Waziri Mkuu Majaliwa: Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuchochea uwekezaji na kukuza uchumi wa Tanzania

Anna Nkya

Member
Oct 21, 2021
69
341
Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Kassim Majaliwa amesema Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan amedhamiria kuchochea uwekezaji na kukuza uchumi wa Tanzania.

Waziri Mkuu ameyasema hayo leo (Jumanne Novemba 16, 2021) wakati akifungua kongamano la biashara na uwekezaji kati ya Tanzania na Uingereza katika Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Julius Nyerere.

Waziri Mkuu amesema katika kipindi kifupi Mheshimiwa Rais Samia ameboresha mahusiano na nchi mbalimbali ikiwemo Uingereza ikiwa ni sehemu ya mkakati wake wa kukuza uchumi.

Amesema Rais Samia ameongeza usimamizi wa sera za soko huria, sera za kiuchumi na kifedha zenye mwelekeo wa kuimarisha mazingira ya biashara na uwekezaji.

Amesema kwa kipindi cha Machi hadi Agosti 2021, Tanzania imeongoza kwa kuvutia kiwango kikubwa zaidi cha uwekezaji kutoka nje kwa ukanda wa Afrika Mashariki ambapo kiwango cha uwekezaji kutoka nje kilifikia Dola za Marekani bilioni 2.9.

Mheshimiwa Majaliwa amesema licha ya janga la UVIKO19, Tanzania katika mwaka 2020 ilipokea uwekezaji kutoka nje wa Dola za Marekani bilioni moja. “Hili limefanikiwa kutokana na juhudi za makusudi zinazochukuliwa na Serikali katika kuimarisha mazingira ya uwekezaji.”

Akizungumzia kuhusu mahusiano ya kibiashara kati ya Tanzania na Uingereza, Waziri Mkuu amesema Uingereza imeendelea kuwa mshirika wa asili, wa kihistoria na wa muda mrefu wa kibiashara wa Tanzania.

Waziri Mkuu ametoa wito kwa mamlaka husika za pande mbili kushughulikia vikwazo vya kibiashara visivyokuwa vya kikodi ili kurahisisha shughuli za kibiashara na huduma kwenye jamii zetu bila kuathiri misingi ya ushindani.

“Uchumi wa Tanzania umeendelea kukua kwa wastani wa asilimia 6.5 kutoka mwaka 2016 hadi 2020 na hivyo, kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi barani Afrika.”

Ameongeza kuwa hivi karibuni Serikali imeendelea kushuhudia uwekezaji mkubwa kutoka kwa makampuni ya Uingereza ikiwemo miradi 956 kutoka Uingereza yenye thamani ya Dola za Marekani bilioni 5.5 imesajiliwa na Kituo cha Uwekezaji Tanzania pamoja na mradi wa upanuzi wa Kiwanda cha Sukari cha Kilombero (Dola za Marekani milioni 238) na kupatikana kwa leseni ya uchimbaji wa madini ya nickel ya Kabanga
 
Majaliwa sio mtu wa kumuamini, ni mtu anayepaswa kupuuziwa kwa 100%. Ni muongo sana.
 
Jafo, makamba January, majaliwa, ndalichako, gwajima dorothy, SSH na mpango, Orodha hii inazalisha kifo cha CCM 2025.
 
Weka hotuba yake yote hapa.

Mods unga huu Uzi kwenye ule wa uwekezaji
 
Hii ndiyo dhamira yenyewe🐒🐒🐒
 
Back
Top Bottom