Serikali: Kuna Jumuiya za Kidini zinatumika kutakatisha pesa, usafirishaji haramu wa binadamu, kufadhili ugaidi na kutoa mafunzo hatarishi

bagamoyo

JF-Expert Member
Jan 14, 2010
21,305
24,200

Utitiri wa nyumba za ibada katika makazi zinasababisha makelele na pia hutumika kuwezesha utakasishaji fedha na ugaidi..

Pia waziri Hamad Masauni asema taasisi na jumuiya ya kidini baadhi yao zinajihusisha na matendo ya kijinai ikiwemo ...

UN- Umoja wa Mataifa imeiweka Tanzania ktk buku jeusi ili ifuatiliwe kwa ukaribu kutokana na kutokuwepo mifumo bora ya ufuatiliaji.
---

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Hamadi Masauni aesema kumekuwa na utitiri wa nyumba za ibada kwenye makazi ya watu ambazo zinageuka kuwa kero kutokana na kelele katika nyumba hizo. Akizungumza jijini Dar es Salaam leo Machi 26, 2024 wakati wa kampeni za ufunguzi wa jumuiya.

Waziri Masauni amezungumzia pia juu ya uwapo wa Taasisi ambazo zinafadhili shughuli za ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, silaha haramu na uwepo wa taasisi za kidini zinazotoa mafundisho potofu ambayo ni hatarishi kwa usalama wa raia. Akiongelea mambo haya katika shughuli hiyo Masauni amesema:

"Zimebainika changamoto za uzalishaji holela za utitiri wa nyumba za ibada katika maeneo mbalimbali hapa nchini. Baadhi ya Jumuiya za dini hususani makanisa na misikiti zimebainika kujengwa katikati ya makazi ya watu.

Kuna mrundikano wa taasisi nyingi katika eneo dogo na baadhi ya taasisi kutumia sauti za juu na hivyo kusababisha adha."

Vilevile baadhi ya Jumuiya za Kiraia zimeripotiwa kushiriki katika kutendeka makosa ya jinai na vitendo vingine ambavyo vina madhara kwa jamii. Baadhi ya vitendo hivyo ni pamoja na Utakatishaji wa Fedha haramu, ugaidi, usafirishaji haramu wa binadamu, biashara haramu ya silaha na uwepo wa taasisi za kidini zinazotoa mafundisho potofu ambayo yanahatarisha usalama wa raia.

Kama ambavyo nimeeleza changamoto za aina hii zinahitaji ushirikiano wa pamoja atika ushughulikiwaji wake ili kuendelea kudumisha hali ya utulivu na usalama.

Hivyo ikiwa kama viongozi mliopewa dhamana ni vyema mkatambua mna wajibu mkubwa wa kuendelea kushirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi katika kuondoa changamoto hizi kwenye jamii
 
Waziri wa Mambo ya ndani tunashukuru kwa kufahamu,,,kuyajua na hatimae kuyasema ya ndani basi tunaomba chukua hatua za kiundani kulidhibiti hilo.
 
Hivi hawa Maccm wameanzisha mpaka combination za udini kwenye mitaala ya masomo wanategemea wanafunzi wakimaliza wafanye nini kama siyo kila mtu kuanzisha kanisa lake au msikiti wake? Na kwa nini walalamike sasa, hawaoni wao ndio wanazalisha makanisa au misikiti siyo rasmi? Tutaona mengi chini ya mafisiemu!
 
Back
Top Bottom