DOKEZO Ngorongoro: OCD Peter Lusesa, awaweka ndani Wananch 17 wa kisangiro kwa siku 8 na kuwatesa, kwa kosa la kwenda Dodoma kuonana na Waziri Mabula

Hili ni dokezo maalum toka kwa mwananchi mtumiaji wa JF mwenye nia ya kuusaidia umma kuwa na taarifa 'maalum'
A

Anonymous

Guest
Kijiji chetu Kinaitwa Kijiji Cha kisangiro kata ya kirangi tarafa ya sale Wilaya ya Ngoro Ngoro.

Kijiji chetu upande wa mashariki kinapakana na Kijiji Cha jema, kusini kinapakana na Kijiji Cha Oldonyo sambu, Magharibi kinapakana na Kijiji Cha Mgholo na Tinaga, kaskazini kinapakana na mpaka wa kimataifa wa Tanzania na Kenya.

Mwaka 1993 wakati wa kiangazi kikali kilichosababisha watu na mifugo kufa Kijiji chetu kilipokea barua ya maombi kutoka Wilayani (Makao makuu ya Wilaya Loliondo) inayotaka tuwape maeneo ya kulisha mifugo baadhi ya kaya kutoka Kenya barua hiyo iliandikwa na chief wa Narok mwaka 1993.( Barua hiyo tunayo na idadi ya kaya zilizoombewa ).

Mwaka 1994 mvua zikanyesha na wageni wakaombwa kurudi kwao kama barua inavoeleza.

Wakakataa kurudi mwaka 1995 wakalazimishwa, hii ilipelekea vita ya kikabila kati ya Wasonjo/ Batemi na Maasai kutoka Kenya hasa Jamii za Loita ambao walipinga kuondoka kwenye maeneo yetu Kwa njia ya amani.

Wamasai jamii za Loita wakawalipa wasomalia kupigana vita. Mwaka 1998 wasomalia wakamwua aliyekuwa OCD.

Ndipo serikali ikaaingilia kati na wahamiaji haramu wote wakafukuzwa makwao.

Mwaka 2002 wakarudi tena Kwa mgongo wa NGOs wakakalia maeneo yetu tena.
Mwaka 2004 wakapigana vita tena kati ya jamii zetu za Wasonjo/Batemi na jamii za Loita kutoka Kenya huku issue ikiwa ni ile ile ya uvamizi wa ardhi.

Mwaka 2005 Mkuu wa mkoa wa Arusha akamwandikia DC Ngorongoro kumtaka maeneo Yale yasimamishe mpka uamuzi wa serikali utolewa (Barua tunayo), maagizo haya yalitoka baada ya Wamasai wanaoishi Tanzania kuwa kichaka cha kuwaficha wamasai wa Kenya na kuungana nao kudai kuwa maeneo waliyovamia ni maeneo yao na kuwa wao ni watanzania hii ilileta utata ndio maana RC akatoa maamuzi hayo.

Sisi tulitii maamuzi ya Mhe RC lakini wenzetu waliendelea kuendeleza maeneo yetu.

Mwaka 2012 wazee wa jadi waliamua kumwandikia Mhe waziri Mkuu enzi hizo Mhe Mizengo pinda kuhusu uporaji wa ardhi yetu ( Barua hiyo tunayo) na mwakaa huo huo tulijibiwa na katibu wa Ardhi akikiri kupokea maelekezo kutoka Kwa waziri Mkuu na akaahidi kwenye barua kuwa Mhe waziri mwenye dhamana ya ardhi atafika kwenye eneo la mgogoro.
( Barua tuliyojibiwa ipo).

Tarehe 21/2/2013 Mhe waziri mwenye dhamana ya ardhi Pro Anna Tibaijuka akiwa na Kamishina wa ardhi na tume ya wataalamu kutoka wizarani, mkoa, Wilaya,kata na vijiji vyote.

( Kumbuka kipindi hicho wahamiaji kutoka Kenya walidai wao ni wakazi wa Kijiji Cha Enguserosambu ambacho kipo kata ya Loliondo na tarafa ya Loliondo na katika Kijiji hicho wanakaa jamii za kimasai kutoka Tanzania, Kwa maana hiyo walitumika kuficha wahamiaji Kwa kudai ni wamasai wenzao.

