Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

Bongo sheria ni kitu kingine na utekelezaji ni kitu kingine. Ni rahisi hapa bongo kupindisha sheria zilizopo kum-favor fulani au vinginevyo ili mradi maslahi ya watu wahusika yamelindwa bila kujali nani anakwazwa!
 
Mtoto wa Wachwi wa Swanga hapa nafikiri ulimi umeteleza na ukimuita ajieleze atalia maana anawaonea huruma waliojenga kwenye hifadhi ya barabara na 2015 anahofia kura zinaweza zisitoshe kwa hiyo njia rahisi ni kupindisha sheria na kucarry forward majukumu ya serikali kujenga na kuboresha miundo mbinu ya Dar es Salaam na pwani.

Kifupi wakati Magufuli anatimiza kazi yake Pinda alikuwa anapiga siasa naninadhani haikuwa busara kumsitisha Magufuli kupitia vyombo vya habari badala ya kutuimia internal memos na vikao vya majadiliano.

Poor them wanazidi kukanganyana
 
Kiutaratibu si sawa kuliongelea hadharani jambo kama hili....angempigia simu tu na kumpa ujumbe....sasa yeye Pinda ameliongelea hadharani tena mbele ya wapiga kura wake ni kum-downsize...halafu hili la kumtembelea mama yake linanikumbusha Makamba alipomtembelea mama mzazi wa Sitta
 
Tumesikia katika vyombo vya habari kuwa Pinda kamsimamishama Magufuli asiendelee na zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa pembeni mwa barabara kinyume cha sheria au kupisha upanuzi wa barabara kwa ajili ya kupunguza msongamano.
Hivi hii ni sawa?

Kwani wanavyoboa wanapesa za kuanza ujenzi mara moja au ni kuwataabisha tuu wananchi?
 
Agizo la waziri mkuu alilolitoa kwenye mkutano wa hadhara huko Chato linalomtaka waziri Magufuli kusitisha mara moja bomoa bomoa ya majengo yaliyoko kwenye hifadhi ya barabara, linamweka waziri huyo kwenye mtihani mkubwa. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati anaingia madarakani aliapa kulinda na kusimamia sheria za nchi; hivi sasa akionekana kutii agizo la Pinda ili kulinda kibarua chake, na hivyo kushindwa kuisimamia sheria, watu wengi makini watamwona kuwa ni mtu hasiyekuwa na msimamo.
 
Tatizo ni kwamba sheria wametunga wao ila wanaona aibu kuzisimamia! Hivi ni nchi gani duniani itaendela bila kuchukua maamuzi magumu na kufuata utawala wa sheria?? Pinda ameteleza sana, sasa foleni itaisha lini ikiwa hata hatua za mwanzo za kupanua barabara zinazuiwa kwa sababu za kisiasa zisizokuwa na maslahi ya umma! Tanzania ni nchi ya ajabu sana.....
 
Wazee nimesikia kwenye taarifa ya habari usiku huu kupitia RFA kwamba Waziri Mkuu Mizengo Pinda amesitisha ubomoaji wa majengo yaliyojengwa ndani ya hifadhi ya barabara nchini kote.

Najua ubomoaji huo ulikuwa unafanywa kwa amri ya Mhe. Pombe Magufuli. Hii amri ya Pinda, imekaaje wazee? Au ndiyo mwendelezo wa tabia ile ile ya serikali yetu ya sasa ambapo kila kiongozi anafanya kazi na kutoa statements kadri anavyojisikia?

Mhe. Magufuli atajisikiaje?

....pinda kapindamana!!!!
 
Insubordination of Magufuli at its highest degree for 2015....... tena kwa kumtumia kiranja mkuu..... CCM hureeeeee............. Kwa wana-mapinduzi lets applaud CCM.....

.....off you vanish!!!! you may applause it yaself!!!!! shudu!!!
 
Hatutapiga hatua yoyote ya maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu kama tutaendelea kubembelezana unavyotaka. Tumekua wa hovyo mno. Tunavunja sheria na taratibu,alafu tunajitetea ujinga. Wengi wa hao unaosema wanaonewa ni ama waliingizwa chaka na wamiliki wa maeneo hayo ambayo tayari walikwisha fidiwa ama walijenga kibabe wakijua watapata utetezi wa wanasiasa aina ya Pinda siku nyumba zao zikitaka kubomolewa.

....yes mkurugenzi!!! hapo umenena!!!!
 
