Waziri Mkuu Pinda asitisha utekelezaji wa agizo la Magufuli la Bomoa bomoa

ccm inataka wachovu sio wafanyakazi. Sasa dr magufuli anafanya kazi wanaingiza siasa. Kazi na siasa havichanganyiki. Na ndo maana miji iko kiholela tu, foleni, kila kitu vululuvululu. Kama vipi dr jiuzulu waachie serikali yao.

kazi gani kama vile kubomoa peterol station kwa madai iko kati hifadhi ya barabara halafu serikali ilazimike kulipa bilioni 3 kama fidia?
 
Kimsingi Mheshimiwa Pinda ni boss wake Magufuli, hatupingi kwa hali ilivyo kwa sasa, taifa hili lenye matatizo lukuki na makali ya umeme si wakati muafaka wa Ndugu Magufuli kupiga chini nyumba zilizoko pembeni mwa barabarani kinyume cha sheria kwa sasa. Labda kisiasa zingeachwa hadi baadaye kidogo baada ya Serikali kutatua matatizo ya kiuchumi, hali ngumu ya maisha na kujibu maswali magumu yaliyo mezani kwao.

Nilitarajia ndugu Pinda amshukuru ndugu magufuli kwa ujasiri wake wa kusimamia sheria za taifa hili kwa ujasiri mbele ya wapiga kura wake.

Baadaye ndug Pinda angemshtua kijane wake ofisini wadiscuss ndani kisha amwache kijana apostpone amri yake mwenyewe. Kazi ya ndg Magufuli ni ndg Pinda. Angetumia busara kidogo kujenga ushikamano ndani ya serikali.

Kwa hali hii.... Sisi wananchi tuwaelewe vipi?

Waheshimiwa penda si msipende kwa upeo wetu sisi watanganyika wa kawaida tunajifunza kwamba ukiwa na moyo wa kufanya kazi na kutumikia taifa kwa moyo wote basi serikali hii si mahali pake.

Mungu baba utuongoze kwa kila kitu.

si wakati muafaka wa Ndugu Magufuli kupiga chini nyumba zilizoko pembeni mwa barabarani kinyume cha sheria kwa sasaUKIACHA PRPAGANDA ZA MAGUFULI UNAO USHAIDI MWINGINE WOWOTE KUWA NYUMBA ZA WANANCHI ZIPO PEMBENI MWA BARABARA KINYUME CHA SHERIA?
 
Kuna mtu alisema na leo napenda nirejee tena kwamba 'huwezi ukawa ccm na ukaendelea kuchapa kazi zako kwa uhuru huku ukizingatia sheria'. Hiki chama kimeshikwa na kikundi kidogo cha watu. Ukifanya kinyume na matakwa yao lazima ukione cha mtema kuni. Magufuli anadhani anaweza kuendelea na style yake chini ya jk!! Amenoa!

huku ukizingatia sheria TUACHE USHABIKI, NAOMABA UNITHIBITISHIE NI SHERIA ZIPI ANAZOZINGATA MAGUFULI ILI TUMPIME? ZITAJE HAPA.
 
Hatutapiga hatua yoyote ya maendeleo ya ujenzi wa miundo mbinu kama tutaendelea kubembelezana unavyotaka. Tumekua wa hovyo mno. Tunavunja sheria na taratibu,alafu tunajitetea ujinga. Wengi wa hao unaosema wanaonewa ni ama waliingizwa chaka na wamiliki wa maeneo hayo ambayo tayari walikwisha fidiwa ama walijenga kibabe wakijua watapata utetezi wa wanasiasa aina ya Pinda siku nyumba zao zikitaka kubomolewa.

tayari walikwisha fidiwa ama walijenga kibabe wakijua watapata utetezi wa wanasiasa aina ya Pinda siku nyumba zao zikitaka kubomolewaTOA UTHIBITISHO WA KAULI YAKO HIYO.
 
Tatizo la kwanza ni kwamba mfumo mzima wa utendaji katika serikali ni mbovu. sasa lazima tuanzie mahali fulani kurekebisha hilo. miradi mbalimbali ya usafiri kama ule wa mabasi yaendayo kasi, inategemea kuwepo na nafasi ya kujenga barabara. ilikuwa ni juu ya serikali kuhakikisha kwamba maeneo hayo hayajengwi. kosa ndio liko hapo.

