Waziri Lukuvi tembelea maeneo ya Dar es Salaam, kuna viwanja vingi havijaendelezwa

Davan

JF-Expert Member
Jun 15, 2020
1,126
1,404
Naongelea maeneo ya Goba, Bunju, Madale, Mabwepande, Kigamboni n.k

Watu wameweka maeneo makubwa yamekuwa mapori. Wengi uwezo wa kujenga hawana sababu walishastaafu na kuuza hawataki.

Wazee hawa wana street mipango mingi ila fedha hawana sasa maeneo yao yamebaki mazalia ya nyoka na kenge na machimbo ya vibaka.

Serikali ichukue haya maeneo ijenge shule, zahanati, vituo vya polisi au viwanja vya michezo ya watoto.

Wananchi tunaingia gharama kubwa kuvuta huduma za jamii kama maji na umeme sababu hadi muzunguke eneo la mtu zaidi ya heka 4.

Wengine wanajenga chumba kimoja ili waonekane wameendeleza eneo.

Kama hawawezi kuendeleza wauze ili Mji uchangamke.
 
Mbaya sana, kama kiwanja hakijajengwa makazi ya kudumu baada ya miaka 10, basi lazima kirudishwe wizarani kipewe wenye uwezo huo. Period..
 
Mbaya sana, kama kiwanja hakijajengwa makazi ya kudumu baada ya miaka 10, basi lazima kirudishwe wizarani kipewe wenye uwezo huo. Period..
Kuna viwanja unavikuta tangia unanunua, unajenga, unahamia, unaoa,unazaa hadi mtoto anaenda shule.
Eneo lipo tu
 
Sio kila eneo lazima lijengwe.Watanzania akili ndogo sana, mji utapumuaje kama kila eneo linajengwa kama mansese.Serikali isioona mbali ndio itakayoshawishi kila eneo lijengwe huku haina open space za kupumulia.Kila kiwanja kikijengwa dar, hali itakuwa mbaya zaidi ya sasa.
 
Lakini si yako maeneo Tengefu ya wazi na ukanda wa kijani kwa ajili ya shughuli hiyo ya upumuaji wa mji!? Hawa wanaomiliki maeneo yaliyopangwa kwa matumizi mengine zaidi ya Uwazi na Bustani kwann hawajengi?

maana kwa haraka haraka naona hasara yake ni kubwa na inamgusa kila mtu.
 
Ni vyema ukajitolea lile la kwako ujitolee litumike kwa matumizi ya umma. Hayo mengine yataangaliwa taratibu, wakati nyoka na kenge wakiendelea kupata hifadhi salama.
 
Ni vyema ukajitolea lile la kwako ujitolee litumike kwa matumizi ya umma. Hayo mengine yataangaliwa taratibu, wakati nyoka na kenge wakiendelea kupata hifadhi salama.
Compact cities are more efficient ... Kuwa na maeneo makubwa katikati ya miji kuna athari kubwa na zinamuathiri kila mtu..

Ninachoona huu mjadala ni mtamu.. tuu boreshe.. tunawezaje kubalance speculation na development kupunguza urbansprawl
 
Mishahara haijapanda kwa miaka mitano na tofali moja sasa hivi ni 1,000. Ninakumbusha tu.
Na miji ikizidi kuwa mikubwa inaongeza gharama za usimamizi na uendeshaji ambazo zingeweza kupelekwa kuongeza mishahara na kupunguza gharama za maisha.

Mfano Laven Ubeligiji haina skyscrapers na ina radius ya 7km ina jumla ya watu milioni Tatu. Kahama ina radius beyond 7km ina watu laki tatu na ishasongamana..

Siku Kahama ikifikisha watu milioni tatu gharama za usimamizi na uendeshaji zitakuwa kubwa mno ukilinganisha na Mji compact kama Laven
 
Lakini eneo ni la makazi
Sio kila eneo lazima lijengwe.Watanzania akili ndogo sana, mji utapumuaje kama kila eneo linajengwa kama mansese.Serikali isioona mbali ndio itakayoshawishi kila eneo lijengwe huku haina open space za kupumulia.Kila kiwanja kikijengwa dar, hali itakuwa mbaya zaidi ya sasa.
 
7 Reactions
Reply
Back
Top Bottom