Waziri Lukuvi tembelea maeneo ya Dar es Salaam, kuna viwanja vingi havijaendelezwa

Kama pamepimwa na kweli barabara ipo.. sioni kwanini mnamchekea... Kama unauthibitisho kuwa barabara hiyo wananchi wa ubavuni mwake wamepima.. na kama ipo inayokatisha katikati ya shamba na ilikuwepo kabla yeye hajamailikishwa hilo ni swala la wazi na lazima waliomilikisha na kumpimia na yeye mwenyewe wawajibike.. na ikibidi mnamdai fidia ya kuwanyima haki ya kupita kwa kipindi hiki chote... Mnaogopa cheo kwenye mambo straight forward!?
Tumefatilia sana mdau, Tatizo ni kwamba huyo masawe anatumia sana Polisi kutisha wananchi wanapotaka kuchonga hiyo barabara, pia anatumia baadhi ya watu Idara ya ardhi ofisi ya Halmashauri Wilaya ya Ilala kupotosha hilo jambo ili hiyo barabara ionekane haina maana kwa wananchi.

Pia huyo masawe anataka kuweka zuio mahakamani kutaka kuzuia hiyo barabara isichongwe na anafanya makusudi kutaka kuweka zuio ili akamilishe mipango yake ya kuuza hilo eneo.

Hilo eneo ni zaidi ya ekari tano lipo katikati ya Makazi ya watu eneo la Kinyerezi pia ni pori kubwa ambalo uhalifu unafanyika usiku wananchi wanaporwa vitu vyao, wezi wanajificha. Imefika hatua wezi wanaiba mifugo maeneo mengine halafu wanakuja kuchinjia kwenye hilo eneo, wananchi tunakuta kwato, vichwa na ngozi za mifugo asubuhi.

Ndio maana tunaomba serikali kuu kupitia Wizara ya Ardhi watusaidie kupata hiyo barabara sababu wananchi hatuna barabara ya kupita pia wamshauri huyo masawe aendeleze hilo eneo ili kuepusha uhalifu katika hilo eneo sababu sasa ni zaidi ya miaka 15 tangu ameanza kulimiliki hilo eneo huyo masawe.

Tunaomba Mh Waziri Lukuvi pia Mh Rais Magufuli waweze kutusaidia katika hili jambo sababu baadhi ya watendaji kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Ilala sio waaminifu kwa kua wanamsaidia huyo masawe.
 
Hiki ulichokieleza hapa ndio uhalisia wa maeneo yote hawa jamaa wana mapori makubwa hata barabara kutoa hawataki.
Hili tatizo ni kubwa mno.
Akifanya hivyo Lukuvi itakua vizuri sana.
Kuna mtu anaitwa masawe ana maeneo mengi huko Tabata Kinyerezi, Segerea, Kifuru n.k ni maeneo makubwa yapo location tofauti na kila eneo ni zaidi ya ekari tano.

Hayo maeneo yake mengi ni mapori, kitu kibaya ni kwamba hayo maeneo mengi kuna uhalifu mkubwa unafanyika ikiwemo kina mama kubakwa, kukabwa, watu kuporwa mali zao, wezi na majambazi kujificha n.k.
Lakini hadi Leo serikali imeshindwa kumwambia aendeleze hayo maeneo sababu yana miaka mingi na yapo katikati ya Makazi ya watu.

Wananchi wamejaribu kufatilia kwenye mamlaka za serikali ila wameshindwa sababu huyo masawe anatumia watendaji wa serikali na Polisi kutisha wananchi kwa kua ana Cheo kikubwa Tanroads.

Nimesikia hata eneo lililopimwa Kinyerezi kwa ajili ya soko la Kinyerezi kalimega na kuweka mashine zake za ujenzi kwa nguvu na mamlaka za serikali zimeshindwa kumuondoa. ( wanasema ana kampuni ya ujenzi inaitwa OSINGO construction).

Kitu kingine kingine ni kwamba mara nyingi ana migogoro mingi na wananchi katika hayo maeneo sababu hayo maeneo alishapima kinyemela bila kushirikiana na wananchi majirani hivyo upatikanaji wa barabara umekua mgumu sababu wananchi wanatakiwa kuzunguka umbali mrefu kukwepa mapori yake.

Amekua akitishia wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kuwapeleka Polisi hasa kituo cha Stakishali.

