Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

dpp anasema pinda hana hatia kwa sababu hakusema pigeni tu na sio piga hadi kuua. Hapo kwenye "wapigeni tu" angetoa pia ukomo wa kupiga. Wakati mwingine kifo huja hata kwa kofi moja tu! Nadhani kama haki itatendeka pinda hatachomoka kwa hili.

mimi nimechoka kabisa yaani huyo dpp kwa njaa yake anajaribu kujitoa ufahamu kulainisha mambo kwani kuna ualali wa kupiga raia?
 
hapa tutaona pia umakini wa huu mhimili wa tatu unasemwa sana, mahakama; kama kweli uko huru na unaweza kutenda haki kwa watu wote!
 
Naomba hao mawakili pia wawe wazalendo ili kuhakikisha pinda anachkuliwa hatua za kisheria.amechoka yeye,wananchi bado.
 
Eti ndo mtoto wa mkulima huyo? Hakika kwa Tanzania sijawahi kuona waziri mkuu wa hovyo namna hii ni mara 10000 Lowassa.

Na huyu mkurugenzi wa mashtaka ndugu Felish nafkiri akiri zake kama za mkuu wa mkoa wa Arusha.





Labda ni mpenzi wa pm hivyo anaogopa KUPIGWA TU.

Inawezekana baba wa pinda ni Mkurya.
 
MBOWE naye afungwe kwa vile ameshindwa kutoa ushahidi wa bomu la Arusha kwa vile alikiri hadharani kwa anao.

Kwa hiyo,pamoja na kumiliki majeshi yote bado mnamtaka "muathirika" wa bomu Mbowe awape ushahidi?Wanalipwa kwa kazi gani sasa?Au ile ya kuwasaidia wauza madawa ya kulevya pale JNIA?
Na sisi wananchi tunasema tumechoka!

MSHITAKIWE TU!
 
wahuni pinda anawapeleka puta kiasi kwamba wako hoi hawajitambui wanabaki kushinda mahakamani kama majaji bado kidogo wataanza kushinda polisi kama lema.
 
Eti ndo mtoto wa mkulima huyo? Hakika kwa Tanzania sijawahi kuona waziri mkuu wa hovyo namna hii ni mara 10000 Lowassa.

Na huyu mkurugenzi wa mashtaka ndugu Felish nafkiri akiri zake kama za mkuu wa mkoa wa Arusha.


Kwani naye ana uzalendo? Hebu angalia kesi ya Uda ilivyofinyangwa. WaTz tuna safari ndefu ya mabonde na milima.
 
Dar/Dodoma.

Alisema mbali na shtaka hilo, kuna la pili dhidi ya Waziri Mkuu Pinda, ambalo hawajalifikisha mahakamani ambalo pia linatokana na kauli hiyo aliyoitoa bungeni kwamba: “Sasa wamechoka

Hili nalo neno.
Atakuwa haja kosea maana kusema kweli Serikali yake imechoka kweli na kama anajitambua ni Bora angeonyesha mfano kwa Kujiuzulu maana mlolongo huu wa mahakamani mbele ya safari utambomoa zaidi yeye na Chama Chake.

 
Wanakusanya wapi hizo sahihi na mm nitie yangu,,,, ni vema pia wamuunganishe na feleshi kwa kumtetea mhalifu
 
Kuna kufungu gani cha sheria kinaruhusu kupiga watu au 'reasonable force' ndiyo kupiga, ninavyojua mimi mtu akifanya kosa lolote lile lazima apelekwe mahakamani, mahakama ndiyo ina uwezo wa kutamka adhabu iwe ya kupigwa viboko au kunyongwa.

Statement ya DPP kusema Pinda hakusema pigeni muue ni perception yake maana neno 'piga' halina mipaka unaweza kumpiga mtu kofi moja tu akafa vilevile unaweza kupiga mtu ukamvunja miguu na mikono yote ukaitenganisha na kiwiliwili ukamtoboa macho bado akabaki na uhai wake,

basi DPP anaposema Pinda hakusema 'pigeni muue' je alisema pigeni ila msiue?

