Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

Mheshimiwa Waziri Mkuu Wakifanya fujo Wananchi wako wewe Piga tu kama anavyopigwa punda mbishi...........







Kama anavyopigwa Pinda/Punda mbishi, kwa hiyo naye Punda/Pinda tumpige si ndiyo? Huyu mtu kweli ni janga la taifa sawa tu na bosi wake.
 
Last edited by a moderator:
Tusigeuke kuwa mahakimu madamu limeshatinga mahakamani tusubiri, ila naamini hakuna hoja ya msingi hapa sana sana, huyu mama BISIMBA anaendeleza tu kule kutumiwa na wanasiasa kuishambulia serikali kwani yapo mambo mengi yanayokiuka haki za binadamu tena yanayofanywa na wanasiasa hayaoni.

Ndo uwezo wako wa kufikiri umeishia!
 
Dr Hellen Kijo Bisimba ni mwanamke na kiongozi bora Tanzania
 
Cha ajabu waheshimiwa wengine wanajitokeza kutetea kauli yake ili mradi tuu wasionekane wapo against naye.
 
safi sana pinda hiyo ndiyo misimamo ya kiumeni twende kazi huyu bibi hana jipya kajaza meno mdomoni tu.
 
Nakumbuka wakati Lowassa anateuliwa kuwa PM wa Tanzania kulikua na maneno mengi kwamba aliye stahili nafasi hiyo alikua Mizengo Peter Pinda,baada ya Lowassa kuanguka,utabiri ukatimia!

Miaka takribani 4 ya utawala wa Pinda imethibitisha kwamba ni mtu ambaye hakustahili kupata nafasi hiyo. Serikali imekua dhaifu kupindukia. Kwangu mimi nimejifunza kwamba hakuna mfumo wa kupima na kutambua kiongozi bora ni mtu wa aina gani kwasababu Pinda alivishwa sifa zisizo mstahili.
 
Imeniuma sana kauli yake, na mifugo itafanywaje ka binadam anambiwa apigwe.
 
we waajabu kweli hukumu mbona haijatoka,huyu bibi mwehu yeye afanye mpango akagombee uenyekiti bawacha sote twajua kuwa chadema ndiyo wanampotosha ila atavitandua tu vitanda alivyotandika.

Ewe kipofu,jiulize mwenyewe:
1.Waliompeleka Sugu mahakamani kw kumpa sifa PM aliyostahili yaani kumwita --------
ni kina nani?

2.Walikuwa wanatumiwa na nani?

3.Walikuwa wanataka umaarufu wa nini?

4.2015 watachukua fomu kugombea ubunge Mbeya mjini.

5.Ni jinai huyo Dr Bisimba kugombea Urais?
 
SASA DPP naye anachekesha na kujidharirisha aisee! Eti alisema "'pigeni tu, hakusema piga ua''!! kwahiyo katiba imesema serikali 'ikichoka' iwapige raia? chombo cha kutoa adhabu ni mahakama, na DPP anajua hilo, sasa kwanini pinda aamrishe polis kupiga watu bila amri ya mahakama? au pinda amejigeuza mahakama? Labda nimkumbushe DPP, kama ana ugonjwa wa kusahau, kauli nyingine aliyowahi kuitoa pinda kuhusu wanaowaua albino. alisema wale wanawaua alibino nao wauwawe!!!!!!!! kwahiyo pinda amezoea,na hata kama atanusurika hadhi yake kitaifa na kimatifa imeshuka na ameweka rkodi chafu katka kiti cha waziri mkuu wa nchi kushitakiwa kwa kuvunja katiba ya nchi. na hapo ndo nakumbuka maneno ya ndg mmnyika kwamba serikali, bunge na JK ni vyombo dhaifu katika kuchukua hatua.vinginevyo pinda alipaswa kufukuzwa kazi na ama bunge au kikwete mwenyewe.DPP FERESHI HUTUFAI NA WEWE UMELEWA MADARAKA KAMA WAKUBWA ZAKO,LAKINI WEWE CHEO CHAKO SIO CHA KISIASA NI CHA KITAALAM NA KITAALUMA ZAIDI, KWA HIYO ULIPASWA KUHESHIM TAALUMA YAKO NA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA SIO KUJIEGEMA KWA WANASIASA.

Nonsence
 
Hakuna lisilowezekana hapa TZ. Tatizo watu wanashindwa kujua wao ni akina nani ktk hii nchi. Ndiyo hao akina Nape wanaosimama mbele za watu na kuwaambia wazee waasu iri kufa kanakwamba kuna kanuni ya kufa. Kujisahau ni kubaya. WM hawezi kusimama hadharani akasema amechoka kwa hiyo watu wapigwe. Kama kweli amechoka dawa ni kuachia ngazi. Mtu aliyechoka ana madhara makubwa sana. Halafu tangu aliposema amechoka sijui ni kwa nini bosi wake hakumpumzisha ili kumwepusha na hii dhahama ambayo imemkuta sasa.

Sent from my BlackBerry 9860 using JamiiForums
 
DPP anasema Pinda hana hatia kwa sababu hakusema pigeni tu na sio piga hadi kuua. Hapo kwenye "wapigeni tu" angetoa pia ukomo wa kupiga. Wakati mwingine kifo huja hata kwa kofi moja tu! Nadhani kama haki itatendeka Pinda hatachomoka kwa hili.

...na ukizingatia ya kwamba mweheshimiwa M.P.u.m.b.a.v.u hakusema watu wapigwe sehem gani ya mwili,hiyo ndo hatari kubwa sana inayoambatana na kauli hii ya kijinga...kibaya zaidi ni aina ya watu waliopo katika majeshi yetu,(ninamaanisha ni watu wanaotumia sana nguvu zaidi ya akili)wao ilimradi wameishaambiwa "piga",kumpiga mwanadamu mwenzake kichwani,kifuani na tumboni kwa rungu,bunguki,ngumi na mateke sio kitu kigumu wanapokuwa katika harakati ya kuitekeleza hiyo amri ya "WAPIGENI TU MAANA TUMECHOKA"...sasa sijui huyo DPP anataka kutuambia polisi huwa hawaumizi na kuuwa watu coz wanatumia ile kanuni ya bibi na bwana "mwanamke hapigwi kwa ngumi na mateka ila kwa upande wa kanga!"...
 
Last edited by a moderator:
Kutengua kauli kulikuwa na manufaa makubwa kwa Mhe.Pinda kuliko kufedheheshwa mahakamani.
 
Ulitaka tufike wapi? Kwa hiyo sheria isimkate Waziri Mkuu?
Mbona iliwakata kina babu seya bila wao kuwa na nyama?
 
...

[h=5]....." Dhambi kubwa na mbaya kuliko zote Duniani ni Uoga " G LEMA........
[/h]
 
Back
Top Bottom