Anatumia mahakama kudhulumu wananchi haki zao sababu, anatumia pesa nyingi kuendesha kesi ashinde pia akitumia mahakama kuweka mazuio kwenye maeneo hayo ili wananchi wakose haki zao. Akiweka mazuio yeye hana cha kupoteza sababu sio mkazi wa maeneo hayo pia hayaendelezi mapori hayo.
Wanaoathirika na zuio za mahakama ni wananchi masikini wanaotegemea Viwanja vyao vidogo kwa ajili ya Makazi.

Hadi sasa ana mgogoro mkubwa na wananchi wa mtaa mmoja Kinyerezi sababu hilo eneo lake kubwa ekari tano limepimwa na serikali imethibitisha kwa michoro na mipaka na anayo Hati na pia wananchi majirani wanazo hati, kitu cha ajabu ni kwamba huyo masawe kafunga barabara iliyopo kwenye vipimo akisema ni eneo lake hivyo hataki wananchi wapite amechimba mitaro na kupanda magogo katika barabara hiyo iliyopimwa na kuthibitishwa na serikali kupitia Wizara ya ardhi.
Wananchi tunataka kuchonga barabara hiyo ila anatumia Polisi kutishia wananchi anakamata kiongozi wa serikali za mtaa, anaenda ofisi ya Mkurugenzi idara ya ardhi kupotosha pia amefungua kesi mahakamani kuweka mazuio ya kuchonga barabara ila hadi sasa hatujajua mahakama imetoa uamuzi gani.

Huyo masawe na kampuni yake OSINGO Construction ni mtu anaefahamika na watu wengi maeneo ya Kinyerezi, Kifuru, Segerea n.k kwa kuanzisha migogoro ya ardhi.

Nimeandika kwa kifupi na nina uthibitisho endapo ukihitajika na Wizara.
Hivyo naomba Mh Waziri Lukuvi au Mh Rais Magufuli utusaidie wananchi wa Kinyerezi, Kifuru, Segerea n.k kuhusu huyo masawe sababu anajisifia kwamba wewe ndie uliempa cheo Tanroads hivyo hakuna mtu wa kumfanya kitu.
 
Kwenye swala la njia au barabara mna haki ya njia... Kama amepima alitakiwa azuie asipite mtu kabisa... Kama njia ameiruhusu na imekuwa ya kutegemewa haipaswi kufungwa.. lazima akae mezani mtikir maridhiano.. na akikataa awape alternative..

Kikubwa wananchi mnakimbiliaga wanasheria tafuteni wataalamu wa mipango miji na wasimamizi wa ardhi Wawa saidie.. Na kama wakati wa upimaji njia aliikuta hapaswi kuifunga hata kama haikuwa rasmi.
Mipango miji wa halmashauri?
 
Hiki ulichokieleza hapa ndio uhalisia wa maeneo yote hawa jamaa wana mapori makubwa hata barabara kutoa hawataki.
Hili tatizo ni kubwa mno.
Ni tatizo kubwa hasa,
Huyo masawe yeye haishi huo mtaa ila ameshikilia hilo eneo ekari tano zaidi ya miaka 15 bila kuliendeleza na lipo katikati ya Makazi ya watu.
Kitu kibaya zaidi ni kwamba anazuia hata barabara halali ambayo imepimwa na serikali inatambua katika huo mtaa, hivyo hadi sasa wananchi wanapata tabu sana kwa kua hamna barabara.

Hivyo tunaomba Mh Raisi Magufuli na Wizara ya ardhi watusaidie hilo tatizo pale Tabata Kinyerezi.
 
Tatizo hawa viongozi wa serikali za mtaa hawajui chochote kuhusu sharia ya ardhi pia waoga na wengi maisha magumu

:) hao hao mkuu :D
Na wengine wapo mitaani registered planners au Fika TPRB (Bodi ya usajili wa Planners watakupa mtu sahihi awasaidie)
Sawa
 
Ni tatizo kubwa hasa,
Huyo masawe yeye haishi huo mtaa ila ameshikilia hilo eneo ekari tano zaidi ya miaka 15 bila kuliendeleza na lipo katikati ya Makazi ya watu.
Kitu kibaya zaidi ni kwamba anazuia hata barabara halali ambayo imepimwa na serikali inatambua katika huo mtaa, hivyo hadi sasa wananchi wanapata tabu sana kwa kua hamna barabara.