lakini lingeweza kurekebishwa bila kumuadhiri Magufuli kiasi hicho. unajua hii ilikusudiwa kuwa ngumi ya kumuumiza magufuli as much as possible. lugha aliyotumia Pinda, mahali alipochagua kutoa tamko hilo, yote ni designed to exact maximum pain and punishment to Magufuli

tayari walikwisha fidiwa ama walijenga kibabe wakijua watapata utetezi wa wanasiasa aina ya Pinda siku nyumba zao zikitaka kubomolewaMOJA YA SABABU ZILIZOFANYA APIGWE STOP NI KUTUMIA SERIKALI NA MIRADI YAKE KUSAMBAZ PROPAGANDA ZAUONGO. WAFADHILI WA MARADI WA MABASI YA KWENDA KAZI NA SERIKALI MWAKA 2008 WALIWALIPA FIDIA WATU WOTE WALIOKUWA WAKIISHI KATIKA ENEO AMBALO AWLI MAGUFULI ALILIITA HIFADHI YA BARABARA. KWA MARA YA KWANZA KATIKA HISTORIA YA TANZANIA FIDIA HIZO ZILIZINGATIA SHERIA YETI YA ARDHI NA FIDIA KIKAMILIFU KWA KUWAHUSISHA WAPANGAJI NA WATU WALIOKUWA WAKITUMIA MAJENGO HUSIKA KUZALLISHA MALI WALILIPWA FIDIA YA UPOTEVU WA FAIDA. WAKATI HUO MAGUFULI ALIKUWA KATIKA WIZARA ZINGINE, HAIKUWA RAHISI WATANZANIA WENGI KUJUA HILO KWA KUWA HAPAKUWEO MALALAMIKO, WANANCHI WALIBOMOA WENYEWE NA KUHAMA. MAMA NTILIE ALITOKA NA MGAHAWA, MWENYE GROSARI ALITOKA NA BAA.

DESEMBA 2010 MAGUFULI ALIPOREJESHWA WIZARA YA UJENZI AKAANZA KUTUMIA JINA LA MRADI HUO MZURI MUWABOMOLEA WATU NYUMBA ZAO, NYUMBA ANAZOTAKA ZIBOMOLEWE ZIKO MITA 120 KUTOKA KATIKA YA BARABARA. NYUMBA HII INAHUSIKA VIPI KATIKAMKUSABABISHA MSONGAMANO WA MAGARI? MAGUFULI ANA AJENDA YA SIRI .
 
Mgufuli kafungwa gufuli! Tuone sasa kama ubavu anao, yale yaleeeee...ya kufyata!
 
Pinda anatumiwa na mafisadi kudhoofisha wachapa kazi na wapinga ufisadi. Hatimaye ameingia kwenye mtego wa RA.

Ila alichofanya Magufuli si kosa kwani alikuwa anafanya hivyo kwa kufuata sheria, kanuni na taratibu. Lakini kikubwa zaidi ni kuwa bomoa bomoa hiyo ni lazima itekelezwe ili kupisha miradi ya upanuzi wa barabara. Kusema kuwa suala la bomoa bomoa lisubiri baraza la mawaziri na bunge maana yake ni kusitisha ama kuchelewesha utekelezaji wa miradi hiyo na hivyo kuchelewesha maendeleo. Kwa maneno mengine huku pia ni kushindwa kutatua kero za wananchi kama vile foleni.

Kingine ninachokiona hapa ni kuwa Magufuli ana-fit popote anapowekwa. Hiki kinawachukiza wakubwa zake. Hawapendi kufunikwa na mtu wa chini yao. Wakati ule magufuli alifanya vizuri sana kwenye wizara ya ujenzi/miundombinu enzi za mzee wa utandawazi, alipokuja mkwere kwa kujua kuwa jamaa atakuwa maarufu zaidi yake akamwamishia wizara ya ardhi akidhani kuwa huko atakuwa "amemficha". Haikuwa kama alivyodhani, akamtoa tena na kumwamishia wizara ya mifugo na uvuvi kwa lengo lile lile "kumficha" tena akidhihaki kuwa "Magufuli nampeleka wizara ya kitoweo". Jamaa aliibua mambo ambayo hatujawahi kuyasikia na kuipa uhai wizara hiyo ambayo ilikuwa kama imekufa.

Baada ya kusoma mazingira na hali ya nchi pamoja na mi-ahadi mkwere akaamua kumrudisha mchapakazi huyu kwenye wizara yake ili atekeleze yale maahadi yake lukuki. Sasa wanaona ameanza wanamfunga luku. Shame on them.
 
mkiendelea kuleta thread za Pinda na JK mnanitafutia ban humu JF, nadhani mmenichoka maana naandika huku maneno mabaya yamejaa mdomoni. basi bwana naishia hapa
 
Kimsingi Mheshimiwa Pinda ni boss wake Magufuli, hatupingi kwa hali ilivyo kwa sasa, taifa hili lenye matatizo lukuki na makali ya umeme si wakati muafaka wa Ndugu Magufuli kupiga chini nyumba zilizoko pembeni mwa barabarani kinyume cha sheria kwa sasa. Labda kisiasa zingeachwa hadi baadaye kidogo baada ya Serikali kutatua matatizo ya kiuchumi, hali ngumu ya maisha na kujibu maswali magumu yaliyo mezani kwao.

