Waziri Mkuu Kassim Majaliwa avamia mwendokasi, ahoji mapato yalipo kama wanashindwa kununua mabasi. Mkurugenzi wa fedha atumbuliwa

Ina maana hadi DART inajiendesha kwa hasara ? Unakuta mjinga mmoja anasema alipambana ufisadi kumbe alipambana na wapinzani na matajiri
 
Majaliwa anaogopeka ila kuna baadhi ya viongozi wanamzidi kete akitembelea maeneo yao.
Wanamuandalia wapambe wenye nguo za rangi ya kijani na njano wana demkaaaaaaa yeye anatabasam na kuondoka
🤣🤣🤣 Wanampampu kujua kua anapendwa
 
Tatizo la kurundika mamlaka yote ya uteuzi wa kila mtendaji mkuu kwa mtu mmoja. Hivi hili shirika halina bodi? Kama ipo, inasimamia nini? ama ni zile teuzi za kufahamiana na ukada?
 
Na sisi wananchi tuna haki ya kufahamu,kama mambo tunayolalamikia yanapatiwa ufumbuzi au S/kali inashughulika nayo vipi.

Wezi hawabembelezwi DART ni kichaka cha wezi hata hasiye na akili anaweza kuona jinsi tiketi zinavyokatwa ni upigaji mtupu hata Waitara alishawai kuongelea hilo swala ila akaishia juu juu hakuna action iliyochukuliwa.

Kongole PM

Umefahamu kitu gani kipya ambacho ulikuwa hukifahamu?

Na kama kila mtu anajua kuwa DART ni kichaka cha wezi (pamoja na aliyekuwa Waziri Mdogo katika wizara husika) umepewa sababu gani ya kwa nini wizi na uzembe huo uliachiwa uendelee kwa miaka mitano?

Unasema kuna upigaji katika ukataji wa tiketi, haujiulizi kwa nini haujaonyeshwa lundo la tiketi feki ambazo watu walikuwa wanauza kwa faida yao wenyewe?

Haujiulizi kwa nini Mkurugenzi ameshutumiwa kwa kutonunua mabasi mapya lakini hapo hapo unaonyeshwa mabasi 70 yaliyoagizwa lakini yameshikiliwa na taasisi moja ya serikali?

Haujiulizi kama Mkurugenzi ana mamlaka ya kujinunulia mwenyewe mabasi mapya bila kupata kibali cha Bodi yake na wizara yake? Haujiulizi kwa nini hasara hii haikujulikana mapema wakati kila mwaka wakaguzi ( wa hesabu na stocks ) wanamkagua na kutoa taarifa serikalini?

Haujiulizi kwa nini kila mwaka kamati husika ya Bunge inamkagua na hakuna lililofanyika mpaka jana?

Hapa tatizo ni kubwa kuliko linavyo onekana na ukweli hauwezi kupatikana kwa ziara ya kustukiza. Sana sana inapunguza morali ya watumishi wa umma ya kufanya kazi.

Amandla...
 
Waziri Mkuu bado yupo zama zile za kutafuta sifa majukwaani. Hakuna ufanisi unaopatikana kwenye majukwaa ya mikutano.

Suluhisho la matatizo siku zote hupatikana ofisini kwa kujadiliana.

PM aache siasa uchwara zilizokuwa zimezoeleka awamu ya 5. Tunataka viongozi wanaochapa kazi, na siyo wanaotafuta sifa ili waonekane wanachapa kazi.
 
Kuna jambo lina tengenezwa. Time will tell. Kuna mtu kesha kamata mshiko wa kumpa mtu tenda. Soin tutasikia kuna kampuni imepewa tenda ya kukusanya mapato. Amri toka juu...
 
sawa sawa

1. utekelezaji
2. uthubutu
3. usimamizi

hivi ni vigezo vitatu viongozi lazima wawenavyo.

ila kutumbua watu leo sio suluhu bali kurudi kwenye mikataba (vyanzo vya yote haya)
 
Tungekuwa serious; Nyumbu ilitakiwa iwe ndio supplier and maintainer wa mabasi ya mwendokasi. Tungekuwa tumekuza uchumi wa ndani; ajira kwa watanzania; na kuongeza uwezo wa teknolojia.

Tunawaza tu kuagiza kutoka nje; hatuwazi ku-innovate na kuwa na vya kwetu no matter how ugly they might be, but gradually will be improved to modern ones!
Dah! Hii safi sana, uzalendo 100%
 
Anamuenzi mwendazake Mkuu. Kumbuka kuna lile kundi linalopigia debe “kumuenzi” mwendazake ili kuendeleza mazuri yake. Na bila ya shaka kwa hawa wakurupukaji hii fukuza fukuza inayorekodiwa LIVE ni jambo zuri.
Tunarudi kule kule. Haya mambo si ya kuulizana jukwaani. Angemwita yeye na viongozi wake ili wakae waone tatizo liko wapi. Kama ni uongozi lingeonekana tu.

Na kama ni serikali ingeonekana tu maana Meneja angeweza kusema kweli yake bila kuonekana kuwa anamdhalilisha WM hadharani. Inabidi viongozi wakuu wabadilike.

Amandla...
 
Ikiwa mimi na wewe tunaona kama mradi dauwendi sawa, inakuwaje wao wenye majukumu hawaoni hayo? Ni usanii mtupu. Hela wanakula wao wao. Mbona hakuvamia miaka 3 iliyopita waliooanza kuondoa system ya kusoma tiketi ya elektroniki? Mushapiga hela ya kutosha ndio munakuja kutuletea chorus hapa!
 
Sisi wabongo ndio mabingwa wa kuharibu...

Bado na SGR kama uendeshaji akipewa mbongo tutarudi kule kule kama hizo BRT...
 
Fukuza yote haya mazembe yasiyojua nini wanafanya, mabasi yanakufa na hata tickets hawawezi kukatisha..fukuza yote haya then sukuma ndani
 
Kuna jambo lina tengenezwa. Time will tell. Kuna mtu kesha kamata mshiko wa kumpa mtu tenda. Soin tutasikia kuna kampuni imepewa tenda ya kukusanya mapato. Amri toka juu...
Ndiyo nchi yetu inavyo enda
 
Huu mradi yaani umekua jinamizi kwa wakaazi wa Dar, japo MATAGA huwa yanasifia humu. Naomba sana tusije kurudia makosa ya Tanzania, tuwe makini sana na kutumia ubongo sio ujinga na ubabe usio na tija.
 
Back
Top Bottom