Karandinga
Member
- Jun 25, 2008
- 66
- 1
mwawado... nyota njema huonekana asubuhi. Wengine tulipoonesha dalili tukaonwa tuna "chuki". Tatizo la viongozi wa Tanzania siyo elimu, siyo kabila, siyo wapi wamesoma, na kwa hakika siyo dini zao.. tatizo la viongozi wetu ni uwezo.
Bado tunafanya makosa ya kufikiria msomi=kiongozi bora! au mwenye mvuto=kiongozi bora..!!! Swali ni tunapimaje uwezo kabla hawajapewa madaraka? Maana kama Lau alipewa nafasi (promotion as a matter of fact) hili linasema nini kuhusu uwezo wa yule aliyemteua? au mchakato wa uteuzi wake?
Wakuu,
Nifahamisheni Ngeleja ana matatizo gani? Najua Masha kweli kazi imemshinda lakini Ngeleja mbona kama anajitahidi japo wizara yenyewe imejaa mizengwe.
Inatakiwa waziri apewe madaraka yote ya kuja na vision mpya juu ya energy. Huo umeme wa mafuta na maji pekee hautatutosha huko tunakoenda na itakuwa gharama kubwa.
Kuna haja ya kuwa na miradi midogo midogo ya umeme ya kiwilaya badala ya miradi mikubwa mikubwa ambayo kukiwa na tatizo nchi nzima inatikisika.
Taarifa ya timu ya wanasheria wa TANESCO ilibaini kuwa mkataba huo hauna nguvu za kisheria na kuamuru uvunjwe. Mkataba ukavunjwa rasmi Agosti mosi, mwaka 2008.
Hata hivyo, wakati mkataba huo unavunjwa uchunguzi wa Raia Mwema umebaini kuwa fedha zilizopaswa kurejeshwa Serikali hazikuwa zimerejeshwa zote.
Imebainika kuwa fedha zilizorejeshwa hadi mkataba unavunjwa ni jumla ya dola 7,674,186 za Marekani (zaidi ya Sh bilioni 7.7), huku dola za Marekani 23,022,412 (zaidi ya Sh. bilioni 23) zikibakia kwa Richmond na mrithi wake Dowans.
at this point ninaungana kabisa na maoni yako kwa 100%, kwamba wakati umefika kwa Lau kufikiria tena kama kweli he belongs kwenye siasa hasa za taifa.
Again, ninajaribu kumtafuta kujua na kusikia his side of this story, kabla sijatoa my final hukumu
mwawado... nyota njema huonekana asubuhi. Wengine tulipoonesha dalili tukaonwa tuna "chuki". Tatizo la viongozi wa Tanzania siyo elimu, siyo kabila, siyo wapi wamesoma, na kwa hakika siyo dini zao.. tatizo la viongozi wetu ni uwezo.
Bado tunafanya makosa ya kufikiria msomi=kiongozi bora! au mwenye mvuto=kiongozi bora..!!! Swali ni tunapimaje uwezo kabla hawajapewa madaraka? Maana kama Lau alipewa nafasi (promotion as a matter of fact) hili linasema nini kuhusu uwezo wa yule aliyemteua? au mchakato wa uteuzi wake?
Hilo mimi nilibishanaga sana na Sam kule bcstimes.com kuhusu Nchimbi na wengine kama yeye. Sijui kama watu walinielewa....
Mkuu Mwawado,
- Hili la vitambulisho limenishitua kuliko yote ya negative yanayomuhusu niliyowahi kuyasikia toka awe waziri, maana kama nilivyowahi kusema huko nyuma siyajui sana yanayomuhusu kwenye level ya uwaziri, lakini hili limenishitua sana kwa sababu on the record personally nilimuonya toka day one anapewa uwaziri wa ndani kuwa stay away form this national ID thing maana kuna wanaokutega wakunase kwenye hilo na nikawaomba ndugu zake wa karibu wamkumbushe maneno yangu kuwa awe muangalifu na hili na ikibidi alikalie mbali sana maana ninawajua wote waliokuwa wakimtafuta kwenye hili la national ID,
Sauti ya umeme - Wazee wa FMES!
Unauma na kupuliza!
Mwawado kasema categorically "siasa sio nafasi yake...ni vema ajiuzulu."
Wewe unamwambia "naungana na maoni yako 100%" halafu unaweka vi-disclaimer!
Simama uhesabiwe. Au kaa chini "tusubiri sheria ichukue mkondo wake."
Na ukisamama nchale!
Ukikaa ukamtetea wakaja kumfire nchale!
Ukikimbia mpaka soo liishe atakuona umemsaliti, nchale!
Mwawado hakusema "huenda"! Understand that. He was categorical, Masha ajiuzulu. Ukikubaliana nae 100% hakuna cha disclaimer za due process hapo!
We'll bypass the other puerile mumbo jumbo. It's just bizarre.
FMES,
Mkuu samahani huyu dogo Masha nadhani LIMBUKENI.. unajua tena kuna vijana waliochukua muda mwingi sana masomoni wakashindwa kuutumia umri wao ktk nyanja nyinginezo, kisha wanapokuja kuwa watu wazima wakakabidhiwa madaraka basi ndio Ujana wao huanza hapo..
Jamaa amekuwa ktk viwanja kama vile ndio kwanza kapata Barekhe..yaani kila kona mshikaji Masha hivi Masha vile halafu anaharibu kishenzi hadi nyumbani.. mimi nadhani Masha hakuutumia ujana wake vizuri...hivyo anachanganya kazi na kile wanachosema wazungu - I want to find myself.. any Idea what that means! - Mtu kachanganyikiwa..