Jamani msisahau kuwa wizara ya ardhi ilishawahi kuwa chini ya bwana RICHMONDULI mnategemea kuna usafi huko??? Magufuri anataka kubomoa nyumba zilizo kwenye viwanja vilivyotolewa chini ya RICHMONDULI watu wameguswa tu wakakimbilia kwa mzee na kumwambia mbona sasa tunaondolewa na ndipo mizani ikamwegemea Magufuri.TOKA MAGUFURI MUNGU AKUONE, VINGINEVYO UTAFIA KTK KIBANDA CHA CCM hutang'ara kama DR.wa ukweli, mkombozi wa taifa hili
 
hapa sio mambo ya kuonyesha mababe....Magufuli atumie busara, Pinda ni boss wa Magufuli ki katiba pia, sidhani kama maendeleo ndio yamefikia mwisho......CCM inahitaji barabara zi jengwe kwa ajili ya campaign zijazo na pia makandarasi (wahisani wa kampeni zao pamoja na 10% ) wagawane mshiko....

cha maana ni Magufuli kujua sababu za msingi za kusimamisha na pia nini kinafuata ....kama Pinda akishindwa kutoa ushirikiano basi Magufuli ateme mzigo!
 
Pinda kapewa maagizo na chama chake ampige stop mshikaji mbele ya wapigakura wake, kampeni za urais 2015 mchakato wa makundi umeshaanza ndani ya CCM kama mlikuwa hamjui. yaani kamfanya mshikaji ka mbwatukaji tu anafanya maamuzi bila reaserch yeyote duh..ningekuwa mimi uwaziri wao nautema kutunza heshima yangu kwa wananchi.
 
Juzi nilikutana na jamaa fulani na kunieleza hatua waliyochukua wakazi wa KIMARA kwa kushirikiana na mbunge wao Mheshimiwa Mnyika kwamba wamemwandikia barua Waziri Mkuu juu ya Bomoabomoa ya maeneo ya Kimara, mbezi na Kibamba. Madai ya wahanga wengi ni kwamba; wengi wao wana hati za umiliki wa viwanja vyao. Katika barua yao walimtaka waziri mkuu kutoa majibu ndani ya siku sita, baada ya hapo jamaa walikuwa wanajiandaa kuandamana mpaka kwa Waziri Mkuu kufuata majibu yao. Inawezekana huu ni utekelezaji wa barua hiyo.
 
Nadhani kilichowashtua ni mpango wa Magufuli kwamba nyumba za serikali zitabomolewa pia-wizara ya maji, ofisi ya mkuu wa mkoa etc. Lakini kwanini Pinda aliongelee kwa wapiga kura? Eti wanasubiri baraza la mawaziri, kwanini naye hakusubiri baraza kabla ya kutamka hadharani kumpiga stop Magufuli? Serikali hii imechanganyikiwa!
 
agizo la waziri mkuu alilolitoa kwenye mkutano wa hadhara huko chato linalomtaka waziri magufuli kusitisha mara moja bomoa bomoa ya majengo yaliyoko kwenye hifadhi ya barabara, linamweka waziri huyo kwenye mtihani mkubwa. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati anaingia madarakani aliapa kulinda na kusimamia sheria za nchi; hivi sasa akionekana kutii agizo la pinda ili kulinda kibarua chake, na hivyo kushindwa kuisimamia sheria, watu wengi makini watamwona kuwa ni mtu hasiyekuwa na msimamo.
kosa la magufuli alishindwa kutambua kuwa mabso wake ni waziri mkuu na rais akaanza kutukuza vyombo vya habari kuliko mabosi wake, kila kukicha mabosi wake wanasikia tu mara hili kesho mara lile, yaani hata briefing hamna. Ikabdi afungwe gavana kwanza.
 
Yale yaliyomkuta spika wa bunge la tisa, Samuel Sitta sasa huenda yakamkuta waziri wa ujenzi Joni Magufuli.Inaaminika Sitta aliwekwa pembeni kwa hila katika kinyang'anyiro cha uspika kwa sababu tu"ya kusimamia bunge la tisa katika misingi ya uwazi,haki,viwango na kuisimamia serikali vizuri.

Sitta alienguliwa kwenye kinyang'anyiro cha uspika wa bunge la kumi kutokana kile ambacho ccm walikiita "mda umefika kwa wanawake kuongoza mhimili ya serikali" lakini ukweli wa mambo zile zilikuwa ni hila za kumwanusha bwana Sitta" zilikuwa njama za mafisadi waliojeruhiwa na bunge makini la tisa"

Pinda waziri kuu amemdhoofisha bwana Magufuli kwa kutoa amri ya kusimamisha zoezi la kubomoa nyumba zilizojengwa karibu na hifadhi ya barabara. Awali magufuli alikuwa ametoa amri ya kubomoa nyumba ambazo zimejengwa maeneo ya hifadhi ya barabara.

