Waziri Lukuvi tembelea maeneo ya Dar es Salaam, kuna viwanja vingi havijaendelezwa

ni kweli kabisa pembezoni mwa jiji la DSM wazee wa zamani wamehodhi maeneo makubwa ambayo ni pori tupu na kusababisha kuzaliana kwa majoka na vichaka vya wezi na hivyo kupoteza maana ya jiji. niwakati sasa sheria ichukue nafasi yake.
 
Unashida na prot ukakosa
Au unatafut watu maneno

Plot nimenunua 2014, 2018 nikapimiwa au nikupe documents uone? niwatafute maneno ili inisaidie nini? lengo langu ni watu wawajibike vile waziri anavyotaka sera za serikali yake zitimizwe
 
Jengeni au uzeni maeneo yenu mnaweka mapori mjini.
Mfano mbezi beach africana ukimaliza sheli mpya ya Total kuna eneo kubwa tu limepandwa mitiki. Unapanda mitiki mbezi beach kama tuko mafinga halafu shule zinajengwa maporini huko wakati maeneo ya barabarani yana mitiki
 
Maafisa mipango miji bila ya hela hatoki ofisini hata kutatua migogoro ya barabara za mitaa tu wanashindwa
 
Huyu Lukuvi anajitahidi sana kuweka mambo sawa ndanin ya wizara yake lakini nafikiri mwingiliano wa wizara yake na Halmashauri za wilaya kiutendaji ndipo balaa linapoanzia, mfano hai kabisa ni pale mie niliponunua kiwanja kule Kibaha kwa Matias na kupimiwa miaka mitatu nyuma mpaka leo sijapata document yoyote ikiniruhusu kuendeleza chochote toka ofisi za Ardhi wilaya lakini ajabu mwaka huu kaja mwekezaji kapewa eneo na ofisi ya ardhi imepima na kumpatia hati zake na tayari ameshaanza kupaendeleza kisheria,

Sasa kwa haraka haraka utaona kuwa mwenzetu kwa taratibu za Halmashauri ( au kwa nguvu za giza) ameweza fanikiwa kwa mwendo wa fastruck na sie tunaomsikiliza Lukuvi na sera zake za hati itolewe mapema ndani ya siku chache bado tunaambiwa viwanja vyetu vina matatizo na barua imepelekwa kwa Mkurugenzi wizarani ili atoe uamuzi na ni mwaka wa tatu huu

Kama Rais alivyoagiza pale alipokuwa anahutubia baraza jipya la mawaziri ... Mr Lukuvi kuna wakati anatakiwa lazima atoe maamuzi hata kama ni mabaya lakini afanye hivyo kwa manufaa ya serikali, Halmashauri na watu wake, haiwezekani ndani ya serikali ya mtaa mmoja kuwe na shida moja lakini ipewe ufumbuzi tofauti kwa kuangalia sura za watu
Hela tu
 
ni kweli kabisa pembezoni mwa jiji la DSM wazee wa zamani wamehodhi maeneo makubwa ambayo ni pori tupu na kusababisha kuzaliana kwa majoka na vichaka vya wezi na hivyo kupoteza maana ya jiji. niwakati sasa sheria ichukue nafasi yake.
Kuna eneo moja la generali fulani ameshafariki sasa limekuwa pori kubwa na watoto hawana uwezo wa kuendeleza kwahiyo limebaki malisho ya mifugo
 
Jengeni au uzeni maeneo yenu mnaweka mapori mjini.
Mfano mbezi beach africana ukimaliza sheli mpya ya Total kuna eneo kubwa tu limepandwa mitiki. Unapanda mitiki mbezi beach kama tuko mafinga halafu shule zinajengwa maporini huko wakati maeneo ya barabarani yana mitiki
Kwani Mashamba hayatakiwi mjini Mkuu!? Tena ningesema tumekuwa nayo machache sana.. mji wetu hauna green belt za kutosha na wengi tunadhani kukua mji ni kuendelea kujenga from upanga mpaka chalinze without a break.. Huo sio mtazamo sahihi kwa mji sahihi.

Lakini pia miti inasaidia kufanya carbon offset... Kwa jinsi tulivyorundikana bila utaratibu... Air quality inapungua.. ndio maana ukiwa Sinza na ukatoka ukaenda dondwe lazima uhisi utofauti katika ubora wa hewa unayoivuta.

Tena ningesema kama wengine wangeweza kutunza na kuweka maeneo ya kijani mjini wangepewe hata punguzo la kodi.. maana yana faida kubwa...sana.
 
Unaweza kujenga na miti ukapanda pia lakini sio ekari 3 zote upande mitiki. Sidhani kama lengo lake yule ni kunyonya hewa chafu ya ukaa.
Hakuna tajiri mwenye moyo huo, hahahaa
 
Pelham Bay Park Bronx 2,765 acres.

Greenbelt, Staten Island 1,778 acres.

Van Cortlandt Park, Bronx 1,146 acres.