Hofstede said:Mimi nafikiri ntaonekana nipo mlengo tofauti. Hivi nchi yetu imekosa priorities? katika kutekeleza miradi yake?. Huu mradi wa National ID mimi binafsi naona ni ULAJI ulitengenezwa makusudi na watu kama ilivyokuwa wa RADA na NDEGE YA RAIS ili kujipatia chao mapema. Kwa mfano mradi huu ungefanyika taratibu katika kipindi cha miaka kumi tukasema tutahakikisha watanzania wote wanakuwa na vitambulisho Serikali ingekosa nini hapo?. Kuchukua $154mill kuzichoma kwa mkupuo ni ufisadi usihitaji any explanations kuu justify. Barabara hazipitiki, wanafunzi wanagoma hakuna mikopo haitoshi, Wananchi hawana ajira kwa nini wasingetumia fedha hizi kuanzisha mashamba ya kisasa ambayo yangeajiri watanzania masikini. Mradi huu nina ufaninisha na Mradi wa "SPEED GOVERNER" Haukuwa chochote zaidi ya ulaji tu. Nani leo anazungumzia speed governor?, basi tusishangae 10 years to come watanzania wote wakawa wametupa ID zao na hakuna wa kuwauliza ID zao popote pale (Tshs 200 Billion kissed on the air and washed in the ocean).
Vitambulisho hivyo hata vikija na chip inayobeba taarifa zote za mtu bado mimi kwa Mtazamo wangu ni "USELESS", kwani watanzania wengi bado masikini na hawatafaidika na chochote kwa mradi huu, wala usalama wetu wa Taifa hautayumba hizi ni mbinu za kuuziwa mbuzi kwenye Gunia. Tuwawezeshe kwanza watanzania ili nchi iwe na Neema mpaka hapo itakapovutia wahamiaji kuja Tanzania basi MRADI Huu utakuwa na maana kubwa.
Hebu tuwe na vipaumbele vya miradi siyo kuangalia miradi yenye ulaji na itakayowahakikishia watawala kuendelea kutawala. This is Nonsense project for the Current situation in Tanzania .
Muzee hapa tupo pamoja..Tena ZAIDI YA 100%.
Kila siku tunasikia jinsi serikali yetu inavyolalamika kusema haina fedha ku-cover mambo mbalimbali ktk kuwahudumia wananchi wake. Iwe ktk kuinua kilimo, kujenga miundombinu, kuboresha huduma za afya, kuwaweza wananchi kujiajiri, n.k.
Akili ya kawaida kabisa inamtuma mtu kuona kuwa kunapokuwa na UHABA au UPUNGUFU, ni shurti kufanya OPTIMIZATION (sijui kiswahili chake, samahani) na kutazama VIPAUMBELE VYAKO. Ktk mduara wa umasikini unaotuzunguka mtu anakuja na kusema tutengeneze vitambulisho kwa bilioni 200, inabidi uanze kujiuliza iwapo kuna- kuishirikisha AKILI..
Ain't a big deal.
Uhondo wote ni huu hapa chini kutoka nipashe la leo: -
Waziri Masha aibua matata
KOSA LA KWANZA
Masha anadaiwa kumfahamisha Mwenyekiti huyo wa Bodi ya Zabuni ya Wizara kwamba, amepokea malalamiko kutoka kwa kampuni hiyo na kumhoji pamoja na mambo mengine, uhalali wa kuenguliwa kwa kigezo cha kutoambatanisha nakala ya mapatano (Joint Adventure Agreement)......(nafikiri ni Joint Venture).......Masha alitakiwa kuomba ushauri tu (kama hajui procurement procedures) kuwa awajibuje hiyo barua......
KOSA LA PILI
.................Masha aliitaka bodi hiyo itoe nafasi kwa waombaji wote wa zabuni waliotimiza vigezo vilivyopo kwenye Nyaraka za Awali za Kuingia kwenye Zabuni (PD) wapewe nafasi ya kuendelea na hatua ya pili ya mchakato huo.........hakuna tofauti na alichokifanya Lowassa kwenye mchakato wa RDC
KOSA LA TATU
......... hali ambayo ilimfanya Waziri Masha awasiliane naye tena na kumtaka apate ushauri kutoka Mamlaka ya Usimamizi wa Manunuzi ya Umma (PPRA) kwa kile alichodai kuwa ni kuepuka hisia na malalamiko kutoka kwa waombaji.....BIG NO Mr Masha........kuingilia kwako zoezi la mchakato wa zabuni ni ukiukaji wa taratibu za procurement........na hii ndio italeta mtafuruku kutoka kwa makampuni mengine (yaliyofuzu) kuishitaki serikali......hence hasara..........
Wakati hayo yakiendelea, habari za uhakika zinasema kwamba Katibu Mkuu Kiongozi alimuagiza Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kupeleka taarifa ya utekelezaji kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri baada ya Katibu Mkuu huyo kumpelekea taarifa ya utekelezaji.............
Hata hivyo, inadaiwa kuwa hatua hiyo ya Katibu Mkuu Kiongozi, haikumridhisha Waziri Masha kwa madai kwamba, hakumhusisha kwa vile yeye ndiye atakayeiwasilisha taarifa hiyo kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri na ndiye atakayewajibika kwa maamuzi yoyote yatakayofanyika wizarani kwake bila kujali kwamba maamuzi hayo yalipata baraka za Katibu Mkuu Kiongozi au la...........Hivi kuna Cabinet Paper inayoandikwa wizarani bila ya Waziri husika kuiona?........
* SOURCE: Nipashe