Waziri Lukuvi tembelea maeneo ya Dar es Salaam, kuna viwanja vingi havijaendelezwa

Serikali imeshaanza kutekeleza Mpango wa upimaji na urasimishaji wa maeneo yote ya DSM,

Hiyo inawapa changamoto wamiliki wa ardhi kulipia viwanja kila Mwaka ambavyo haviingizi kipato chochote mwishowe wataamua kuviuza wenyewe!

Zoezi la upimaji na urasimishaji likishakamilika watu wenye maeneo makubwa watalazimika kuuza sababu haitakuwa na faida kumiliki eneo tupu halafu ulilipie kodi serikalini kila Mwaka.

Watauza tu ni swala la muda.
 
Unadhani hayajui hayo? Anajua sana! Mfano Viwanja vya Mradi Kwembe, Wilaya ya Ubungo ni ufisadi mtupu hawezi kuvigusa miaka 800! Watu wameuziwa viwanja wawili mpaka watatu sehemu moja, hakuna miundo mbinu ya barabara, wananchi wanachonga wajuavyo, umeme na maji vinapitishwa hadi kati ya kiwanja cha mtu! Mheshimiwa analijua hili!
 
Assuming hawawezi kulipa kodi.. what if wanaweza na wanalipa kodi ila hawaendelzi!?
 
Unadhani hayajui hayo? Anajua sana! Mfano Viwanja vya Mradi Kwembe, Wilaya ya Ubungo ni ufisadi mtupu hawezi kuvigusa miaka 800! Watu wameuziwa viwanja wawili mpaka watatu sehemu moja, hakuna miundo mbinu ya barabara, wananchi wanachonga wajuavyo, umeme na maji vinapitishwa hadi kati ya kiwanja cha mtu! Mheshimiwa analijua hili!
Hii kwa sasa imepatiwa ufumbuzi... Ni ngumu sana kuuza kiwanja mara mbili.. maana taarifa zinatunzwa kwenye mfumo.. na viwanja vya serikali vinauzwa kupitia mfumo.
 
Serikali imeshaanza kutekeleza Mpango wa upimaji na urasimishaji wa maeneo yote ya DSM,

Hiyo inawapa changamoto wamiliki wa ardhi kulipia viwanja kila Mwaka ambavyo haviingizi kipato chochote mwishowe wataamua kuviuza wenyewe!

Zoezi la upimaji na urasimishaji likishakamilika watu wenye maeneo makubwa watalazimika kuuza sababu haitakuwa na faida kumiliki eneo tupu halafu ulilipie kodi serikalini kila Mwaka.

Watauza tu ni swala la muda.
Kodi ya ardhi ni kiasi gani?
 
Unadhani hayajui hayo? Anajua sana! Mfano Viwanja vya Mradi Kwembe, Wilaya ya Ubungo ni ufisadi mtupu hawezi kuvigusa miaka 800! Watu wameuziwa viwanja wawili mpaka watatu sehemu moja, hakuna miundo mbinu ya barabara, wananchi wanachonga wajuavyo, umeme na maji vinapitishwa hadi kati ya kiwanja cha mtu! Mheshimiwa analijua hili!
Nampongeza kwa upimaji ila kwa mambo mengine wizara ya ardhi bado ina changamoto nyingi
 
Hii kwa sasa imepatiwa ufumbuzi... Ni ngumu sana kuuza kiwanja mara mbili.. maana taarifa zinatunzwa kwenye mfumo.. na viwanja vya serikali vinauzwa kupitia mfumo.
Watu wanauziana kienyeji wakati mwenye hati ni mwingine
 
Hiyo ni elimu duni.. Kuuziana kienyeji ardhi ni ujinga wa mnunuaji..