Flushing Meadows/Corona Park, Queens 898 acres.

Central Park, Manhattan 843 acres.

Marine Park, Brooklyn 798 acres.

Bronx Park, Bronx 718 acres.

Ukitoa Jangwani zaidi ya ekari 200 na Coco beach zaidi ya ekari 90 hatuna park nyingine yoyote sizable.. na hiyo itaathiri ubora wa hewa wa jiji.

Kwa jiji hili at least 10pc ilitakiwa iwe eneo Tengefu kwa ajili ya ukanda wa kijani.. kukabiliana na JOTO, MAFURIKO na Kushuka kwa ubora wa hewa... Na kingine usafi na uzuri wa mji.

Hizo parks hapo juu zote ni kwa New York pekee.. na hizo hazina Neighborhood parks wala cluster open spaces ambazo ni.mandatory kwenye uendelezaji wa miji.

Ardhi ni rasilimali, hebu fikiria ikiwa Mtu ana Ekari 100 na hajajua azifanyie nn... Anaiomba serikali impe matumizi ya Shamba la miti serikali inakubali na anaendeleza kwa kupanda miti.. sisi faida yake tutaipata.. hewa itakuwa safi na mji utakuwa wa kijani

Akishakujua nini anataka kufanya atarudi kuomba kufanya mabadiliko ambayo serikali inaouwezo wa kumbana aendeleze bila kukata miti yote nakuacha sehemu kubwa na eneo lake kuendelea kuwal la kijani.. Hii inawezekana kabisa.. kama taasisi zinajengwa kwa thabiti.
 
Kwani Mabwe ni katikati ya mji mkuu

Sent from my SM-J530F using JamiiForums mobile app
Katikati ya mji ni Subjective... Ukiwa Ubungo upo katikati ya mji... Ukienda ukifika Kiluvya uko nje ya mji... Lakini ukifika Maili Moja uko katikati ya mji wa Kibaha..

Ubaya ni kuwa na maeneo makubwa Kariakoo, Au Magomeni ambayo yamepangwa kwa matumizi ya Ujenzi ila hayakuendelezwa... Nadhani mtoa mada anazungumzia katikati kwa mrengo huo.
 
Naongelea maeneo ya Goba, Bunju, Madale, Mabwepande, Kigamboni n.k

Watu wameweka maeneo makubwa yamekuwa mapori. Wengi uwezo wa kujenga hawana sababu walishastaafu na kuuza hawataki.

Wazee hawa wana street mipango mingi ila fedha hawana sasa maeneo yao yamebaki mazalia ya nyoka na kenge na machimbo ya vibaka.

Serikali ichukue haya maeneo ijenge shule, zahanati, vituo vya polisi au viwanja vya michezo ya watoto.

Wananchi tunaingia gharama kubwa kuvuta huduma za jamii kama maji na umeme sababu hadi muzunguke eneo la mtu zaidi ya heka 4.

Wengine wanajenga chumba kimoja ili waonekane wameendeleza eneo.

Kama hawawezi kuendeleza wauze ili Mji uchangamke.
Akifanya hivyo Lukuvi itakua vizuri sana.
Kuna mtu anaitwa masawe ana maeneo mengi huko Tabata Kinyerezi, Segerea, Kifuru n.k ni maeneo makubwa yapo location tofauti na kila eneo ni zaidi ya ekari tano.

Hayo maeneo yake mengi ni mapori, kitu kibaya ni kwamba hayo maeneo mengi kuna uhalifu mkubwa unafanyika ikiwemo kina mama kubakwa, kukabwa, watu kuporwa mali zao, wezi na majambazi kujificha n.k.
Lakini hadi Leo serikali imeshindwa kumwambia aendeleze hayo maeneo sababu yana miaka mingi na yapo katikati ya Makazi ya watu.

Wananchi wamejaribu kufatilia kwenye mamlaka za serikali ila wameshindwa sababu huyo masawe anatumia watendaji wa serikali na Polisi kutisha wananchi kwa kua ana Cheo kikubwa Tanroads.

Nimesikia hata eneo lililopimwa Kinyerezi kwa ajili ya soko la Kinyerezi kalimega na kuweka mashine zake za ujenzi kwa nguvu na mamlaka za serikali zimeshindwa kumuondoa. ( wanasema ana kampuni ya ujenzi inaitwa OSINGO construction).

Kitu kingine kingine ni kwamba mara nyingi ana migogoro mingi na wananchi katika hayo maeneo sababu hayo maeneo alishapima kinyemela bila kushirikiana na wananchi majirani hivyo upatikanaji wa barabara umekua mgumu sababu wananchi wanatakiwa kuzunguka umbali mrefu kukwepa mapori yake.

Amekua akitishia wenyeviti wa serikali za mitaa kwa kuwapeleka Polisi hasa kituo cha Stakishali.