Mkuu, ukitafsiri reasonable force utajumuisha humo pamoja na "kupiga" reasonable force ama niseme nguvu stahiki, ama reasonable use of force, inatumika katika kutuliza ghasia ama kupambana na uhalifu, ufahamu kuwa kuna haki za wengine zinazolindwa na pia kumantain public order. Pinda alikua sahihi, na ukae ukijua kua kuna parliamentary immunity, kama ukikumbuka ile ishu ya Adam Malima na bwana Mengi, haikwenda mahakamani bali Mengi alishtaki kwa spika, na si mahakamani, Pinda angeweza kushtakiwa kama wengi mlivyoelewa kama angefanya jambo la kihalifu bungeni kama kuua, ama kuhamasisha mauaji, jambo ambalo hakufanya, kinachofanyika hapa ni kutafuta tafsiri ya maneno aliyotamka pamoja na kinga ya bunge, jambo ambalo ni lakawaida, tafsiri ya mahakama inaitwa declaratory orders, na hizi hazina mamlaka ya kumfunga mtu bali ni kutoa tu msimamo wa mahakama kuhusiana na jambo hilo, tatizo hapa, ni kua nchini kwetu tuna tatizo la kukosa waandishi wa habari wenye uelewa wa kisheria, na hapa wanapotosha umma kwa kudai Pinda kashitakiwa badala ya kuandika kua Mahakama imeombwa kutoa tafsiri ya matamshi ya Pinda. Hilo tu.
 
Good, hata kama UCCM utatumika, heshima yake mbele ya jamii imeshuka na ataingia katika kumbukumbu mbaya duniani. Hakuna kinga ya Bunge wala Mbunge, alijibu swali kama Waziri mkuu. Maneno yake, utekelezaji wake umavuka mipaka ya Bunge. Ndugai na hao waji nga wengine wa CCM wataumbuka
Sawa kabisa mkuu,impact ya maneno yake mbele ya wananchi na wale anaowaamrisha wapige hapo ndio kuna tatizo,na tukumbuke kuwa hata kabla ya amri hiyo kutolewa tayari vyombo vya dola hasa polisi walikuwa wanapiga watu hasa kwenye mikutano ya vyama pinzani.Ni suala la kusubiri tu lakini hapo mahakamani Pinda atalia kwa kujutia tamko lake hilo.
 
Tena natamani asimame mwenyewe Kizimbani na siyo kumtuma WAKILI. Tuone mtu mzima atakavyolia machozi tena.



MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
Wanasema kitaaluma yeye ni mwanasheria,sasa apambane na hilo jopo la wanasheria 20 sipati picha kwa ninavyomuelewa huyu PINDA ingekuwa ni mahakama ya wazi mbona tungefaidi mtoto hatumwi dukani mtu mzima michozi saa zote.
 
Wanasema kitaaluma yeye ni mwanasheria,sasa apambane na hilo jopo la wanasheria 20 sipati picha kwa ninavyomuelewa huyu PINDA ingekuwa ni mahakama ya wazi mbona tungefaidi mtoto hatumwi dukani mtu mzima michozi saa zote.


Ni hapo sasaa......

pinda-bungeni-mawazo.jpg


MIZAMBWA
INANIUMA SANA!!!
 
Good, hata kama UCCM utatumika, heshima yake mbele ya jamii imeshuka na ataingia katika kumbukumbu mbaya duniani. Hakuna kinga ya Bunge wala Mbunge, alijibu swali kama Waziri mkuu. Maneno yake, utekelezaji wake umavuka mipaka ya Bunge. Ndugai na hao waji nga wengine wa CCM wataumbuka

Kumbe maneno ya Sugu yalikuwa sahihi, HAJAWAHI TOKEA WAZIRI MKUU ********** TANZANIA KAMA HUYU, na sasa sio Tanzania tu bali ulimwenguni.
 
Na mimi nasema,wamburuze
kortin tu..maana tumechoka na kauli zake kuanzia ile ya kutaka wauaji wa
Albino wauawe

yeah nakumbuka siku ile pale mjengoni jamaa mpaka mishozi ilimwagika.. kile kilio si kwamba aliwalilia albino lah bali alikuwa anaona sasa uwaziri hooo unanitoka kwa muda mfupi tu loh
 
Mimi sio mwanasheria,lakini kwa mtazamo mwepesi wa kimamlaka,bunge,mahakama na dora/serikali kuu
zote kwa pamoja zina namna zake za uendeshaji wa shughuli zake kwa kufuta kinga na taratibu zake.
Ndio maana mambo yaliyoko mahakamani ni marufuku kujadiliwa bungeni,sasa iweje mambo yaliyojadiliwa
bungeni yapelekwe mahakamani?Hivi hapo uoni kama kuna tatizo la kisheria juu ya mipaka ya kimamlaka?
Anyway tuendelee kuelimishana kwakua hapa JF ni sehemu ya elimu pia.Kwani kwa upande wako ni kipi
hasa alichokosea PM? Na je ipi ni tafsiri sahihi ya kauli yake?