Sasa mgogoro ukawa ni kati ya Kijiji chetu Cha kisangiro kata ya Kirangi tarafa ya sale na Kijiji Cha Enguserosambu kata ya Loliondo tarafa ya Loliondo.

Kwa hiyo mgogoro ukawa ni kati ya Kijiji na kijiji, ambapo kila Kijiji kina kata yake na tarafa yake.

Baada ya kikao cha maridhiano kufanyika mbele ya Mhe waziri pande zote mbili walikubaliana kuheshimu mipaka yake na Mhe waziri akabainisha mipaka upya.

Mhe waziri akatoa angalizo kuwa isifanyike Shughuli yeyote kwenye maeneo Yale mpaka pale tume ya wapimaji kutoka wizarani itakapokuja kuweka beacons hivyo wote tulisimamishwa!.

Mwaka 2014, tume ilifika Wilayani lakini wakarudi pasipokutekeleza jukumu lao.( Barua ipo).

Mwaka 2015 wenzetu wakafungua mashamba wakishirikiana na matajiri wa mji wa liliondo na wasso pamoja na maafisa waandamizi kutoka Wilayani. Orodha ipo

2016, tukalalamika Wilayani lakini DC aliekuwepo enzi hizo alikuwa Rashid Taka, akatujibu twende wizarani.

Mwaka huo huo na sisi tukaenda kwenye maeneo Yale lakini tulipigwa na kushambuliwa na Risasi ndugu zetu watatu wakauawa pale pale nao ni MBURUDUKA, KASERIA, NA TIMOTHY ( aliyekuwa mkt wa kijiji chetu.)

Baada ya hapo ikawa kila mwaka lazima tushambuliwe na Watu kufa ili kutuogopesha kabla hawajalima na hii ilikuwa inafanyika kati ya mwezi kwanza Hadi wa 5.

Mwaka 2017 wakavamia shambani Kwa watu na kujeruhi mmoja na mwingine kumwuua Kisha kupelekwa kusikojulikana na kilichotumika kutekeleza tukio Hilo ni Gunshot (PF3 imeeleza).

Mwaka 2018 wakamjeruhi tena Kwa Risasi bwana Ruben aliyekutwa shambani kwake alipoamuriwa alale chini akakkimbia ndipo alipo jeruhiwa mguu (PF3 imeeleza).

Mwaka 2019 wakasajili eneo lile kuwa kitongoji Chao ndani ya Kijiji Chao Kwa hiyo ikawa vitongoji viwili ndani ya eneo Moja.

Mwaka 2020 wakawavamia ndugu wawili wakiwa wamelinda mashamba yao wakawapiga mishale na kuwajeruhi na mapanga Hawa walinusurika kifo lkn OCD Peter Lusesa alinyima PF3 na akaamuru Daktari awatibu bila PF3 alipokataa akaambiwa anunue PF3 lkn mwisho walitibiwa bila PF3.

Mwaka 2021 mwezi wa 3 tukavamiwa tena Kwa Risasi lakini hakuna aliyejeruhiwa lakini nyumba zetu zilivunjwa zote ambazo zilikuwa karibu na maeneo ya mgogoro .

Kumbuka kila tukio linapopokea huwa tunatoa taarifa na badala yake sisi ndio huonekana ni wachochezi hivyo huwa tunakamatwa na kupigwa na Askari Kwa mfano tukio la mwisho la kuvunjiwa nyumba walikamatwa wanakijiji 15 wakaambiwa kuwa wao ni wachochezi badala ya kupelekwa kituo Cha polisi walipelekwa Serengeti huko mbugani walichapwa chini ya miguu na kurudishwa nyumbni mpaka Leo wapo ndugu zetu hawawezi kuvaa viatu. Aliyeongoza utekelezaji huu ni OCS Fatma Juma na mara kadhaa amekuwa akisema ni Bora hao wakenya kuliko sisi watanzania maskini.

Kumbuka kipindi chore hiki tume haikurudi tena mpka mwaka Jana 2022 mwezi wa kumi.

Walipofika waliotupa semina juu ya matumizi Bora ya Ardhi na zoezi la kupima na kuweka mipaka kwenye vijiji.

Tulipima vizuri na kuweka bekon na majirani zetu isipokuwa tatizo likatokea kwenye lile eneoa mgogoro.

