Waziri Masauni akutana na kuzungumza na Mabalozi wa Uingereza, India, Palestina na UNHCR Nchini, Jijini Dar Es Salaam Leo Januari 24, 2023

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,813
11,991
Na Mwandishi Wetu, MoHA

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mhandisi Hamad Masauni amekutana na kufanya mazungumzo na mabalozi wa nchi za Uingereza, India, Palestina pamoja na Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) kwa nyakati tofauti kuhusu ushirikiano baina ya nchi hizo na Tanzania kwenye maeneo mbalimbali ya ulinzi na usalama.

Mazungumzo hayo yamefanyika leo Januari 24, 2023 katika ofisi ndogo za Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi jijini Dar es Salaam huku yakihudhuriwa na baadhi ya viongozi wa Wizara na walioongozana na mabalozi hao.

Katika mazungumzo yake na Mabalozi hao nchini, wamejadili maeneo ya ushirikiano ambayo yakiwemo kutoa mafunzo mbalimbali kwa Askari, masuala ya Wakimbizi pamoja na ushirikiano katika masuala ya ulinzi na usalama.

Akizungunza katika Kikao hicho Waziri Masauni amewashukuru mabalozi hao kwa nyakati tofauti kwa ushirikiano wao wa kuisaidia Tanzania kupitia misaada mbalinbali wanayoitoa na pia amewakaribisha wawekezaji wa kutoka katika nchi zao kuja kuwekeza nchini kwa kuwa Tanzania ipo salama na itaendelea kuwa salama hivyo inamazingira mazuri kwa ajili ya uwekezaji.

Kwa uoande wake Balozi wa Uingereza nchini, David Concar amesema Serikali ya Uingereza ipo tayari kutoa msaada kwa Serikali ya Tanzania kwenye masuala ya mbalimbali Wakimbizi nchini hasa kuhusiana na Wakimbizi wa Burundi kurejeshwa nchini kwao.

Naye Balozi wa India nchini, Binaya Pradhan amesema SAerika ya India imetoa misaada mbalimbali kwa Serikali ya Tanzania, ikwemo katika sekta ya maji, msaada wa mafunzo ya elimu ya muda mrefu pamoja na kutoa mafunzo ya kupambana na uhalifu wa mtandao kwa Maafisa wa Jeshi la Polisi.

Kwa upande wake Balozi Palestina, Hamdi Mansour AbuAli amesema Serikali yake ipo tayari kushirikiana na Srerikali ya Tanzania katika mapambano ya uhalifu na ugaidi.

Naye Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Wakimbizi (UNHCR), Mahoua Parums ameishukuru Serikali ya Tanzania kwa ushirikiano katika masuala ya Wakimbizi na hivi karibuni shirika hilo linatarajia kufanya zoezi la uhakiki wa wakimbizi walipo nchini katika kambi zote za wakimbizi nchini na pia amesema hivi karibuni Mabalozi wanaowakilisha nchi zao nchini wanatarajia kufanya ziara katika Kambi za Wakimbizi nchini Tanzania.
IMG-20230124-WA0006.jpg
IMG-20230124-WA0007.jpg
IMG-20230124-WA0010.jpg
IMG-20230124-WA0013.jpg
IMG-20230124-WA0008.jpg
IMG-20230124-WA0011.jpg
IMG-20230124-WA0012.jpg
IMG-20230124-WA0005.jpg
 
Back
Top Bottom