi? Wana vyeti halali kweli? Maana nilitegemea wangeambiana wenyewe,Magufuli angekuja kusawazisha mwenyewe jukwaani.

  Japo namuunga mkono PM (katika hili tu )kusawazisha huu uozo wa Magufuli kabla haujafanyiwa kazi, eti angevunja na jengo la tanesco..
   
 19. Cynic

  Cynic JF-Expert Member

  #19
  Mar 6, 2011
  Joined: Jan 5, 2009
  Messages: 5,154
  Likes Received: 628
  Trophy Points: 280
  HTML:
  Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, amemwagiza Mkuu wa Mkoa wa Kagera Mohamed Babu, ampatie orodha ya wafanyabiashara wanaonunua sukari kutoka katika Kiwanda cha Sukari cha Kagera, ili ajue sababu za kuuza bidhaa hiyo kwa bei ya juu.
   
  Source - Mwananchi 
  WM wetu ni kama employee tu anayefanya kazi ili mradi kusubiri ujira mwisho wa mwezi! Mara nyingi anatoa statements zinazoishia hewani tu .... na zingine hazina mantiki kama hiyo hapo juu.
   
 20. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #20
  Mar 6, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Sasa angekulaje huu ujiko wa kuzima kauli ya Magufuli? Ukiangalia kwa jicho la tatu kuhusu hili utaona kuna hoja zaidi ya hii ndani yake!

  Kama mimi ningekuwa Pombe, ningejiuzulu!
   
Loading...