#COVID19 Wizara ya Afya yakanusha uvumi kwamba Waziri Mkuu alisema hakuna Wimbi la Nne la UVIKO-19

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,796
11,959
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHAJI WA MATAMKO YA VIONGOZI JUU YA MWENENDO WA UVIKO-19 NCHINI

Dodoma, Tarehe 20 Disemba, 2021.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imebaini taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii, kati ya taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu kwamba hakuna wimbi la nne la UVIKO-19 na ile iliyotolewa na Katibu Mkuu Afya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya UVIKO-19.

Kimsingi taarifa zote hizi ni sahihi na wala hazipingani kabisa. Hii ni kwa kuwa, kuongezeka kwa maambukizi au Visa hakumaanishi kuwa tayari ni wimbi jipya la maambukizi na kitaalamu hii hujulikana kama resurgence of new cases (kuongezeka kwa maambukizi mapya). Kwa tafsiri halisi iliyotolewa na Stephen X. Zhang et al kwenye Jarida la Risk Management Health Policy la tarehe 13 Septemba 2021 “wimbi ni tofauti na ongezeko linalotokea ghafla na kwa kipindi kifupi (resurgence); ili kusema kuna wimbi jipya ni lazima hali ya ongezeko iendelee kwa kipindi fulani (walau kati ya siku 14-21)”.

Hivyo, kwa maelezo haya ya kitaalamu wananchi wapuuze upotoshaji wa taarifa sahihi za viongozi wote wawili na zimetolewa kwa wakati tofauti kama mwendelezo wa Serikali kuwasiliana na Umma. Aidha, wananchi wanakumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari na kujikinga kwani ugonjwa wa UVIKO-19 bado upo na maambukizi yamekuwa yakiongezeka. Wizara inaendelea kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huu na itakuwa inatoa taarifa kulingana na mabadiliko kadri yanavyotokea kwa mujibu wa takwimu za kila siku.

Imetolewa na;

Prof Abel N. Makubi
Katibu Mkuu (Afya)
Screenshot_20211220-203329.png
 
View attachment 2051611
Kwahiyo mnataka kusema alinukuliwa vibaya au hakusema kabisa ? naombeni jibu ili nimalize mchezo
 
Kwa nini wanakanusha leo.... Toka wiki iliyopita walikuwa wana goja nini...!!? Na kwa nini Wizara ya afya inakanusha badala ya Ofisi ya Waziri Mkuu....!!? Hawa watu wanatuchezea akili....!!
 
Wameamua kuchutama wao ili kumsitiri kassim.

Ewe Kassim acha uongo mzee tumekuchoka.
 
Kiongozi mkuu anaropoka mambo yasiyomuhusu, hana utaalamu nao, anaishia kukonfyuzi watu tu! Shame!

Na Katibu Mkuu huna maana, unatetea nini sasa wakati tunajua na wataalamu wanasema Omicron ipo inazunguka tena kwa nguvu! Shame, shame, shame!
 
MP inaonekana uwongo, ulaghai na unafiki, vipo damuni.

Yupo ofisini anachapa kazi, mara nasikitika kutangaza ksiba wa ...

Wawekezaji njooni, t7na umeme mwingi wa kutosha, mara t7na upungufu wa umeme kutokana na ukame.
 
Sasa tunaongelea semantics ? Naona hii imezidi kuchanganya kuliko kuelekezea...

Unapoongea na wananchi taarifa muhimu kama hii inabidi utumie lugha inayoeleweka kwa wananchi hao..., sasa kama mpaka kuelewa inabidi upitie majarida tofauti ya wataalamu nadhani huko ni Wizara kutokujua kazi yao
 
Kwa taarifa hiyo je mzigo mpya upo mtaani au ni seasonal flu tu😁?
 
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA. WIZARA YA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO.

TAARIFA KWA UMMA KUHUSU UPOTOSHAJI WA MATAMKO YA VIONGOZI JUU YA MWENENDO WA UVIKO-19 NCHINI

Dodoma, Tarehe 20 Disemba, 2021.

Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, imebaini taarifa za upotoshaji kwenye mitandao ya kijamii, kati ya taarifa iliyotolewa na Waziri Mkuu kwamba hakuna wimbi la nne la UVIKO-19 na ile iliyotolewa na Katibu Mkuu Afya kuhusu kuongezeka kwa maambukizi ya UVIKO-19.

Kimsingi taarifa zote hizi ni sahihi na wala hazipingani kabisa. Hii ni kwa kuwa, kuongezeka kwa maambukizi au Visa hakumaanishi kuwa tayari ni wimbi jipya la maambukizi na kitaalamu hii hujulikana kama resurgence of new cases (kuongezeka kwa maambukizi mapya). Kwa tafsiri halisi iliyotolewa na Stephen X. Zhang et al kwenye Jarida la Risk Management Health Policy la tarehe 13 Septemba 2021 “wimbi ni tofauti na ongezeko linalotokea ghafla na kwa kipindi kifupi (resurgence); ili kusema kuna wimbi jipya ni lazima hali ya ongezeko iendelee kwa kipindi fulani (walau kati ya siku 14-21)”.

Hivyo, kwa maelezo haya ya kitaalamu wananchi wapuuze upotoshaji wa taarifa sahihi za viongozi wote wawili na zimetolewa kwa wakati tofauti kama mwendelezo wa Serikali kuwasiliana na Umma. Aidha, wananchi wanakumbushwa kuendelea kuchukua tahadhari na kujikinga kwani ugonjwa wa UVIKO-19 bado upo na maambukizi yamekuwa yakiongezeka. Wizara inaendelea kufuatilia mwenendo wa ugonjwa huu na itakuwa inatoa taarifa kulingana na mabadiliko kadri yanavyotokea kwa mujibu wa takwimu za kila siku.

Imetolewa na;

Prof Abel N. Makubi
Katibu Mkuu (Afya)
View attachment 2051611
 
Ile ya kusemea msikitini ya kwamba chuma kina hali njema na kinachapa kazi na yenyewe walikanusha?
 
Nadhani PM bado ana yale mawazo ya awamu ile. Mtaji wa nchi yote ni nguvu kazi tusicheze na maisha ya watu.
 
Back
Top Bottom