Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

kUMBE KUPIGA MTU SI KOSA BALI KOSA NI KUUA?KWELI TUNA MIZIGO YA VIONGOZI WA SERIKALI ONA KAULI YA LIMWANASHERIA LA MZEE WA MSOGA!

“Hii haikuwa kuchochea apige watu, alichosema ni kupiga wale wasiotaka kutekeleza amri halali na zaidi alisema piga lakini si kupiga na kuua,” alisema.
 
Taratibu tunaenda vizuri, itafika mahala wang'oa kucha, warusha mabomu watafikishwa mahakamani na watafungwa tu, tumechoka.
Kinga ya Rais iondolewe, apandishwe mahakamani akipatikana na kosa afungwe tu, tumechoka.
 
Kulia ni jadi yake sasa kwa hili atalamba udongo. Nawapongeza sana LHRC maana hii itafanya viongozi watafakari kauli zao kabla ya kulipuka kama wamekula viroba. Hizo sahihi ni wapi na mimi nikasaini? Mungu ni mwema kwa hili HACHOMOKI
 
alafu kuna watu walikua wanasema kua anafaa kua rais.... kama kiongozi anasema hadharan na kutoa ruhusa kwa polisi kupiga watu je akiwa ndio amir jeshi mkuu itakuaje!!! mahakama itatupa haki kwa hili!!!
 
Aaagghhh......!!!! wananchi tumeshachoka...kama vipi serkali ivunjwe tu kila mtu afanye chenye akili inamtuma manake kwa serikali hii tuliyo nayo ingekuwa haipo tungekuwa mbali
 
Ndhani kama ni kufungwa angeanza kufungwa SUGU au yeye hakukiuka haki za binadamu kummtukana? mengine haya mbwembwe tu za watu kujitafutia umaarufu wa kisiasa. Huyu mama huenda akachuua fomu ya urais mwaka 2015

Mh. Sugu alifunguliwa mashitaka kuwa kamtukana Pinda, mahakama ilitoa hukumu kuwa hakuna tusi, wewe bado unasema Sugu alimtukana Pinda! Tengua kauli, please!!!!!!
 
huyu binti wa ngara nadhani atakuwa mhaya na wahaya kazi zao tunazijua sote.
 
Sakata la Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupelekwa mahakamani na kituo cha sheria na haki za binadamu (LHRC) limekuwa gumzo nchini. Mimi namtazama mshitakiwa kama Waziri Mkuu na siyo tu mtu binafsi yaani Mhe.Mizengo Pinda maana vinginevyo ataitwa Mbunge,Mjumbe wa Halmashauri kuu ya CCM na mtoto wa mkulima. Tujiulize, Waziri Mkuu ana impact gani ya kitaswira kama nembo ya nchi na serikali mbele ya mataifa ya kigeni? Kwangu mimi, Waziri Mkuu siyo tu kwamba ni mtendaji mkuu wa serikali bali pia ni "brand image of our nation in foreign relations and recognition". Msimamo wa Mhe.Pinda kugoma kutengua kauli ya kuvitaka vyombo vya dola kupiga raia wanaokaidi amri ni fedheha kwa taifa kwani si kila amri halali ni haki mbele ya umma. Our Prime Minister should not wear a mask,people will not greatly respect him.Ignoring complaints of the people isn't good governance at all.
 
Mh. Sugu alifunguliwa mashitaka kuwa kamtukana Pinda, mahakama ilitoa hukumu kuwa hakuna tusi, wewe bado unasema Sugu alimtukana Pinda! Tengua kauli, please!!!!!!

we waajabu kweli hukumu mbona haijatoka,huyu bibi mwehu yeye afanye mpango akagombee uenyekiti bawacha sote twajua kuwa chadema ndiyo wanampotosha ila atavitandua tu vitanda alivyotandika.
 
Viongozi wetu kwa kweli ni vichwa ngumu kwani muda mwingi umepita licha na vyombo mbalimbali kulalamikia kauli hiyo pamoja na wananchi lakini Pinda ameendelea kuwa na kiburi kisicho cha kawaida. Dawa ya kuwafikisha mahakamani viongozi wa aina hii ni sahihi.

