Nilivyoilewa hati ya mashitaka, si kwamba Pinda anashitakiwa bali unatafutwa ufafanuzi wa kisheria wa wa vifungu vya katiba, kama ifutavyo: (1) Ibara ya 100(1) inayowapa wabunge uhuru (uso kikomo) kujadili ndani ya bunge hata mambo ambayo yanavunja haki ya watu wengine bila kushitakiwa ambayo wanadai inakinzana na ibara ya 13(2) ya katiba, inayokataza ubaguzi katika sharia yoyote. Wanaomba mahakama itamke kuwa ibara ya 100(1) inakinzana na ibara ya 13(2). (2) Mahakama itamke kama kauli ya Pinda, ya kuwataka polisi wawapige watu wanaokiuka amri zao, nayo inalindwa na kinga ya kutoshitakiwa kwa mujibu wa ibara ya 100(2) ya Katiba ya JMT ya mwaka 1977.