Tulifanya vikao vingi sisi tukawa tunasimamia maamuzi yale ya Mhe waziri ya mwaka 2013, lakini wenzetu wakakataa na kusem maaamuzi Yale ni ya kisiasa na kihistoria.

Wenzetu wakasimamia mipaka ya NGOs na Laigwenan ambayo inachukua kitongoji chetu kizima, vyanzo vyetu vya maji na mashamba yetu ya siku zote. Lkini pia mpka wao waliodai ni WA Laigwenan na NGOs za LADOW, NA PWC zililenga kututoa kwenye mpaka wa kimataifa wa Tanzania na Kenya.

Kwenye kikao cha tar 2 /12/2022 kilichoongozwa na Mkurugenzi wa Land use Bwana Jonas Nestori Masingija na DC wa Ngorongoro mwalimu Raymond Mangwala walikana maaamuzi ya Mhe waziri na kukubali maamuzi ya NGos. DC Mangwala aliunga mkono kuwa maamuzi ya Mhe waziri Tibaijuka ni Historia na siasa.

Tulipinga lakini walitutukana na tutuita wezi, wapumbavu na wasiokuwa na busara. haya aliyasema DC Raymond.

Tarehe 10/12 2022. Mkurugenzi wa matumizi Bora ya Ardhi na mipaka Jonas Nestori Masingija akiwa na tume ya usalama Wilaya wakiongozwa na OCD Lusesa wakaenda kuweka bekon Kwa nguvu pasipo kutushirikisha

Hapo ndipo tulipoamua kwenda Dodoma.

Tulienda wizara 3 ambazo ni Ardhi, Mambo ya ndani na TAMISEMI Kwa ajili ya hicho kitongoji haramu.

Mimi nikiwepo Mhe waziri wa Ardhi Dkt Angelina Mabula alimuamuru Prof Magige ambaye ni Mkurugenzi mkuu wa land use atekeleze ombi letu la kubatilisha maamuzi ya tume yake na kuamuru ramani itumike kuweka mipaka.

Hiyo ilikuwa ni tarehe 27/12/2022 alimuamuru ifikapo January 2023 awe amempelekea ripot Mhe waziri lakini mapaka Leo hajafanya lolote tukimkubusha anadai maandalizi ya tume Bado mwisho wa siku akawa hapokei simu zetu.

Kuhusu TAMISEMI waligundua kitongoji ni batili na taratibu za kukifuta zitakamilika mwezi wa huu tarehe 14.

Kuhusu mambo ya ndani tulilalamikia askari wanaolima maeneo yetu pamoja na wahamiaji haramu lakni hawajatujibu.

Lakini pia mwezi January walifika waandishi habari wa ITV wakiongozwa na Khalifani Lihundi walifika Kijijini na tukatoa malalamiko yetu kwenye vyombo vya habari ( nitakutumia clip)

Kilichotushangaza
Tare 9 mwezi wa 2 akaja OCD Peter Lusesa Kijijini kwetu akatuuliza nani alituongoza kwenda Dodoma? Na ni Nan alituruhusu tuzungumze na vyombo vya habari?

Akaahidi atatukamata walioenda Dodoma na waliozungumza na vyombo vya habari.

Wiki iliyopita Kijiji wakakubaliana kuhamisha wahamiaji wa ndani ambao sio wakenya baada ya hao wageni kuhusishwa na wizi wa mifugo.

Walihalimishwa na mifugo yao na OCD alisapoti wahame lakn baadae walirudi tena pasipo kufuata utaratibu walioambiwa na serikali ya Kijiji ikiwa ni pamoja ja barua za utambulisho
Kutoka vijiji vyao.

Waliporudi tena wakahamisha tena na mifugo yao lakini fance na nyumba zao zikaondolewa.

Walienda kulalamika kuwa nyumba zimevunjwa na mali zao zimeibiwa.

Hapo ndipo OCD alipotumia nafasi kuwakamata viongozi wetu na kila nae enda kuwawekea mdhamana anakamatwa na kuwekwa ndani.

Mpka Sasa hivi wamefika 17 na tumepokea taarifa kuwa kati hao mmoja aliyekuwa kiongozi wa msafara kwenda Dodoma amepigwa na kuumizwa vibya sana na Hali yake sio nzuri.