Jana nimeona kwanza kwenye taarifa ya habari kwenye Luninga nikaona kumbe sasa kumekucha Picha kulalishwa kwenye gunia la misumari.

Halafu DPP anaonongea u haro akimtetea PM kuwa hakumaanisha kupiga na kuua!!!!
Ikiwezekana naye aunganishwe ktk Kesi hii ya kikatiba awe mshitakiwa wa tatu,kwani
nisheria gani inaruhusu polis kupiga????hawa watu mbona wamelewa madaraka vby?

DPP asimtilie maneno kinywani PM,akajibu mashtaka yeye mwenyewe,pia mm nashauri
asipewe dhamana kwa sababu za usalama wake mana akiachiwa wananchi wanaweza
kumdhuru kwa hiyo apelekwe Segerea.

Heshima kwenu watetezi wa haki za binadamu.
Tunaomba mahakama nayo ilinde heshima yake kwa kutocheka na kima.
Na mahakama itambue kuwa amri iliyotolewa na PM kw mapolis kupiga raia imeanza
kusababisha vifo mfano ni yule mtu wa Kurasini aliyeuliwa na polis na maiti yake ikatelekezwa mwananyamala.
 
SASA DPP naye anachekesha na kujidharirisha aisee! Eti alisema "'pigeni tu, hakusema piga ua''!! kwahiyo katiba imesema serikali 'ikichoka' iwapige raia? chombo cha kutoa adhabu ni mahakama, na DPP anajua hilo, sasa kwanini pinda aamrishe polis kupiga watu bila amri ya mahakama? au pinda amejigeuza mahakama? Labda nimkumbushe DPP, kama ana ugonjwa wa kusahau, kauli nyingine aliyowahi kuitoa pinda kuhusu wanaowaua albino. alisema wale wanawaua alibino nao wauwawe!!!!!!!! kwahiyo pinda amezoea,na hata kama atanusurika hadhi yake kitaifa na kimatifa imeshuka na ameweka rkodi chafu katka kiti cha waziri mkuu wa nchi kushitakiwa kwa kuvunja katiba ya nchi. na hapo ndo nakumbuka maneno ya ndg mmnyika kwamba serikali, bunge na JK ni vyombo dhaifu katika kuchukua hatua.vinginevyo pinda alipaswa kufukuzwa kazi na ama bunge au kikwete mwenyewe.DPP FERESHI HUTUFAI NA WEWE UMELEWA MADARAKA KAMA WAKUBWA ZAKO,LAKINI WEWE CHEO CHAKO SIO CHA KISIASA NI CHA KITAALAM NA KITAALUMA ZAIDI, KWA HIYO ULIPASWA KUHESHIM TAALUMA YAKO NA KUFANYA KAZI KWA WELEDI NA SIO KUJIEGEMA KWA WANASIASA.
 
Good, hata kama UCCM utatumika, heshima yake mbele ya jamii imeshuka na ataingia katika kumbukumbu mbaya duniani. Hakuna kinga ya Bunge wala Mbunge, alijibu swali kama Waziri mkuu. Maneno yake, utekelezaji wake umavuka mipaka ya Bunge. Ndugai na hao waji nga wengine wa CCM wataumbuka

wewe siyo mfafanuzi wa kanuni za bunge, tusubiri tuone
 
Sheria sheria sheria!!!!!

Washauri wake wapo na yeye mwenyewe ni mwanasheria so wanajua walifanyalo.
 
Mkuu , hapa tulipofikia hakuna kuonea huruma wala aibu , LIWALO NA LIWE ! Hawa viongozi wamejisahau sana kiasi kwamba mtu kama Mwigulu anaweza kupanga lolote bila kukemewa ! Wacha aburuzwe , mahakamani na kuna wengine wanafuatia akiwemo Lukuvi .
 
Back
Top Bottom