Nilitarajia ndugu Pinda amshukuru ndugu magufuli kwa ujasiri wake wa kusimamia sheria za taifa hili kwa ujasiri mbele ya wapiga kura wake.

Baadaye ndug Pinda angemshtua kijane wake ofisini wadiscuss ndani kisha amwache kijana apostpone amri yake mwenyewe. Kazi ya ndg Magufuli ni ndg Pinda. Angetumia busara kidogo kujenga ushikamano ndani ya serikali.

Kwa hali hii.... Sisi wananchi tuwaelewe vipi?

Waheshimiwa penda si msipende kwa upeo wetu sisi watanganyika wa kawaida tunajifunza kwamba ukiwa na moyo wa kufanya kazi na kutumikia taifa kwa moyo wote basi serikali hii si mahali pake.

Mungu baba utuongoze kwa kila kitu.

Well said...; this would have been a logical and sound approach :painkiller:
 
Haya mambo ya SIASA yanashangaza sana hasa siasa zinapotumika kwenye masuala ya kitaalamu. Najua Magufuli ni mhandisi, najua kwamba anajua namna gani anaweza kuliepusha taifa na gharama zisizokuwa na msingi. Hivi kuvunja kwa mfano jengo la Tanesco Ubungo ni cost effective?
Hawa ndiyo wanatufanya mara nyingine tuamini kwamba SIASA ni uvuvuzela.
 
huwezi fuata sheria ukiwa ndani ya ccm. ccm hakuna haki na kufuata sheria. if you are of that type they sacrifice you.
i wonder if magufuli will still call himself a minister. a toothless minister
 
Sijui hata huyu magufuri atafanyaje manake alibanwa kwao kabisa yaani. Nimegundua kwanini tibaijuka aliacha kuongelea suala ya majumba ya dar kubomolewa nadhani alikanywa naye!
 
hapo pinda kamdhalilisha tu magufuli, na mwishowe anayeonekana hasimamii watu wake ni JK. nchi inaongozwa kutokea barabarani
 
Kiukweli sishangai kwa mtu kama pinda kutamka hayo , ni mtu anayeropoka tu any way tuachie hapo maana ke anaudhi kama nini mpaka tunamkumbuka eddyL
 
Sisi ni CCM. we unaleta sifa kuwazidi wengi hata kiranja mkuu na heady teacher. Kaa kimya.

teh teh
 
Don't worry Dr Magufuri, we Tanzanians know that wewe ni mchapakazi wa ukweli na si mbabaishaji.Huyo jamaa called Pinda anafanya hiyo stop kisiasa zaidi na siyo kwa ajili ya manufaa ya taifa kwa baadae.Isitoshe tunahisi tunahisi wanakuonea wivu kwa sababu ya utendaji wako uliotukuka, na hivyo wanataka wakudhoofishe.Ukiona mizengwe inazidi achana na CCM na ujiunge na chama chochote utakachoona kinamuelekeo na dira ya kuongoza nchi.Mya God bless your, I salute you Dr Maguduri.
 
Agizo la waziri mkuu alilolitoa kwenye mkutano wa hadhara huko Chato linalomtaka waziri Magufuli kusitisha mara moja bomoa bomoa ya majengo yaliyoko kwenye hifadhi ya barabara, linamweka waziri huyo kwenye mtihani mkubwa. Hii inatokana na ukweli kwamba wakati anaingia madarakani aliapa kulinda na kusimamia sheria za nchi; hivi sasa akionekana kutii agizo la Pinda ili kulinda kibarua chake, na hivyo kushindwa kuisimamia sheria, watu wengi makini watamwona kuwa ni mtu hasiyekuwa na msimamo.

Pinda ameingia kwenye mtego wa mafisadi. Na ndio maana ameamua kumdhalilisha mchapakazi magufuli tena kwenye jimbo lake la uchaguzi mbele ya wapiga kura wake. Ni sawasawa na baba kutukanwa nyumbani kwake mbele ya wapiga kura wake. Kazi ipo.
 
Sitaki kuamini kama Pinda alimaanisha alichokisema. Nionavyo mimi ni kama vile alikuwa anafurahisha baraza mithili ya tamthiliya ya Jiji na Wamachinga.
 
Back
Top Bottom