Amri ya magufuli ipo katika misingi ya sheria za nchi ambazo kamwe hazitakiwi kuvunjwa wala kupindishwa kama amri ya Pinda alivyopindisha. Lakini bwana Pinda ameamua tu kumdhoofisha, kumdhalilisha maghufuli mbele ya umma wa watanzania. Pinda anatumiwa,pinda yupo kimkakati.

Wakati sasa wakosaji na waliovunja ile sheria ya kujenga kwenye hifadhi ya barabara wanamzomea Magufuli anaonekana kachemka ukizingatia Pinda aliotoa amri hii ya kinafiki akiwa jimboni kwa Magufuli.

Lakini kuna haja ya kutafakari kwa undani juu ya kile kilichomsukuma Pinda kutoa amri ya kupindisha taratibu,kama anasukumwa, basi ni kwa maslahi ya nani.Pinda amenukuliwa na gazeti la mwananchi akisema bomoabomoa isimishwe kwanza mpaka hapo baraza la mawaziri litakapoketi kujadili suala hilo. Magufuli anateleza sheria ambazo zimewekwa na bunge kwa niaba ya wananchi.

Kabla ya kupelekwa bungeni baraza la waziri liliridhia sheria hiyo. pinda anataka kuwaaminisha kwamba Magufuli anakurupuka ,amri ya kubomoa haina baraka za baraza la mawaziri.

Kule kukaa tena kwa baraza la mawaziri ni kwa maslahi ya nani. Mafisadi?

Serikali hii imelala, inathibitiwa na mafisadi kwa "REMOTE"

Pole sana Magufuli kwa kudhalilishwa na bosi wako pinda,chukua maamuzi magumu. Fanya kama Martha Karua, aliyekuwa waziri sheria wa kenya katika serikali ya mseto.

(1) Amri ya magufuli ipo katika misingi ya sheria za nchi ambazo kamwe hazitakiwi kuvunjwa wala kupindishwa NAOMBA UTO THIBITISHO WA KAULI HII

(2) Lakini kuna haja ya kutafakari kwa undani juu ya kile kilichomsukuma Pinda kutoa amri ya kupindishataratibu NAOMBA UTOE USHIHIDI WA PINDA KUPINDISHA TARATIBU

(3) Magufuli anateleza sheria ambazo zimewekwa na bunge kwa niaba ya wananchi. KWAHIYO MAGUFULI KAJITEUA MWENYEWE KUWA WAZIRI, ANA WAKU WAKE ANAOPASWA KURIPOTI KWAO NA WANAOPASWA KUCHUKUA HATUA ENDAPO KUNA KASORO ZOZOTE KATIKA UTENDAJI WAKE?
WAZIRI MKUU KWA KUTAMBUA UNYETI WA SUALA HILI AMELIAMBIA TAIFA BARZA LA MAWAZIRI LITAKKA KUJADILI, LAKINI WEWE KIBANO DICKSON UNATHIBITISHA KUWA BARAZA LA MAWAZIRI LIMEWAHI KUKAA NA KUMPATIA BARAKA WAZIRI MAGUFULI KUBOMOA NYUMBA ZA WANANCHI ANAVYOPENDA? JE UNAWEZA KUTUAMBIA LILIKAA LINI NA WAPI?

USHAURI ULIOUTOA KWA MAGUFULI WA KUJIUZULU NI MUAFAKA KABISA KWA MAKOSA YAFUATAYO:-
A) KULIDANGANYA TAIFA KUWA MABANGO YA MATANGAZO YANASABABISHA AJALI ZA BARABARANI HIVYO YAONDOLEWA NA KUACHA MAGARI MABOVU YANAYOTELEKEZWA BARABARANI YAKIENDELEA KUSABABISHA AJALI NA KUUA NA KUJERUHI
B) KULIDANGANYA TAIFA KUWA WANANCHI WALIOJENGA NJE YA FUTI 75 KATI YA UBUNGO HADI KIBAHA WAPO KATIKA HIFADHI YA BARABARA WAKATI AKIJUA SIO KWELI HATA KIDOGO KWA MUJIBU WA VIFUNGU 15 NA 16 VYA SHERIA YA ARDHI YA VIJIJI NAMBA 5 YA 1999 ALIYOSHIRIKI KAMA MBUNGE KUIPITISHA.(SOMA KIAMBATANISHO)
C)KULIDANGANYA BUNGE LA FEBRUARI 2011 KUWA HIFADHI YA BARABARA JIJINI DAR ES SALAAM NI FUTI 400 WAKATI KANUNI ZILIKWISHA BADILIKA NA ENEO HILO KUBAKI MITA 60 TU.
 
Back
Top Bottom