Anatumia mahakama kudhulumu wananchi haki zao sababu, anatumia pesa nyingi kuendesha kesi ashinde pia akitumia mahakama kuweka mazuio kwenye maeneo hayo ili wananchi wakose haki zao. Akiweka mazuio yeye hana cha kupoteza sababu sio mkazi wa maeneo hayo pia hayaendelezi mapori hayo.
Wanaoathirika na zuio za mahakama ni wananchi masikini wanaotegemea Viwanja vyao vidogo kwa ajili ya Makazi.

Hadi sasa ana mgogoro mkubwa na wananchi wa mtaa mmoja Kinyerezi sababu hilo eneo lake kubwa ekari tano limepimwa na serikali imethibitisha kwa michoro na mipaka na anayo Hati na pia wananchi majirani wanazo hati, kitu cha ajabu ni kwamba huyo masawe kafunga barabara iliyopo kwenye vipimo akisema ni eneo lake hivyo hataki wananchi wapite amechimba mitaro na kupanda magogo katika barabara hiyo iliyopimwa na kuthibitishwa na serikali kupitia Wizara ya ardhi.
Wananchi tunataka kuchonga barabara hiyo ila anatumia Polisi kutishia wananchi anakamata kiongozi wa serikali za mtaa, anaenda ofisi ya Mkurugenzi idara ya ardhi kupotosha pia amefungua kesi mahakamani kuweka mazuio ya kuchonga barabara ila hadi sasa hatujajua mahakama imetoa uamuzi gani.

Huyo masawe na kampuni yake OSINGO Construction ni mtu anaefahamika na watu wengi maeneo ya Kinyerezi, Kifuru, Segerea n.k kwa kuanzisha migogoro ya ardhi.

Nimeandika kwa kifupi na nina uthibitisho endapo ukihitajika na Wizara.
Hivyo naomba Mh Waziri Lukuvi au Mh Rais Magufuli utusaidie wananchi wa Kinyerezi, Kifuru, Segerea n.k kuhusu huyo masawe sababu anajisifia kwamba wewe ndie uliempa cheo Tanroads hivyo hakuna mtu wa kumfanya kitu.
 
Kwenye swala la njia au barabara mna haki ya njia... Kama amepima alitakiwa azuie asipite mtu kabisa... Kama njia ameiruhusu na imekuwa ya kutegemewa haipaswi kufungwa.. lazima akae mezani mtikir maridhiano.. na akikataa awape alternative..

Kikubwa wananchi mnakimbiliaga wanasheria tafuteni wataalamu wa mipango miji na wasimamizi wa ardhi Wawa saidie.. Na kama wakati wa upimaji njia aliikuta hapaswi kuifunga hata kama haikuwa rasmi.
 
Kuhusu njia ipo miaka yote kabla hata huyo masawe ajanunua hilo eneo, watu wa mipango miji na Idara ya ardhi ofisi ya Halmashauri wilaya ya Ilala wanafahamu hilo jambo, ila wanaogopa kutekeleza kwa kuchonga hiyo barabara sababu wanamuogopa huyo masawe kwakua anapesa nyingi pia anacheo kikubwa Tanroads.

Ni kwamba huyo masawe ameshapima hilo eneo lake na anayo Hati ila anasema pia eneo la barabara iliyopo katika eneo hilo ni eneo lake hivyo kaifunga kwa kuchimba mitaro na kupanda magogo.

Barabara hiyo ndio inayotenganisha yeye na wananchi wengine na hata hao wananchi wameshapima Viwanja vyao, pia barabara hiyo ndio inategemewa na wananchi kuweza kupita,
Serikali ilishathibitisha huo upimaji tangu mwaka 2008 na 2009 na inatambua hiyo barabara.

Hili jambo analofanya huyo masawe ni la ajabu na aibu sababu nae ni mtendaji wa serikali tena yupo ngazi ya juu Tanroads ila ndio anaefanya mambo ya hovyo kwa kutaka kuchukua eneo la barabara ya wananchi kwa nguvu kwa kutumia pesa na Cheo alichokua nacho.

Hivyo tunaomba serikali kupitia Wizara ya Ardhi au Raisi Magufuli kuingilia kati kuhusu hili jambo ili hiyo barabara iweze kuchongwa sababu anachofanya huyo masawe ni unyanyasaji na uonevu kwa wananchi.
Wananchi hatuna barabara nyingine ya kupita.
 
Kama pamepimwa na kweli barabara ipo.. sioni kwanini mnamchekea... Kama unauthibitisho kuwa barabara hiyo wananchi wa ubavuni mwake wamepima.. na kama ipo inayokatisha katikati ya shamba na ilikuwepo kabla yeye hajamailikishwa hilo ni swala la wazi na lazima waliomilikisha na kumpimia na yeye mwenyewe wawajibike.. na ikibidi mnamdai fidia ya kuwanyima haki ya kupita kwa kipindi hiki chote... Mnaogopa cheo kwenye mambo straight forward!?
 
Back
Top Bottom