Tunaomba Serikali tusaidie Wanakijiji hawa waachiwe.
IMG_8856.jpeg
IMG_8857.jpeg
IMG_8858.jpeg
IMG_8853.jpeg
IMG_8854.jpeg
IMG_8855.jpeg
IMG_8850.jpeg
IMG_8851.jpeg
IMG_8852.jpeg
IMG_8847.jpeg
IMG_8848.jpeg
IMG_8849.jpeg
IMG_8844.jpeg
IMG_8845.jpeg
IMG_8846.jpeg
IMG_8841.jpeg
IMG_8842.jpeg
IMG_8843.jpeg
IMG_8838.jpeg
IMG_8839.jpeg
IMG_8840.jpeg
IMG_8835.jpeg
IMG_8836.jpeg
IMG_8837.jpeg
IMG_8832.jpeg
IMG_8833.jpeg
IMG_8834.jpeg
IMG_8831.jpeg
 
Aisee...!

Mpaka kufikia hatua hii watu kuweka wazi migogoro rahisi kama huu inayopaswa kutatuliwa kwa kufuata mifumo ya kiutawala, basi hii ni ishara ya wazi kuwa mifumo na mamlaka zinazozohusika zimeshindwa kufanya kazi kushughulikia kero na matatizo ya wananchi hawa kiasi cha kupelekea upotevu wa maisha (vifo) vya watu visivyokuwa na sababu....

Poleni sana. Tunatumaini viongozi na mamlaka husika zitachukua hatua ikiwemo kuwajibika kwa walioshindwa kutenda wajibu wao..
 
Serikali iamke. Wahamiaji haramu wanalindwa na jeshi la polisi kwa maslahi ya askari.

Mama weka ukali japo kidogo.
 
Ingekuwa hoja kuhusu siasa ving'ora na vuvuzela vingepigwa vingi mno watu wanashindwa kutambua kuwa uhai ndiyo msingi wa yote hayo,jamani viongozi husika mbona hamsaidii watu hawa au kwa kuwa hao wahamiaji haramu wanatoa rushwa?
 
Safi sana JF. Mtaokoa maisha ya hawa watu. Ila kwa awamu hii ya Samia najua huyo mafia aliiyewaeka ndani ataendelea kula kiyoyozi tu. Nchi haina Rais
 
Safi sana JF. Mtaokoa maisha ya hawa watu. Ila kwa awamu hii ya Samia najua huyo mafia aliiyewaeka ndani ataendelea kula kiyoyozi tu. Nchi haina Rais
Nchi hii yaan polisi wamekua ni kichaka cha ukatili sijui ni nini kimeitokea hyo sehemu ya polisi, watu wanakufa mahabusu kwa kupigwa, watu hawana amani mbele ya polisi tena
 
Miaka yote hiyo hajawahi kutokea kiongozi mwenye akili ya kumaliza huu mgogoro! Prof Tibaijuka ndio pekee alitoka na suluhisho lakini nalo limefutwa na viongozi wengine!

Nchi moja, lugha Kiswahili, viongozi wengi wale wale, Chama kile kile! Sarakasi zile zile!

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Hivi inakuwaje Ocd anakaa eneo moja muda mrefu hivi hapo hawezi kutoa msaada zaidi ya kuegemea upande wa wenye pesa.
 
Raia unatakiwa uchukue tahadhari na usalama wako mambo yamebadilika hii sio serikali ya kuwajibishana, hawa ni wale waonevu na waporaji wa haki za raia hasa maskini.

Kila sehemu serikalini imeoza ghafla, huku uraiani watu wameamua kutafuta distraction zingine kuondoa hasira za uongozi mmbovu, hakuna wakukulinda ukijifanya unatafuta haki kuna wenye uwezo na mamlaka yakukudimiza tu.
 
Umeandika uwongo mtupu.
Chuki zako za kisonjo dhidi ya wamasai wa loita ndizo zinazokusumbua.
Utawaitaje wamasai wa engusero sambu ni wakenya???
Poor,poor.
Na mkamatwe tena
 
Kifo cha ocd wala hakijasababishwa na huu mgogoro .

Jamaa kaungaunga sana matukio kwa interest zake binafsi
Kifo cha OCD kilisababishwa na nini? Naomba kujua sababu unaonekana una taarifa zaidi.
 
Back
Top Bottom