Waziri Mkuu: Mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora Serikali iyauze kuliko kuyaacha yakiozea pale yard

Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Kwani shida haijulikani? Tatizo ni pale awamu ya 5 walipoamua Serikali iendeshe huo mradi. Serikali ua JMT haijawahi kuendesha mradi wowote ikapata faida.

Ni dhahiri ndani ya Serikali, ubunifu ni zero.
 
Duh!auziwe nani na akataye nunua atayatumia wapi?

Ova
Magari ya mchina, life span yake huwa ni miaka 3. Uchumi wa Afrika unaharibiwa na mchina. Waafrika wanaamini wanafaidika kwa kununua bidhaa za viwango vya chini kutoka China kwa bei ya chini, kumbe wanakula hasara, na wachina kipitia hizo bidhaa zao hafifu wanazidi kupaa kwa gharama ya waafrika kuzidi kudidimia.
 
Nani anunue hio shida? Yani shida yao badala waitatue wao wanataka wamuuzie mwingine? Na biashara ya basi wameshaivuruga sana.
Huyo wa kununua gari used ya Mchina, labda awe taahira. Gari jipya ya mchina life span yake ni fupi kuliko gari used ya Mjapani
 
Fukuza,chunguza, fungulia mashtaka management yote kwanza then mazungumzo yaanze namna ya kuweka sawa kampuni
 
Magufuli amefeli vitu vingi na amehujumu hii nchi. Vyote UDA na UDART kwisha kabisa.
huu mradi wangepewa watu binafsi waendeshe kibiashara au wengeruhusu wenye daladala kununua share tuone kama kutakuwa na haya mambo, halafu magari hayo yalikuwa ni used, pili njia za bongo changamoto sana angalia maji jangwani pale!?

hivi mtu akinunua atayatumia wapi!?
 
Huu mradi unaendeshwa kipuuzi Sana, inaonekana hata service hawafanyia Hawa

Haiwezekani mradi umeanza 2018 na mabasi 140,
takribani Miaka 2 na nusu TU tangu uanzishwe.

Eti mabasi yamebaki 100 tu ndo yanayotembea, yaani mabasi 40 yako juu ya mawe.

Yaani tayari 1/3 ya mabasi yamekufa, ndani ya Miaka 2 na nusu tu.

Ina maana, wskiendelea kwa trend hii wanayokwenda nayo.
Miaka mitano ijayo kuanzia sasa, mradi utakua hauna Basi ata Moja.

KUNA SHIDA MAHALI
Walipoteza magari mengi kwa sababu karahana na mahali pa kuegesha mabasi usiku paliwekwa Jangwani, kwenye bonde, sehemu ya mafuriko ya uhakika. Nakumbuka taarifa mabasi yalizamishwa kwenye maji, wakubwa walijadiliana eti wahamishe au la, waliacha palepale hadi mafuriko yaliyofuata, tena mabasi sijui mangapi yaliharibika. Sijui jini gani aliwaandalia mipango hii? Karahana iko hadi leo nisipokosei.
 
Waziri mkuu mh Majaliwa ameshauri mabasi mabovu ya mwendokasi ni bora yauzwe kuliko kuyaacha yakioza pale yard

Waziri mkuu amesema hayo baada ya kushuhudia mabasi takriban 50 yakiwa yamelala kabisa kwa ubovu na yakizidi kuchakaa.

Chanzo: ITV habari

Ramadhan Kareem!
Ni kosa kubwa kwa serikali kufanya biashara! Narudia tena ni kosa kubwa mno kwa serikali kumiliki asilimia zote kwenye biashara yoyote! Nenda USA, Uingereza, popote walipoendelea sehemu kubwa ya biashara wanaachiwa sector binafsi! Sijui tutajifunza lini!
 
Muongo huyo vyuma vipya vile na vingine vipo bandari kavu ya ubungo
Ila hii nchi yetu noma Sana, kwahiyi wameshindwa kabisa kufikia muafaka wa hayo mabasi yaliyopaki hapo miaka?? CAG akisema 60% uwezo wako ni mdogo watasema ametumwa na mabeberu
 
98% ya coment zote kwenye huu uzi ni konki!

Hizo 2% kama kawaida ni coment za wale vilema wa akili kutoka ufipa!

Nashauri selikali ipitie kwenye maoni ya huu uzi watajifunza kitu kuhusu jinsi ya kuendesha huo mradi.

Kingine kwa mujibu wa coment nyingi za wadau hapa inaonekana shida ni mbili:

1. Yale mabasi hayafai
2. Upigaji.
 
Hii picha ni ya basi la mwendo kasi?
IMG_20210421_090431_023.jpg
 
Mnataka mabasi yafanye kazi ya treni. Wenzao wanatengeneza "commuter train" wao bado wanapigana na diesel engine zisafirishe watu kwenye busy chaotic city kama dar. Mi nilishangaa sana huu mradi back in the days enzi za JK.
Mradi ni mzuri sana,shida kubwa ni jinsi ya kuundesha,na unaweza kukuta kuuendesha pia sio shida ila kuna upigaji ndio tatizo,business as usual,mindset ya wizi ni mbaya sana kwenye nchi inayotafuta maendeleo,hakuna anaewaza kufanikiwa kwenye maisha bila ya kufikiria kuiba...
 
Back
Top Bottom