Soma hapa huenda uakapata mwanga.

UAMUZI wa Kituo cha Haki za Binadamu wa kumshitaki mahakamani Waziri Mkuu Mizengo Pinda kwa kauli yake ya kuagiza wananchi wapigwe, imelitikisa taifa kiasi cha kuisukuma ofisi ya Bunge kumkingia kifua.
Huku idadi kubwa ya taasisi na wanasheria mashuhuri wakiungana na kituo hicho katika kumfungulia Waziri Mkuu Pinda mashitaka yanayotarajiwa kufunguliwa kesho jijini Dar es Salaam, Naibu Spika wa Bunge, Job Ndugai amesema jana kuwa hawezi kushitakiwa popote kutokana na kuwa na kinga ya kibunge inayomlinda.
Katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, Ndugai alisema Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inatoa uhuru wa mawazo, majadiliano na utaratibu katika Bunge, na uhuru huo hautavunjwa wala kuhojiwa na chombo chochote katika Jamhuri ya Muungano, au katika mahakama, au mahali pengine nje ya Bunge.
“Ninashangaa sana wanasheria hawa, tena ni Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu, wameacha kabisa kufuata sheria, sasa naona wanafanya siasa, wanatafuta umaarufu tu na mahakama haitaweza kusikiliza kesi hiyo,” alisema Ndugai.
Hata hivyo, utetezi huo wa Ndugai, umepingwa na wanasheria wengi waliohojiwa wakisema kuwa tamko la Pinda linavuka mipaka ya kinga za kibunge, na hivyo anaweza kufikishwa mahakamani kwa tuhuma zinazomkabili.
Mkurugenzi wa asasi ya kiraia ya kufuatilia mwenendo wa Bunge, Marcus Albany pamoja na kukipongeza Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu kwa hatua hiyo, alisema tamko la Waziri Mkuu Pinda ni la hatari na lenye madhara makubwa kwa usalama wa nchi.
Albany alisema waziri mkuu anapaswa kuongezewa mashitaka kwa sababu kauli yake inagusa kosa jingine kwa kulitangazia taifa kuwa serikali iliyoko madarakani imechoka.
“Waziri Mkuu hakusema piga tu peke yake, bali alisema pia serikali imechoka, hili nalo ni kosa jingine kwa Waziri Mkuu kulitangazia Bunge kuwa serikali imechoka halafu hataki kujiuzulu, hivyo ashitakiwe tu,” alisema.
Mkurugenzi huyo alisema wataungana nao kituo hicho katika mashitaka hayo kwa sababu yana uzito mkubwa na athari kwa taifa ikiwa hakutachukuliwa hatua dhidi ya kiongozi huyo kwa sababu yanaweza kuleta maafa makubwa.
Mwanasheria wa kituo hicho, Harold Sungusia alisema utetezi wa Ndugai umejaa siasa zaidi na ametafsiri kimakosa kifungu hicho cha katiba kinachompa kinga mbunge.
“Pinda hataepuka kikombe hiki, ni lazima wafike mahakamani ili mahakama ndiyo iseme kama Pinda alikosea au la.
“Sisi tulijua kuwa watajiegemeza katika kipengele hicho cha kinga ya Bunge, lakini tunaenda mahakamani kuiomba mahakama ituambie kama kinga dhidi ya Bunge inamlinda mtu anayevunja katiba, tunataka mahakama ituambie kama mtu anayesema watu wapigwe ni sahihi au la,” alisema Sungusia.
Alisema katiba ndiyo sheria mama ambayo Waziri Mkuu Pinda aliivunja kwa tamko lake la hatari na linaloweza kusababisha vurugu na umwagaji wa damu. Hivyo hawatarudi nyuma kumfikisha mahakamani.
Aliongeza kwamba kipengele cha katiba alichoshikilia Ndugai bado kinasisitiza kuwa bila kuathiri katiba, na Waziri Mkuu Pinda hakuvunja kanuni za Bunge tu, alivunja katiba aliyoapa kuilinda, na hivyo kipengele ambacho Bunge kinang’ang’ania kipo kinyume cha katiba, na katiba inasisitiza bila kuathiri.
