Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

Waziri Mkuu Pinda ashtakiwa mahakamani

DPP anasema Pinda hana hatia kwa sababu hakusema pigeni tu na sio piga hadi kuua. Hapo kwenye "wapigeni tu" angetoa pia ukomo wa kupiga. Wakati mwingine kifo huja hata kwa kofi moja tu! Nadhani kama haki itatendeka Pinda hatachomoka kwa hili.
Bila shaka huyo DPP naye ni Pinda!
 
Na mi nasema ashtakiwe tu! Maana tumechoka kupigwa.. Hadi wajeda wanatukong'oli kiasi kile cha viongozi wa CUF!
 
watu wanatafuta umarufu kupitia waziri mkuu kamwe hawataupata,polisi wapigeni tu tena wapigwe sana.
 
Nikumabie JAMBO!

The trend will continue ... Kwa sababu hili limwezekana siku si nyingi utasikia Serekali yeneywe ikuburuzwa mahakamani kwa mambo ya msingi kabisa.

1. Bomu lililorushwa Olasiti na soweto na kuleta mauuji nani haswa alikuwa muhusika?
2. Kuzorota kwa mambo mengi ya kijamii Mali asili kufanyiwa mzaha, viogozi kutajwa waziwazi madwa ya kulevya nk ..-

... Suburi Utaona ...!!

Nadhani hata mabomu ya mbagala na gongo la mboto yanafaa kuisukuma serikali kwa pilato. Yale maafa hayakulipwa ipasavyo. Wapigwe tu na kundi lake la ndovu lager watapata shida mpaka kufikia 2015.
 
i personally think this is the most important part of a historical imprint!!

na ashitakiwe tu!!

kipindi cha skonga kiandae swali hili;

1.Taja jina waziri mkuu wa kwanza kupelekwa mahakamani Tanzania na kwa kosa gani?
 
Kumshitaki Waziri Mkuu ni kuvunja katiba.

Kumfungilia mashitaka mahakamani ni kulidhalilisha bunge.

Mambo ya kibunge ufanyika na kumalizwa kibunge-bunge.

Labda tu kama hakuna kingine cha kufanya kwa sasa.

Ni vema LHRC wakatazama upya shauri lao kwani
tafsiri ya kauli ya PM bado inawasumbua kuitafsiri
kwa maana halisi na dhima yake kwa wakati
ilipotolewa.

Na ikumbukwe kuwa cheo cha PM sio cha kubabaisha
ni cheo kikubwa hasa kwa upande wa utekelezaji wa
sera,kanuni na miongozi kwa upande wa Tanzania bara.

Hivyo kumfungulia mashitaka si tu kumdhalilisha bali ni
kuondoa dhima nzima ya cheo cha PM.

Ni vema LHRC wakapima na ikiwezekana kufanya maamuzi
ya kisheria ya kitu gani kilichomfanya PM akatoa kauli ile ili
nako huko waweze kuwajibishwa kisheria.

La sivyo kituo mahili hiki cha wanasheria kitaonekana kama
ni mojawapo ya tasisi za kimkakati za upande fulani katika
kuinyong'onyesha dora kwa kutumia sentensi na baadhi ya
kauli tata za kitawala.
 
Hizi ndizo aina kuu tatu za mawaziri wakuu wa Tanzania

1. Mawaziri wakuu wastaafu mfano Joseph Warioba, Salim Ahmed Salim, Cleopa Msuya na Fredrick Sumaye.
2. Wazirim Mkuu aliyejiuzulu Mh. Edward Lowassa
3. Waziri Mkuu aliyepo madarakani ambaye amechoka na wa kwanza kufunguliwa mashtaka akiwa madarakani mtoto wa mkulima Mh. Mizengo Pinda
 
safi sana pinda hiyo ndiyo misimamo ya kiumeni twende kazi huyu bibi hana jipya kajaza meno mdomoni tu.


kweli kabisa PINDA tupigwe tuu... ila tukipigwa tunaruhusiwa kujitetea sasa hivi tukienda kwa mikutano chukua ka sime kako kadogo... mawe ya kutosha na mtu atatusaidia mkituletea mabomu ya kichina ... alimradi tuwe na silaha za kutosha... na vijibunduki vya kichina vya bei rahisi.... Kwa sasa wakikupiga kimbia wasubirie mtaani wakiwa hawana mabomu wala risasi na wewe PIGA TU....
pia tukimaliza hawa mafisadi kwa sababu nao tumechoka nao tuwapige tuuuu ... Tanzania nchi ya AMANI bwana tupigane tuuuuuuuuuuuuuuu
 
aaa pinda.waziri mkuu wa zamani berluscon.amefungwa miaka 3 sembuse pinda
 
huyu feleshi anayepinga na kusema hamna kesi ye ndio hakimu? shauri lifunguliwe sheria itazamwe na uamuzi utatolewa kwa mujibu wa sheria na sio kukingiana kifua. hakuna aliye juu ya sheria
 
Back
Top Bottom