Hivyo tunaomba Mh Raisi Magufuli na Wizara ya ardhi watusaidie hilo tatizo pale Tabata Kinyerezi.
Huyo anavuna kupitia Watu wanaoendeleza wanaomzunguka.

Hao wanaojenga ndio wanaoongeza thamani, ndio wanaoongeza idadi ya Watu na kuboresha na yeye anaoona thamani inapanda kwa eneo lake.

Hivyo yeye anawaibia ninyi. Maana hashiriki kuboresha ila anafurahia faida..na tena haimtoshi anaendelea kutaka kupata zaidi!? Mwizi huyo wa juhudi za umma.

Andikeni kuomba eneo hilo litwaliwe na manispaa kwa matumizi ya huduma za kijamii. Na kumuandikia na Rais kumuomba itwaliwe kwa maslahi ya mtaa.. zahanati, shule ya awali, msingi, secondary... Halafu mnaazimia kuanzia vikao vya mtaa kama shamba pori ...
 
Tatizo hawa viongozi wa serikali za mtaa hawajui chochote kuhusu sharia ya ardhi pia waoga na wengi maisha magumu

Sawa
Kisheria serikali za mitaa hawana mamlaka ya kutatua migogoro ya Viwanja ambavyo vimeshapimwa na vina Hati,

Jukumu la kutatua matatizo ya Viwanja vilivyopimwa ni la Halmashauri husika na serikali kuu.

Hivyo huyo masawe anatumia baadhi ya watumishi Idara ya Ardhi, Halmashauri ya Wilaya ya Ilala ili kuzuia hiyo barabara ambayo ipo katika Viwanja vilivyopimwa hapo tabata Kinyerezi ishindwe kuchongwa kwa maslahi yake binafsi.
Wananchi wanapata tabu, serikali haichukui hatua yeyote dhidi ya huyo masawe.

Pia huyo masawe analaumiwa na wananchi wengine maeneo ya Kifuru na Hapo Kinyerezi kwa kuzulumu maeneo yao, anatumia Polisi kutisha na baadhi ya watumishi Idara ya ardhi Halmashauri Wilaya ya Ilala kuzulumu haki za wananchi.
 
Huyo anavuna kupitia Watu wanaoendeleza wanaomzunguka.

Hao wanaojenga ndio wanaoongeza thamani, ndio wanaoongeza idadi ya Watu na kuboresha na yeye anaoona thamani inapanda kwa eneo lake.

Hivyo yeye anawaibia ninyi. Maana hashiriki kuboresha ila anafurahia faida..na tena haimtoshi anaendelea kutaka kupata zaidi!? Mwizi huyo wa juhudi za umma.

Andikeni kuomba eneo hilo litwaliwe na manispaa kwa matumizi ya huduma za kijamii. Na kumuandikia na Rais kumuomba itwaliwe kwa maslahi ya mtaa.. zahanati, shule ya awali, msingi, secondary... Halafu mnaazimia kuanzia vikao vya mtaa kama shamba pori ...
Wazo zuri sana mdau, Kinyerezi ni mji mkubwa, wakisasa na ulishaendelea ila huyo masawe ndio anamiliki hilo pori ekari tano katikati ya mji,
Kwa jeuri ya Cheo chake pale Tanroads na pesa zake ndio anafanya hivyo vituko vya kufunga barabara halali iliyopimwa na kuthibitishwa na serikali,

Pia katika hilo eneo ekari tano Kuna uhalifu mkubwa unafanyika usiku.

Kitu kingine cha kushangaza ni kwamba huyo masawe ana Cheo kikubwa sana Tanroads na anafahamu Sheria za barabara ambayo imeshapimwa ila anajitapa na kufanya makusudi kwamba hata hicho Cheo hapo Tanroads kapewa na Mh Rais Magufuli hivyo hakuna mtu wa kumfanya chochote.

Mh Rais Magufuli tunakuomba mfatilie huyo masawe, binafsi sina hakika Mh Rais akawa na mafungamano na mtu kama huyo masawe anaezulumu maeneo wananchi huko Kinyerezi, Kifuru n.k imefika hatua anazuia barabara halali iliyopimwa na kuthibitishwa na serikali
 
Back
Top Bottom