“Chukulia kuwa ikatokea siku moja mbunge ama kiongozi mkubwa kabisa akasema wanawake wote wabakwe, asichukuliwe hatua kwa kuwa alisemea bungeni?
“Ikitokea waziri akaamuru watu wauawe asishitakiwe kwa kigezo kuwa alisemea bungeni? Tunataka mahakama ndio itoe tafsiri ya kifungu hicho,” alisema.
Mwanasheria mwingine maarufu ambaye jina lake linahifadhiwa kutokana na dhamana aliyonayo serikalini, alisema kuwa sheria ya haki na wajibu inayotekelezwa na mahakama ya mwaka 1994, inatoa mwanya kwa Waziri Mkuu kushitakiwa hata kwa alichokisema bungeni.
“Hii ni kwa kutumia madaraka ya Mahakama Kuu ya kutengua uamuzi unaolalamikiwa, ili mamlaka husika itoe amri nini kifanyike au mahakama ilazimishe jambo fulani lisifanyike (Prerogative of certiorari, mandamus et Prohibimus),” alisema mwanasheria huyo.
Alisema Pinda alikiuka Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ibara ya 13(2) inayosema: “Ni marufuku kwa sheria yoyote iliyotungwa na mamlaka yoyote katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuweka sharti lolote ambalo ni la kibaguzi ama wa dhahiri au taathira yake.
“Kifungu cha nne cha ibara hiyo hiyo kinasema ‘ni marufuku kwa mtu yeyote kubaguliwa na mtu au mamlaka yoyote inayotekeleza madaraka yake chini ya sheria yoyote au katika utekelezaji wa shughuli yoyote ya mamlaka ya nchi’. Pinda alitoa kauli hiyo akiwa anatekeleza kazi yake kama kiongozi wa serikali bungeni.
“Katiba Ibara ya 13 (6) (e) inaonya kuwa ‘ni marufuku kwa mtu kuteswa, kuadhibiwa kinyama au kupewa adhabu zinazomtweza au kumdhalilisha’. Pia Ibara ya 16 ya Katiba inasema ‘kila mtu anastahili kuheshimiwa na kupata hifadhi ya nafsi yake, maisha yake binafsi na familia yake na pia heshima na hifadhi ya maskani na mawasiliano yake binafsi’,” alisema.
Akijibu swali la nyongeza kutoka kwa Mbunge wa Kilwa Kaskazini, Murtaza Mangungu (CCM) katika kipindi cha maswali ya papo kwa hapo kwa Waziri Mkuu, bungeni Dodoma aliyetaka kujua serikali inavyoshughulikia tuhuma za vyombo vya dola kutuhumiwa kuwapiga wananchi kama ilivyotokea Mtwara na kwingineko, Pinda alijibu:
“Ni lile lile nililosema... mwishowe unaona anasema vyombo vya dola vinapiga watu. Ukifanya fujo, umeambiwa usifanye hiki, ukaamua kukaidi, utapigwa tu. Hakuna namna nyingine, maana wote tukubaliane kwamba nchi hii tunaiendesha kwa misingi ya kisheria.
“Sasa kama wewe umekaidi, hutaki unaona kwamba ni imara zaidi, wewe ndiye jeuri zaidi, watakupiga tu. Mimi nasema muwapige tu, kwa sababu hakuna namna nyingine, maana tumechoka.”
Tamko hilo lililoshangiliwa na wabunge karibu wote wa CCM huku wale wa upinzani, wakitikisa vichwa vyao kwa masikitiko lilizua malalamiko mengi kutoka kwa Watanzania wa kada mbalimbali, na wengine kwenda mbali zaidi wakimtaka kiongozi huyo kujiuzulu.
Ikiwa atafikishwa mahakamani, itakuwa tukio la kwanza katika historia ya Tanzania kwa Waziri Mkuu kushitakiwa kutokana na matamshi yake bungeni, ama akiwa nje ya Bunge.
 
Back
Top Bottom