Waziri Makamba: Kila nyumba itakuwa na mtungi wa gesi

BARD AI

JF-Expert Member
Jul 24, 2018
3,379
8,123
Serikali imesema ina mikakati ya kuhakikisha kila nyumba inakuwa na mtungi wa gesi ya kupikia na kuandaa mifumo mbalimbali kupitia uvumbuzi wa kibiashara ikiwemo kutumia teknolojia ya kupima gesi kidogo kidogo.

Hayo yamesemwa leo Ijumaa, Oktoba 21, 2022 na Waziri wa Nishati, January Makamba alipokuwa akihojiwa katika kituo cha televisheni cha Clouds kupitia kipindi cha Clouds 360.

Amesema utamaduni wa Watanzania ni kununua vitu kidogo kidogo hivyo wengi hawaoni unafuu wa gesi kwa kuwa inauzwa katika mitungi mikubwa.

“Kuwa na mtungi wa gesi kila nyumba inawezekana ni suala la kujasiliana maeneo ya vijijini wengi wanasema hawawezi kumudu, wakala yuko mbali siwezi kujaza. Ifike wakati mtu akiishiwa gesi kuna namna anaweza kuipata kwa haraka ukiangalia takwimu Tanzania tupo chini ya kilo 2 kwa matumizi ya mtu mmoja kwa mwaka wenzetu wapo kilo 46 lazima tuangalie tunafanya nini.

“Serikali tumechukua hiyo changamoto na tunaifanyia kazi, tunaona kama Je? Serikali iweke ruzuku, kodi iondolewe au ni vinginevyo,” amesema.

January amesema wengi wana kipato kidogo na matajiri na wenye kipato cha kati wanaomudu ni wachache, hivyo inabidi Serikali iangalia namna ya kulisaidia kundi hilo.

“Mitandao ya simu walifanikiwa baada ya kuweka vocha ndogondogo, ili nishati safi ya kupikia ishindane na mkaa itawezekana tukitumia teknolojia kuwezesha hata gesi iuzwe kwa bando, pale pana mita unaweka mpesa unafungua mita unaingiza gesi ya Sh100 unapika inaisha zipo vumbuzi ikawa moja ya majawabu inawezekana kuweka mitungi kila nyumba, kupitia uvumbuzi wa kibiashara,” amesema.

Mwananchi
 
Inaonekana Makamba hajui huo "utamaduni" wa kununua vitu kidogo kidogo umesababishwa na umasikini wa watanzania wengi chini ya utawala wa CCM, hivyo kwa hiyo kauli yake, ni sawa na anatuambia umasikini wa hili taifa umekuwa utamaduni wetu.

Kama mtu anaamka asubuhi kwenda kutafuta chakula cha siku hiyo, hiyo pesa nyingi ya kununua mtungi mkubwa wa gesi ataitoa wapi?

Asije kushangaa hiyo kidogo kidogo ya gesi inakosa wanunuzi, kwasababu mtumiaji lazima atapiga hesabu ya bei, na muda wa matumizi, ndio akanunue, kama jibu likija nafuu mkaa ajue hiyo biashara yake itakosa wateja.

Kidogo kidogo sio tabia inayopendwa, tumelazimishwa kuishi hivyo na CCM, hakuna mtu asiyependa kuona ndani kwake kumejaa mahitaji ya ndani ya mwezi mzima kama wanavyoishi wabunge na mawaziri, kidogo kidogo ni pasua kichwa sana, inasababisha wengi waishi kwa kuwaza kula tu.
 
Bila kutuambia hilo litawezekana lini linabaki kuwa siasa. Mitaa ya Sinza kuna mabomba ya gesi mitaani lkn TPDC hadi sasa wamefeli kuwaunganisha wateja wa majumbani wanaosuburi huduma hiyo kwa miezi sasa.

Vv
 
Mkaa ni ghali kuliko gesi,hiyo ya kidogokidogo nzuri,ukweli ni watz masikini,ugumu upo kununua mtungi mwanzo au ukiisha Kisha unalazimika kujaza kwa 60k wakati mambo mabaya
 
Mbona watu wanafunga namm natangaza kila siku. Piga simu hii tukufungie 0747744895
 
Watu wananunua kila siku nasisi ndio tunawauzia piga simu hii 0747744895
 
Mkaa ni ghali kuliko gesi,hiyo ya kidogokidogo nzuri,ukweli ni watz masikini,ugumu upo kununua mtungi mwanzo au ukiisha Kisha unalazimika kujaza kwa 60k wakati mambo mabaya
Mkaa ni ghali kuliko gesi? Kwa dar au nchi nzima? Maana mikoani gunia elfu 10 ambalo mtu mwenye familia anatumia miezi miwili. Ila gesi ya elfu 60 hata wiki mbili hatoboi.

Ukweli kwa hili mm toka siku ya kwanza natamani nikutane na makamba nimueleze
 
Hapo tunacholenga ni kutunza mazingira boss.
 
Back
Top Bottom