Ardhi Tanzania ni ya Umma.. sisi tunakodi kutumia.. so unapolipa kununua kiwanja ..unalipa kupewa access ya kuitumia ardhi.. to put its simply unakodishwa kwa term ya miaka 33/66/99

Ardhi ni yetu... Custodian ni Rais... Na yeye humteua Kamishna Asimamie. Hiyo hiyo ardhi tumeigawa kwenye makundi matatu.. Ardhi ya Umma, General land ambayo ndiyo hii ardhi ya Mijini... Village land (ardhi ya vijiji) na Reserve Land (Ardhi ya Hifadhi)

Taratibu za access to each group ni tofauti.. lakini haiishii kwenye Access tu kuna taratibu za kuitumia nazo zinatofautiana na zina mlolongo tofauti.

Elimu ya Matumizi ya Ardhi na Umiliki Tanzania ni ndogo sana.. na kwa sababu ya how sensitive this issues is wanasiasa wanaitumia sana kujijengea umaarufu..

Ukweli ni kuwa strict measures lazima zichukuliwe otherwise huo ujinga wa kuvamia.na kuuza ardhi iliyotwaliwa kisheria unaua Uchumi na kuzorotesha mazingira ya uwekezaji..

Pinga kabisa huo ujinga wa kuuziana ardhi na matapeli. Wanaua uchumi
 
Nampongeza kwa upimaji ila kwa mambo mengine wizara ya ardhi bado ina changamoto nyingi
Wizara ya ardhi haiwezi kupanga na kupima na kusimamia utekelezaji wa mipango ya uendelezaji miji.. ukiwa na watu tena wasomi wananunua ardhi zisizopimwa na kujenga kiholela..

Watanzania hawana Adabu... Na kuishi kwenye modern towns or cities kunahitaji Discipline.
 
Ndiyo nyie mnaporaga ardhi za watu vijijini. Kama haifanyii kazi wewe inakuhusu nini?
Njoo usafishe walau majirani zako tukujue mnachelewesha sana maendeleo ukijenga mtaa unachangamka sasa wewe unabanana Manzese huko badala ya kuja kujenga plot yako
 
Wizara ya ardhi haiwezi kupanga na kupima na kusimamia utekelezaji wa mipango ya uendelezaji miji.. ukiwa na watu tena wasomi wananunua ardhi zisizopimwa na kujenga kiholela..

Watanzania hawana Adabu... Na kuishi kwenye modern towns or cities kunahitaji Discipline.
Kama hamupimi maeneo watu wafanyeje, kipindi cha nyuma tu hapo mlikuwa mnapima viwanja mnaviuza vyote kwa mafisadi wachache na vingine kugawana nyie na ndugu zenu ili baadaye mviuze kwa bei kubwa, halafu unakuja hapa kuongea pumba hizi!
 
Huyu Lukuvi anajitahidi sana kuweka mambo sawa ndanin ya wizara yake lakini nafikiri mwingiliano wa wizara yake na Halmashauri za wilaya kiutendaji ndipo balaa linapoanzia, mfano hai kabisa ni pale mie niliponunua kiwanja kule Kibaha kwa Matias na kupimiwa miaka mitatu nyuma mpaka leo sijapata document yoyote ikiniruhusu kuendeleza chochote toka ofisi za Ardhi wilaya lakini ajabu mwaka huu kaja mwekezaji kapewa eneo na ofisi ya ardhi imepima na kumpatia hati zake na tayari ameshaanza kupaendeleza kisheria,

Sasa kwa haraka haraka utaona kuwa mwenzetu kwa taratibu za Halmashauri ( au kwa nguvu za giza) ameweza fanikiwa kwa mwendo wa fastruck na sie tunaomsikiliza Lukuvi na sera zake za hati itolewe mapema ndani ya siku chache bado tunaambiwa viwanja vyetu vina matatizo na barua imepelekwa kwa Mkurugenzi wizarani ili atoe uamuzi na ni mwaka wa tatu huu

Kama Rais alivyoagiza pale alipokuwa anahutubia baraza jipya la mawaziri ... Mr Lukuvi kuna wakati anatakiwa lazima atoe maamuzi hata kama ni mabaya lakini afanye hivyo kwa manufaa ya serikali, Halmashauri na watu wake, haiwezekani ndani ya serikali ya mtaa mmoja kuwe na shida moja lakini ipewe ufumbuzi tofauti kwa kuangalia sura za watu
 
Back
Top Bottom